TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

SIRI YA MOYO 02

Riwaya:SIRI YA MOYO.
Watsapp:0747995035.
SEHEMU YA PILI (02)..

Misholi akaanza kutoka ndani ya kile chumba huku akiwa hana wasiwasi,alijiamini mno na alijua hakuna wa kumshtukia yeye ni mtumishi wa Mungu mambo mengine ni siri yake.Alifanikiwa kuchomoka humo na kwa bahati nzuri kwake hakuna aliye mshtukia kama alikuwa akitoka ndani ya gesti house kufanya zinaa na yule binti wa kuitwa Judith.Sasa aliishikilia vizuri Biblia yake akawa anatembea kwa mwendo wa haraka haraka kwani ule muda muafaka wa kufanya mazoezi kule kanisani ulikuwa ukikaribia,,,Basi kwa mwendo wake huo akafanikiwa kutumia dakika kama kumi hivi ,maana yake kule kanisani alifika saa tisa kamili akawa ndani ya muda uliokuwa umepangwa.Baada ya kufika aliwakuta wanakwaya kadha wa kadha wakiwa wana mngojea wakiwemo kina Diana pamoja na mwenzake Neema.....Bwana asifiwe kama salamu yao maeneo hayo ikatembea kama njugu,anga lote likajua ni kweli aliyeingia pale ni mtumishi wa Mungu full package ."Jamani kaka Misholi leo umependeza sana".Hiyo ilikuwa ni sauti ya Neema mara baada ya kumuona kijana huyo wa kidato cha nne akiwa ndani ya suti nyeusi."Asante mama askofu hii ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu,ila ubarikiwe sana".Misholi alijibu muda huo akiletewa kiti na binti mmoja na kisha kuketi.Ndani ya dakika tano tu tayari wanakwaya wote walifika eneo lile na mazoezi yakaanza mara moja.Walianza kufundishwa wimbo ule mpya ,wimbo ukawa ni mtamu sana na kwa namna ulivyokuwa ukiimbwa ikaonekana utabamba sana.Basi wimbo ukaendelea kufundishwa huku sololist yaani muimbishaji akichaguliwa kuwa ni Diana,na kiukweli huyu binti kama ni sauti pia alijaliwa,Mungu kwa kweli alimpa kila kitu msichana huyu,,,yaani katika umri wa miaka kumi na sita tu aliyokuwa nayo kwa kipindi kile alikuwa akianza kuimba na sauti yake ile ya kuvuta hata kama hukuwa uweponi unajikuta unaingia uweponi bila kujua umeingia ingiaje,,,Akianza kuimba hususani kama nyimbo ni ya kusikitisha basi hata kama machozi yako huwa yanakuaga ni umbali wa maili miatano basi yatakusogelea kwa kasi na kukufikia tu na hatimaye yataanza kukutoka,huyu ndo Diana.Ule wimbo ukatumia dakika thelasini kuuelewa,kila mmoja sasa akawa na uwezo wa kuuimba,,,Ulipoeleweka vizuri staili zikafuata mwishoni.Mpaka mishale ya jioni jioni inawadia tayari ule wimbo ulikuwa umeshakaa kwenye melodi sawa sawia kabisa...Hatimaye saa kumi na mbili ikawadia,wana kwaya wote wakatawanyika kila mmoja akarudi nyumbani kwake au nyumbani kwao,,,Misholi nae akarejea sehemu ile aliyokuwa akiishi huku akiwa na ile pesa yake ambayo wanakwaya walimpatia.Misholi hakuwa na wazazi,wazazi wake wote wawili kwa muda wote ule walikuwa washatangulia mbele za haki maana yake walikuwa wameiaga dunia kwa ugonjwa hatari wa ukimwi ,na Misholi alizaliwa akiwa na virusi vya ukimwi na tangu anakuwa amekuwa akiishi kwa vidonge vya kupumbaza virusi hivyo.Sasa kutokana na kwamba dawa zile zilimkubali mno huku akizipata bure mwili wake ulikuwa umenawili mno kumtambua kiuepesi kwamba ni mwasirika wa virusi vya ukimwi lilikuwa ni jambo gumu mno.Kijana Misholi alikuwa ni kijana mmoja mtanashati safi,mwenye mwili wa kiume uliojengeka vizuri na alikuwa ni bonge la handsome boy hilo mabinti hususani wale wa kanisani walilielewa na kila mmoja usiku na mchana alikuwa akimuomba Mungu Misholi aje kuwa mume wake.Uzuri wa Misholi hakuwa ni mtu mwenye shobo nyingi nyingi au maneno mengi mengi yeye alikuwa hana mambo mengi ,alikuwa ni kijana mkimya na asiyekuwa na makundi makundi,tabia zile zile ambazo Diana alikuwa nazo na Misholi pia alikuwa kama vile,tofauti yao ilikuwa ni jinsia tu.Sasa jambo ambalo Misholi hakutamani mtu alijue ni ile hali yake,Misholi hakutaka kabisa kujulikana kama yeye  ni mwasirika wa virusi vya ukimwi na kweli katika hilo alifanikiwa,hakuna hata mmoja aliyekuwa akijua kama Misholi ana ngoma,si mabinti si vijana wa kiume au hata wale marafiki zake.Mtu pekee aliyekuwa akilitambua hilo alikuwa ni baba yake mdogo....huyu baba alijulikana kwa jina la Yakobo,ambapo nae pia alimtunzia siri ile mwanae na hakuwa tayari kuiweka wazi,kwa kuogopa kuwa wanadamu wataanza kumnyanyapaa mwanae au hata kumtenga kabisa.

     Kwa vile baba yake huyo mdogo aliachiwa mali nyingi na wazazi wake na Misholi haikumpa tabu kumlea kijana huyo,maana yake kama ni kumpatia diet ya maana kwenye mambo ya msosi alimpatia.Na kutokana na hilo Yakobo aliapa hataoa kabisa kazi yake itakuwa ni kuhakikisha ana mlea Misholi kwa namna yoyote na gharama zozote ili tu asije akakongolozoka na hatimaye watu kuanza kumshtukia kama mwasirika.Imani yake ilimtuma endapo akioa basi itajulikana tu siri ile kama kijana wake ni mgonjwa,,,Hivyo alitafuta house girl wa kufanya kazi za pale nyumbani huku akimjengea nyumba maalumu kijana wake kwa ajili tu ya kumeza zile dawa watu wasigundue,na hiyo nyumba yenye chumba kimoja na sebule hakuruhusiwa yeyote kuingia mule zaidi ya Misholi na baba ake huyo mdogo,hata yule house girl alipigwa marufuku kuingia ndani ya nyumba ile iwe kwa kukusudia au kwa bahati mbaya."Agatha,mambo yote yaliyomo ndani ya nyumba hii unaruhusiwa kuyafanya au kuingia popote,ila angalizo ni moja tu,ile nyumba yenye rangi ya kijani unayoiona pale huruhusiwi kuingia kabisa,mambo ya usafi na nini utakuwa ukiyafanya ndani ya nyumba hii na vyumba vyake,kule niachie mimi mwenyewe ndiye nitakaye kuwa na hiyo kazi ya kufanya mambo ya usafi katika nyumba hiyo".Hayo yalikuwa ni maelekezo ya kwanza kabisa siku ambayo Agatha analetwa kufanya kazi kama house girl maeneo hayo,hivyo tangu Agatha anafika hapo hakuwahi kujua ni kwa nini nyumba ile haruhusiwi kuingia mtu yeyote zaidi ya Misholi na baba yake pekee.Hata hivyo hilo hakulitilia manani sana,mwanzo aliamini halimhusu cha msingi nikufuata maelekezo pesa ipatikane.Sasa  ile nyumba,Misholi hakuwa akiitumia kwa ajili ya kulala,Ile nyumba ilikuwa na kazi mbili tu,kazi ya kwanza ni kuhifadhi dawa za ARV za kupumbaza virusi vya ukimwi na kazi ya pili ilikuwa ni kwa ajili ya Misholi kuingia kunywa dawa zile.Yakobo katika hilo hakuwa na masihara kabisa wala mchezo ,na kwa kuhakikisha hafanyi makosa hata ya kuingiwa na tamaa za kuoa aliamua kukata kabisa mishipa ya hisia maana yake aliamua kujifanya towashi kwa hiari,akawa hana nguvu za kiume wala hisia ili kazi ya kumlea Misholi bila ile siri kufichuka iende sawa.

             *************************

Basi tuachane na mambo ya Misholi na baba ake,turejee kwa upande wa Diana.Jioni ile baada ya binti huyu kutoka mazoezini huku akiwa ameambatana na rafiki yake kipenzi Neema,tayari kuna hali furani ilikuwa imeshaanza kumvamia na hakuielewa ni kwa nini imemtokea na hakutaka mtu yeyote ajue iwe mama yake au rafiki yake .Hali yenyewe ni hisia za mapenzi,na hisia hizo zilikuwa ni juu ya kijana Misholi,,,,Ikawa kama ghafla sana,mwanzo katika historia ya maisha yake kuanzia anaanza shule hadi hapo alipo ambapo ni kidato cha nne hakuwa amewahi kumzimia kijana yeyote wa kiume ,ina maana Misholi alikuwa ni mwanaume wa kwanza kumpenda,mbali na kwamba alikuwa na baba lakini hakuwa ametokea kumpenda kama ambavyo ametokea kumpenda kijana Misholi.Sasa ikawa kila akikaa anaanza kumwaza Misholi tu,akianza  kula anamwaza Misholi tu,akilala napo alikuwa akiishia kumuota Misholi tu ...Binti akajua huenda Mungu ameamua kumuonyesha mume wake mapema mapema.

ITAENDELEA............................................

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post