SIMULIZI_____JICHO LANGU
SEHEMU____ 01
“Tamara nambie kitu cha uzuri hivi mpaka lini utakuwa singo dada?! Hivi hukutani na changamoto za wanaume wa kijiji hiki?” Alinihoji Esha rafiki yangu kipenzi niliyesoma naye shule moja katika shule ya Msingi na Secondary Kitumba. Wakati huo mie nilikuwa natoka zangu nyumbani kwenda gengeni kwa mama kumsaidia kuuza mboga mboga.
“Mhu, Esha na hali ilivyo sasa unambie nikimbilie kuolewa? Hivi huigi mifano ya watu walioshindwa ukapata jibu la swali hili? Hapana, kwangu mimi hapana, kwa sasa acha niwe singo hivi hivi miaka 23 nikimbilie ndoa ya nini?” Nilimjibu Esha, Esha akacheka kisha akatua ndoo chini nakuinua uso kunitazama kisha akasema.
“Nakwambia umesema hivyo umenikumbusha tukio la Pili, Pili sialijifanya Mzuri, nikwambie katiwa mimba halafu katelekezwa yupo nyumbani kwao na tumbo hilo!” Alisema Esha huku akipiga mikono yake. Taarifa ile ilinishitua sana, kwani nilimjua vizuri Pili ni msichana mwenye maringo tele kiasi cha kupachikwa jina la (maringo tele), na mara kadhaa alikaririwa akisema hawezi kuzaa na maskini aliamini katika uzuri wake anaweza kuolewa na mwanaume mwenye pesa, hapo nikamakinika haraka nikamuuliza Esha.
“Wewe!! Yupo kwao?” Nilihoji kana kwamba sijasikia vema alichokisema.
“Mbona siku nyingi, kwani we’ huna hizi habari?!”
“Hata sina, miye niko bize muda wote unafikiri nina-time ya kufatilia mtu?!”
“Ndiyo hivyo aibu tupu, kakongoroka huyo, na lile tako lake lote kwisha aahahaaa haa!”
“Usicheke hivyo sasa! Mhu, nani kamtia hiyo mimba?”
“Nanilii yule, naniii.. John!”
“John? John huyu msukuma torori?”
“Ndo’ ushangae mwenzangu!”
“Agh, basi naona kuna dalili ya mvua hapa, hebu acha nimuwahishie mama hizi mboga nisije mkuta amevimba huko.” Nilisema na huku nikijitwisha dishi langu la mboga!
“Aahhh! Na kweli ila ndio hivyo nikipata wasaa baadaye nitakuja home tuongee poa?”
“Poa!” Nilimjibu kifupi kutorefusha mada, kwani Esha mbali na urembo wake, alikuwa na changamoto ya ulimi wa upanda, kifupi ni mnoko mno, tuliagana kila mmoja akashika njia yake yeye akipeleka maji kwao nami nikishika njia kuelekea gengeni!
“Eti kuolewa, kuolewa gani huko?! Siwezi kuolewa ilhali sijaanzisha msingi wa maisha yangu, nataka nipambane kwa nguvu nihakikishe mama yangu anaishi maisha mazuri jambo la ndoa lifuate, siwezi kuolewa nikamuacha mama yangu anateseka na huku mvua ikinyesha jumba lageuka bahari hapana, ndoa nipishe kidogo!” Nilijiwazia huku nikitembea taratibu kulisogelea genge, japo hapakuwa mbali kihivyo lakini kwa mwendo wa kutembea kwa miguu palichukua takribani dakika 30 hivi njiani hapo ni mwendo wa haraka. Lakini nikiwa pembezoni kwa barabara moja la vumbi nyuma yangu nilianza kuhisi hali ya tofauti ila sikutaka kujiaminisha, niliamini huwenda ni miongoni mwa magari yapitayo lakini kadiri muda ulivyozidi kusonga gari lile lilizidi kunifuata hali ambayo ilianza kunitia hofu ukizingatia kumekuwa na kesi za watoto wengi wa kike kutekwa na kupelekwa kule kusiko julikana! Nilijikaza kiume ijapo mie ni mwanamke nakutembea kwa tahadhari huku macho ya hofu nikiyageuza mara kwa mara nyuma! Piiiii piiiii piiii!! Honi nyingi mfululizo zikanifuata nakunichanganya mno, nilidhani hata huwenda nimejichanganya nakuingia njia ya vyombo vya moto lakini wapi ni fujo za gari hilo miye nilikuwa kando kabisa!
Nikageuka nakusonya niliamini dereva huyo ni mpumbavu tu, ndiyo ni mpumbavu kwani hakujua matumizi sahihi ya honi yake! Mbali na kutembea kwa wasiwasi lakini gari hilo lilikuwa kama kivuli changu, nikaona hata nikaanza kutembea kwa kasi, lakini sikufika mbali gari lile likafunga breki mbele yangu, halafu dereva wa hilo gari akashusha vioo nakutoa kichwa chake nje, nilishituka kidogo.
“Hallow madam samahani!” Ilitokeza sura ya mwanaume mmoja mzuri mno nadhifu , mwenye sura ya uchangamfu niligeuka nyuma kuhakikisha kama ni miye, akanicheka kuonesha ni miye japo nilikuwa na wasiwasi lakini nilijikuta napata ujasiri wa kusogea sijui siye wanawake tukoje?! Nikasogea nikidhani huwenda ni mteja wa mboga mboga” Nilijiuliza huku nikiukaribia mlango wa gari hilo!
“Mambo?!” Alinitolea salamu kwa uchangamfu na huku akifungua tabasamu jepesi usoni mwake, kwa aibu na haraka nikamdakia.
“Poa!” Nilimjibu kifupi tu.
“Agh, samahani dada miye ni mgeni maeneo haya, nimeelekezwa kwa Mzee Gadafi lakini nahisi nimepotea sijajua napita kwa uelekeo gani maana aliyenielekeza alinambia nikifika karibu na soko sijui nikunje kushoto sijui nini sasa sijalipata hata hilo soko!” Alieleza kijana huyo, nilitamani kucheka kwa namna ambavyo alionekana kuchoka lakini nilijizuia na kisha nikamjibu.
“Anhaaa!!! Kwa Mzee Gadafi??” Nilihoji kwa mtindo wa dharau kwani hilo jina alikosea, naye akadakia.
“Yeah! Yeah! Unamjua?”
“Hamna! Ndiyo namjua, lakini anaitwa Kadafi siyo Gadafi!”
“Eeh! Ni huyo huyo, sasa ni wapi eti?”
“Umeona hii kona hapo? Unakunja hivi, unanyooka kwa mbele yake kuna bango la bar limeandikwa Eden Park panda na hiyo njia juu yake kuna kituo kidogo cha boda boda ulizia hapo hakuna asiyemjua!” Nilimjibu.
“Nashukuru sasa dada hapa nimepata mwangaza kupitia wewe!”
“Hata usijali!” Nilimjibu kisha nikarudi nyuma nakuanza kutembea lakini gari ile ilinifuata nakusimama tena!
“Samahani kama hutojali wewe unaelekea wapi?”
“Nafika hapo sokoni mara moja.”
“Njia sinimoja?! Njoo nikupe lifti.”
“Hapana, nashukuru mie nishafika!”
“No, noooo.. Usiogope we njoo!” Alisisitiza kijana huyo, nilijishauri mara mbili mbili kichwani mwangu nipande ama nisipande, huku nikitazama njia ya kulifikia soko, hapakuwa mbali kutoka hapo tuliposimama pembezoni kidogo mwa barabara.
“Hey dada!” Alinistua.
“Nafikiri kaka miye nimefika we nenda!”
“Hapana bhana sio ungwana kukuacha katika hali hii na ilhali umenisaidia, hebu panda bhana usiogope!” Alisisitiza sana kijana huyo, nikaangaza huku na huku kidogo nilishituka mara baada ya kumuona mama Wambura akija kwa njia hiyo haraka mno nilishusha beseni langu nakuingia ndani ya gari hilo pasi na hodi.
“Mungu wangu! Huyu mama anakwenda kumdai mama! Oh, oh, samahani kaka unaweza niwahisha haraka?” Nilijikuta nikipayuka.
“Usijali!” Alijibu, na hapo akakoa gia na kuondoka huku macho yangu yakisalia nyuma kumtazama mama Wambura mama mshari katika kudai madeni yake.
“Na leo mama atakuwa amepata hiyo hela yake kweli?!” Bado mawazo mengi yalinifuata kichwani mwangu. Kidogo hivi nikashitukia swali.
“Unapenda mziki?” Aliniuliza.
“Hapana!” Kifupi nikamjibu.
“Kwaya Je?”
“Hapana!”
“Singeli nazo?”
“Eh, kaka!”
“Usijali, Je kaswida?”
“Samahani kaka unajua naweza kuruka nje?! Sitaki maswali mengi!” Nilimjibu kwa ukali kitendo kilichopelekea apunguze mwendo kisha mkono wake wa kushoto ukapandisha juu kulipokuwa na kioo kidogo akakielekezea kwangu kisha akasema.
“Naitwa Stanley, sijui we nani mwenzangu?!”
“Naitwa Pili!” Nilimuongopea makusudi kwani sikutaka alijue jina langu.
“Ooh, Pili! Nice name.” Alijibu.
“Ahsante!”
“Kisesa ndo nyumbani?”
“Ndiyo!”
“Umeo..” Kabla hajauliza suali hilo nilimkatisha.
“Ni hapo tumefika nishushe!” Nilisema haraka huku nikichungulia dirishani pale sehemu alipo mama, alikuwa amezingirwa na wateja na mezani pake hapakuwa na baadhi ya mboga mboga. Nilishuka haraka nakutaka kukimbia lakini nilikumbuka sijatoa fadhila kwa kumshukuru kwa kuniokolea muda nikarudi nakusimama dirishani kisha nikasema.
“Kaka ahsante, umeiona hiyo njia hapo ndiyo ifuate moja kwa moja halafu ukunje hivi kama nilivyokueleza utampata huyo mzee unayemtafuta.”
“Njoja kwanza huyo hapo ni mama yako?”
“Ndiyo.”
“Sawa, sasa shika hivi!” Alisema kisha akafungua kitu fulani kwenye gari lake nakutoa kibasha fulani nakunipatia nilipotaka kukifungua alinizuia nakusema.
“Hiyo ni zawadi utampa mama na wewe yako ni hii hapa!” Alisema nakunipatia bahasha nyengine.
“Utaifungulia nyumbani!” Alisema kisha akawasha Endicator nakugeuza gari, niliangalia gari hilo plate namba zake na rangi nikaliweka moyoni kisha nikakimbia haraka hadi pale mama alipo.
“Umechelewa Tamara ulikuwa unafanya nini muda wote hadi wateja wamesambaa?! Huu ujinga utaacha lini mwanangu, badala uchangamke unakuwa unajivuta vuta sasa tizama hela ngapi zimenipita hapa. Umenikera basi tu, sasa haya mamboga unaleta saa saba hii nimuuzie nani?” Mama alinipokea kwa sauti ya ukali, nilijihisi vibaya kwani watu wengi walinigeukia mimi nakunitazama hususani wauza samaki na vile wanajua kunena kwa kashfa nilijihisi vibaya nakuvunga kama siwaoni.
“Nisamehe mama, kwa wakati mwengine nitafanya bora zaidi ya leo, jamani wateja msife moyo wacha tukate haraka haraka eti eeh?!” Niliongea na kujaribu kuwatuliza wale wateja waliomzunguka mama pale, lakini kidogo likanirudi wazo la mama Wambura nikamsogelea mama nakumng'ata sikio! Mama alishituka mno kusikia taarifa hiyo.
“We niachie mimi hapa niwatengenezee chapchap tufunge, we nenda ukajifiche siunamjua huyo mama kwa kelele?! Nenda mama mie nitasimama hapa!” Nilimwambia mama, haraka mno mama alitoka nakuniachia, hakuzipita dakika mama Wambura alitia nanga kabla hata hajafika alishaanza kutia kelele..
“Yani nakwambia leo hapa hapatoshi, hapakaliki leo mmekuwa kila siku wakunizungusha pesa zangu, nikija mnanikimbia, nasemajeee leo mtazitapika mlipokuja kukopa mlitegemea mtalipa kwa nini?! Nataka hela zangu!” Maneno ya mama Wambura yaliwavuta watu nakuwasogeza karibu kusikiliza umbea wabongo bhana! Nilimgoja hadi akafika kwenye kichanja chetu!
“Shikamoo Anti!”
“Shikamoo nyoko! Nataka hela yangu sina shida na salamu yako!” Alijibu kwa dharau huku akibana pua yake.
“Najua umamdai, mama hela nyingi lakini bado hajapata biashara mbaya Anti Mama Wambura!”
“Mi usiniambie habari ya biashara mbaya nataka hela yangu!” Alizidi kuwa mkali mama huyo.
“Tafadhali Anti!”
“Eh, Eh, Eh! Usiniite Anti, sina ukoo na nyie nataka mlipie pesa zangu nimechoka kusubiri kila siku mnanipanga mnanipanga, nimechoka alo mwambie mama yako aniletee hela yangu leo sitoki hapa!” Alijibu mama Wambura.
“Mama anakutafutia!”
“Ananitafutia nini? Siku zote hizo ananitafutia tu?, wewe, tena na wewe ufunge mdomo nitakuchenjia kibao sasa hivi, sitaki kusikia sauti yako kahaba wewe!” Alisema mama huyo neno baya lisomithilika, lilipita kama sindano moyoni mwangu hata hivyo sikutaka kuwa mkali kwa kuwa nilijua mie nimdaiwa nisimpandishie mori mama huyo, nililikumbatia rohoni nakusema.
“Sawa Anti mie nakubali yote lakini vumilia hizi siku mbili tatu mama akipata hela atakuletea!”
“Sitoki, mniulie hapa nasema hivi hela zangu leo mtatoa!”Alijibu mama huyo, sikuwa na lingine la ziada nilibaki kumwangalia mama huyo nisijue nini nifanye, dakika kadha wa kadha zilipita mama huyo akitukana na kuongea maneno ya kebehi mengine yaliushinda uvumilivu, Nilishindwa kabisa kuyavumilia.
“Upumbavu huu, najuta hata kwanini niliyapa hela zangu majitu ya namna hii wewe, we binti naomba uuze k*m umsaidie mama yako kulipa hela yangu, bila hivyo mtaniona mbaya!” Alinyanuka yule mama nakusema neno chafu kupitiliza.
“Nifanye nini??” Nilihoji kwa hasira huku nikimtazama kwa jicho kali la uchu!
“Hivyo hivyo ulivyosikia, kwa hivyo unataja ufanye nini? Unipige? Aya njoo unipige, we si malaya tu, nani asiyekujua unajifanya mweeemaa kumbe malaya tu nipige nikuoneshe malaya wewe! Nasema hivi nataka hela yangu.” Mama huyo alizidi kunichafua roho yangu, hasira kali zilinipamda hata mdomo kuanza kutetemeka nilinyanyua mkono nimpige ila kabla kofi halijamfikia nilihisi nikidakwa mkono, haraka niligeuka kutazama, alikuwa ni mama. Huwenda yale maneno machafu aliyasikia vyema.
“Mama!”
“Muache mwanangu usije zalisha mengine!” Alinijibu mama kinyonge!
“Enhee!! Wewe ndiye niliyekuwa nakusubiri kwa hamu. Naomba hela yangu.” Aliongea mama Wambura mara baada ya kumuona mama na huku akitazama pembeni. Mama hakusema chochote alifungua tenge lake na kufunga fundo na kutoa kiasi chote cha pesa alichouza nakumpa huku akimuomba kwa sauti ya chini.
“Hii napunguza deni, ila naomba unipe siku mbili tatu nitaongezea nyingine!”
“Hela gani hii?? Uchafu mkubwa! Yani katika laki mbili na ushehe unipe elfu ishirini wewe mama wewe, unanitafuta ubaya eti?! Nipe hela yangu sitaki nenda rudi mshanichosha!”
“Lakini mama Wambura hicho ndiyo kiasi chote nilichouza tazama sina hata mtaji mkubwa wa kurudisha pesa zako tafadhali pokea hata hicho huku nikiendelea kukukusanyia, nasubiri wiki ijayo nipokee mchezo.” Mama alijitahidi kumueleza kwa upole lakini mama Wambura alikuwa katafuna mbegu ya Limau na Pilipili sura yake ilikuwa chungu mno kila neno hakutaka kulielewa kabisa.
“Hujanishawishi wewe mama, nataka pesa zangu full stop!”
”Mama niachie nilipige linatuabisha mama!”
“Mh, Mh, Tamara naomba kuwa mpole!”
“Nahesabu moja hadi kumi uwe umepata hiyo hela.. Mojaaaa.. Mbili.. Tatu..Nne..Tano..Sita..Saba..Bado uko hapa tu? Aya.. Nane.. Tisa.. Ku..” Kabla hajafunga hesabu ya namba kumi alishikwa mkono na mtu asiyemjua aligeuka haraka kumtizama hapo Tamara alipigwa na bumbuwazi mara baada ya kumuona!
“Unadai shilingapi mama?” Aliuliza kwa upole Stanley huku akimtazama Tamara!
“Nawadai hela zangu nyingi halafu kutwa yananizungusha tu!” Alijibu kwa kupayuka mama huyo.
“Ah, ah. Taratibu mama unawadai shilingi ngapi?” Alihoji Stanley.
“Laki mbili kama na arobaini hivi tulikubaliana na riba!” Alijibu.
“Okey!” Stanley alijibu na kupekua mfukoni mwake kisha akatoka bunda moja kubwa lililoshiba noti mpya mpya nakumuhesabia pesa yake na nyengine ya kupigia kelele akampa alafu akasema!
“Pesa siyo kila kitu mama, jaribu kujali utu wa mtu, huyu ni mwanamke mwenzako tena anakuzidi rika kwa uliyoyafanya sijapendezewa nayo kabisa! Bado unadai nyengine labda?”
“Hapana baba!”
“Haya ondoka na usiifuate tena familia hii!” Alisema Stanley, mama Wambura aligeuka kwa aibu nakumtazama mama Tamara kisha akasema.
“Mna Mungu! Nasema hivi mna Mungu leo ndio mngekubali shoo!” Alisema na kisha akaondoka!
Stanley alimsogelea Tamara na mamaye kabla hajasema lolote mama huyo alianguka chini nakumshukuru kijana huyo kwa ukarimu wake.
“Mwanangu sina chakukulipa mwanangu mie maisha yangu magumu mwanangu!” Alisema mama huyo.
“Usijali mama, wala miye sitarajii malipo yoyote kutoka kwako!” Alijibu Stanley na huku akimuinua mama huyo.
ITAENDELEA..
Tags
simulizi