SARAFINA 5
Baada ya sarafina kuanguka waliingia wanaume wawili wakiwa wameziba uso.mama sarafina alisimama huku akiwa anatetemeka.
" Nyie ni wakina Nani
" Sio muhimu Sana kutujua Ila utakuwa unajua Nini kimetuleta hapa type mzigo haraka kabla hatujamwaga damu hapa.
" Hakuna mzigo hapa .... Alidakia sarafina kabla hajamaliza alizibwa mdomo na mwanaume mmoja
" Nyamaza wewe Tena mkileta ubishi wewe ndio utakuwa wakwanza kufa. Wewe mama utatupa documents au tummalize mwanao.
" Hapana msifanye hivyo nitawapa muacheni mwanangu.
" Haya tupe documents. Mama sarafina alitoa na kuwapa alizochukua na kukuangalia Kisha wakaondoka mama sarafina alimkumbatia mwanae wakawa wanalia.
" Amakweli wa moja havai mbili kile tulichotegemea kimeshapotea.
" Siwezi kukubali mama nitahakikisha nalipiza Roman utajuta kutufanyia hivi sitakuacha.
Baada ya siku mbili kupita mama sarafina aliondoka na kuelekea kijijini huku wakiwa wamekubaliana sarafina abaki kwaajili ya kutafuta kazi. Sarafina aliondoka pale wanapoishi na kwenda kukaa kwa mama yake mdogo
Maisha ya kwa mama yake mdogo yalikuwa magumu wakati mwingine alilala na njaa Nice na somoe watoto wa mama yake mdogo kila siku jioni waliondoka na kurudi usiku wa manage wakati mwingine walilala hukohuko na kurudi asubuhi waliporudi wakirudi na vyakula kipindi cha mwanzo walikuwa wanampa lakini alipozoea walimnyima
Siku moja usiku mida ya saa Saba somoe na Nice wakirudi wakiwa na chipsi kuku walifika chumbani na kuanza kula wakati huo sarafina alikuwa akijigeuza hakupata usingizi kutokana na njaa aliamua kunyanyuka akaenda kunawa alipopeleka mkono kwenye chakula somoe akamshika mkono
" Wewe hebu kuheshimu hata kidogo unajua in nimezipataje hizi alafu umezoea kila siku kuletewa Kama kinda la ndege Sasa Leo Ni mwisho ukiona tunakula kaa mbali.
" Somoe naomba nigaie hata kidogo njaa inaniuma.
" Wewe hebu achana na Mimi. Somoe alinyanyua chips zake na kimgeukia sehemu nyingine sarafina alimuangalia Nice kwa huruma
" Utaishia kumuangalia kwa huruma sikupi labda uombe Mungu nishibe ndio utakula. Walikula waliposhiba ndio wakamuachia amalizie kwakuwa sarafina alikuwa na njaa hakuvunga alikula Kisha akapanda kitandani kulala kulipokucha alitoka kwenda kutafuta kazi akizunguka kutwa nzima bila mafanikio aliporudi nyumbani akakuta wamesha kulaakamuuliza mama yake mdogo
" Mama mdogo nja inaniuma mmeniwekea chakula
" Mmh hivi wewe ubongo wako umelala huwa hufikilii Mimi hicho chakula nakitoa wapi Kil siku nakwambia fuatana na wenzako mkatafute hela unajifanya huna unalolielewa kazi kujifungia ndani Kama utumbo kwanza sitaki kabisa kuulizwa habari sijui ya sabuni Mara mafuta imeshakuwa mkubwa jitafutie.
Hali ilizidi kuwa ngumu kwa sarafina aliamuo kuwaomba wakina nice waende wote huko wanakoendaga Nice na somoe wakicheka Kisha wakagonga
" Mambo si hayo Somoe hebu mpe nguo za kazi . Somoe alitoa sketi fupi na kiblauzi kinachoacha kitovu wazi na kumpa sarafina
" Jaribisha hizi Kama zitakutosha .
Sarafina alijaribisha
" Sasa mbona Kama nipo uchi .
" Acha ushamba hizo ndio nguo za kazi Habu vua vaa nguo zako hizi utaenda kuvaa mbele ya safari .
Waliondoka walipofika huko walienda kwenye chumba kimoja wakakuta wadada wengi nice na somoe waliwachangamkia
" vipi huyu Ni Nani
" Hii ni Mali mpya amekuja kuanza kazi leo
" Mbona Sasa anajikunyata ataweza kazi kweli?
" Ataweza si unajua mwanzo mgumu. Somoe pamoja na wasichana wengine walibadilisha nguo na kuvaa nguo za ajabu Wala hawakuona aibu ndio kwanza walisifiana wamependeza
" Acha kushangaa badilisha nguo alafu uende ukajipambe uwe na muonekano mzuri na tukifika huko unatakiwa kujichetua usikae kizembe. Sarafina alivaa zile nguo lakini zilimnyima Uhuru kwani hakuzoea kuvaa nguo fupi na zakumuacha wazi mwili wake alianza kuivuta Ile sket iliyokuwa juu ya magoti na kuacha mapaja yakiwa wazi
" Hebu acha kupoteza muda unajishukashika Nini hebu njoo nikupodoe. Somoe alimwambia huku alimvuta akae kwenye kiti alianza kumpodoa alipomaliza walitoka kwenda kutafuta wateja sarafina alijikunyata huku alishangaa wenzake wanavyo changamkia wateja somoe alipata mteja na kuondoka . Alifika Kaka mmoja na kuanza kuangalia atskaemfaa kwa usiku huo alipofika kwa sarafina alisimama na kumuangalia Kisha akamwambia
" Twende zetu. Sarafina alirudi nyuma nice alimuangalia Kisha akamfuata
" Wewe unafanya Nini Sasa hebu changamka
" Hebu niache bwana siendi popote.
" Has Sasa umekuja kufanyanini hapa hebu twende huko. Aliongea yule Kaka huku alimvuta mkono
" Niache kwani lazima .
" Unajua unazingua sarafina Kama ulikuwa hutaki ulikuja kufanya Nini.
" Mimi siwezi hii biashara. Nice alifyonza Kisha akamgeukia yule Kaka
" Achana na nae hataimi nakufaa twende zetu basi. Aliongea nice huku akizunguka huku yule Kaka akimuangalia
" Sio mbaya twende . Walishikana mikono na kuondoka sarafina alisogea pembeni akakaa huku akiwa kajiinamia alipita Dada mmoja ambae walikuwa nae mwanzo Ila alipata mteja na kuondoka nae alimuangalia sarafina Kisha akamsogelea
" Oya vipi? Sarafina alinyanyua kichwa na kumuangalia.
" Wewe ni mgeni ? Sarafina aliitikia kwa kichwa
" Sasa huoni hatari kubaki hapa peke yako unaweza ukafanyiwa kitu kibaya. Sarafina alimuangalia bila kumjibu
" Hebu nifuate. Sarafina alinyanyuka akamfuata yule dada bila kujua wakaelekea wapi.....
Kwa mwendelezo Wasiliana Na MWANDISHI
Queen Lizzie
0683944333
Tags
simulizi