je Umekuwa Ukikumbwa Na Hofu Maishani Mwako? Hizi Hapa Ndizo Sababu Ambazo Hupelekea Hofu...
________________________
Sehemu Ya Pili...
Makala iliyopita ilidokeza hoja tano kuhusu sababu za hofu!
Makala hii ni mwendelezo wa makala iliyopita...
Kwa leo nitadokeza hoja nyingine tano zinazodokeza sababu za watu kuhofu!
Karibu sana ufuatilie makala hii...
6. Kukosa Imani Na Mungu…
Watu wengi wanamwabudu Mungu lakini ni watu wachache sana wanamwamini Mungu kwamba anaweza akatenda.
Sasa kama kwake Mungu kila jambo lawezekana ni kipi kitakuwa dhidi yako kikutie hofu endapo utamwamini yule wa yawezekanayo?
Mtu ambaye ana hofu kuna wakati anakuwa amekosa Imani na Mungu akaamua kutumainia akili zake pamoja na njia zake zenye ukomo, mwisho wa siku yanamshinda anaanza kuhofu na kujihisi mnyonge. Mithali 3:5-6 Neno la Bwana linasema,
“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako mkiri yeye, naye atanyoosha mapito yako”
Friend mpe Mungu nafasi katika maisha yako, ndiyo maana unafundishwa uenende kwa imani na siyo kwa kuona kwa maana ukienda kwa kuona utaanza kuhofia.
Kuna mambo mengine kibinadamu hayawezekani lakini kwake Mungu yanawezekana.
Hivyo basi unavyoamua kumuacha Mungu na kuamini akili zako zenye ukomo maana yake unakuwa umeamua kuhofu.
Kwa maana yatakushinda nawe utaanza kuyahofia.
Kuna wakati mwingine siyo kwamba unahofu kwa sababu unatakiwa uhofu ila ni kwa sababu umeacha chanzo chako (Mungu).
Kumbuka hata mto ambao haukumbuki chanzo chake utakauka muda siyo mrefu.
7. Taarifa Zinazovuma Kila Siku…
Habari zinazotangazwa kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii, huweza kusababisha watu wengi watengeneze hofu kwenye fahamu zao.
Ubaya zaidi ni kwamba habari mbaya huvuma zaidi na hutangazwa zaidi kuliko habari njema.
Kutokana na hilo wengi hujikuta wakiingiwa na hofu kutokana na habari zilizotangazwa.
Kwa mfano utakuta wachambuzi wanakuja na takwimu zinazoonesha kwamba kutakuwa na anguko la uchumi miaka kadhaa ijayo, au watakuja na takwimu inayoonesha kuwa kati ya ndoa kumi ni ndoa moja tu huwa na amani.
Au watakuja na takwimu zinazoonesha kwamba kutakuwa na mlipuko wa ugonjwa Fulani ambao utaua watu wengi sana na hauna tiba.
Vilevile wanaweza kuja na ripoti inayoonesha kwamba, kutakuwa na hali mbaya ya hewa hivyo watu wanatakiwa wachukue tahadhari mapema.
Uvumi wa taarifa hizo huathiri mfumo wa ubongo kufanya kazi na kumuacha aliyesikiliza abaki mdomo wazi huku ajiuliza itakuwaje sasa?
Mwisho wa siku ataanza kuhofu kutokana na habari alizosikiliza…
Na, hii ni kwa sababu ubongo wako huwa unakuwa na ajenda moja tu yaani wewe uishi, hivyo basi endpo matumaini ya kuishi yatakuwa hayapo, ubongo wako utashindwa kufanya kazi vizuri na kanza kukutengenezea hofu…
Mwisho wa siku utajikuta ukingia kwenye na kupoteza kabisa matumaini…
8. Umaskini/Hali Ngumu Ya Maisha…
Hii inatokea pale ambapo mtu hana tumaini lolote lile lililo jema kuhusu maisha yake ya sasa pamoja na kesho yake.
Labda kipato chake ni cha chini sana, yamkini hana kazi ya kumuingizia kipato, yamkini biashara yake haifanyi vizuri na huenda akawa hana matumaini yoyote yale kuhusu kesho yake.
Kwamba akiangalia pale alipo hana tumaini, hata hivyo akiangalia kule anakotakiwa afike ndiyo kabisa anakufa moyo na hajui hata afanye nini.
Mwisho wa siku fahamu zake zinafungwa na akili yake inaanza kumtengenezea hofu hali ambayo itamfanya ashindwe kuchukua hatua stahiki.
Unachatakiwa kujua ni kwamba hofu humuua kabisa yule mwenye kuihifadhi pamoja na kumfanya akate kabisa tamaa.
Na, ndiyo maana kuna watu wengine utakuta hali zao ni ngumu, na hawafanyi chochote kile.
Hali hii imechangiwa na hofu ambayo imewafunga fahamu zao na kuwafanya washindwe kufanya mambo ya maana yanayoweza kuwatoa pale na kuwapeleka hatua nyingine…
Hii ni kwa sababu hofu imeua kabisa ule uwezo wao wa kufanya mambo yatokee.
Kutokana na hilo watu hawa hukaa tu huku wakisubiri mambo yakae sawa badala ya kuweka mambo yawe sawa.
9. Kukosa Imani Na Uwezo Wake…
Mathayo 21:21
Yesu akajibu, akawaambia, “Amini nawaambia: Mkiwa na Imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mtini huu: Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka”
Mtu mwenye hofu wakati mwingine huwa haamini uwezo wake, badala yake anakuwa anatilia shaka juu ya kile anachoweza kufanya.
Kuna watu ambao wana uwezo mkubwa sana ndani yao sema changamoto yao kubwa ni kwamba hawaamini katika uwezo wao hali ambayo imewafanya wabaki na hofu maisha yaao yote.
Unachotakiwa kujua ni kwamba usipouamini uwezo wako hakuna atakayekuamini.
Sasa mtu mwingine atakuaminije ilihali wewe mwenye suala lako hujiamini.
Friend unatakiwa uamini katika uwezo wako kwa maana ni kupitia kutumia uwezo wako ndipo utaweza kufanikisha safari yako.
Kwa mujibu wa tafiti za kisaikolojia zimeonesha kwamba kila mwanadamu ndani yake kaumbwa na uwezo mkubwa sana wa kufanya jambo Fulani, hata wewe umeumbwa na uwezo huo.
Badala ya kuamua kuhofu tafuta namna sahihi ya kuutumia uwezo wako ili ukunufaishe.
Amini katika uwezo wako, ndani yako unamiliki mgodi wenye thamani sana hutakiwi hata kuthubutu kuwa na hofu…
10. Kutokuwa Na Utaratibu Wa Kujiwekea Malengo…
Hakuna mtu ambaye huwa anakuwa na amani akiwa kwenye safari ambayo hata haijui vizuri.
Kwa mfano tufanye upo safarini lakini safari yenye huijui ipoje, hujui njia ya kupita, na hujui hata hatima yake itakuwaje.
Hebu jaribu kuvuta picha amani utaipata wapi?
Kwenye maisha watu wengi wana hofu siyo kwa sababu wanatakiwa kuhofu ila ni kwa sababu hakuna chochote walichokikusudia kukikamilisha katika maisha yao.
Kukosa malengo katika maisha ni moja ya sababu ambayo huwafanya watu wengi waweze kuhofu, kwa maana hata wakipambana hawajui mapambano yao yataleta nini.
Na, kama utakuwa unapambana huku ukiwa hujui matokeo mazuri yatakayotokana na mapambano yako utaishia kukata tamaa mwisho wa siku utaanza kuhofia kuhusu kesho yako.
My friend, kesho haiogopwi bali inatengenezwa, itengeneze kesho yako kwa kuiwekea malengo mahususi.
Je Ni Nini Madhara Ya Hofu?
Usijalii Kesho Litajadiliwa hilo!
Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya Mazuri!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; Mwl Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza Kuwasiliana Nami Kupitia Whatsapp No +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com
Tags
Elimu