TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

JICHO LANGU 03

SIMULIZI_______JICHO LANGU
SEHEMU________.       03
ILIPOISHIA..

“Nilikuwa nakutania tu Pili, hapa kwangu nilikuwa nahitaji mtu wakunisaidia kazi nafikiri hata hii itakufaa sawa, umepata wala usiwaze, mhu, utakuwa tayari muda gani nikuijie?” Alihoji nilimtazama mama machoni kisha nikajibu.
“Hata leo miye niko tayari..” Nilimjibu.

ENDELEA..

“Oh, umeshajiandaa?”

“Kaka, mimi muda wowote, hata ukisema sasa.”

“Kweli eeh?!”

“Ndiyo kaka!”

“Basi usijali, kwa sasa niko bize kidogo mizungukoni jioni majira ya saa kumi na mbili kasoro nitakujia, hii namba ni yako?”

“Hapana si yangu, nimeazima kwa jirani!”

“Ow! Kwani wewe huna simu?”

“Ndiyo mie sina kaka yangu!”

“Ah, vipi mama yeye anayo?”

“Hamna, hata yeye pia hana.”

“Mnaishije bila mawasiliano na dunia ya sasa imekuwa kijiji jamani.”

“Aah! Kaka siunajua hali yetu tena.”

“Basi sawa usijali, kwa hivyo nitakupataje?”

“Jioni huyu aliyeniazima simu huwa anaingia kibaruani hivyo jioni hiyo hatokuwepo nafikiri utanikuta pale tuliposimama muda ule kwenye kale kaduka!”

“Anhaa, poa nimekuelewa.”

“Ahsante kaka!”

“Ahsante pia, mama yupo?”

“Eeh, yupo anakusikiliza.”

“Hahaha.. Msalimie sana!”

“Anakusikia tu hapa.”

“Aya byee!”

“Bye2!”

“Poa!”

“Poa!” Alijibu kisha nikakata simu nikiwa nafuraha kubwa moyoni mwangu kwa kufanikiwa kupata habari zile njema.

“Kasemaje?” Mama aliniwahi kabla sijafungua kinywa kumuelezea, nilitabasamu kisha nikamkumbatia kichwa na kumchumu halafu nikatulia na kujibu.

“Kasema kuna kibarua nyumbani kwake, nafikiri ninaenda kuwa dada wa kazi, mimi naona hata hii yatosha mama kuliko kubweteka nyumbani siingizi hata mia hii hali inaniuma acha nikateseke huko mama nipate pesa mimi sasa nimekuwa, sitaki kusubiria ndoa, ndoa za sasa mama si ndoa ni mateso matupu mama bora nikachakarike nipate chochote kitu!” Nilimjibu.

“Kwa kweli binti yangu sasa umekuwa, sikutegemea kama ungelikuwa na akili nyingi hivi, Mungu akubariki binti yangu.” Alisema mama.

“Aya, aya binti Athumani nisuke chapchap nirudishe simu ya watu nijiandae, mida yenyewe hii inayoyoma balaa!” Nilimwambia mama huku nikijitenga mbele yake ili kusudi amalizie kunifunga funga nywele zangu ambazo baadhi zilikuwa bado hajazifunga.

Baada ya muda kadhaa mama alikuwa amekwisha nifunga vizuri, nilirejesha simu na kisha nikajiandaa vizuri kwa kuoga nakupakia nguo zangu kwenye salfeti kwani sikuwa na begi lolote la nguo. Nikiwa namalizia kukunja vitenge vyangu baadhi mama aliingia chumbani kwangu na vitenge pea mbili mkononi nakuketi kitendani akinitazama kisha akasema.

“Mwanangu, ijapo huu ndiyo ulikuwa mtoko wangu lakini sina budi kukupa, utakusitiri. Hivi vitenge unavyopakia humu vimechoka sana! Angalia hicho ulichojifunga kimepauka kweli, agh, hapana! Hata kama ni umasikini siyo hivo, hebu vaa hivi sawa.” Alisema mama huku akinikabidhi pea hizo za vitenge (Wax) mpyaa kabisa, nilimtazama mama kwa uchungu imani ya huruma iliukanyaga moyo wangu kiasi cha kuyafungua machozi yangu, yalipotoka sikujua ila nilishitukia yakianguka tu!

“Ahsante mama!” Nilipokea na kukivua kile kitenge nakujifunga hicho alichonipa zawadi.

“Ahsante pia mwanangu!” Mama aliniambia kisha akainuka nakutoka nje akaketi ngazini nje ya mlango wa chumba hicho, nami baadaye nilitoka nikiwa nimejiweka vyema nakuhakikisha niko katika muonekano mzuri.

“Jicho langu nitizame hapa naonekanaje?” Nilimuuliza mama kwa utani huku nikitanua mikono yangu nakugeuka ili aliangalie vyema!

“Nitasema nini juu ya urembo wako mwanangu, hata uvae batiki wewe ni mrembo tu, umependeza mno! Mno!” Alisema mama huku akitupia macho yake usoni mwangu na kisha akainuka pale ngazini.

“Eeeh, mama nauzuri gani huo?”

“Hujui tu!” Alijibu mama huku akitembea kuniongoza njia ikiwa ni sehemu ya kunisindikiza. Njiani hakuacha kunipa wasia juu ya maisha nitakiwayo kuishi mjini, muda mwengine niliona kama mama anawasiwasi kuondoka kwangu ila hilo nilipinga kwa kumuhakikishia nitakuwa salama na hapa kila mara nitakuwa narejea.

“Nakuacha pekee yako mama roho yaniuma lakini nitafanyaje nami nimekuwa siyo tegemezi tena kwako, vumilia hakuna namna mama.” Nilimjibu tukiwa karibu na ile sehemu ya makutano tulipokubaliana na Stanley.

“Usijali binti yangu mimi nimebakiza mwendo kidogo wa maisha yangu, miaka 49 siyo mchezo, wewe bado ndiyo uanze kuyajenga maisha yako usinitazame zaidi mimi binti yangu. Uwe na amani uwapo sawa?” Alisema mama na kisha akachezesha sikio la kulia kama ambavyo mara nyingi afanyavyo!

“Sawa, mama wewe rejea nyumbani nami nibaki hapa kumngojea Stanley!”

“Sawa, ufike salama binti yangu!”

“Amina mama!” Tuliagana kwa unyonge na kumbatio dogo, japo nilionesha kutabasamu usoni lakini siyo moyoni, moyo wangu uliungua kwa maumivu makali, kwani hata siku moja sikutamani kuondoka nakumuacha mama nyumbani mpweke lakini ningefanyaje? Sina budi kukubaliana na hilo, nilimtazama mama yangu akiondoka asteaste na huku mara kwa mara akigeuka kutizama nyuma.

“Mama nitarudi kwa ajili yako, nitarudi kulirudisha tabasamu lako, mama yangu u mrembo nitaurejesha urembo wako, huna sababu ya kuogopa mama!” Nilijisemea kisha nikageuka nakupiga hatua hadi pale dukani, niliomba ridhaa ya kukaa hapo kwa muda mhudumu wa duka hilo hakuwa na ajizi alinipa ridhaa hiyo, nikaketi huku macho yangu yakiangalia njia ni wapi gari lile litatokea, nilikaa hapo kwa muda mrefu sana hakukuwa na dalili zozote za kutokea mtu wala gari lile, hapo roho yangu ilianza kuingiwa shaka kwani ukiza ulikuwa umeanza kulifunika jua.

“Kaka samahani, hivi sangapi hapo?”

“Kumi na mbili na dakika arobaini na nane!”

“Oh, ahsante!”

“Usiwaze dadake!” Alikuwa ni mkaka mmoja aliyekuwa anajaza vocha aliyonunua dukani hapo. Nilijaribu kujiambia subira yavuta kheri nisubiri lakini nilianza kuchoka hasa muda ulivyozidi kusonga mbele. Masaa yalikatika bila kuona chochote, nilikaa nikasimama, nikatembea lakini hola hakuna dalili wala ishara ya kutokea kwa mtu, katikati ya ukimya likaibuka wazo  nikanyanyuka haraka nakusogea pale dukani kumuuliza mhudumu wa duka hilo kama anasalio la kupiga kwenye simu yake, bahati iliyo yangu nilifanikiwa kupata salio kwa kuwa namba ya Stanley niliinakili kichwani nilimuomba aipigie!

“Doh! Mbona naambiwa siyo sahihi nihakiki sijui nini..” Kijana huyo mhudumu wa duka hilo alisema, hapo nusu nichanganyikiwe kwani niliitaja namba hiyo kwa usahihi kabisa.

“Hebu ihakikishe ni yenyewe kweli!” Alisema huku akinipatia simu yake hiyo ndogo ya Nokia, niliipokea nakuingalia hapo niligundua alikuwa amezidisha namba moja ya mwisho kwenye tisa moja aliweka 9(9). Nilicheka nakuandika upya kisha nikaipigia lakini hata hivyo haikuwa hewani pia. Nilichoka, nilichoka mwili na akili.

“Vipi?”

“Dah, haipatikani, nifanye mpango nirudi nyumbanu tu hamna namna.” Nilimjibu huku nikipenyeza mkono wangu kwenye kitundu cha nondo za duka hilo nakumpatia simu yake.

“Na kweli, maana umemgoja sana tangu muda ule sijui ilikuwa sangapi hadi sasa saa tatu kasoro hii!” Alisema kijana huyo, niliona wazi siku hiyo imeishia hapo huku nikiamini Stanley hawezi kuja tena.

“Simu yenyewe sina, simu yake haipatikani nitajuaje kama atakuja ama haji Je kama kapata dharura?! Eeh, mie nijirudie nyumbani na kesho nayo ni siku nitajaribu bahati.” Nilijisemea kisha nikanyanyua salfeti yangu tayari kwa kurudi nyumbani.

“Aya kaka, nashukuru!”

“Poa poa, dada!” 

Nilianza kutembea mithili ya mgonjwa wa homa kali, miguu haikuwa na nguvu hata, nilijikuta nimechoka mno na huku tumboni vurugu za minyoo zilikuwa zikizidi kuchoa njaa yangu, niliacha ukingo wa duka hilo kwa kuvuka kidaraja cha mbao kisha nikaungana na barabara kurudi nyumbani, lakini kidogo hivi nilisikia honi za gari zikipiga kwa fujo, niligeuka bila matumaini kwani nilikuwa nimekwisha kata tamaa. Lakini ghafla moyo wangu uliruka nakushangiria kwa nguvu hii ni mara baada yakuliona ni gari la Stanley! Nilipata tumaini jipya nakujikongoja kurudi pale liliposimama, Stanley alishuka nakunipokea huku akiniomba radhi kwa kuchelewa akisema alikuwa gereji gari ilipata hitilafu.

“Simu yenyewe nilizima kuna mshenzi mmoja ananisumbua sana!” Alisema huku akizama garini.

Niliingia garini humo nakuketi siti za nyuma nakujituliza kwani nilikuwa nimechoka mno! Stori za hapa na pale zikaendelea hata nilipopitiwa na usingizi, nilikuja kushituka ni baadaye mara baada ya honi za gari hilo kuwa zimefika kwenye moja ya jengo kubwa, mlango ulifunguliwa gari hilo likazama ndani hadi sehemu ya kupaki.

“Oh, umeamka nilikuwa nakusemesha naona kimya kugeuka kumbe ushalala muda mrefu tu. Aya tushafika hapa ndiyo kwangu.” Alisema Stanley, nilishuka huku nikiangalia mjengo huo mkubwa wa horofa moja hivi, hakika nilijihisi ningali ndotoni, sikuyaamini macho yangu kabisa, sikuamini kile nilichokuwa nakiona mbele yangu, sikudhani siku moja naweza kukanyaga sehemu nzuri vile, sikuamini kabisa!

“We’ Kizota, hebu njoo ushushe hii mizigo humu!” Alimwita mlinzi wa geti kuja kushusha mizigo!

“Mhu, Karibu sana Pili jisikie kama upo nyumbani!” Alijibu Stanley huku akinishika mkono kuniongoza njia kuzama ndani ya jengo hilo.

Ama kwa hakika nilijiona ni mtu mwenye bahati kufika katika jumba hilo ambalo sikuwahi kabisa kuliota kama siku moja naweza kanyaga hadi nakufa, nilishangaa mno!

“Tuingie ndani. Usiogope!” Alinishika mkono Stanley hadi ndani, ndani ya jumba hilo sitoacha kupasifia kwa namna palivyokuwa pazuri pakuvutia, vitu vingi vya urembo wa kisasa darini vilielea.

“We keti hapa chakula nitakutengea sawa?!” Alisema Stanley huku taratibu akitabasamu nakutoka akiniacha mwenyewe nimezubaa nikishangaa uzuri wa jengo hilo.

“Nyumba yote hii anaishi peke yake tu?” Niliwaza hivyo huku macho yangu yakizunguka mithili ya feni ndani humo, punde alirudi Stanley sijui nguo alibadili muda gani, alikuja kavaa kipensi kilichombana na juu alivaa vest, Stanley si mwanaume haba. Alikuwa amejazia kifua na hata mwili wake ulikuwa umekaa kimapenzi, nilipomtizama kifuani nakuona manyoya mwili wangu ulisisimka sana na akili ikaruhusu mawazo ya ajabu kuniingia.

“Pili!” Nilishtukia mkono umetua begani mwangu, sikuuona pengine ni kutokana na kuzubaa kwangu, hapo nilizinduka nakurejesha fahamu zangu kisha nikajibu.

“Abe!” 

“Unashangaa nini?” Alihoji kwa sauti ya chini huku akitua mikono yake mezani.

“Hapana!” Nilimjibu kwa uoga, nahisi aligundua nilichokuwa naangalia maana niliona akijifunika vest yake halafu akaniuliza.

“Kinakutosha hiki?”

“Ah, eeh ndiyo.”

“Okey, bomba hilo hapo unakwenda kunawa unachukua tishu unajikausha ndiyo unakuja kula, mezani kuna kila kitu matunda na vyakula utavyotamani kula jiachie mimi niko pale.” Alieleza Stanley huku akiondoka.

“Kaka!” Kabla hajafika mbali nilimwita, bila kuchelewa akageuka.

Nilimtazama kwa zaidi ya sekunde kumi ndipo nikazungumza.
“Ahsante!” Nilisema huku nikiangalia chini.

“Ahsante ya nini Pili, hebu punguza bhana hilo neno kuna muda linanichosha sana sawa?” Alijibu alionesha ni wazi hapendezwi, nami nikatingisha kichwa.

“Haya kanawe uje ule, ukimaliza nambie nikuoneshe chumba chako cha kulala!” Alisema kaka Stanley nilimtazamana naye machoni kisha akageuka nakuondoka nami nikaelekea pale aliponionesha bomba. 

“Mashikoro mageni! Hili bomba linafunguliwaje?” Nilipokuwa hapo bombani nilijicheka, kulikuwa na kioo ukiwa unanawa, na kubwa zaidi aina ya koki za bomba hilo ulikuwa tofuati na yale niliyoyazoea, nilijaribu kulizungusha litoe maji lakini wapi nilidunda nikabaki kuhangaika.

“Leo hili bomba lanitoa ushamba!” Nilijiwazia moyoni huku nikigeuka pale ilipo meza, niliona kuna vijiko na uma nikawaza sikuona sababu ya kunawa, “Bhana eeh! Nitatumia kijiko.” Nilijisema kisha nikageuka nirudi mezani lakini kabla sijatoka niligonganga kifua na Stanley.

“Oh, samahani. Unajua nimerudi haraka mara baada ya kukumbuka hili bomba halifunguliwi hapa bali unakua unabonyeza hapa unafungua sawa?!” Alisema huku akinishika mkono nakunibonyezea pale kwenye kitufe, maji yalipoanza kuchuruzika aliondosha mkono wangu na kisha ule mwengine huku akisema kiutani.

“Mgeni lazima akirimiwe! Hapo vipi?!” Mara baada yakumaliza kuniosha alivuta tishu nakunikausha mikono yangu kisha akainua uso na kunitazama.

“Oh, samahani nahisi nimekuboa kukushika bila ridhaa yako, nisamehe bure!” Alijishitukia kwa namna nilivyokuwa namtazama kumbe wala sikuwa hata na wazo hilo. Ili kumtoa hofu nilitabasamu kisha nikajibu.

“Hamna kaka usijali!” Nilimjibu taratibu.

“Aya nashukuru, sasa naomba ukale, tulipokuwa pale nilisikia miungurumo ya tumbo nikajua tumbo halina kitu hivyo naomba ule ushibe sawa?” Alimaliza nami nikamjibu kwa kichwa kama kawaida yangu, naye akatoka akaniacha nikielekea pale mezani palipopambwa na kila aina ya chakula.

ITAENDELEA.... 
Tamara amekwisha fanikiwa kuingia mjini. Je! Nini kitakachojiri huko?

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post