Riwaya:SIRI YA MOYO.
Watsapp:0747995035.
SEHEMU YA KWANZA (01)..
Mnamo majira ya saa kumi na moja za jioni,ulionekana msururu mrefu wa watu wengi sana wanaume kwa wanawake ukitokea maeneo ya makaburi ya kanisa furani ndani ya mji wa Nashville.Watu hao walikuwa wametoka kumzika binti mmoja wa miaka ishirini na mitano ambaye alikutwa amejinyonga ndani ya chumba chake alichokuwa akiishi.Inasemekana msichana huyo aliamua kujiua kwa sababu ya msongo wa mawazo pamoja na shida mbalimbali za kimaisha zilizokuwa zikimsumbua japo sababu hizo hazikuwa na uhakika sana .Katika msafara huo makundi kadha wa kadha ya watu yalianza kuonekana,na miongoni mwa makundi hayo walikuwemo marafiki wa karibu wa marehemu majina yao wakiitwa Neema pamoja na Cathe,walitembea kwa mwendo wa taratibu ili kuendelea kujadiri ni sababu zipi ambazo zilipelekea hadi rafiki yao akachukua uamuzi wa kujitia kitanzi.
"Neema labda wewe unaweza kutuambia ni kwa nini rafiki yako Diana aliamua kujiua ili hali ndo kwanza wiki iliyopita tu alibahatika kupata ajira serikalini?" .Lilikuwa ni swali moja kutoka katika kinywa cha mwana mama furani hivi aliyekuwa amejifunga kilemba kichwani mwake."Hata mimi kifo cha Diana kimenishtua sana,sikuwahi kufikiria kama angechukua uamuzi kama huu,na sijajua ni sababu zipi zilizopelekea hadi akafanya vile".Alijibu Neema,hata yeye ikaonekana hana uhakika na hana jibu la moja kwa moja lililo mfanya Diana akachukua uamuzi wa kujinyonga.Wiki kama tatu zilizopita kabla ya kifo chake,ilikuwa siku moja ya jumapili binti huyu alionekana kanisani akiwa anaongoza kipindi cha sifa na hakuna hata mmoja ambaye alitegemea kama angekuja kujiua namna ile.Sasa Diana alikuwa ni msichana mmoja ambaye alijariwa urembo wa aina yake,hakuwa na urembo wa rangi ya chungwa tu bali pia alikuwa na umbo la kumtoa nyoka pangoni,,,Unaweza sema miongoni mwa warembo waliokuwa wakikimbiza ndani ya mji wa Nashville,Diana alikuwa ni miongoni mwao.Alizaliwa mwaka wa 1980 ndani ya familia ya kitajiri ya mzee Filemoni akiwa ni mtoto wa pili wa familia ile ,,,Wazazi wake walimsomesha hadi chuo kikuu ambapo mara baada ya kufika chuoni alisomea mambo ya udaktari.Maisha ya msichana huyu yalikuwa ni ya kipekee sana,,,Tangu akiwa sekondari mbali na kuwa na marafiki kadha wa kadha akiwemo Neema muda mwingi alikuwa akipenda kukaa peke yake,hiyo haikuishia shuleni tu,nyumbani napo muda mwingi alikuwa akiutumia kukaa chumbani,akionekana sebuleni ni ule muda wa kula tu,muda wa kula ukimalizika anarudi chumbani kama kawaida.Mwanzo hii tabia ilikuwa ikiwakera sana wazazi wake lakini baadae ilibidi wamuache tu huenda ndivyo alivyo.Sasa kuna siku moja Neema alimpitia mishale ya alasiri waende kanisani kwenye mazoezi ya kwaya kwani walikuwa wakiimba wote kwaya mbali na kwamba walikuwa wakisoma.Siku hiyo ilikuwa ni ya jumatatu,,,Neema akafika na kukaribishwa na mama ake na Diana wakaketi sebuleni huku Diana akiwa hayupo maeneo hayo."Mama nimemkuta Diana?" Neema aliuliza swali hilo huku akimtazama usoni mama Diana.
"Ndio mwanangu!! Diana yupo".Mama Diana alijibu huku akimkazia macho usoni msichana huyu."Yupo wapi?" Neema akahoji tena."Yupo chumbani kwani hujamzoea tu,yupo huko chumbani kwake".Mama Diana alijibu."Amelala au?" Neema kwa mara nyingine tena akauliza."Hapana nadhani hajalala,unaweza kwenda kumuona ".Mama Diana akajibu na hapo ndipo Neema aliponyanyuka na kuanza kuzipiga hatua kuelekea chumbani kwa rafiki yake huyo.Baada ya kufika alimkuta rafikiye ameketi kitandani huku akijisomea vifungu mbalimbali vya Biblia maana hii nayo ilikuwa kama desturi yake.Sasa Neema alimtazama mara moja tu usoni kisha akakaa karibu yake,Akatulia kwa dakika kama tano hivi baadae akawa amepata cha kuzungumza."Diana Bwana Yesu asifiwe?" Neema alianza kwa kumsabahi namna hiyo,Diana akaachia tabasamu hafifu na la kichovu usoni mwake."Amina Neema,vipi mzima wewe?" Aliitikia Diana mara hii akiwa hamtazami usoni Neema."Daah!! Rafiki yangu hivi kwa nini unapenda sana kukaa peke yako peke yako ? Kibaya zaidi hapa nyumbani napo unapenda sana kukaa chumbani muda mwingi kuliko kuchangamana na wenzako,kwa nini?".Neema aliamua kuyauliza maswali hayo ili apate kujua ni kwa nini rafiki yake anapenda kujitenga tenga na wenzake."Neema wala usiwaze hii ni kawaida tu na usiogope sijui kwa nini niko hivi,nimezoea ni staili yangu tu ya maisha,,,kukaa peke yangu namna hii huwa kunanipa wigo wa kufanya tafakuru yakinifu juu ya maisha yangu".Diana alijibu,Neema akaona akiendelea kumhoji namna hiyo wanaweza chelewa kwenda mazoezini,akaamua kulipotezea jambo lile."Nimekupitia twende mazoezini Diana". Alizungumza Neema,na hapo ndipo tabasamu la waziwazi likaanza kuonekana usoni mwa Diana,,,,Walisimama kwa pamoja kisha wakaanza kuzipiga hatua kuelekea kanisani,,,Maana hiyo siku pia mwalimu wao alikuwa na wimbo mpya wa kuwafundisha.
******************
"Sikiliza Judith,hela nyingine nitakupa jioni nikitoka kwenye mazoezi ya kwaya maana kuna wimbo mpya naenda kuufundisha huko,nitakuja kukupa tu usiwaze".Maneno hayo yalisikika yakitokea ndani ya chumba kimoja cha kulala wageni,na aliyazungumza kijana mmoja aliyekuwa akionekana ni mpole na mlokole wa kupindukia kuanzia sura yake,vaa yake mpaka tembea yake,,,Kijana huyu maarufu sana katika kanisa la kina Diana alikuwa ni mwalimu wa kwaya na alikuwa akitunga nyimbo nzuri zinazogusa sana.Kijana huyo alijulikana kwa jina la Misholi,hakuwa ameoa lakini alikuwa na tabia za chini chini chafu sana na hakuna hata mtu mmoja pale kanisani awe mchungaji au mzee wa kanisa aliyekuwa akizifahamu tabia zile zaidi ya kumfahamu tu kama mtumishi wa Mungu aliyeokoka vizuri kabisa."Misholi.....Misholi,,narudia tena kukuita,we Misholi,yaani usipo nilipa hiyo hela nitakuanika kweupe tena mchana mchana,naondoka".Yule binti aliongea kisha akavaa nguo zake akatoka nje na kuondoka maeneo yale.Misholi akabaki peke yake mule chumbani,akavaa nguo haraka haraka ili awahi kanisani,na alipohakikisha amechomekea vizuri,alichukua Biblia yake kubwa akaibeba waziwazi mkononi ili watu wasimshtukie,waone kama ametoka kwenye masuala ya ushuhudiaji.
ITAENDELEA.............................................
Tags
simulizi