TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

WIFE MATERIAL 03

WIFE MATERIAL 03.
WhatsApp:0755184460
NIliporudi kazini jioni Natasha alinipokea na kuniambia kuwa baby nna ujauzito.aisee hizo zilikua ni taarifa nzuri Sana kwa upande wangu.nilifurahi sana,ule  upendo niliona sio kitu kwake nilitamani nimfanyie atakacho ilimradi afurahi.

Nilimuuliza unapika nini usiku huu?akasema anataka kupika ugali nilimwambia hapana,acha nakutoa nje ya nyumba uende ukale kitu utachokipenda.alijiandaa tukatoka.

Nilimpeleka sehem nzuri na tulivu.nilimuagizia chakula kizuri sana,nikaanza kimwambia mke wangu usitoe mimba yangu,nitafurahi Sana siku nitayoitwa baba,aliniangalia Kisha akasema,Freddy sijalazimishwa na mtu kuwa na wewe hata kuzaa pia sijalazimishwa ni upendo wangu tu kwako ndo umenisukuma.

Nilimshika mkono nikamkiss nikamwambia sawa nafurahi kuwa nawe.natasha your my life.nataka nikuoe,akasema nitafurahi Sana siku ukinivalisha Pete.

Nikamwambia sawa Sina muda wa kupoteza nataka nikutambulishe nyumbani wote wakujue wewe ni Nani alafu mipango mingine iendelee.

Vipi kuhusu dini?akasema dini sio shida kwake atanifata tuu mimi.nkamwambia sawa.tulifurahia muda wetu mahali pale Kisha tukarudi nyumbani.kesho yake sikutaka kusubiri nilianza kuwapigia ndugu wa karibu wote na kuwapa taarifa kuwa nimepata ubavu wangu nahitaji kuoa.kwa upande wa mama ni alifurahi Sana tuu.wakasema kuwa wanahitaji kumuona.

Niliwaambia likizo ikifika nitampeleka...nayeye alisema anaumwa mala kwa mala hivyo awezi kuendelea na kazi.nilimwambia pumzika tu mke wangu nitakuhudumia.basi nimlimuhudumia vizuri siku zote ndugu zake walinijua ikiwemo dada na mama yake.

Ilipita miezi mitatu ya ujauzito nilimwambia twende ukaanze clinic aliniambia kuwa ataanza tu muda ukifika hataki kuwai sana.

Siku zilienda nikiwa nasubiri likizo ya kazini ifike ili twende mbeya kwa wazazi,maana walikua wakimsubiri kwa hamu Sana.
B
Siku iyo ilikua ni alfajiri Sana mida ya saa 11.nilishtuka usingizini,nikachukua simu yake na kuangalia saa,nikagundua kuwa bado akujapambazuka vizuri.nilichukua simu yake na kuanza kuikagua bila sababu yoyote ya msingi.katika kukagua moyo ulishtuka Sana nilipoona Natasha anachart na rafiki yake,mazungumzo yao yalikua hivi:

Shoga ake:Natasha una hatari Sana wewe umemdanganya kaka wa watu akijua itakuaje??

Natasha:atajua Nani atamwambia??

Rafiki ake:siku zote uongo nikama mafuta na   ukweli ni kama maji hivi vitu ukivichanganya kwa pamoja lazima vitajitenga hata hayo unayofanya Leo shoga ipo siku utajulikana tuu.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post