TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

MAMA ONGEA NA BINTI YAKO

MAMA ONGEA NA BINTI YAKO
1. Mama mwambie binti yako uzuri, elimu kubwa na kipato kikubwa ni neema tu wala asiwe na kiburi cha kutomheshimu mwenza wake. Mwambie kuwa mwanamke anayeweza kufurahia neema zake na mwanaume wake kwa upendo bila kinyongo analo pendo la dhati ndani mwake.

2. Mama mwambie binti yako, dada wa kazi atakayeishi naye hapaswi kifua nguo za ndani mume au zake. Hizo azifue yeye na mashuka watuamiayo usiku yasiguswe na dada wa kazi (kwa dada wa kazi ni najisi). Aheshimu utu na staha ya dada wa kazi na aishi naye kwa wema.

3. Mama mwambie binti yako kitanda hakitandikwi na dada wa kazi wala usafi wa chumbani haufanywi na dada wa kazi. Hilo so jukumu lake.

4. Mama mwambie binti yako nguo za mume zinaandaliwa na yeye si dada wa kazi wala chakula alacho mume hakipakuliwa na dada. Yeye anapaswa kujua chakula cha mume wake hata kama hajapika anapaswa kukihakiki.

5. Mama mwambie binti yako, kuzaa ni jambo moja ila kumwachia JUKUMU la kulea watoto wa kazi ni ujinga wale ni watoto wake. Atenge muda wa kuwa mama kwa watoto, awaogeshe na ale nao pia asiache kuwasikiliza.

6. Mama mwambie binti yako ajue kuficha nguo zake za ndani, anaishi na familia ya watu asianike nguo zake za ndani kama aanikavvyo gauni zake ajifunze kuzifunika na nguo kwa juu.

7. Mama ongea na binti yako, mwanaume ndiye kichwa cha familia aheshimu na alinde heshima na statusa yake.

8. Mama ongea na binti yako, akubali kuwa mshirika wa imani ya mume (wasali pamoja) hakuna ndoa iliyo bora ya watu wanaosali kila mtu kivyake) akubali kubadilisha dhehebu lake ili wawe wamoja katika ushirika asiwe mpumbavu katika hilo. 

Mimi naishia hapa yako mengi utaongeza na wewe uonayo yafaa kwa binti yako.

Kaka Milton Tunge
0676151067

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post