Riwaya:SIRI YA MOYO.
Watsapp:0747995035.
SEHEMU YA TATU (03)..
Ndivyo alivyoamini Diana,kwa hiyo tangu siku ile alimbeba Misholi ndani ya moyo wake,akawa anakula nae,anaishi nae,anatembea nae na analala nae japo hakutaka kabisa kumwambia juu ya hisia zake hizo au kumfungukia ukweli eti kwamba amempenda.Kwa hiyo ile ikawa ni ndoto yake akaamini ipo siku itatimia,Misholi atakuwa mume wake na watazaa watoto wazuri.Mwanzo kutokana na kwamba alikuwa bado ni mwanafunzi tena wa kidato cha nne,ilimbidi atulie kwanza atulize na akili yake pia asije akakurupuka akaishia kujuta maishani,Hakutaka kumwambia mapema Misholi alitaka kwanza amalize masomo yake salama mpaka huko chuo kikuu ndipo atakapo mwambia sasa halafu wanafunga na ndoa wanayaanza maisha mapya.Kidogo hali ya uchangamfu kwa binti huyu ikawa ni kubwa japo kwa kiasi chake ,tofauti na alivyokuwa mwanzo,jambo ambalo liliwashangaza wazazi wake .Mara hii Diana hakuwa anakaa kaa peke yake tena iwe chumbani au hata kule shuleni,na hii ilitokana na amani yake ya moyo iliyomuijia kama muujiza kwa kumpenda kijana Misholi.Siku ya kesho yake ikawadia,nayo ilikuwa ni siku ya jumanne....Siku hiyo ilikuwa ni ya shule,Hivyo wanafunzi wote walienda shuleni kama kawaida.Diana pamoja na marafiki zake nae akaenda shule kama kawaida,Misholi nae mara baada ya kunywa chai yake asubuhi ile alienda shuleni na akawa amewahi tu kama wengine.Sasa kwa bahati nzuri,Diana pamoja na Misholi walikuwa wakisoma darasa moja ,masomo yalipokuwa yakiendelea muda mwingi sana Diana alikuwa akimtazama tazama Misholi kwa macho ya wizi,Misholi akimshuku anajifanya kama hakuwa akimtazama.Muda wa mapumziko ulipowadia na wanafunzi wote kutoka madarasani mwao,Diana aliamua kubaki darasani na si kwamba alibaki kwa bahati mbaya aliamua kufanya hivyo mara baada ya kumuona Misholi amebaki humo akijisomea.Ikumbukwe huyu Misholi alikuwa na tabia kama za Diana,nae muda mwingi sana alipenda kukaa peke yake na katika hilo alijihisi amani kabisa,,,,alikuwa na muda mchache mno wa kukaa na marafiki zake muda mwingi ni kukaa peke yake tu kwa madai ya kwamba anafanya hivyo kwa ajili ya kutengeneza chakula kizuri cha akili yake.Sasa Diana akawa anazuga kama anasoma lakini macho yake yote yalikuwa yakimtazama Misholi."Mmh!! Huyu msichana mbona ananitizama sana,amenipenda nini? Sijui nimuibukie nini? Ila huyu ni mlokole na mimi ananikubali sana kama kijana mtulivu,nikifanya pupa nitaangukia pua,ngoja nikaushe niusikilizie huu mziki utaishaje" .Kimoyo moyo Misholi alijisemesha,,,kisha akazidi kusolve maswali aliyokuwa nayo.Sasa huku uvumilivu ulimshinda kabisa Diana,akaamua kuinuka na kisha kuzipiga hatua kuelekea pale alipokuwa amekaa Misholi,,,alipomfikia alimgusa begani, Kijana akashtuka ikabidi ageuke nyuma,huku akijua fika kabisa huyo ni Diana.Kabla Diana hajaamua kuzungumza chochote, dirishani alionekana Neema akichungulia wakati huo akiwa na mwenzake Cathe,na hicho kitendo kikawafurahisha mno,mwanzo furaha yao ilikuwa ni kumuona rafiki yao Diana akiwa anafanya kampani kama zile tofauti na kukaa peke yake idol jambo ambalo si zuri kabisa."Cathe unamuona Diana,unamuona?" Kwa sauti ya chini Neema aliuliza huku akijitahidi asije akaonekana na kina Misholi mule ndani."Nawaona,daah!! Afadhari Diana siku hizi amekuwa na furaha,hichi ndo kitu ambacho tulikuwa tukikitamani,soon hapa tutampata shemeji sasa".Alizungumza Cathe kisha wakatoka pale dirishani kimya kimya.
Sasa Diana huku akimtazama Misholi kwa macho ya huruma alijiandaa kutamka jambo,"Ni...ni....ni...?" Alijaribu kuzungumza Diana lakini akawa anaona kama kinywa chake hakimpi ushirikiano kabisa."Vipi Diana mbona uko katika hali hii nini shida? Au unaumwa?" Aliuliza Misholi,Diana akakataa kwa ishara ya kutikisa kichwa."Ila? Maana nakuona dada yangu ukiwa kama una majonzi vile". Alizungumza Misholi lakini Diana akakataa kwa kusema yupo sawa hana shida yoyote."Niko sawa Misholi,sema we uwe unaniita tu kwa jina la besti hakuna haja ya kuniita dada".Alisema Diana,Misholi akatabasamu kidogo,huyu jamaa mbali na kwamba alikuwa ni kijana mpole lakini saikolojia ya wanawake alikuwa akiifahamu acha kabisa.Mpaka pale yale maneno yake aliyokuwa akiyahisi akaona kama ni kutimia yameshatimia,kilichobaki ni kuyathibitisha tu."Pale mwanzo,besti Diana ulionekana kama una jambo unataka kulisema ila ukaishia njiani,hebu limalizie besti".Aliongea Misholi,Diana akamtazama kidogo akatabasamu kisha akasema "Nilikuwa nataka kusema hivi......kusema hiviii....hebu sogea kidogo nikae ndo nikuelezee vizuri".Baada ya kusema namna ile,Misholi alijisogeza kidogo na kisha kuacha nafasi kwa ajili ya msichana huyu kuketi.
Huku hayo yakiendelea,siku hiyo Yakobo alifunga safari kwa ajili ya kumfuatia kijana wake Misholi dawa za ARV ,,,Na hakuwa akizichukulia ndani ya mji wao wa Nashville,alikuwa akizifuata mji wa jirani mbali kabisa ambapo hakuna hata mmoja angemshtukia au hata kumtambua.Alipanda ndani ya gari yake akapiga mafuta hadi huko,kwani alitumia dakika thelasini hivi akawa amewasili.Alimkuta daktari wake aliyekuwa akielewana nae vizuri kwa mambo yote,wakapiga na stori kadha wa kadha kabla ya kuzichukua dawa zile."Oooh!! Mr Yakobo karibu sana mzee wangu naona mambo si mabaya kabisa".Yule daktari aliyatamka maneno yale baada ya kumuona Mr Yakobo akiingia ndani ya ofisi yake."Ndio Dokta,si unajua ninavyo mkubali jembe langu,huyu ndo anaye niweka mjini namna hii".Alisema Mr Yakobo huku akikaa kwenye kiti."Vipi lakini Misholi anaendeleaje?" Alihoji daktari kwa sauti ya chini huku akigeuka huku na huko."Misholi yupo vizuri kabisa na yupo fiti hana shida yoyote".Alijibu Mr Yakobo."Ila hatima ya maisha yako mzee wangu umeiriski sana,daah,sasa itakuaje,Misholi mwenyewe ndo kama vile,wewe nawe umeamua kujitoa sadaka na kuamua kuwa towashi ,itakuaje sasa mzee wangu?" Aliuliza yule dokta,Mr Yakobo akacheka kidogo."Hapa duniani sisi ni wapitaji tu,hata nikisema nioe na nipate watoto wangu ni sawa na bure tu,kwani siku ya kufa nitatambalizika peke yangu,zingine ni mbwembwe tu.Huyu mtoto wa kaka yangu ananitosha kabisa na hii ni kama sadaka kwangu na kwa maisha yangu".Alijibu Mr Yakobo."Haya bwana,Vipi zile dawa zimeshaisha?" Dokta alihoji kwa mara nyingine."Ndio zimeshaisha na ndio maana nikaja hapa tena kuchukua zingine".Alijibu Mr Yakobo."Sawa haina shida".Baada ya dokta kujibu swali lile alichukua dawa zile kisha akamkabidhi Mr Yakobo."Dokta,mimi naenda tutawasiliana". Alijibu Mr Yakobo akaagana na daktari huyo kisha akaondoka kurudi nyumbani kwake."Duuh!! Huyu mzee sijui amerogwa? Daah haya bwana". Alijisemesha Dokta huku akitikisa kichwa chake.
*************************
Sasa kwa upande wa Misholi na Diana,walikaa pamoja,lakini mara baada ya Diana kukaa huku Misholi akitazamia neno kutoka kwake cha ajabu ni kwamba Diana aliamua kukaa kimya tu huku akiishia kumtazama Misholi.
ITAENDELEA......................................
Tags
simulizi