TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

MADHARA YA KUAMINI KATIKA IMANI POTOFU

Madhara Ya Kuamini Katika Imani Potofu...
_______________________
Makala nilizofanikiwa kuzituma hapo awali zilidokeza kuhusu jinsi imani huwa haimsaliti muamini wake!
Kutokana na hilo msisitizo mkubwa ukawekwa kwa kumtaka kila muamini aamini kwenye imani thabiti! 
Kwa leo naenda kudokeza Madhara Ya Kuamini Katika Imani Potofu! 
Madhara hayo ni kama ifuatavyo:  
1. Utampoteza Mungu Katika Maisha Yako…
Mungu hapendi watu wenye imani ya kusitasita kwa maana hao hawawezi kujibiwa maombi yao.
Watu hawa hawana imani juu ya uweza wa Mungu, hii inamaanisha kwamba, hata wanapoomba wanatilia shaka kile waombacho kuwa hakitawezekana, na kweli hakitawezekana kwa sababu imani yao ipo kwenye kutokuwezekana...

Kutokana na hilo watajikuta wakishindwa kutambua uweza na nguvu za Mungu katika maisha yao, hali itakayowapelekea washindwe kumpa Mungu nafasi kwenye maisha yao!

Kwa kulitambua hilo ndiyo maana Yakobo 1:6 inasema; "Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku"...
Msisitizo umekwa kwenye kuomba kwa imani! 
Na ifahamike kwamba Mungu ni Muumba wa mbingu na nchi hivyo basi, kwake yeye kila jambo lawezekana...
Sasa basi inakuwaje unampoteza Mungu wa yawezekanayo kwa kuamini katika imani potofu?

Hebu tazama kile Neno la Mungu linasema katika, Mwanzo 1:26 “Mungu akasema na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi”

Mpendwa msomaji wewe ulishafanywa kuwa mtawala, na kikubwa zaidi umeumbwa kwa mfano wa Mungu! 
Sasa kwanini unampoteza huyo aliyekupa hayo mamlaka kwa kuamini katika imani potofu?

Unatakiwa kujua kwamba, Mungu wetu ni Mungu wa yawezekanayo kwamba akiahidi hutenda. 
Uthibitisho wa jambo hili upo kwenye, Isaya 55:11 Neno la Mungu linasema: “ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu: halitarudi bure, bali litatimiza mapenzi yangu nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyoyatuma”…
Sasa kama Mungu anasema neno lake litatimia inakuwaje unampoteza kwa kuamini katika imani potofu?

Mpenzi, unatakiwa kujua kwamba, ahadi za Mungu ni za milele na Kila ahadi mungu ambayo huiahidi huitekeleza na hili tunalipata katika:
Isaya 14:24 “Bwana wa majeshi ameapa, akisema, hakika yangu kama vile nilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea”
Hebu vuta picha Mungu mwenyewe anaapa! Halafu bado unaamini katika Imani potofu, je itakuwaje Mungu akuamini ikiwa wewe hujiamini na humuamini kama anaweza kubadili maisha yako?

My friend fanya yote lakini usimpoteze Mungu, kwani Mungu wetu ndiyo chanzo halisi, na yeye ndiyo anaujua mwanzo na mwisho wa kila mmoja wetu, hivyo ukimpoteza Mungu kupitia kuamini katika Imani potofu, utakuwa umepoteza chanzo chako na hatima yako.

Unatakiwa uwekeze msingi wako imara kwa Muumba Yaani Mungu Mwenyezi! 
Na, ndiyo maana hata wafilipi 4:13 Neno la Mungu linasema “nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”. 
Kumbe hutakiwi tu kuamini katika uweza wako pekee bali kuna yule akutiaye nguvu!
Sasa kama yule akutiaye nguvu unampoteza kwa kuamini katika imani potofu ni nani atakayekutia nguvu? Jaribu kufikiri tu...

Je bado unaamini katika Imani potofu ikiwa yupo Mungu mbinguni asikiaye maombi yetu?
Friend imetosha sasa, umeteseka vya kutosha kama ni kutumia fahamu zako zinazoamini katika upotoo, ukomo wake umefika sasa…

Hebu yakabidhi maisha yako kwa Mungu! Imetosha sasa kuamini katika imani potofu kunakoplelekea umpoteze Mungu ambaye ndiye chanzo chako halisi...

Jambo hili limedokezwa kwenye Mithali 3:5-6 “Mtumaini bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe katika njia zako mkiri yeye, naye atanyoosha mapito yako”.

Ndugu, huu siyo wakati wa kubaki gizani tena ni wakati wa kurudi nuruni. 
Rudi nuruni kwa Kuamini uweza wa Mungu pamoja na kuyakabidhi Maisha Yako kwake!

Luka 15:18 “Nitaondoka nitakwenda kwa baba yangu”…
Ndugu achana na Imani potofu halafu urudi nyumbani kwa baba yetu, kwani nyumbani kwa baba kumenoga…

2. Utaendelea Jubaki Na Hofu
Watu wanaoamini katika imani potofu daima huwa na hofu kubwa sana kuhusu maisha yao ya sasa hata yale yajayo!
Unatakiwa kujua kwamba, hofu huja pale ambapo mtu kifikra kaona mwisho mbaya wa jambo fulani na akaamini kuwa jambo hilo litakuja kutokea, hali ambayo humjengea hofu kubwa sana!

Mtu mwenye hofu huwa anahofia fikra zake na imani yake mwenyewe, kwani ni yeye mwenyewe ndiyo kahusika katika kutengeneza fikra hizo na akawekeza imani katika fikra hizo.
Ambapo mwisho wa siku atajikuta akihofia. Na ifahamike kwamba hofu siyo kitu halisi...

Friend, sahau kabisa kupata ujasiri na uthubutu kama utakuwa umeamini katika imani potofu, kwani hakuna imani potofu ambayo huzaa matunda mema!

Kwa mfano tufanye unaamini kwamba huwezi ukifanikiwa kifedha kwa sababu unatokea familia ya kimaskini.
Imani hiyo itakujengea hofu kiasi kwamba hata kama mtu atakuja kukupa maarifa, taarifa au namna ya kutengeneza pesa utajikuta unakosa ule uthubutu kwa sababu ndani yako unaamini wewe huwezi ukafanikiwa kifedha.

Wapo watu wengi ambao hukutana na fursa nzuri lakini kwa sababu ya kuwa na imani potofu juu yao na juu ya fursa hizo hujikuta wakishindwa kufanya maamuzi sahihi, ambapo mwisho wa siku watashindwa kuzifikia hatima bora za maisha yao.  

3. Utashindwa Kujijua Wewe Ni Nani
Huwezi ukajiona wewe ni mtu mkuu, ilihali umeweka imani potofu juu yako kwamba wewe ni mnyonge, dhaifu na fungu la kukosa! 
Sasa utauonaje ukuu wako ilihali umeamini kwamba wewe ni mnyonge, dhaifu na fungu la kukosa?
Unahitaji kufikiri juu ya swala hili!

Unatakiwa kujua kwamba watu wengi tumejitengeneza kuwa wajinga kwa kuwekeza kwenye imani potofu dhidi yetu, hali ambayo imepelekea wengi wetu tuzidi kuzunguka kwenye mduara wa ujinga.
Kwa mfano imani potofu imetufanya Wengi wetu tushindwe kujijua: mimi ni nani, ninamiliki nini ndani yangu, ninaweza nikafanya nini, nidhibiti nini katika maisha yangu na niishi kwa namna gani…
Hali hii inazidi kutudumaza, kwani ujinga ni giza na palipo na giza pana kifo, kwani giza huashiria kwamba hakuna Nuru!

Mpenzi msomaji ukiona umefika hatua ya kutokujijua wewe ni nani, maana yake utakuwa ni sawa na umeyapa maisha yako fursa ya kukufanya yanavyotaka, na yatakufanya kweli kwa kuwa ni wewe mwenyewe umeyapatia fursa yakufanye hivyo!…

Huu siyo wakati wa kuendelea kuamini katika imani potofu tena, bali ni wakati wa kusonga mbele, ni wakati wa kujiona unaweza, unastahili na uliumbwa uje uwe mtu mkuu na mtawala.

4. Hutoweza Kubadili Maisha Yako
Sasa utabadilishaje maisha yako ilihali umeamini wewe upo kwenye kundi la kukosa, unatokea kwenye familia ya kimaskini na umezaliwa katika nchi maskini?
Unatakiwa kujua kwamba kuamini katika umaskini huvuta umaskini, ilihali kuamini katika utajiri huvuta utajiri!

Jaribu tu kuwaza na kuwazua utapata wapi nguvu na hamasa za kubadili maisha yako wakati unaamini huwezi ukafanya hivyo?

Awali nilidokeza kwamba imani yako uliyoweka juu ya jambo Fulani haitaweza kukusaliti, kwamba utapokea kwa kadri ya uaminivyo!
Sasa kama umeamini huwezi kubadili maisha yako, utawezaje kuyabadili?
My friend kuamini katika imani potofu ni kujikatili nafsi na kujinyima raha, furaha pamoja na matumaini…
Kumbuka yule anayeamini anaweza ataweza na yule ambaye anaamini hawezi hataweza.
Na si kweli kwamba anaweza au hawezi bali imani yake ndiyo itamfanya aweze au asiweze.
Mpenzi huna budi kufutilia mbali imani potofu kwani itakufanya ubaki katika kiwango duni cha kuishi?

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya!

Somo Lihusulo Tatizo Siyo Kilichotokea Tatizo Ni Kile Unachokiamini Litaendelea Kwa Siku Ya Kesho!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no 0744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post