SIMULIZI______JICHO LANGU
SEHEMU_______. 02
ILIPOISHIA..
Stanley alimsogelea Tamara na mamaye, kabla hajasema lolote mama huyo alianguka chini nakumshukuru kijana huyo kwa ukarimu wake.
“Mwanangu sina chakukulipa mwanangu, mie maisha yangu magumu mwanangu!” Alisema mama huyo.
“Usijali mama, wala miye sitaraji malipo yoyote kutoka kwako!” Alijibu Stanley na huku akimuinua mama huyo.
ENDELEA..
Nilikuwa katika ukiza mnene uliofunika mboni zangu, sikujiona kama ni mtu niliyekamilika, kila nilipokuwa namtazama Stanley sikujua lengo lake nini kwangu. Sikujua hata ni kwanini aliamua kuingia katika gharama kubwa vile kulipa kiasi chote kile cha pesa, nilibaki nikimtazama bila kupata majibu ya maswali yangu. Yamkini nilikuwa timamu kwa akili nilihisi tu na kitu nilihisi kilikuwa kigumu mno kuamini, ila yote nilimshukuru Mungu kwa kunivua na kunisitiri na aibu za mama Wambura!
“Sawa mama, ila mie ni kama kijana wako huna haja yakushukuru sana mshukuru Mungu kwa kuniongoza kupita njia hii!” Alijibu Stanley huku akinitizama usoni, niliona aibu kumtizama nilijikuta nayatupa macho chini huku masikio yangu yakisimama wima kumuelekea!
Stanley aliingiza mkono wake mfukoni mwake nakuibuka na wallet kisha akatoa karatasi ndogo nakumpatia mama huku akiambatanisha na maneno yaliyonifanya niinue sura na kumuangalia.
“Namba yangu hii mama, utapopata shida usisite kunipigia!” Alitamka waziwazi kwa sauti ya juu kidogo, nilihisi mwanga wa faraja ukiwaka moyoni mwangu sehemu ambayo ilikosa nuru kwa muda, hakika Stanley ni kijana wa tofauti kabisa na wengine niliowahi kuwaona.
“Nashukuru sana mwanangu, umekuwa msaada wangu siku ya leo, hakika sina chakukulipa zaidi ya kukuombea dua kwa Mungu. Mungu akubariki, akufungulie kipato chako kwa hiki ulichotoa akuzidishie mara dufu!” Mama yangu alilia kwa furaha hakuamini kabisa kama siku moja anaweza kutokea mtu mwema kiasi hicho, hii ilikuwa hi kama ndoto ya alinacha hakuna siku tuliyotaraji kutokewa na mtu mwema, ama kwa hakika bahati ya mtu hailaliwi mlango wazi, siku hiyo ilikuwa siku njema ya furaha, genge lote lilitulia tuli na hata wengine kurejea kwenye maeneo yao ya kazi! Stanley alitufichia aibu.
“Uko salama Pili?” Alihoji, nilishituka kwa kunitaja jina la Pili kwani jina hilo nililikopa kwa rafiki yangu Pili wala halikuwa sahihi, nilitamani nimwambie ukweli lakini nilisita kwa muda huo kwani asingelinielewa vizuri ikanibidi nitulie tuli nisimweleze chochote!
“Ndiyo, mie niko poa!” Nilimjibu.
“Anha, nimefurahi kusikia hivyo, mama nimemuachia namba yangu ya simu mtaitumia kunitafuta mtapohitaji msaada wangu, nitakuwa nanyi karibu. Labda itakuwa unajiuliza mengi kuhusu mimi ila hata mimi sijui nini ila tuyaache hayo, nashukuru nimekufahamu Pili na kama nilivyotangulia kusema nitarudi hapa.” Alieleza Stanley kwa sauti ya chini mno sauti ambayo hakuna aliyeweza kusikia, nilijipatua nakufunga kitenge changu vizuri kisha nikamjibu!
“Nashukuru sana kaka, kwa dunia ya leo wachache sana kama wewe mwenye moyo wa kujitoa bila kujali malipo, hakika umeniachia deni kubwa la kulipa fadhila zako, nakushukuru sana kaka umemfanya mama yangu awe huru umemtoa kifungoni, tizama hata alivyokonda yote ni kwa ajili ya deni hili, nashukuru sana kaka!”
“Aagh, usiseme hivyo pesa kiduchu hizi ndiyo shukurani zote hizi? hapana inatosha pesa ni kidogo sana hizo.” Alijibu Stanley.
“Poa Pili mie naondoka ila usiache kufanya nilichokueleza poa?” Alisema nami nilimuitikia kwa kichwa kisha Stanley akaondoka nakutuacha pale huku ule umati mkubwa wa watu ukisambaa, nilimuendea mama nakumueleza mwanzo wa kukutana na kijana huyo mama alisema tu.
“Mungu amlipe kheri katutoa kwenye shari huyu kijana!” Alisema mama kisha tukafunga biashara kurudi nyumbani, haikuwa siku nzuri tena mama alichoka na ile aibu ndiyo usipime, hakutaka kuendelea kuuza kwa yale matusi kama mvua kutoka kwenye mdomo mchafu wa mama Wambura!
******
Tukiwa nyumbani yapata majira ya saa kumi na moja za jioni mimi na mama tukiwa nje ya nyumba yetu kando kidogo ya msingi wa nyumba hiyo, mama alikuwa akinisuka nywele za mkono huku tukipiga stori za hapa na pale!
“Moyoni mwako naona bado kuna jina la yule kijana wa mchana?” Aliniuliza kwa utani mama.
“ Ndiyo mama mtu kama yule kwanini jina lake lifutike haraka, tena nimekaa nimewaza sana inaonesha huyu kijana anapesa chafu, kwanini mama tusimtumie ili tutajirike?!”
“Tutajirike!”
“Ndiyo mama!”
“Unamaana gani kusema hivyo?” Alihoji.
“Katika kitu kinaniumiza kichwa ni haya maisha tunayoishi, nimesoma ndiyo, nimepata Division 2 ndiyo ila sina pakwenda, hela pia hakuna, kila unapogusa magumu wote wanasema hali ngumu, huu mwaka sasa umepita tangu matokeo yatoke nipo nyumbani sina pakushika, vibarua navyo vimekuwa vigumu, hii inatengeneza picha kwa watu ndiyo yanakuja yale maneno ya yule mama aduwalahu, sasa mama labda kama wazo langu litafanikiwa huwenda tukauaga umaskini!” Nilizungumza nakutia kituo kidogo, lakini ilionesha mama hakufurahi maneno yangu kwani alikuwa akinifunga butu nilihisi mkono wake ukitulia kichwani kwa muda kisha kikafuata cha kufuatia..
“Kwanza wazo gani hilo?” Alihoji mara baada ya kufikiri kwa muda nakuibuka na swali kwa kile nilichotangulia kukizungumza, lakini kabla sijamjibu alidakia kwa kuongeza swali.
“Uolewe naye?!” Alidakia, nilikurupuka mithili ya mtu aliyezinduliwa katika usingizi mzito kisha nikamgeukia nakujibu kwa mtindo wa swali.
“Kuolewa?? No, sijasema kuolea mama.” Nilimjibu.
“Sasa kufanyaje? Labda unieleze wewe.”
“Nimewaza kwa muda mama, nikapata jibu kuwa niongee naye anipatie walau kibarua chochote kitachoniingizia pesa, hiyo pesa itayopatikana mama tuiweke katika mradi kama ni nyingi tufungue genge kubwa siyo kutwa unauza elfu5 hapo bado hujala hivi haya maisha tutaishi hadi lini mama? Hilo ndilo wazo langu anitafutie kibarua huko mjini nifanye kazi lengo langu mama wewe uishi vizuri na tuuage umaskini, tizama kijumba chetu ndiyo kinatia huruma mtaa huu mzima kwanini tusidharaulike mama? Hapana, mie najitoa muhanga kumuomba kibarua akinipa haya akinyima pia haya nitaridhia!” Nilimweleza mama, mama alitingisha kichwa akionesha maneno yangu yamemwingia lakini alitia pingamizi.
“Inaweza ikatokea akakubali lakini siunajua mabalaa ya huko mjini yalivyo mwanangu, sikatai wewe kwenda na tena hili umetoa wazo la kiutu uzima kabisa ila shida ni huko mjini tu ndiyo nakuwazia!”
“Ondoa shaka mama, umezaa mtoto jembe, hili nafanya kwa malengo kuja kuwakata watu ngebe mama! Mimi ndiyo mtoto wa pekee niliyesalia, kaka zangu umesema hujui walipotokomea kwanini nisijitoe nikabeba nafasi zao?! Kikubwa dua mama, wewe ndiyo jicho langu niombee dua, nifanikiwe hakika hutojuta kumzaa Tamara!”
“Eti eeh?!” Akatabasamu mama.
“Ndiyo,”
“Basi fanya upesi kamuazime simu mama Dani uje umpigie!” Alisema mama huku akinikabidhi kile kikaratasi cha namba ya simu, bila kujali sijakamilisha kusuka niliingia ndani nakujifunga kitambaa kisha nikatoka haraka na kwenda nyumba jirani kwa mama Dani kumuazima simu yake kwani mama yangu hakuwa na simu, nashukuru Mungu mama huyo ni muelewa tena hakuwa na bughudha kabisa alinipatia simu yake huku akinisisitiza nisimmalizie salio, taratibu nilinakili namba kwenye simu hiyo na kisha kuzipigia, simu iliita na hatimaye kukata bila kupokelewa, haikunivunja moyo nilirejea tena kupiga!
“Vipi amepokea!” Mama alihoji aliponiona nahangika kupiga bila mafanikio.
“Hapana hajapokea huwenda labda atakuwa bize!” Nilijibu huku nikipandisha sikioni simu kusikilizia tena.
“Eh! Kama yupo bize achana naye usimsumbue!”
“Hamna ngoja nijaribu ya..” Kabla sijamalizia kusema kwa kuwa muda huo simu tayari ilikuwa sikioni nilisikia sauti upande wa pili ikijibu.
“Hellow!” Moyo ulishuka pwaah mara baada ya kusikia sauti hiyo.
“Hellow!” Ilirejea tena.
“Siuongee!!” Mama aliposikia sauti hiyo alinizindua kunitoa katika ukimya, nilikuwa nimepigwa na bunbuwazi la ghafla nisijue nini nijibu.
“Halloow!!”
“Eeh, kaka?!”
“Naam, nani wenzangu?”
“Unaongea na Tamara!”
“Tamara? Tamara gani?”
“Tamara huyu binti uliyemsadia na mama yake hapa sokoni. Nanilii Pili!” Nilikumbuka hanitambui kwa jina Tamara haraka mno nilimbadilishia kibao nakumtambulisha kama Pili, ilisikika sauti akicheka tu kisha akasema.
“Hahahaa.. Umenifurahisha sana yani hata jina lako unasahau?”
“Hapana, siunajua tena kaka yangu!”
“Nakuelewa, leta habari mzima wewe?”
“Mie mzima sijui wewe?!”
“Me niko poa.”
“Sasa kaka!”
“Naam! Nakusikiliza,”
“Nilikuwa nashida fulani naomba unisaidie kama hutojali.” Japo kwa hofu nilijikakamua nakusema kisha nikangoja jibu lake kwa hamu na ghamu.
“Mh, nieleze!” Alisema.
Nilivuta pumzi nakuikumbatia kisha nikaitoa kidogo halafu kisha nikaseme.
“Mie nashida, nataka walau nipate ajira kaka yangu.” Nilijibu.
“Hilo tu?” Alihoji.
“Ndiyo kaka.”
“Ajira gani unataka?”
“Mimi yoyote, yoyote ile kaka yangu, yani hata kama ni ya house girl sawa tu kaka sichagui sibagui!”
“Mmmmh, habari mbaya, ajira umekosa!” Alinijibu kisha akatulia kimya.
“Nimekosa?? Jamani kaka hamna hata kazi yoyote tu huko? Tafadhali kaka hebu niangalizie nakuomba!”
“Umekosaaaa!” Alirejea tena kauli hiyo, kauli hiyo ilikuwa kauli chungu moyoni mwangu kwani moyo ulijikuta ukijikunyata nakujifinya, nilihisi nikikata tamaa hata ile ndoto niliyokuwa nikiiota niliona ikizimika, nilimtamaza mama nakumtingishia kichwa kuashiria mpango umedunda, lakini ghafla katikati ya ukimya iliibuka sauti kicheko kidogo halafu ikafuata sauti ya Stanley ambayo kidogo iliibua tumaini jipya ambalo lilikwisha anza toweka.
“Nilikuwa nakutania tu Pili, hapa kwangu nilikuwa nahitaji mtu wakunisaidia kazi nafikiri hata hii itakufaa sawa, umepata wala usiwaze, utakuwa tayari muda gani?” Alihoji nilimtazama mama machoni kisha nikajibu.
“Hata leo miye niko tayari..” Nilimjibu..
ITAENDELEAA... Utamu wa ngoma ingia ucheze utamu wa simulizi hii isome mwenyewe usikubali kupitwa, hakika palipo na moshi hapakosi moto, unataka kumjua Tamara?? Fuatana nami katika kigongo hiki cha kusisimua, maisha ya Tamara yanataka kuhamia mjini, je atafanikiwa kile alichokipanga au mjini kutakuwa kutamu zaidi, JICHO LANGU tukutane sehemu ya tatu!
Tags
simulizi