WIFE MATERIAL 02.
Abely alipoondoka niliona aibu Sana,kuongea na natasha,lakin cha kushukuru ni kwamba aliweza kuwa muwazi na kufunguka juu yangu,alisema mambo yasiwe mengi tuanzishe ukurasa wa mahusiano baina yangu Mimi na yeye.tulishikana mikono ikiwa ni ishara ya umoja wetu.
Na huo ndo ukawa mwanzo wa mahusiano yangu na yeye....alionesha kunijali na kunipenda Sana,ikumbukwe tuu sikuwai kuwa na mahusiano hapo nyuma...tuliendelea kuwasiliana kila mtu aliishi kwake,kazi kubwa iliyokuwepo kwangu ni ile nashindwa kumuita kwangu Yani naogopa Sana nitaongea vyote ila ikifika ilo swala domo linakua zito sana.
Nilimgharamia natasha kwa kila kitu nilisimama Kama mwanaume ndani ya miezi mitatu kwenye mahusiano,bila kufanya kitu chochote....nakumbuka ilikua siku ya jumapili sikuenda kazini Natasha alinipigia simu akaniuliza nnafanya nini?nikamwambia nimelala nataka kuamka ili nianze kazi ya kufua,akasema ok!naomba unielekeze kwako nakuja nitakusaidia,nikasema afadhari amesema mwenyewe,sikuchelewa nilimuelekeza Hadi mahali ninapoishi.
Alipanda usafiri akafika kwangu nilitoka barabarani nikampokea,tulifika kwangu akaniuliza fredy unaishi na Nani hapa??nikamwambia nipo mwenyewe vipi Kuna shida??akasema hapana akuna tatizo lolote,isipokua una matumizi mabaya ya pesa umepanga nyumba kubwa Sana alafu unaishi mwenyewe.
Nikamwambia nimefanya hivyo sababu ya ndugu zangu wakija siwez lala nao pamoja walau Kila mgeni alale kwa kujiachia.akasema ok wazo zuri,basi nilitoa nguo zangu nje akasema acha nitakua nafua wewe unaanika.alifua nguo zote mie nikawa naanika,tulipomaliza tukaamia ndani,mie nilifanya usafi wa nyumba nzima yeye nikamuelekeza vitu jikoni akaingia kuanza kupika.
Tulipomaliza tuliketi tukala,nilimshukuru kwa kuweza kunisaidia baadhi ya kazi,tulipomaliza hapo tukawa tumekaa tunaangalia tv.akaama kutoka Kochi moja hadi mahali nilipokaa Mimi alinisogelea akaniangalia usoni huku akitabasam namimi nikatabasamu pia.
Akasema Freddy ni miezi kadhaa Sasa kwenye mahusiano lakini hatujawahi shiriki kitu chochote Cha kutuunganisha sisi.nikamwambia ndio ni kweli.akasema sawa kwaio wewe unalichukuliaje hili swala?
Nikamwambia vyovyote utavyoamua wewe.yani muda huo namjibu lakini moyo wangu unakwenda Kasi Sana sababu ya uoga na aibu.akasema basi sawa,akaniuliza chumba unacholala wewe ni kipi?,nikamwambia Cha mwisho kabisa upande wako wa kulia.akasema sawa twende tukaongee huko.tuliinuka pale Hadi huko chumbani.
Nilimwambia karibu hapa ndo chumba nnachopumzika Mimi.akajilaza kitandani akasema njoo tupumzike,nilipanda kitandani huku naona aibu siamini kabisa kinachoendelea.akaniuliza hivi Freddy wewe una aibu Sana eeee!!!nikamwambia hapana,akasema Sasa mbona sikuelewi upo upo tuu...nilinyamaza kimya nikamsogelea karibu yake Kisha nikamkis ili aone tuu nnajiamini.
Alivoona hivyo akanipa kumbato,ilikua ilivokua tukawa tumeunganisha miili yetu.kwanzia hapo upendo ndani yangu ukawa umezid kufunguka,baada ya kumaliza aliniuliza hiv hii ndo mala yako ya Kwanza?nikamwambia yes!akasema ndo maana ila siku zinavoenda utazidi tu kuzoea.
Hakulala kwangu,aliondoka saa nne usiku,kwanzia iyo siku nilianza kuwa na wivu Sana juu yake,Yani ni mtu ambaye siwezi kukaa masaa sita bila kumuona nitampigia simu mala kwa mala asipopokea naumia sana.aliendelea kunipa huduma za penzi na zingine ambazo mke inabid amfanfanyie mume Kama kawaida.alikua ni mtu ambae akija kwangu anajituma Sana,anafanya kazi kwa bidii anahakikisha Mimi ni msafi muda wote.
Pendo liliponizidia nikasema hapana uyu naoa,anasifa zote za *wife material* ,lakin kabla sijamwambia chochote alisema mwenyewe,baby Mimi sitaki kuendelea kukaa mwenyewe nahitaji kuja kukaa na wewe huko nikamwambia sawa Haina shida.
Alikua amepanga chumba kimoja aliruhusu chumba na vitu vyake vyote alipeleka kwao.akaja tukawa tunaishi huku anaendelea na kazi ya kuuza vipodozi kwenye duka boss wake,ilienda hiyo Hadi pale aliponiambia babe najihis mchovu Sana siku hizi naumwa mala kwa mala kizunguzungu Cha hapa na pale.
Nikamwambia sawa pole mke wangu naomba asubuhi uwahi hospital ukapate matibabu.akasema sawa.asubuhi nilienda kazini niliporud jioni ananiambia Freddy nna ujauzito.
Tags
simulizi