SIFA YA HEDHI BORA YA MWANAMKE.
Hedhi ni kipindi maalumu katika mzunguko wa siku za mwanamke mwenye umri wa kuzaa. Hedhi bora ni dalili ya afya njema ya uzazi. Kama wewe ni mwanamke na utaona kuna kitu hakipo sawa katika hedhi yako ni vema uwahi kupata msaada ili kuboresha afya yako ya uzazi.
*𝙯𝙞𝙛𝙪𝙖𝙩𝙖𝙯𝙤 𝙣𝙞 𝙨𝙞𝙛𝙖 𝙯𝙖 𝙝𝙚𝙙𝙝𝙞 𝙞𝙡𝙞𝙮𝙤𝙗𝙤𝙧𝙖:*
1️⃣. Hedhi ilibora hupatikana mara moja kwa mwezi yaani kama mzunguko wako ni siku 28 basi hedhi yako itapatikana kila baada siku 28. Kama hedhi haitabiriki ujue kuna shida ambayo unapaswa kuitatua ili upate hedhi iliyobora.
2️⃣. Hedhi iliyobora haiambatani na maumivu makali, kwa kawaida maumivu ya hedhi hayapaswi kumfanya mwanamke kuacha kufanya shughuli zake za kawaida. Kama unapata maumivu makali sana wakati wa hedhi kiasi cha kushindwa kufanya kazi zako za kawaida basi ujue hedhi yako ina shida.
3️⃣. Hedhi iliyobora hupatikana siku tatu mpaka saba. Katika mzunguko wa mwezi siku za hedhi zinapaswa kuwa tatu mpka saba. Chini au zaidi ya hapo ni ishara ya hatari katika afya yako
Tags
AFYA