*SAFARI YA TANGA ILIVYOGEUKA KUWA SAFARI YA KUZIMU*.
*SEHEMU YA TANO*
______________________________________
"Aaanh hapa kaka..nadhani hotel hii itakuwa bora sana kwako , huduma zao ni nzuri pia hata mandhari yametulia sana kaka..."
Alisema yule dereva wa bodaboda dakika chache tu baada ya kufika katika ile hotel ambayo alikuwa amenishauri nifikie,
tulikuwa tumesimama mbele ya geti moja kubwa lililopambwa kwa rangi nyeusi na kuongezewa nakshi chache za kuwakawaka ambazo zilitengeneza maandishi yaliyosomeka "MOREN HOTEL" upande wa juu kidogo.
pia kulikuwa na bustani ndogodogo ambazo zilikuwa zimetapakaa eneo la pale nje hakika palipendeza sana, hii ilinipa furaha na hamu ya kutaka kuingia ndani haraka.
nilijikuta nikimshukuru yule dereva lakini kitu kimoja kilinishangaza kuhusu dereva yule ni kwamba, kwa muda wote niliokuwa nikiongea naye alikuwa akiangalia pembeni, na nilipomkazia alikuwa haishiwi kujaribu kukwepesha macho, hakutaka nimtizame usoni hata kidogo, lakini hilo sikulipa umakini kwani lilikuwa halinihusu na wala sikutaka kujihusisha nalo, nilipogundua hataki tukutanishe macho nami niliamua kuongea huku nikiwa simtazami, ili nimpe uhuru wa kujiachia.
"aah..ulisema shingapi.."
"Aaah tutakutana tena kaka wala usijali"
alinijibu , kauli yake hii iliniacha njia panda kwani sikumuelewa hata kidogo.
"hahah acha zako bhan.."
nilisema kimzaha kisha nikaliinamia kidogo begi langu ambalo lilikuwa chini , na kuanza kusachi katika zipu chache za begi lile ili nitoe pesa ambazo nilikuwa nimeziweka humo,ili nimkabidhi dereva yule ujira wake.
"Aaah hii hap kaka asant..."
nilisema baada ya kuinuka na kugeuka upande ambao yule dereva wa bodaboda , alikuwa amesimama lakini nilichokiona sikuamini macho yangu.
yule dereva wa bodaboda alikuwa tayari kashatoweka eneo lile , hakuwepo tena.
nilipigwa na butwa, mikono yangu niliipachika kiunoni kisha nikaanza kuangaza huku na kule lakini hata hivyo sikumuona yule dereva.
"khaaa...kaondoka saa ngapi..mbona sijamsikia akitoka hapa...."
nilijisemea kimoyomoyo lakini nilipokosa majibu, niliamua kukubali yaishe huku nikiiruhusu hofu icheze na moyo wangu.
"hahahahah halafu ni kijana mdogo sana...kazaliwa mwaka 89 tarehe 3 mwezi wa tano , siku ya Alhamisi , nyota yake ni ya simba...hahaha"
"kwahiyo Tanga kaja leo...kule atakuja kesho..?"
"enhee kesho muda kama huu atakuwa katika makazi mapya..."
zilikuwa ni sauti mbili ambazo zilikuwa zinatoka katika vinywa vya wanaume wawili ambao walikuwa wamesimama takribani hatua ishirini tu kutoka pale nilipokuwa nimesimama nikizubaa zubaa.
japokuwa walikuwa mbali kidogo lakini walichokuwa wakikiongea chote nilikuwa nakisikia na kukielewa pia na niliposikiliza kwa umakini kwa kiasi fulani nilihisi kama wananiongelea mimi kwani walitaja mwaka na tarehe ambayo ndiyo niliyokuwa nimezaliwa, pia walitaja nyota yangu na pia walitaja kwa uchache kuhusu safari yangu. nilipigwa na butwaa kwa mara nyingine , niliacha kuhangaika na yule bodaboda badala yake nilitulia tuli masikio yangu yakiwa wazi kwa lengo la kusikia zaidi walichokuwa wakikiongea.
"Anaitwa Razack, yeye tarehe yake ni kesho tarehe 24, kama sisi tu...hahahah "
maneno ya mwanaume mmoja kati ya wale wawili, niliyasikia vyema na hapa ndipo nilipopata uhakika kwamba walikuwa wananizungumzia mimi.
macho yalinitoka niliacha kuzuga badala yake niliwakodolea macho kwa sekunde chache.
walikuwa ni vijana tu kama mimi kiumri, kanzu nyeusi ndefu zilizofunika mpaka nyayo zao na kofia nyeupe kichwani kisha wakapiga na makoti meusi yaliyowapa unadhifu , na wote walikuwa wamevalia sare sare.
baada ya kuwakodolea macho kwa sekunde chache, walinistukia.
"kasikia..anatusikiliza..."
alisema mmoja kisha yule mwingine akamuitikia.
"atafanya nini sasa.."
kisha kimya kizito kikafatia, hawakusema neno tena badala yake walinikodolea macho.
niliwaangalia kwa sekunde kadhaa lakini utulivu wa mwili na roho ulinitoka nilijikuta napiga hatua kuelekea upande walipo na kichwani nikiwa na wazo la kuwahoji mpaka wanieleze wamenijuaje na walikuwa wanaongea nini kuhusu mimi, wanajua kilichonipeleka Tanga..?, waniambie.
lakini hata hivyo nilipopiga hatua tano tu nao taratibu walianza kuondoka eneo lile , nilikaza miguu hatua ndefu ndefu nilizipiga, nao wakafanya hivyo hivyo hatua ndefu walizipiga.
nilipiga tena hatua tano zingine kubwa nao walitembea kwa kasi ile ile, hapo niliona wananichezea na kama nisipokaza miguu sitowapata, niliacha kutembea badala yake nikaanza kukimbia lakini hata hivyo nao hawakutembea tena, walianza kukimbia , lakini kamwe hawakugeuza shingo zao nyuma.
wao walikuwa mbele mimi nilikuwa nyuma, begi langu kubwa ambalo lilikuwa na nguo zangu pamoja na mali zangu zingine nililiterekeza pale chini na wala sikulikumbuka tena.
Itaendelea...
Kwa mwendelezo Wasiliana Na MWANDISHI
Queen Lizzie
Simu Namba 0683944333
Tags
simulizi