SAFARI YA TANGA ILIYOGEUKA KUWA YA KUZIMU
_______________________________________
SEHEMU YA NNE
Safari ilikuwa ndefu yenye kuchosha ukizingatia ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kusafiri umbali mrefu kama ule lakini kwa neema za mungu pamoja na ustadi wa dereva , tulifanikiwa kufika kituo kikuu cha mabasi cha korogwe ambapo hapo ndipo palipokuwa mwisho wa safari yetu hasa mimi ambaye sikuambiwa hata ninapoelekea zaidi ya kupewa amri tu na mkuu wangu wa kazi kuwa nielekee Tanga, japokuwa hakunipa taarifa nyingi za kutosha zaidi ya kuniambia nielekee Tanga na itakapofika tarehe 24 niwe ndani ya Tanga, lakini kwangu wala sikuona shida wala noma, sababu mbali kupewa amri nije Tanga pia nilikuwa na ndoto siku moja nifike jiji hili ambalo linasifika kwa wasichana wazuri, pia mfukoni nilikuwa na pesa ya maana hivyo wala sikuwa na wasiwasi wala hofu.
*******
gari ilitia nanga hapo mimi pamoja na abiria wachache tulitakiwa tuanze kushuka ,lakini hata pale watu walipoanza kushuka mimi wala sikujiharakisha kushuka badala yake nilibaki nimetulia nikimtegea mrembo yule aanze kushuka ili nimfate kwa nyuma lakini naye alionesha kutokuwa na haraka yoyote ile alikaa kwenye kiti 'hearphone' zake bado zikiwa masikioni. nilikuwa nikimtizama mno na mara chache tuligongana uso kwa uso, alitabasamu na kuangalia pembeni kwa aibu hii ilinifanya nizidi kuchanganyikiwa mbichwa ukazidi kuota mapembe, nikajikuta mwamba kwa sana.
wakati nimekaa namtazama yule mrembo mara ghafla nilistuka napigwa mgongoni, nilistuka lakini nilipokaa sawa niligundua alikuwa ni yule mzee ambaye alikuwa jirani yangu pale pembeni.kumbe naye alikuwa bado hajashuka
"vipi bwana...mbona waduwaa na wenzie washuka.."
"Aah...na..na..na.."
kigugumizi cha ghafla kilichotokana na ukosefu wa majibu kilinikaba na nikashindwa kutoa neno hata moja lakini hata hivyo yule mzee aliniwahi.
"aaah bhana...ndio ushaingia Tanga..kuwa makini, yale niliyokwambia yaweke kichwani..sawa.."
"sawa mzee..."
"Haya karibu Tanga..,"
yule mzee alisima kisha akasimama na kuanza kushuka , nilimuangalia kwa dakika kadhaa kisha nikaachana naye na kuyarudisha macho yangu mahali ambapo yule mrembo alipokuwa lakini daah!, nilistuka baada ya kupaona peupe pee, siti ilikuwa tupu na yeye mwenyewe alikuwa tayari kashashuka kwa dakika kadhaa nilijikuta namlaani yule mzee na kumshushia matusi ya kila aina kimoyomoyo lakini kwani pamoja na tamaa zangu pia nilikuwa na nidhamu ya uoga, nidhamu ambayo ilinifanya niongope kama nina heshima ili nijiepusha na madhira ya dunia, nilitembeza macho ndani ya gari zima lakini kamwe sikumuona tena mrembo yule hapo niligeuza macho yangu nje ndipo nilipofanikiwa kumuona kwa mbali mkononi akiwa na begi lake akiongea na moja wa madereva wa tax ambao walikuwa maeneo yale , nilimtizama kwa sekunde chache kisha haraka niliinuka na kuanza kukazana hovyo kiasi cha kumpita mpaka yule mzee ambaye aliinuka kabla yangu na pia niliwapiga vikumbo abiria kadhaa ambao nao walikuwa wakishuka kwa muda ule, nilifika mpaka mlangoni lakini kabla ya kukanyaga ngazi za kushukia nilikumbuka kwamba nimesahau begi langu la ambalo lilikuwa na nguo zangu simu laptop pamoja na nyaraka chache za kazini . haraka niligeuza safari na nikajikuta narudi tena ndani ya gari kwa mara nyingine tena niliwachapa vipushi vya maana abiria ambao nao walikuwa wanashuka tena safari hii mpaka yule mzee aliyekuwa akinipa ushauri naye alikula kikumbo, aliyumba kwa sekunde chache na alipokaa sawa maneno makali yaliyojaa hasira yalimtoka lakini aliponitazama vyema na kugundua kuwa ni mimi jirani yake ambaye tulikaa siti moja toka tukiwa Dar es salaam, hasira zilimpungua aliishia kunitazama tu lakini mimi wala sikuwa na muda naye, haraka niliokota begi langu kisha nikaanza kushuka tena
"upo sawa bwana..."
yule mzee aliniuliza akiwa amesimama akinitizama.
"eeeh babu..."
nilimjibu juu juu na wala sikuwa na muda wa majadiliano.
nikiwa na begi langu mkononi macho yamenitoka nilitazama upande ule ambayo yule mremb alikuwa amesimama lakini hata hivyo sikumuona tena pia hata yule dereva wa Tax ambaye alikuwa akiongea naye sikumuona ilikuwa ni dhahiri kwamba mrembo alikuwa tayari kashaondoka, kwa mara nyingine tena nilijikuta namkosa, hasira zilinipanda nilitamani nilitupe lile begi chini kwani kama lisingekuwa begi basi nisingemkosa mrembo yule lakini nilipokumbuka kwamba vilivyo ndani ya begi lile ndivyo vilivyokuwa vikiendesha maisha yangu na wala si yule mrembo, hapo hasira zilipungua kwa sekunde chache nilijiona mzembe ,mpuuzi, mshamba wa wanawake ambaye yupo tayari kuharibu kazi yake kwa ajili ya wanawake lakini nilipoikumbuka sura ya yule mrembo pamoja na tabasamu lake mwanana ambaye liliusugua moyo wangu nilijikuta najilaumu tena kwa mara nyingine tena ,
"kwanini sasa nimeruhusu kumpoteza kirahisi hivi, nitamuona wapi tena...aaah"
nilijisemea moyoni lakini nilipokosa cha kufanya nilikubali yaishe.
kinyonge nililitia begi langu mgongoni, kisha nikatambuka upande wa pili huko nilidakwa na bodaboda ambaye nilimuelekeza anipeleke hotel yoyote ile ambayo itanifanya niupumzishe mwili wangu vyema huku nikiisubiria hiyo tarehe 24 inikute, kama vile ambavyo nilielekezwa na bosi.
Itaendelea....
Tags
simulizi