TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

SAFARI YA TANGA ILIOGEUKA SAFARI YA KUZIMU 02

*SAFARI YA TANGA ILIVYOGEUKA KUWA SAFARI YA KUZIMU*
*SEHEMU YA PILI*
______________________________________ 
"Razack..!, Razack..!..Razack..!"
sauti nyepesi ya kike ilipenya katika masikio yangu, haikuwa sauti ngeni sana katika masikio yangu. 
"wew Razack wew..weeweeeee.....hamka bhana wewe una nini lakini.."
Sauti ile iliendelea kupenya katika masikio yangu tena safari hii ilikuwa ikiita kwa hasira kuonesha kila dalili ya kutoridhika na ukimya wangu.
aliendelea kuniita na alipoona sihamki alianza kunitikisa, hapo nilistuka.
"hapana sijakufaaa...sijakufaaaaa"
nilisema kwa nguvu huku nikirusha miguu na mikono.
Jasmine alibaki ameduwaa.
"una matatizo gani Razack...mbona sikuelewi"
"Aaah eti mimi nimekufa...? mimi nimekufa "
"hapana huja.. huja.. kuna nini kwani"
"Aaaah...."
nilihema kwa nguvu, kumbukumbu mbaya za kutisha zilizotokana na ndoto mbaya ambayo nilikuwa nimeiota ziliendelea kunitesa kwa dakika kadhaa, mapigo yangu ya moyo yaliendelea kudunda kwa kasi pia hata macho yangu hayakutulia sehemu moja lakini kadri jinsi ambavyo sekunde zilivyoenda ndivyo kadri ambavyo hofu,  ilikuwa ikipungua na hii yote ilikuwa ni baada ya kuzungusha macho yangu kila upande na kujikuta nipo juu ya kitanda changu kile kile cha kila siku ndani ya chumba changu mwilini nilikuwa na boksa na vest na wala sio 'sanda' na nilipojiingiza vidole puani na masikioni wala sikuwa na pamba ,pia pembeni yangu alikuwepo Jasmine, msichana ambaye nilikuwa na mahusiano naye ya kimapenzi japo sikuwa nikimpenda.
hapo hofu ilishuka kabisa nilirudi katika hali yangu ya kawaida, ile ndoto mbaya nilimuhadithia Jasmine.
"Aaah sidhani kama itakuwa na maana yoyote ile..ni ndoto tu kama ndoto zingine.."
Jamsine alisema huku mikono yake miteke ikiwa juu ya kifua changu taratibu akinipiga piga, angalau aliituliza presha yangu.
"kweli..eenh.."
"yeah..."
Jasmine, alisema.
stori chache tulipiga kuhusu ndoto ile, Jasmine alijitahidi kunipa moyo hata kwa stori za uongo na ukweli ilimradi tu nirudi katika hali yangu ya kawaida.
"hata mimi pia nikiwa kidato cha kwanza niliota naoshwa kama maiti,watu wanalia kabisa niliogopa sana, lakini hakuna chochote kilichotokea mpaka leo"
Jasmine alisema na ndani ya dakika kadhaa nilijikuta nikisahau kila kitu kuhusu ndoto ile.
tulipiga stori chache za hapa na pale hatukujali kama ilikuwa bado hapajapambazuka saa kubwa ya ukutani ilikuwa ikisoma saa 10 na nusu alfajiri, lakini hata hivyo stori zetu hizi zilitamatika sekunde chache tu baada mlio wa simu yangu, kusikika.
tulistuka wote kwa sekunde zisizopungua kumi tulitazama, tulipigwa na butwa maana haikuwa kawaida simu yangu kuita majira ya usiku wala alfajiri mara chache ilikuwa mchana na mara nyingi ilikuwa jioni.
hofu kubwa ilinitawala, kitu cha kwanza kunijia kichwani mwangu ni usalama wa watu wangu wa karibu, je wapo wazima..?, maana simu za usiku huwa zina mengi taarifa mbaya zikiwemo kwa kiasi asilimia tisini, hivyo  nilihofia sana.
"mmmh kwema kweli..., nani huyo"
Jasmine aliniuliza lakini sikutambua hata alikuwa anahitaji jibu la maana gani maana wote tulikuwa pale kitandani na wote tulikuwa na hisia sawa ,za hofu, lakini nilijizuia kumtolea maneno au kumfanyia kitendo chochote ambacho kingemkasirisha badala yake nilimpa amri.
"kaielete.."
Haraka Jasmine aliinuka akiwa ndani ya 'night-dress' iliyotangulia na ch#p¥ kisha shanga chache zikapita kiunoni na kijionesha vyema kwa nje na hata pale alipopiga hatua za madaha , huko nyuma alishawishi haswaa lakini sikuwa na hisia hata chembe, zaidi ya kukasilishwa na ule mwendo wake wa madaha ambao ulinifanya nione kama anachelewa.
"embu harakakisha bas..."
nilisema kwa hasira , lakini ilisaidia kwani sekunde mbili tu Jasmine alirudi tena kitandani akiwa na simu, alinikabidhi.
nilipiga macho yangu kwenye kioo cha simu,akili nikaituliza kisha nikalisoma jina la mpigaji, angalau sasa kidogo nilipata amani, pumzi ndefu niliivuta kisha nikaishusha.
"bosi huyu...sijui anataka nini"
nilisema kwa sauti.
"mpokelee sasa"
Jasmine alinijibu.
dole langu gumba lilitua katika batani ya kupokelea kisha haraka  nikaipandisha simu mpaka sikioni na kukaa kimya kwa sekunde chache huku nikitarajia 'Bosi' ndiye awe wa kwanza kufungua mazungumzo, 
"Razack..."
"naam bosi.."
"Aaah kuna SAFARI ya ghafla imetokea hapa na unatakiwa uelekee TANGA,..kesho ambayo itakuwa ni tarehe ishirini na nne itabidi ikukute kule.."
bosi, aliongea lakini kwa namna alivyokuwa akiongea ilionesha dhahiri kama hakuwa sawa hata kidogo, kwanza alikuwa anaongea haraka haraka , pili alikuwa anaongea huku akihema mithili ya mtu apandaye mlima mkubwa tena kwa kasi na tatu alikuwa akiongea kwa ukali.
kwa maelezo yake alinitaka tarehe ishirini na nne ambayo ilikuwa ni kesho ya siku ile, inikute Tanga hivyo basi siku ile ile nilitakiwa nielekee Tanga, hii kwangu ilikuwa ni ghafla sana na sikukubaliana nalo lakini ujasiri wa kumpinga nilikuwa sina sababu maisha yangu yote pamoja na ya  wale wachache waliokuwa wakinizunguka yalikuwa yakitegemea mshahara na huyo bosi ndiye alikuwa mtoaji, hata wewe msomaji ungebisha..?
"bosi mbona ghafla sana.. na ni jukumu lipi hilo na pia Tanga sehemu gani..."
"jukumu lipi..Tanga sehemu gani utajua ukishafika Tanga pale pale ila kwa sasa unachotakiwa kufanya ni kujiandaa, pia  nakutumia laki tisa hii ni mbali na mshahara pia utaniambia kama kutakuwa na lolote utahitaji, lakini leo unatakiwa ufike Tanga.."
Bosi, alisema kisha akakata simu.
nilibaki nimepigwa na butwa macho yalinitoka kijasho chembamba kilinitoka, moyoni sikuwa na furaha lakini nilipokumbuka kwamba aliniahidi kunipatia kiasi cha shilingi laki tisa kama maandalizi ya safari pesa ambayo ilikuwa mara mbili ya mshahara wangu na pia ukizingatia juzi yake ambayo ilikuwa ni tarehe ishirini na moja ambapo nilipata mshahara wangu wote, niliachia tabasamu , kwani nilijiona nikijaa pesa ndani ya muda mchache sana, nilijikuta nikiachia tabasamu"
"vipi mbona unacheka cheka.."
Jasmine, aliniuliza.
"Aaah kuna safari ya ghafla nimeipata hapa, itanibidi nielekee Tanga leo leo.."
"what..."
Jasmine alisema kwa mshangao na usoni alionesha kila dalili ya kuchukizwa lakini hata hivyo nilimuelezea kwa ufupi kwanzia mwanzo mpaka mwisho mpaka kiasi cha pesa ambacho bosi aliniahidi kunipa, pia nikamuahidi kumpatia shilingi laki mbili ili na yeye akanunue chochote akipendacho, alijikuta akitoa makasiriko na kukaribisha furaha, wote tulitabasamu.

*********
Japokuwa sikuwa najua naelekea Tanga sehemu gani na kwa jukumu gani hasa, lakini siku hiyo maandalizi makubwa niliyafanya na nilijitahidi nifanye kama vile ambavyo bosi ameamrisha.
kwa msaada mkubwa wa Jasmine, mpaka kufika majira ya saa moja kamili asubuhi, nilikuwa tayari nishaiva kwa safari.

Itaendelea....

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post