WIFE MATERIAL 04.
WHATSAPP 0755184460
Waliendelea kuchart Natasha na rafiki yake,rafiki yake akamwambia siku zote uongo hutengana na ukweli ipo siku utabainika.
Lakin Natasha alidai kuwa awez kugundulika.Rafiki yake akamwambia siku zitapoenda utamueleza nin akigundua kuwa Mimba huna???akasema kwamba awez kugundua nataka nijifanye imetoka bahati mbaya najua ataniamini.
Rafiki yake aliguna tu mhhhh!!!!sawa bwana unachokitafuta utakipata.huo ndo ukawa mwisho wao wa kuchart na walichat usiku wa kuamkia siku iyo,inamaana kabla atujalala ndo alikua akiwasiliana na rafiki yake.
Nilijawa na jazba.nikamuangalia usoni Natasha,nikasema hapana Natasha sio wa kunifanyia hivi.inamaana kumbe mimba Hana???hii aiwezekani.kwanini ameamua kunifanyia hivi?mbona ninachoamini ni kwamba ananipenda Sana sasa imekuaje??
Nilijiuliza maswali mengi ambapo nilikosa majibu kabisa kiukweli,niliamka nikaenda kuoga nilijiandaa nikasema nisimwambie kitu chochote ili nikamueleze rafiki yangu abely mambo ya Natasha alionifanyia.
Nilipomaliza kujiandaa nafsi ilisema hapana huyu lazima ajue hili swala kabla sijaondoka.ilinibidi nimuamshe alipoamka nikamuuliza Natasha nataka kujua asha ni Nani???Kwanza alishtuka Sana akasema amefanyaje?nikamwambia nimekuuliza naomba unijibu.akasema ni rafiki yangu nilisomaga nae primary ila kwa Sasa yupo dar.
Nikamwambia ok! ndo ukaamua kunidanganya kuwa una ujauzito kumbe huna?Natasha kwanin umeamua kunifanyia hivo?alipigwa na butwaa akaanza kutetemeka.nikamwambia naomba unijibu basi.akasema ni kweli baby mimba ninayo huoni inavonipelekesha?
Kinachonifanya nimuongopee asha ni mtu ambae anapenda Sana kunifatilia maisha yangu.ndio maana nmemwambia hivyo.nikasema ok jiandae naenda kazini kuomba ruhusa naenda kununua kipimo nakuja kukupima mwenyewe hiyo itakua aitoshi baada ya hapo nitakupeleka hospital kwenda kupima.akasema sawa siwezi kukupinga Freddy.
Niliondoka Hadi kazini nikiwa nimevulugwa nikasema kama kweli Hana kulikua na sababu gani ya kunidanganya?niliona navulugwa sana,nilimuita Abel nikamwambia my friend Natasha ameni disappoint pakubwa sana....akaniuliza imekuaje?nikamueleza kila kitu.akasema usifanye Mambo kwa haraka,tuliza moyo mfatilie vizuri hata mienendo yake.
Nikamwambia sawa best unaweza kunishikia vipindi vyangu vya mchana hapa kazini ili Mimi nimuwai nataka kwenda kumpima.akasema hapana mie sipo vizuri kiafya leo sitaweza kumudu.nikasema sawa.ilipofika mida ya kufundisha ilibidi niingie class nikafundisha wanafunzi wangu maana nafundisha form2 na form4 masomo ya sayansi.
Nilipomaliza tu nikaondoka kabisa eneo la kazi nilipofika kwangu nimekuta geti lipo wazi lote,nikaingia nikafunga.naingia sebleni nakuta seble ipo tupu inaniangalia...nilishtuka kidogo,nikasema inamaana Natasha ameamua kuama bila kunishirikisha???
Naingia dining akuna kitu naenda jikoni akuna kitu niliisi kuchanganyikiwa.naenda chumbani kwangu hakuna kitu Hadi nguo zangu zimebebwa,miguu iliisha nguvu nikakaa chini nikampigia simu Natasha alipokea nikamuuliza uko wapi?akasema nipo nyumban baby nikamuuliza nyumban wapi?akasema kwako.nikamwambia mbona hapa haupo?akasema nimeshamaliza kilichokua kimenileta Kisha akakata simu.
Hivi inamaana kumbe uyu mwanamke kwangu alifata Mali?nilitoka pale nikaenda chumba kimoja cha wageni nilikuta begi ninaloifadhia vyeti vyangu vyote vya masomo lipo chini.maana Hilo ndo muhimu.nililikagua nikakuta vyeti vyangu vyote vipo salama.nikasema afadhari.napiga jicho pembeni nakutana na karatasi,nikaiokotana kuanza kupitia yale maandishi.
*Wako Natasha,*
*Pole kwa kila kitu nilichokufanyia fred.kiukweli sikuwai kukupenda maishani mwangu,siku zote niliforce tu kuwa na wewe lakini nilijitahidi Sana usiweze kujua kuhusu ilo Jambo.*
*Sasa ni wakati sahihi wa Mimi kuondoka na kukuacha na maisha yako.kwakua ulinitumia kwa muda nisingeweza kuondoka hivi hivi,nimebeba vitu vyote viwe Kama fidia ya kunitumia siku zote.*
*Nilikudanganya kuwa ni mjamzito ilimradi niwe karibu na wewe unifanyie Mambo makubwa pia uniamini.kiasi nilichokipata katika kabati kinaweza kwenda kunifanya niishi vizuri na nimpendae huko mbele ya safari.nakutakia maisha mema stay blessed.*
Hapo ndo ulikua mwisho wa barua ile lakini ndo nikakumbuka kuwa ndani nilikua nna akiba ya milion 1 na laki 5.kumbe alizibeba.nilitoka nje ya myumba,sikutamani Tena kuendelea kuishi pale,nilimpigia simu Abely nikamueleza mkasa wote kwa yalionikuta.alisema nimsubili anakuja.zilipita Kama dakika kadhaa nilimuona abely amefika akaniliza ticha vipi?nikamwambia ndo Kama nilivokueleza.akasema ebu ngoja nihakiki.aliingia ndani baadae akatoka
,akassma kumbe huyu mwanamke ndo mjinga kiasi hichi.kwa yote uliomfanyia upendo uliompa lakini haya ndo majibu yake.nikamwambia ndo ivo.akasema cha kufanya twende tukatoe taarifa police.nikasema yes wazo zuri.tulienda Hadi police ilimrad lolote litalomkuta huko Mimi wasinihusishe.
Tulienda police tukatoa riport wakat tunarudi njiani nikapata wazo la kwenda kwa wazazi wake pengine amekimbilia huko.nikamwambia abely ebu twende kwao kwanza.akasema hapana tusiende uyo atakua njama moja na wazazi wake unaweza kuitiwa hata mwizi.nikasema sawa tu liwalo na liwe.akanisihi Sana nisiende,nilirud kwangu nikachukua kibegi changu cha vyeti nikampigia mwenye nyumba kuwa nimeama akaangalie nyumba yake.
Nilienda kwa abely ambae yeye alikua ameshaoa na ana mtoto mmoja.abely alisema kaa hapa Hadi mshahara utapotoka ndo utafute nyumba ununue vitu ukapange.nikasema sawa.usiku huo sikulala kabisa niliwaza mengi mno.lakini nafsi bado ilinisukuma kwenda kwao.
Asubuhi ilifika ambapo ilikua jumamosi sio siku ya kwenda kazini.nilinawa tu uso hata chai sikunywa nikamwambia abely kuna mahali naenda sitachelewa Sana kurudi.
Nilitoka pale moja kwa moja Hadi kwao kwa kina Natasha nilikuta wadogo zake na mama yake.alinipokea vizuri sana.huku akiniuliza Kama Natasha ajambo.niliishia kutingisha tu kichwa.nilipoulizwa nikasema mama mwanao ametoroka na vitu vyote,akaniuliza shida nini au mligombama???nikamwambia hapana mm nimeishi na Natasha Kama malaika atukuwai kutofautiana hata siku moja.
Nikamueleza mkasa wote jinsi ilivokua.nikamwambia naweza kumpata wapi?yule mama aliinama chini Kisha akasema kijana mie Hadi nakuonea aibu.nikamwambia kwanini mama?akasema naomba nisamehe sana,Natasha sio mwanangu ni mtu ambae tumejuana ukubwani/kimjini mjini na aliniambia anakuja kukutambulisha kuwa Mimi ni mama yake lakini ukweli ni kwamba hata familia yake siijui kabisa....
.
ITAENDELEA.....
Tags
simulizi