WIFE MATERIAL 01.
Habari zenu wapendwa wangu ni Mimi mwandishi wenu wa Mikasa ya kweli miriam,nilikua kimya kidogo kukusanya maelezo ya story hii wife material kwa muhusika hivyo naomba support yenu mkasa huu ni mzuri mno na wa kusisimua twende pamoja.
👇👇👇👇👇👇👇👇
Naitwa Freddy ni mtoto wa Kwanza katika familia ya watoto wa tano,Leo hii moyo umenisukuma Sana kuleta kisa changu,naomba tufatane pamoja ili tuweze kupata kitu.
Nimelelewa katika maadili ya kidini sana,familia yetu ni ile familia yenye misingi ya dini sana.siku zote mama pamoja na baba walinisihi kuhusu kusoma kwa bidii na kuachana na Mambo ya kidunia...
Nilikua kwenye misingi hiyo Hadi pale nilipofika kidato Cha tano ndipo nilipoanza kujiona ni mwenye matamanio ya kimwili kutokana na barehe...ila kila nikikumbuka kauli za wazazi wangu niliachana na hisia zangu na kufanya kilichonipeleka shule,
Nilihitimu masomo yangu na kufanikiwa kumaliza chuo,nyumbani kwetu ni jijini mbeya,nilifanikiwa kupata kazi serikalini.
Nilifanya kazi vizuri,lakini siku zote hizo sikuwahi kuwa na mpenzi Wala kushiriki tendo la ndoa.siku moja tukiwa tupo mapumziko kazini Mimi na rafiki angu Abely tulienda kupata lunch.
Tulipofika hotel tuliagiza vyakula na katika mazungumzo yetu abely aliniuliza,hivi fredy kwako unaishi na mpenzi?nilicheka Kisha nikamjibu,hapana rafiki angu.akaniuliza Tena kwanini inamaana Kuna mpenzi kabisa?nikamwambia abely tuachane na hizo habari maana nilikua nikisikia mtu anazungumzia mwanamke Basi naona aibu Sana.
Kesho yake Tena kama kawaida,tukiwa tunapata kifungua kinywa abely alinifata na kuniuliza Tena like swali.nikamwambia jamaa mbona Kama umetilia mkazo Sana swala la mimi kuwa na mwanamke???
Abely alitabasam akashusha kikombe Cha chai chini Kisha akasema, Freddy jichanganye ,mh!!?kujichanganya kivipi?wewe ni kijana na kwa umri wako lazima upate Dem mkali Sana utulie nae,nilicheka Kisha nikamjibu Mimi kuoa kwa Sasa bado Sana kiufupi maisha yangu bado sijajipanga labda hadi nitakapojenga nyumba yangu.
Abely akasema sawa haina shida,Maisha yangu yaliendelea lakin hapo baadae niliona kweli nnahitaji kuwa na mtu,ila kila nilipowaza jinsi ya kumuingia mwanamke na kumwambia kuwa nampenda,nilijikuta nashindwa.
Ilibidi nitoke niende Tena kwa Abely kuomba ushauri,nikamwambia my friend kweli kabisa mie siwez ku aproch mwanamke na sijui maisha yangu yatakuaje,alitabasam Kisha akasema hizo ndo story nnazotaka kusikia kutoka kwako.
Nikamwambia nipange Sasa,akasema Kwan unampenda Nani???nikamwambia Kuna binti mmoja Anauza duka la vipodozi hapo mjini,anaitwa Natasha,akasema oooh wow Yan umelengesha mule mule ila hizi hisia jaman.hivi Freddy utaamini kuwa huyu Natasha ndo mtu nilitaka nikuunganishe nae???
Nikamwambia hapana sijui.akasema Basi ndo ivyo,siku zote huwa nakwambia uoe lkn Natasha ndo huwa ananituma kwako nimsaidie ila huwa naogopa kukuambia sababu haukua tayari.
Nikamwambia Basi sawa,tuweke mipango sawa ya kuweza kuwa nae karibu.kesho yake jioni tulimualika chakula cha usiku Natasha ili abely aweze kutuunganisha.
Tulienda hotel moja kubwa,Kisha nae Natasha akaja,kiukweli niliona aibu Sana nikawa nakosa hata Cha kusema,abely akasema naomba niwaache kidogo nitakuja baadae ili muongee,
Abely aiondoka akaniacha mim na Natasha,niliangalia chini kwa kuona aibu.sikuongea kitu chochote ndani ya dakika tano.natasha akaniambia Freddy usijali nmeshaambiwa Kila kitu na abely mie ni wako kwanzia Sasa mambo yasiwe mengi.
Tags
simulizi