TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA NAZI

Mahitaji 
Nazi 
Maji

Njia ya Kwanza

Chukuna nazi iliyokomaa sio zile changa.
Kuna nazi kwa kutumia njia yeyote uliyonayo kama una mbuzi, food processor, blender, grater au grapefruit spoon.
Baada ya hapo changanya na maji ya baridi halafu kamua kwa kutumia cheese cloth au chujio  kama unalo kuoata tui la nazi.
Weka katika chupa yenye mdomo mpana na uiweke itulie kwa masaa 24. Au weka kwenye fridge. 
Toa mapovu ya juu. Toa mafuta ya katikati weka kwenye chupa nyingine ambayo ndio utayatumia.  maji yanayobakia mwaka chini mwaga.

Uzuri wa kutumia njia ya maji ya baridi ni kuwa mafuta yanakuwa na virutumisho vyake vyote lakini hayakai muda mrefu. Huwa yanaharibika mapema sana.

Njia ya pili

Chukua nazi iliyokomaa sio zile changa
Kuna nazi kwa kutumia njia yeyote uliyonayo kama una mbuzi, food processor, blender, grater au grapefruit spoon. 
Chukua maji ya vuguvugu halafu changanya na nkikono yako kwa dakika moja hivi
Kamua kwa kutumia chujio la nazi au cheese cloth. Unaweza kurudia mara kadhaa kuweka maji ya vuguvugu ili kutoa mafuta yote
Ukishapata tui  weka katika chupa na kuiweka masaa 24 ili mafuta yajitenge na maji. Au unaweza weka jikoni (medium heat) kwa muda wa saa moja au mpaka maji yameondoka na iliyobakia ni mafuta. Toa mapovu ya juu halafu weka mafuta yako katika chupa utakayotumia.

Njia ya tatu 
Chukua nazi iliyokomaa sio zile changa
Kuna nazi kwa kutumia njia yeyote uliyonayo kama una mbuzi, food processor, blender, grater au grapefruit spoon. 
Weka nai yako na maji katika jiko (medium heat). Chemsha mpaka uone mafuta yanatokea juu
Ondoa kwenye sufuria. Tumia kijiko kutoa mafuta na kuweka katika chupa yako

Njia ya nne
Chukua nazi iliyokomaa
Iache mpaka iharibike
Baada ya hapo toa nazi na usiwekek kwenye blendder, food processor  ili iweze kulainika
Chukua maji ya vuguvugu na kukamua tui
Chemsha tui na mchai chai pamoja mpaka uone mafuta yanabakia
Ondoa majani na kutoa mafuta yako na kuyaweka kwenye chmbo chako ili utumie

Njia hii inakufanya uweze kupata mafuta mengi zaidi na pia mchai chai unamanufaa sana katika kufanya mwili uwe unarelax sasa ukichanganya wakati wa kuchemsa utaweza kupata virutumisho vyingi zaidi.


Kuweka harufu katika mafuta yako ya nazi
Chukua safuria kubwa weka maji na kuyaweka kwenye moto. (medi-High). 
Chukua sufuria ndogo weka mafuta yako ya nazi. 

Chukua mchai mchai (green tea. Changanya kwenye mafuta yako. 
Weka safuria ndio juu ya safuria yenye maji na kupika kwa muda wa dakika kama 30 hivi.
Ondoa majani na weka mafuta yako kwenye chmbo cha kutumia.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post