TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

JICHO LANGU 04

SIMULIZI_______JICHO LANGU
SEHEMU________.       04
ILIPOISHIA..

“Aya nashukuru, sasa naomba ukale, tulipokuwa pale nilisikia miungurumo ya tumbo nikajua tumbo halina kitu hivyo naomba ule ushibe sawa?” Alimaliza nami nikamjibu kwa kichwa kama kawaida yangu, naye akatoka akaniacha nikielekea pale mezani palipopambwa na kila aina ya chakula.

ENDELEA NAYO....... 

Nilianza taratibu kula nyama za kuku zilizochomwa kwa ufundi mkubwa huku nikisafirisha na pilau tumboni, nilikula tani yangu hadi pale nilipohisi tumbo limefikia levo yake, nikashushia na sharubati kisha nikatoa vyombo lakini kabla sijainuka kutoka alirudi Stanley nakunipokonya kisha akasema.

“Leo sio siku yako ya kufanya kazi we kaa hapa utulie umechoka na safari kazi hizi zote mie nitafanya!” Alisema na huku akiondoka. 

Kila alichokifanya Stanley kilikuwa kinaingia moyoni mwangu kisha kinapanda kichwani kwangu, lakini nilipokuwa nachukua fursa ya kutafakari sikupata majibu ya yale ayatendayo, nilimuona ni kijana Mkarimu, Mcheshi na Mchangamfu mno! Aliondoka Stanley na kisha akarudi na kunishika mkono kuniongoza chumbani bila shaka, nilimfuata tu bila kuuliza chochote hadi kwenye chumba kimoja hivi kizuri mno, kila kitu kipo ndani ya chumba kile.

“Hiki ndiyo chumba chako kuanzia sasa na kuendelea utalala hapa utajirusha unavyoweza, Tv ipo kama unapenda vipindi vya katuni ni wewe tu, njoo huku..” akanivutia upande wa mwengine wa chumba hicho.

“Bafu na choo, huduma zako binafsi utazitimizia hapa hamna haja yakutoka toka nje sawa?!” Alisema Stanley, nilitamani hata nimkumbatie nimlipe fadhila walau kiduchu lakini nilishikwa na aibu mwisho nilijikakaza tu.

“Pili, umenielewa?” Alihoji aliponiona niko kimya pasi na kumjibu.

“Ndiyo kaka!”

“Haya pumzika, kuhusu kazi utaanza kesho na kuhusu mshahara we usijali.” Alimaliza na kisha akaniacha nimesimama ndani ya chumba hicho, kila kitu kilikuwa kigeni kwangu, uzuri wa chumba hicho ungelidhani labda ni chumba cha Rais ama mtu yoyote wa hadhi ya juu siyo kapwela kama mimi.

“Mh, hapa nimefika!” Nilijisemea huku nikiendelea kuangaza kila kitu ndani ya chumba hicho kwangu kilikuwa kigeni, vingine vilinitisha hata kugusa ikiwemo taa iliyokuwa kwenye kifaa kimoja cha udongo hivi ikiwaka mwanga wa njano. 

Niliketi kitandani nisiamini kile nikionacho. Ama kwa hakika tembea uyaone!

Mwisho nilivua malapa yangu nakuyasukuma uvunguni kisha nami nikajilaza pasi na kushusha chandarua wala kujifunika hadi pale nilipokuja kupata fahamu ikiwa ni siku nyingine asubuhi tena ni mara baada ya kusikia vishindo vya mlango.

“Nkoo! Nkooo.. Pupupupuuu!.” Mlango wa chumba changu ulipigwa kwa nje sikushituka sana akilini mwangu nilijua wazi apigaye mlango hatokuwa mwengine ila ni ni Stanley tu, hapo nilijifuta tongotongo kisha nikasogea mlangoni nakufungua.

“Hallow dada, naitwa Rose. Nimeambiwa na boss nikuletee chai.” Alijieleza dada yule.

“Alah! Uniletee chai?” Nilishtuka.

“Ndiyo. Hivyo nimekuja kuchukua oda yako, nikuletee supu ya Samaki ama ya Kuku?” Alihoji dada huyo jambo ambalo lilizidi kunikanganya.

“Ngoja kwanza, kwani yeye yuko wapi?”

“Ameshakwenda kazini, ila aliniachia maagizo ikifika saa mbili nikuamshe!” Alijibu binti huyo.

Nilishindwa kuelewa kinachoendelea, nilimtazama huyo dada sikupata majibu hakika.

“Okey nimekuelewa, tangulia nakuja!” Nilimjibu kisha nikafunga mlango nakurudi kitandani kuketi, bado maneno ya Roae yaliusakama mno ubongo wangu.

“Mh, nimekuja kufanya kazi kweli ama? Hebu ngoja nione!” Nilikuwa nawaza nisijue mzigo huo wa maswali nimtwike nani anisaidie kunijibia, lakini katikati ya mawazo yangu nilishitukia vishindo vingine vya mlango vikipigwa kwa awamu, nilijawa hasira kwani nilihisi yule binti amerudi nami nikiwa katika mawazo yangu sipendi kabisa kusumbuliwa, niliamka kwa jazba nakufungua mlango huku nikitanguliza maneno ya lawama.

“Hivi Rose..” Nilisita, nilichotaka kusema kilikoma mara baada yakuona ni sura nyenyine imefika, alikuwa ni mwanamke mwengine wa maji ya kunde, mrefu kiasi na umbo lake lilionesha kuvutia kiasi chake, alikuwa kavalia kigauni kifupi na epron ya rangi nyeupe kama vile mhudumu wa hotel fulani kubwa.

“Jina langu ni Scorah nimepewa mzigo huu nikuletee!” Alisema huku akinikabidhi kijibox fulani kidogo tu, sikuelewa badala yake niliushugulisha ubongo wangu kuwaza mambo mengi kwa muda mmoja!

“Nani amekupa? Na nini hicho?” Nilihoji mfululizo.

“Boss, Stanley ndiye amenipa.”

“Unahakika kakwambia ulete hapa?” Bado sikumuamini licha ya kunitamkia jina la Stanley ili kuniaminisha.

“Ndiyo dada!”

“Okey!” Nilijibu kifupi kisha nikapokonya kwa shari kile kibox cha zawadi nakufunga mlango sikumuwaga wala sikumfukuza nahisi huko nje alijiongeza, moja kwa moja nikarudi kitandani nakuketi.. Nililiangalia lile box kwa muda kisha nikalivaa jukumu la kulifungua, moyo uliripuka mithili ya bomu la kurusha hii ni mara baada yakuona zawadi iliyomo ni simu tena simu ya gharama!
“Hii ni yangu??” Niliwaza huku ile hali ya kukunja sura ikiwa inafutika usoni, kwa bashaha niliibusu simu ile ajabu ni kuwa hata laini ilikuwamo tayari, mara baada ya kuitia mkononi tu iliita kwani ilikuwa wazi labda ndiyo ulikuwa mpango wa Stanley! Sikujiuliza sana kuhusu hilo bali akili yangu ilihamia juu ya screen kwenye namba iliyonipigia muda huo. “Stan? Stan ndo nani? Anhaaaa.. Nimegundua atakuwa ni Stanley.” Niliwaza kabla sijapokea kisha nikafuta batani ya kijani iliyoruhusu simu hiyo kuingia katika orodha ya simu zilizopokewa!

“Umeamkaje?” Kwa sauti ya uchangamfu ilipenya nje ya spika ya simu hiyo.

“Nimeamka salama Mungu anasaidia.” Nilimjibu, nilimjua na hata sauti tu ilitosha kuwa jawabu la swali langu.

“Umeshakunywa chai?” Aliniuliza tena.

“Hap.. Nakaribia kunywa nimeshampa oda yangu.”

“Vyema, umeshituka?” Alihoji kitu alichokijua.

“Sana! Hadi sasa sijaelewa kabisa!”

“Usiogope Pili!” Alijibu kunitoa hofu.

“Mie siogopi hata, ila nawaza tu vyote vyangu hivi?”

“Yeah! Nataka uishi maisha ambayo wanawawake wakisasa wanaishi.” Aliniacha njia panda hakika sikuelewa alichomaanisha.

“Umesemaje hapo, sijaku..”

“Potezea tu!” Alinikatiza.

“Uko wapi sasa?” Nilibadilisha mada.

“Nipo kazini now, ila baadaye nitageuka!”

“Anha, poa kaka. Nashukuru kwa zawadi yako imefika salama.”

“Nami, nashukuru kwa hilo.”

“Nikushukuru wewe!”

“Agh, huna haja Pili usiogope sana haya ni mambo kidogo kidogo tu.”

“Kweli eeh?!”

“Niamini.”

“Sawa, acha imani hiyo nikupe Stan maana unaonekana ni kama mkombozi wa maisha yangu.”

“Hahaha.. Hapana siyo hivyo bhana!”

“Nina kila sababu ya kukushukuru!”

“Usijali, sasa we kunywa chai baadaye tutawasiliana poa?” 

“Poa kaka!”

“Bye!”

“Byeee!” Ni ajabu! Ni jambo gumu kulielewa, labda sababu sikupenda kuutesa ubongo wangu kufikiria sana lakini kifupi jambo hilo liliniweka kwenye wakati mgumu, nakumbuka mara baada ya kukata simu ile nilipata wazo la kumpigia yule jirani aliyekaribu yetu lengo langu ni kuwasiliana na mama kama u mzima.

Niliihamisha namba yake kichwani nakuinakili kwenye simu hiyo nakuipigia iliita nakukata bila kupokelewa, hilo halikunikatisha tamaa nikaipiga tena hapo haikuchukua muda ikapokelewa.

📞Hallow!” Sauti yake ilipenya upande wa pili wa spika ya simu yangu, nilipata faraja na ahueni ya moyo wangu uliokuwa juu juu kwa hofu tele.
“Hellow, mamdogo mambo vipi?”
📞Poa tu, sijui naongea na nani?” Alijibu na kuhoji kwani namba ile ilikuwa ngeni kwake.
“Tamara!” Nilimjibu kifupi hapo akagundua anayeongea naye.
📞Ohhh! Tamara nimeambiwa umesafiri bila hata kuaga shost yangu, habari za huko?” Alihoji.
“Huku kwema namshukuru Mungu.”
📞Mwenzangu nilikuwa naoga, siunajua tena??”
“Najua, hivi unaweza kunisaidia jambo moja?”
📞Nambie dogo!”
“Mpelekee simu mama niongee naye siunajua tena?”
📞Ahaaha haaa.. Najua siunajua tena mie na wewe hatushindwani?”
“Nakujua.”
📞Aya usikate, ngoja nimkimbizie!” Alisema, hapo nikatulia nakumsikiza akipumua juu tu, punde simu yake ilihama.
“Ongea na Tamara!”
“Tamara mwanangu?”
“Ndiyo yeye mama simu ipo hewani!” Alisema nikimskiiza hewani miye nilikuwa kimya nikiwasikilizia tu.
📞Tamara mwanangu!
“Abee mama shikamoo!”
📞Marhabaa, nimekumiss mwanangu umefika salama?”
“Ndiyo mama namshukuru Mungu nimefika salama habari za hapo nyumbani?”
📞Hapa siye tupo kama unavyojua, halafu unajua kuna vitu ulivisahau kwenye dishi la mboga mboga?” Alisema mama hapo nikakumbuka kuhusu zile bahasha!
“Ahaaa! Unaona sasa?! Yule mama alinichanganya kabisa sikuwa hata na hilo wazo, mama hizo bahasha moja nilipewa na Stanley nikupe wewe na nyengine ni yangu utachukua moja uangalie inanini maana sikuzifungua kwa sababu ya fujo za yule mama.” 
📞Usijali, vipi lakini kazi umeanza?”
“Ndiyo mama lakini nakutana na vitu vigeni tu!”
📞Eeh, ndio ujifunze.”
“Eh, mama na wewe hutaki hata kujua.”
📞Najua umekutana na mali huko jiandae tu kuniletea mkwe!”
“Mama.”
📞Nakutania mwaya!
“Basi hebu angalia hizo bahasha zina vitu gani unambie kabla sijakata simu!”
“Aya, we nanilii hebu nipe hilo dishi!” Alipewa na kisha akachagua moja na kuichana, alishituka mno mara baada ya kugundua kilichomo.
“Mwanangu ni pesa! Tena nyingi tu! Kiriiii riiiii!!” Alishangilia mama kwa kupiga vigelegele!
“Pesa?! Hebu angalieni na ile nyengine?!” Nilisema kisha nikasubiria kwa muda huku nikiwasikia wakihebabu.
📞 Mwanangu hii moja ina laki tano!”
“Laki tano?”
“Ndiyo.”
“Na ile nyenyine.”
“Ngoja ahesabu!”
“Aya.”
“Nishingapi?” Aliuliza mama.
“Ni lakini tatu hii!”
📞Tamara hii ni laki tatu.”
“Waoh! Kumbe zilikuwa ni pesa?! Sikuwa na haja ya kuja hapa kumbe, mama itumie hiyo pesa huo utakuwa mtaji pamoja na matumizi mengine mpe mama mdogo elf 50 anatusaidia sana!”
📞Hilo silo lakunimbia mwanangu heheheeee!”

Furaha ya mama ilionekana kuongezeka mara dufu! Nilifurahi mno kugundua kumbe zile bahasha zilikuwa zimebeba pesa, niliongea na mama mambo mengi kisha tukaagana nami nikakata simu, niliingia bafuni kuoga kisha nikatoka nje mara baada yakujiadaa kwa kila kitu.

Kila nilipoangalia pakuanzia sikuelewa kwani kila kitu kilikuwa kimesafishwa tayari na kuwa katika hali nzuri ya kuvutia na pale sebuleni alikuwapo mama mmoja hivi akifuta futa makosa na vitu vingine, nilishituka kwani nilipokuja usiku ule hapakuwa na mtu. “Au ni Lodge hapa? Lakini hapana Lodge gani kubwa kiasi hiki? Mh, nisije kuwa nimeuzwa mie hapana hebu ngoja niuulize maana kuuliza siujinga!” Niliwaza hivyo kisha nikamsogelea yule mama aliyekuwa bize akifanya kazi yake kwa uweredi huku akiimba wimbo wa Kisukuma “Kobyala mayoo, kobyala shawiza sana!”

“Habari yako mama mdogo?” Nilimshitua upande wake wa nyuma kwa kumpiga kidogo mgongoni, aligeuka kama mshare kisha akatulia mara baada yakuwa amegeuka.
“Salama haujambo?” Alijibu kwa sauti ya mshituko uliochanganyika na hasira, pengine hii ilitokana na kumshitukiza!

“Sijambo, samahani naomba kuuliza.” Nilimjibu kwa sauti ya chini.

“Bila samahani!”

“We ni mwenyeji wa jumba hili?”

“Ndiyo kwanini?”

“Ni nyumba ya mtu ama hoteli?”

“Hahahaha! Hii ni nyumba ya mtu!” 

“Nawe ni nani hapa?”

“Mie mfanyakazi wa hapa, saa aaagh we mgeni machoni mwangu halafu tulipewa taarifa na boss wetu atatuletea maddam hapa, nafikiri huyo maddam ni wewe itakuwa.” Alisema yule mama.

“Maddam???” Niliuliza kwa hamaki ya hali ya juu maneno ya huyo mama yalinikanganya mno.

“Eeh ndiyo, yani mke inamaana hujui?” Aliuliza kwa mshangao mama yule..

ITAENDELEA.. 

Jamani eh, Tamara kaingia kwenye penati box kumbe kaletwa kuwa maddam na sio mfanyakazi wa ndani? Makubwa! Nini ataamua Tamara wacha tusubiri na tuone nini kitajiri, maana mie mwenyewe sijui. 😂😂 dondosha like.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post