GAIDI MWENYE MOYO WANGU
1-5
________________________________________ KARIBU.
Brendaaaaa!!!!! Iliita sauti moja ya kizee na kumsukuma binti mmoja kutoka juu ya ghorofa huku yeye akimaliziwa na risasi za kutosha mwilini mwake.
"Aaaaaaahhhhh" kelele za wanawake zilisikika sasa baada ya mtu kutua mzima mzima kwenye swimming pool.
"Kuna nini??"
"Jamani kuna nini?"
"Tunapaswa kuondoka hapa dili limesha haribika" Alexia alimwambie Issan ambaye ni muuwaji mwenzake waliomkosa kosa Brenda na kumuuwa baba yake tu.
Alexia alijifanya ametoka uwani huku Issan akiwa kama muhudumu aliyekuwa amefuata vinywaji ndani.
"Brenda" aliita Fredy Sumaye baada tu ya Brenda kutolewa kwenye swimming pool akiwa ameshazimia.
"Iteni ambulances!!!
"Brenda" alizidi kumtikisa na Issan aliondoka baada ya kuona hakuna nafasi ya kumuulia pale.
Gari lilifika likiwa na kijana wake mmoja ambaye pia ni mtaalamu wa I.T
Waliingia ndani ya gari na Issan alianza kupunguza nguo zake akitoa Tai.
"Vipi una hofu kama amekuona?" Aliuliza Alexia
"Siyo nina hofu ni kwamba ameniona maana alikuwa mbele yangu, Sharukh utafuatilia wapi atakapokuwa amelazwa unijulishe kesho niende nikamalize kazi yangu"
"Sawa Boss" alijibu Sharukh mwenye asili ya kihindi.
🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼 🥷🏼
Palipambazuka asubuhi na milio tu ndani ya chumba alicholazwa Brenda ndiyo ilisika.
Mipira ikiwa kwanzia puani kwake kumuwezesha kupumua , mkononi mwake akiwa na kifaa cha presha na drip ya maji.
"Hali ya Mjomba wangu ni vipi?" Aliuza Bwana Modest Sumaye.
"Aammmhh Brenda amepata koma"
"Whaaat?" Aliuliza kwa mshtuko na kumfanya ainuke alipokuwa ameketi.
"Amepata koma? Aliuliza Mama yake Brenda akishangaa.
"Ndiyo ni kwamba siyo koma kama koma hapana ila ni kama ubongo wake ume freez na hatujui utafanya hivyo kwa muda gani, tutamuacha hapa kwa muda wa wiki moja tukizidi kufanya vipimo zaidi kama kuna lolote litaendelea tutawajulisha"
Yalikuwa majibu ya Dr yaliyoweza kunyong'onyeza mioyo ya wapendwa wa Brenda isipokuwa nyumba aliposimama mtoto wa mjomba wake Brenda. Wengaa yeye alionyesha kutabasamu.
Nyuma ya Wengah alisimama Issan aliyevalia koti la ki daktari na baada ya kusikia habari hiyo hakuona haja ya kwenda kumuuwa tena Brenda.
Aliondokea hapohapo huku akivulia nguzo zile za Dr akiwa anashuka ngazi badala ya kutumia lift ya hospital.
Alitupia koti lile pahala ambako ulikuwa mwili wa Dr Halisi aliyekwisha mzimisha na kwenda kwenye gari.
"Vipi Boss?" Aliuliza Sharukh
"Yuko kwenye koma , hatuna kazi naye" alijibu Issan na kuketi vyema kisha akafungua friji iliyopo ndani ya gari na kutoa kinywaji alikifungua na kuanza kunywa.
Wakati yeye akijiaminisha hilo huku Brenda alifumbua macho yake katika hali ya ajabu na kuanza kutikisika mwili wake.
"Dr!!!!!" aliita Nesi Aliyekuwa ndani kwa wakati huo .
Dr aliita kwa nguvu na zaidi na kutoka njee ya chumba hadi kufanya Dr aliyekuwa akipita pale akimbilie ndani.
"Nini kimetokea?" Aliuliza Bibi yake na Brenda waliopenda kumuita Madam Suuh.
"Sogeza hiyo mashine" alisema hilo Dr Lulu akimuagiza nesi huku akitizama macho ya Brenda aliyetulia ghafla.
"Anakuwaga na kifafa?" Aliuliza ndugu zake.
Mjomba wake alimtizama Mama yake na Brenda aliyekataa mwanaye hana kifafa.
"Hanaaa!!" Alijibu Mjomba Fredy na kusogeza hatua zake zaidi.
"Dr mashine......
"Acha, alitizama namna mapigo ya moyo yanavyoenda kwenye mashine na kumtizama Brenda ambaye bado hakuwa na faham zake.
Walirudi tena ofisini kwa Dr Lulu
"Aaammm nadhani nahitaji kumfanyia uchunguzi zaidi leo na kesho kisha keshokutwa mtafuata majibu"
"Ulisema ana kifafa?" Alihoji Madam Suu ambaye umri wake ulisha sogea na alikuwa akitembelea fimbo kwaajili ya kumsaidia kutembea.
"Ni hisia zangu tu kama Dr pia yawezekana akawa amepata kifafa badala ya koma kama tulivyo tarajia ila naomba mje kesho kutwa kwaajili ya majibu yanayo eleweka"
Madam Suu alimkata jicho mama yake na Brenda ambao hazikuwahi kuivaa tangu aolewe na mwanaye.
Susan anafaham tabia za mkwe wake huyo hivyo alibaki kimya tu.
Fredy Sumaye aliweka mikono yake mfukoni huku akionekana kutafakari jambo kidogo kwa kina simu yake ili vibrate na alipotizama alishtuka na kuwatizama watu kama wanamtizama alipogundua bado wako busy kum hoji hoji maswali Dr Lulu basi aliondoka na kutafuta kona yake moja.
"Halooo!!! Najua umemaliza kazi yako unanidai nitakulipa usinipigie pigie simu kwanza hata kazi yenyewe hujaifanya kwa usahihi na unanisumbua tu nitakutumia hela yako kata simu"
Alikata simu mwenyewe na kupepesa pepesa macho yake huku na kule
"Uuuuhhhhh" alishusha pumzi ndefu na kusema
"Huu ndiyo ulikuwa wakati sahihi wa kuiba pesa lakini namna tu ambavyo Mungu hayupo upande wangu kamfanya Brenda awe kwenye koma ili tu nisipate pesa ya kulipa madeni yangu"
🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼
"Embu fuatisha hichi kidole" Dr Lulu alimtaka Brenda afuate namna kidole chake kinavyo enda baada ya kukaa miezi miwili hospital na hatimaye faham ilimrudia akiwa hana baadhi ya kumbukumbu.
"Ok Brenda umefanya vizuri, Dr Lulu alichukua picha yake yeye mwenyewe na kumuonyesha
"Unamfaham huyu?"
"Ni mimi Brenda"
"Na huyu?"
"Bibi yangu Madam Suu"
"Vizuri na huyu?" Dr Lulu alitoa tena picha nyingine ya mama yake na Brenda na Brenda aliishia kuitizama ile picha kwa muda kidogo.
"Mama yangu? Aliuliza.
"Una uhakika?"
"Hapana" alijibiwa Dr Lulu
"Sawa na huyu Je?" Alionyeshw picha yake baba yake na kilichofuata na milio mfululizo ya risasi kichwani mwake iliyoanza kumpa shida na kujikuta alitikisa tikisa kichwa chake huku akiweka mikono yake kichwani.
Basi.... basi... usifikirie sana acha.
Dr Lulu alimgeuka officer aliyekuwa akisimamia kesi ya kuuwawa kwa Mr Modest na kumpa ishara ya kuwa hatapata chochote kwasasa.
Officer Tilya alikubaliana na majibu ya Dr na kwenda njee, wakati huo huo nao Madam Suu aliingia akiwa na mkwe wake Susan aliyeyabeba mauwa.
"Fredy nilikwambia nini kuhusu askari wa polisi kuja kumuona mjukuu wangu?"
"Madam Suu nilihakiki...... kabla hajamalizia neno lake aligongwa na mkongojo mguuni mwake kwa kidole chake cha gumba na kubaki akiguguma tu.
Huyu ndo Madam Suu umri umeenda lakini korofi sana.
"Officer" alimuita askari yule
"Ndiyo Madam Suu"
"Hivi huo muda mwingi mnao utumia kuja kumtizama mjukuu wangu alioko kitandani kw zaidi ya miezi miwili si mngemshapata muuwaji?"
"Madam Suu tunafuata Protocol za ki askari na kama unavyofaham hakuna shahidi mwingine aliyekuwa eneo la tukio zaidi ya mjukuu wako"
"Kwahiyo asingekuwepo kabisa shida kesi mngeifuta na kuifunga sindiyo? Kama hamuwezi kutafuta ushahidi ninyi binafsi kuna haja gani ya kuwa na askari wa polisi....
"Mama" aliita Susan
"Kelele muuwaji wewe" alijibu Madam Suu na kupiga chini kwa nguvu mkongojo wake.
Susan alirudi nyuma tu na kunyamaza
"Kwasasa namshughulikia mjukuu wangu, akikaa sawa nitaihamisha kesi yangu na kupeleka kwenye sekta za watu binafsi wanajua namna halisi ya neno mteja siyo nyie wala kodi zetu za bure"
"Madam Suu unalikosea heshima jeshi la polisi"
"Heshima imeanza kunikosea hilo kesi miezi 2 hamna lead yoyote ya nani kamuuwa kijana wangu? Kaa mbali na mjukuu wangu" Madam Suu aligonga fimbo yake chini na hiyo huwaga ni kawaida yake kila mara anapozungumza kwa msisitizo.
Aliingia ndani ya chumba alicholazwa mjukuu wake na alishangaa baada ya kumkuta amekataa.
"Heeeee!!!! Alipiga makofi na kuangusha fimbo yake kisha akamfuata Brenda.
"Mjukuu wangu jamani"
"Madam Suu!!" Aliita Brenda na kumkumbatia bibi yake kwa furaha.
"Oooohh Modest weeeee, bora hata hujaichukua nafsi ya mjukuu wangu jamani Dr ana endeleaje?"
Uncle Fredy alikuwa wa mwisho kuingia ndani na alipomuona Brenda ameamka.
Alimkimbilia mbio mbio..
"Brenda binti yangu, ooohhhh Brenda mwanangu umeamka binti yangu"
Toka hapa Madam Suu alimtaka asogee mbali naye wakati huo Susan mama yake na Brenda alikuwa akifuta machozi yake ya furaha baada ya kumuona binti yake.
"Mama" aliita Brenda akinyoosha mkono kumshika mama yake aliyeenda na kumpatia mkono huku akitabasamu na kulia zaidi ila Madam Suu alizidi kumkata jicho lenye chuki ya wazi kabisa.
Jamani mbona kama kila mtu ni mwema kwa Brenda? Sasa nani kahusika na kifo cha Mr Modest na anataka kupata urithi original ulioweza kuachwa mikononi mwa Brenda?
*SEHEMU YA PILI*
"Whaaat? Ame amka?" Alihoji Issan aliyekuwa katika safe ya nyumba ya kina Brenda na kushindwa kuifungua.
"Sawa nakuja kumaliza kazi yangu" alijibu Issan na kuitizama ile Safe akijatibu tena kwa mara nyingine kama ataweza kuifungua.
"Babaaaaaa!!" Aliisikia Sauti ya mtu ikiita na aliona tayari siyo kwema tena pale alipo.
Aliweka vifaa vyake kwenye briefcase na kuondoka
"Huyu Mzee kaenda wapi tena?" Alitoa simu yake mfukoni na kupiga.
"Halooo!! Nini ka amka?" Aliuliza Wengah akishtuka
"Anaongea?"
"Ndiyo anaongea"
"Anaongea? Amesema chochote kuhusu mtu aliye muuwa baba yake?"
"Kwanini unaniuliza maswali ya ajabu hivyo? We ulitaka mtoto wa dada yangu asiamke au?" Alihojia Uncle Fredy.
"Hapana baba nimeuliza tu kwa....kwahiyo anaweza kuongea?" Aliuliza tena.
"Embu usinipotezee muda njoo muone ndugu yako hospitalini na usije ukiwa na hayo maharufu yako ya mapombe Madam Suu yuko hapa"
"Ndiyo baba" alikata simu Wengah na haraka haraka naye alipiga simu huku akikimbilia chumbani kwake alifika na kufunga mlango.
"Haloo nyie washenzi, ameamka Brenda ame amka fanyeni haraka mje mmalize kazi yenu"
"Sawa Boss" alijibiwa na vijana wawili waliokuwa wakivuta zao vitu vyao vya kuwapa stim.
"Anasemaje huyo Mr Makelele?" Aliulizwa na mwenzie.
"Eti Brenda ameamka angejua hata siyo sisi tuliyo muuwa huyo Mjomba ake sijui baba yake Mr Modest sidhani kama angekuwa na hofu ya kuwa atajulikana"
"Alafu ile siku ilikuwaje mbona kama mimi siku ielewa?"
"Nani ali ielewa? Tunachoshukuru ni kuwa mikono yetu haija ingiza damu lakini tumeingiza million 50"
"Kwahiyo vipi tuka muuwe au?" Aliulizwa tena
"Wanini na sisi hatu husiki? Nasikia aliyefanya hivi kuna uwezekano mkubwa alimuona kwasababu Mr Modest alipigwa risasi kwa mbele kwahiyo aliye ianzisha kazi hii ataenda kuimalizia sisi tusubiri tu pesa"
Sasa mbona aliyewatuma Wengah siyo wakina Issan? Huyu Gaidi mwingine nyuma ya pazia ni nani?
🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼
Susan alitoka chooni na kukutana na Madam Suu akiwa anamsubiria.
"Umemuuwa mwanangu na sasa unazunguruka tu kwa raha zako"
Susan hakumjibu chochote zaidi ya kuelekea bombani.
"Mala*** wewe nakusemesha unanipita" alimkamata nywele zake na kuwasha bomba kisha akamdumbukiza kichwa chake kwenye sink na kumtoa.
Alimsukumia ukutani baada ya kumaliza kumlowanisha na maji.
"Unajua haukuwahi kuwa chaguo langu Susan na wala hutawahi kuwa hata kama umemzalia kijana wangu Brenda, sikuwahi kukupenda na sitawahi kukupenda" alimkandamiza na fimbo yake upande wa begani ambayo chini aliichongea ncha yenye dhahabu na kuwa kama kifuniko cha kalamu.
"Mshenzi wewe" alimtema mate na kutoka njee.
Susan aliinuka akiwa analia tu na kutizama mwili wake ambao ulikuwa na majeraha ya namna huyo na hiyo ilikuwa tabia ya Madam Susan kila alipokuwa akimuona ila ilikuwa siri yake hakuwahi kumwambia binti yake anayoyapitia kwa mama yake huyo mkwee akiamini atasababisha mtafaruku baina yao.
Alirudi ndani ya chumba alicholazwa binti yake akiwa amelowa.
"Mama nini kimetokea?"
"Aaammmhh niko sawa naenda nyumbani kidogo, kubadili nguo utabaki na bibi yako vipi nikuletee nini?" Aliuliza Susan
"Umefanyaje kwenye bega lako?" Aliuliza tena Brenda aliyeona damu upande wa kushoto wa bega la mama yake karibu na kifua chake.
"Nikuletee nini?"
Brenda alimtizama bibi yake japo mama yake hakuwahi kumwambia anayofanyiwa ila alishawahi mkutaga mara kadhaa.
"Bibi umemfanyaje mama yangu?"
"Unamuona kama mama yako lakini ni muuwaji huyu Mwanamke usimuone hivi na upole wake"
"Bibi kwani huwezi kukubali ya kuwa huyu ndiyo baba yangu aliyemchagua na siyo huyo kipenzi wako Vivian mtoto wa rafiki yako?"
"Huelewi kitu Brenda ila ipo siku utanikumbuka baada ya huyu shetani kutaka kukuuwa na wewe"
"Bi........
"Brenda acha" Susam alimkanya mwanaye.
"Umeamka muda siyo mrefu, na siyo vizuri kugombana na Madam Suu kumbuka yeye ndiyo damu yako ya pekee iliyobaki katika dunia"
"Yani kama Malaika Gabriel kumbe Israel mtoa roho" Madam Suu alifyonza na kufyonza kabisa.
"Nikuletee nini binti yangu, nataka nikakupikie"
Brenda hakumjibu mama yake zaidi ya kumtizama namna alivyolawa na alama ya damu kifuani mwake.
"Usiwe hivyo sema mama akakupikie nini?"
"Kampikie sumu umlete ili uwe ume angamiza sasa kizazi changu chote" jibu lilitoka kwa Madam Suu aliyechangamka.
"Madam Suu lak.......
"Ni kelele wewe unataka kunifundisha nini? Huyo mwanao muhuni mbona mpaka muda huu hajaja kumuona ndugu yake?" Alimuuliza Uncle Fredy
"Wengah anakuna kuna mambo anaweka sawa ofisini anakuja"
Susan alimuaga mwanaye taratibu na kuondoka akiwa na tabasamu.
Alitoka kabisa hadi njee ya hospital na kupanda gari lake huku dereva akiwa ni mwanaume aliyeenda makamo kidogo.
"Uko sawa?"
"Huo usawa nautolea wapi? Unaona namna huyu kizee alichonifanya? Natamani angekufa yeye wa kwanza kabla ya mtoto wake" alijibu Susan huku akijitizama alivyo na kupiga kelele kama mwendawazimu.
"Nikupelekeeee?" Aliuliza Dereva Sajad.
"Nipeleke kwa Vivian".
"Vivian? Unataka kwenda kumfanya nini Vivian?"
"Yani kadri huyu mama yake mkwe anavyonitesa na mimi ndo nitamtesa zaidi, alichonifanyia mimi naenda kumfanya yeye"
"Lakini kumbuka Vivian hayupo sawa kiakili, tangu umuibie mwanaye Brenda. Mi sidhani kama tunapaswa kumjadili huyo kichaa bali Brenda. Vipi amesema chochote?"
"Amepoteza kumbukumbu hakumbuki chochote na hata sijui huo urithi original tutaupataje. Bora hata ulivyoona huyu Mzee alimridhisha mwanaye kila kitu na kuniacha mimi mtupu... yani nimekuwa mke wake kwa zaidi ya miaka 27 nimemlea Brenda mimi nimefua mimavi yake na kuamka usiku pindi alipokuwa analia nimekuwa mama bora kwa mwanaye lakini mwisho wa siku anaandika kila kitu kiende kwa Brenda yani hakuna hata senti tano aliyo iweka kwenye jina langu"
"Usijali Susan kila kitu kitakuwa sawa mke wangu ni swala la muda tu, wewe endelea kufanya Brenda akuamini na katika kipindi hichi ambacho hana kumbukumbu ndiyo muda wetu mzuri wa kuzidi kutafuta huo urithi original na tukiupata tu basi tuna ubadilisha na huu wa kwetu tulio uandaa"
"Yani nilimtelekeza binti yangu kituo cha Yatima kwaajili ya kumlea huyu mshenzi alafu baba yake anamrithisha kila kitu huku akiniacha mimi Modest mshenzi sana tena mshenzii kabisa, vipi uliwapigia simu hao magaidi?"
"Ndiyo niliwaambia wamuuwe Brenda"
"Wewe una kichaa nini? Wamuuwe kivipi na urithi original hatujui mahali ulipo? Waambie waache mara moja!! Wanapaswa kupata kwanza urithi ndo mengine yaendelee. Fanya haraka "
Oky.....
Dereva Sajad alipiga simu na simu yake iliita kwa Issan aliyefika tayari hospital na alikuwa mbele ya kitanda cha Brenda.
Brenda alifumbua macho yake baada ya kusikia mlio wa simu na kukutana na Issan aliyevalia Kota laki Dr.
"Tafadhali Dr naomba niitie Dr Lulu, mwambie namuhitaji miguu yangu haisogei"
Issan alibaki akimtizama na simu iliita tena.
"Halooo" aliipokea huku akiwa anataka kuchoma sindano ya sumu kwenye drip
"Abort the mission hakumbuki chochote kuhusu kilicho tokea, hivyo unapaswa kupata urithi original tu"
"Oky" alijibu Issan na kurudisha sindano yake kisha akataka kuondoka.
Brenda alimshika mkono.
"Tafadhali kaniitie Dr Lulu haraka nitajikojolea"
Issan aliutoa mkono wake kwa nguvu na kufanya Brenda atake kudondoka chini.
Dr Lulu aliingia muda ule ule.
"Mkojo umenibana and miguu yangu haisogei"
"Hahaha ngoja nikusogezee ndoo" Dr Lulu alicheka na kuleta ndoo karibu na Brenda akimwambia ashuke.
"Siwezi"
"No ni uwoga nani vile umekaa miezi zaidi ya miwili bila kutembea ila miguu yako haina shida, njoo nikusaidie"
Brenda alijitahidi kusogeza mguu wake na ulisogea.
Aaaaa kumbe unasogea kweli, hhahaa nilijua nimeshakuwa kilema tena cha mguu baada ya kupata kilema cha akili"
"Noooo why useme hivyo?" Alihoji Dr Lulu na kumketisha kwenye ndoo kisha akaingia chooni na kumletea tissue.
"Kwasababu hawa watu waliokuja hapa nimeongea nao tu ila hata siwafaham, nimetumia tu akili yangu ila sina ninaye mkumbuka"
Brenda aliweka ukweli wake kwa Dr Lulu.
"Nooo yeeaaahhh, sina ninaye mkumbuka zaidi ya wewe tu"
*SEHEMU YA TATU*
"Mimi tu"
"Ndiyo"
"Mimi unanikumbukaje?"
"Kama Dr wangu" alijibu Brenda.
"Are you seriously Brenda?"
"Ndiyo, hivyo nilikuwa na ombi kidogo kwako unitafutie habari nzima za kila mmoja wao ili kutowapa mashaka ya kuwa sikumbuki chochote"
Dr Lulu alimtizama Brenda na aligundua anamaanisha ni kweli kwamba hakumbuki chochote.
"Pia naomba uniweke hapa hata kwa muda wa wiki moja itanitosha mimi kufuatilia taarifa zao kujua tabia zangu na namna ya kuziishi"
🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼
Issan aliingiza password kwenye mlango wake na kuzama ndani alipokutana na Alexia.
"Vipi umemaliza kazi yako?"
"Haiwezi kuwa rahisi, Alexia yule binti hakumbuki chochote kile siyo kuhusu sisi tu hata familia yake na kwa maelezo ya Dr hali hiyo itamkuta mara kwa mara yani anaweza kukutambua sasa hivi wewe ni nani na baada ya masaa kadhaa akashindwa kukutambua tena"
"Whaaaat? Huo ni ugonjwa gani?"
"Tunapaswa kupata urithi original alioachiwa na baba yake , kuna locker yake moja nadhani hiyo itakuwa ndo yenye urithi nimejarib kufungua na kufungua lakini imegoma"
"Hivyo unapendekeza nini?" Aliuliza Alexia akimpatia kinywaji kwani Issan ni mpenzi sana wa vinywaji vikali.
Sharukh alitoka uwani.
"Aise alafu huyu nani kamruhusu aingie chumbani kwangu?" Alihoji Issan
"Kwanini upange nyumba yenye choo kimoja ndani kwako?"
"Eeeehhh" aliguna Issan.
"Embu achana naye , niambie tunafanyaje?"
"Unapaswa kuingia katika kampuni yao, nimeona tangazo la kutafuta sekretari nadhani ukimuweka karibu tutafaham mahala huo urithi ulipo"
"Oky kwahiyo unamaanisha anapaswa kuniamini sindiyo?"
"Ndiyo, jenga uaminifu kwake kuwa rafiki yake baada ya hapo tumemaliza kazi" alijibu Issan na kuweka kinywaji mdomoni.
🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼
"Tafuta mtu ambaye atakuwa karibu na Brenda"
"Madam Suu labda sijakuelewa, yani mtu wa karibu unamaanisha yule mchumba wake aliopo Marekani" Aliuliza Uncle Fredy.
"Mmmhhh we kuelewa inachukua muda sana sindiyo? Nimesema mtu wa karibu nikimaanisha bodyguard ambaye atalinda maisha ya Mjukuu wangu"
"Ahaaaaa, nimekuelewa Madam Suu hapo sasa twende kwenye haya makampuni makubwa makubwa Yama security .......
"Aise Fredy sitaki maelezo nimesema katafute bodyguard kwaajili ya Brenda"
"Ndiyo Madam Suu" alijibu Uncle Fredy.
"And hili liwe baina yetu, yoyote asifaham" alitoa angalizo Madam Suu.
"Hatimaye kesho mjukuu wangu anatoka sasa baada ya kumaliza wiki yake hospital "
Alitizama picha ya mwanaye Modest.
"Umezikwa bila mwanao kushuhudia mwili wako, Modest mwanangu nakuhakikisha kumlinda mwanao".
🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼
Palikucha na ilikuwa siku ya Brenda kurudi nyumbani baada ya kumaliza wiki kadhaa ku recover akili yake kwa kusoma soma mambo yote yanayo wahusu watu wake wote wa karibu.
"Ooohhhhh mjukuu wangu huyo"
Madam Suu alinyoosha mikono yake kumpokea mjukuu wake.
Brenda alimkumbatia bibi yake.
"Karibuni tena nyumbani kwako, karibu tena kwenu mjukuu wangu"
Leta yake mafuta ya upako.
"Eeeee Bibi umeanza sasa"
Uncle Fredy alileta kichupa na Madam Suu alipaka mafuta mikononi mwake kisha akaanza kumpaka Brenda usoni mwake huku akikemea kweli kweli.
Susan alibaki akimtizama tu.
Leta chumvi alipewa chumvi na Uncle Fredy aliyekuwa kijumbe wa karibu na Madam Suu.
Alipoipokea tu alimgeukia Susan na kumlenga nayo mwilini.
"Ushetani wako na uchawi wako usiwe na nguvu kwa mjukuu wangu" .
"Bibi" aliita Brenda na kwenda kumzuia acha.
"Ushindwe" alimtupia na chumvi ya usoni kabisa Susan aliyevumilia tu vituko vya mkwe wake huyo.
Alimeza mate ya hasira lakini hakuwa na chakumfanya.
Madam Suu alionyesha chuki zake waziwazi kwa Susan hadi kufanya wafanyakazi wamuonee huruma Susan kwa namna anavyoteseka.
Brenda aliondoka na bibi yake kumtoa pale alipo mama yake.
Susan aliingia chumbani kwake na kutupa chini picha ya mume wake Modest.
"Umenifanya nimepitia mengi na hata baada ya kifo chako bado nayapitia mengi kwaajili ya huyu mama yako kizeeee... asubiri aone pindi nitakapopata huo urithi ataishi katika maisha haya haya anayonipitisha yani nitamfanya ayaishi mara kumi yake"
Alisikia vishindo vya kiatu vikiwa vinakuja chumbani pale alipo.
Aliinama na kuanza kuokota vipisi vya picha.
"Mama uko sawa?" Aliuliza Brenda akienda kumshika na kumuinua.
"Am oky" alijibu Susan aliyejifuta machozi yake ya uwongo.
Picha ya baba yako ilidondoka chini kwa bahati mbaya. Alijizungumzisha Susan
Brenda alimsimamisha na kumkumbatia mama yake huyo.
"Naomba umvumilie tu bibi unajua ni mtata kwa kila mtu, hayuko hivi kwako tu hata kwababa alikuwa hivi"
"Usijali, mimi niko sawa na nina furaha kukuona mwanangu umekuja tena katika nyumba yako. Karibu shoga angu" Susan alimuachia tabaasamu la kutosha Brenda.
"Asante shoga angu" alijibu Brenda na kumkumbatia zaidi Susan aliye badilisha sura yake baada tu ya kuwa nyuma ya mgongo wa Brenda.
🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼
Madam Suu alipita akiwa anakagua hao vijana walioletwa kama ma bodyguard na Uncle Fredy.
Alimtizama Uncle Fredy aliyetabasamu.
"Hawa wametoka kwenye kampuni moja ambayo inatoa ma security konki kabisa yani wako vizuri"
Madam Suu alimtoboa mmoja mguuni na fimbo yake na aliishia kupiga kelele na kuruka ruka kama kinjiwa kinachokata roho.
"Ma security konki kabisa eeee?" Aliuliza Madam Suu baada ya kumjaribu mmoja tu.
Uncle Fredy alianza kutizama pembeni.
"Hivi wewe mjinga nakupa pesa yangu ukanitafute ma bodyguard unaenda kuniletea wacheza kamari wenzako? Hela yangu umepeleka wapi? Aliuliza Madam Suu na kuanza kumchapa na fimbo.
"Mama yangu..... Madam Suu!!! Madam Suu!!!. Alianza kupiga kelele na wale bodyguard wake wa mchongo wote walikimbia mbio.
"Nakupe pesa yangu ,mjinga wewe unaenda kwenye makamari yako" alizidi kupigwa hadi alipo kuja Brenda na kumzuia bibi yake.
"Bibi!! Nini unafanya? mbona unam treat Uncle Fredy kama mtu wa njee? Siyo vizuri kumfanya hivyo"
"Yani najiuliza ilikuwaje wewe ukawa baba yangu? Inamaana mama yangu alikosa wanaume wa maana hadi akaja kukupata wewe mwoga na mjinga? Utazidi kupigwa na wanawake mpaka lini? Umemtumikia Modest kwa zaidi ya miaka 20 ila sina uhakika kama una hata asilimia 2 kwenye huo urithi wake. Baba unani aibisha sana ni vyema usimame kama mwanaume na baba kwangu ".
Wengah alimuacha baba yake pale chini na maneno hayo yenye kuumiza hisia zake.
Fredy aliingia ndani akiwa anapata kinywaji kikali kwa hasira.
Susan alimpatia kibag chenye ice ili ajikande kande huko alikopigwa na fimbo na Madam Suu.
Alilitupa chini kwa kulipiga mkono.
Susan aliinama na kuokoka kisha akamshika.
"Mimi na wewe wote tunapitia hali moja , nafaham hali unayo ipitia kwasababu hata mimi naipitia hiyo" Susan aliondoka na kumuacha Uncle Fredy ambaye aliona tangu dada yake kufariki ambaye alifika kwenye ajali na kaka yake na Modest huku akimuachia jukumu la kumlea Brenda hadi atakapo olewa basi atakuwa na hiyari ya kuondoka kwenye nyumba ile.
"Hukuwahi kuzaa mtoto katika hii nyumba, ulifariki pamoja na mume wako kwanini ulinipa jukumu mimi la kumtizama Brenda hadi aolewe ndo niondoke? Nimechok kudhalilishwa mimi katika hii nyumba dada yangu natamani hata kesho nirudi kwenye nyumba yangu ya nyasi"
Alilalama Uncle Fredy kwa nguvu na Madam Suu aliyasikia maongezi hayo.
"Inamaanisha huna tamaa na mali, hisia zangu zitakuwa sahihi tu Susan ndo ame husika na haya"
*SEHEMU YA NNE*
Madam Suu aliondoka na kumuacha pale Fredy.
Brenda alirudi chumbani kwake na kuanza kukagua kagua ili akifaham chumba chake kikoje kwani alisha sahau hata droo zina nini.
Alianza kufungua fungua na hapo alikutana na Dayari yake.
"Hope itakuwa na vitu vyangu vya muhimu"
Alichukua na kwenda kuketi kitandani akianza kupitia pitia ili akumbuke chochote.
Akiwa anaendelea kusoma soma mlango uligongwa na Mama yake Susan.
"Ooohhhh Mama karibu"
"Nikasema nimlete shoga angu japo juisi anywe"
"Ooohhh hapana hapa yenyewe napaswa kwenda gym sasa embu ona kitambi"
Brenda alikataa na kumuonyesha kitambi chake
"Unasoma dayari yako?"
"Ndiyo najaribu kupitia pitia nione kama kuna nitakachokipata chamaana hapa"
"Lazima upate vingi tu vya maana kwasababu hujawahi ruhusu mtu ashike kabisa"
"Really?" Aliuliza Brenda na kuitizama.
"Ndiyo" alijibu Mama yake na kuichukua akaweka kitandani kisha akampatia Juice.
"Brenda najua hutaki kuliongelea hili, lakini nilikuwa naham ya kujua mume wangu alifarikije?"
"Mama sitaki kukuvunja moyo lakini sitaki pia kukupa matumaini, sikumbuki chochote yani hata siku yenyewe ilivyo anza sikumbuki hata tone" alijibu Brenda na Susan alizidi kumchokonoa zaidi.
"Mmmmh hukumbuki hata kama ilikuwa birthday yako?'
"Mmmmmhhh, sitaki umwambie hili Bibi kwasababu atakuwa na hofu sana juu yangu sina chochote cha nyuma ninachokumbuka niliwasoma tu mtandaoni nikawafaham ndo mnaona namna nawachangamkia"
"Hiyo ni kweli kwasababu tabia yako imebadilika kidogo, wewe siyo charming hata kidogo una tabia za bibi yako ukali ukali na kufoka sana pia uko straight kwenye mambo yako hupendi kona kona, kwahiyo hukumbuki hata karatasi za urithi wapi umeweka?"
"Sikumbuki hata kama nilikabidhiwa Inshort kichwa changu kiko empty kabisaaa" alijibu Brenda na kumwambia Mama yake.
"Ila usijali Mama naamini nitakumbuka kila kitu taratibu tu Dr Lulu amesema mwanzo niliparalaizi yani sehemu ya ubongo ilikuwa imelala wakahisi sita amka ila niliamka nikiwa na kama kifafa wanadhani nina kifafa na mwishowe Nime amka nikiwa na tatizo la kusahau hivyo amesema nikipata muda mzuri na kutumia dawa vizuri basi huwenda nikapona tu"..
"Ahaaaa kwahiyo bado una sahau sahau?"
"Mmmhhh unaweza ukatoka njee na utakapo rudi nikawa nimesha kusahau wewe ni nani" alijibu Brenda.
"Nawaza hata kampuni nitawezaje kuisimamia"
"Kuisimamia kampuni?' Aliuliza Susan kwasababu yeye ndo alikuwa Vice President chini ya mume wake Modest aliyekuwa President "
"Ndiyo Bibi kasema napaswa kwenda kuisimamia kampuni kama President muda nilio upoteza hospital unanitosha"
Susan alikamata shuka lililokuwa pale kitandani kwa hasira.
"Ni kweli lazima usimamie mali za baba yako, unajua wewe ndiyo mrithi wa pekee na ninataka kukwambia hili Brenda utaweza haijalishi upo katika hali gani, ila mimi kama Mama yako nauelewa uwezo wako namna ulivyo mkubwa kazini na I.Q yako ilivyokubwa".
Nakupenda Mama yangu, nafurahi kwakuwa wewe bado upo karibu yangu.
Brenda alimkumbatia Susan akijua ni mama yake na yuko mikono salama hakuna baya lolote litakaloweza kumpata.
Susan aliingia ndani ya chumba chake na kumpigia Dereva Sajad simu.
"Kesho Brenda anaenda kwenye kampuni, hakikisha huyo mtu anapata nafasi kama Sekretar wake sawa?"
"Usijali limeshaisha hilo" alijibu Sajad na kumpigia simu Issan ambaye hakuwahi kumtia machoni.
"Haloo, natumaini umefanya vile nilivyokwambia kesho Brenda anarudi ofisini"
"Usijali nimeshamaliza kila kitu kwa upande wangu, imebaki kwenu tu"
"Sawa' alijibu Dereva Sajad na alipokata simu iliingia picha ya Alexia aliyotumiwa na Issan kama ndiye atakayekuja kama Sekretari.
"Dah!!!! Chombo kabisa hichi mtoto mbichi!!!, Fredy hawezi mkataa"
Dereva Sajad alitaka kutumia udhaifu wa Fredy ili kumuingiza Alexia katika kampuni.
🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼
Palipambazuka asubuhi na mapema na Brenda aliamua kuanza zoezi kama alivyo shauriwa ili kuuweka mwili wake sawa.
"Anatoka" alizungumza Issan akiwa ndani ya gari lake na kumtizam Brenda aliyeweka headphone zake masikioni kisha akaanza kukimbia taratibu kuelekea gym.
"Ok" alijibu Alexia aliyekuwa mbele kidogo ya alipo Issan.
Alishuka na yeye ndani ya gari huku akimuacha Sharukh.
Alianza kukimbia uelekeo ule ule ambao alikuwa na uhakika Brenda ataupitia ili kujenga ukaribu naye.
Brenda alimpita pasina kumsemesha akiwa katika mbio za Taratibu vile vile.
"Plan B boss" alizungumza akiwa na kifaa sikioni mwake maana hiy ya kumtega njiani amsemeshe haikufanikiwa.
Brenda akiwa anatembea walikuja vijana watatu kwenye pikipiki na kuanza kuzungumza Brenda aliyesimama na kuwatizama.
Walianza kumshika shika nywele zake na kuvuta headphone katika masikio yake.
Alecia alijitokea na kuanza kuwazuia.
"Mnafanya nini?" Aliuliza na walisimama wale vijana waliokula naye dili moja.
"Oya mrembo hatutaki shida na wewe, tumemfuata huyu kichuna wa kitajiri nenda zako"
"Kaeni mbali na mdogo wangu mimi ni dada yake" alijibu Alexia akijizolea maujiko kwa Brenda na akiwa amemuweka mbele yake.
"Nikikufinya tu kimbia"
"Na vipi kuhusu wewe? Aliuliza Brenda.
"Niko sawa" alijibu Alexia na kumsukuma mmoja kwenye pikipiki
Kimbiaaaaa!!!! Alitoa sauti kubwa na ya ukali Alexia iliyomfanya Brenda akaanza mbio bila kujua ni mtego tu.
"Nipige" alimuamuru kijana mmoja kufanya hivyo na alitandikwa kibao cha haja.
"Nipige kwa nguvu"
Aliwekwa ngumi na kijana wa pili puani.
"Sijasema ngumi mshenzi wewe"
Brenda alikimbia na mbele akakutana na Issan tafadhali twende ukanisaidie kuna vijana watatu wanampiga binti mmoja.
"Mi siyo askari" alijibu Issan na kutoa mkono wake kwa nguvu kama alivyofanya mara ya kwanza hospital na hivyo kumfanya Brenda kukumbuka.
"Wewe mkaka!!! Nakukumbuka wewe ndo yule Dr wa siku zile eeee?"
Brenda alisikia kelele za Alexia akiomba msaada na aliona bora arudi akamsaidie tu hivyo hivyo.
"Anakuja" alizungumza Issan na kumfuata nyuma Brenda.
Alifika pale na kuanza kuwakunja kunja wale vijana.
Wakati huo Alexia alikuwa mikononi mwa Brenda aliyemtuliza na kumtizama majeraha yake.
"Utakuwa Sawa polisi wanakuja muda siyo mrefu"
Vijana wale baada ya kuguswa guswa pale, wote walitimua mbio na kuanza pikipiki zao.
Issan aliwatizama na Alexia alienda kumshika mkono akimshukuru kwa kuwasaidia.
Issan aliutoa tu mkono wa Alexia kisha akampita Brenda huku akiwa anamtizama tu na kuendelea kukimbia kwani alikuwa amevaa mavazi ya kufanyia mazoezi.
"Naomba nikupeleke kwetu ukapate matibabu"
"Hapana ahsante usijali ni lazima sisi kusaidiana"
"Nitakulipa wewe twende tu"
"Nashukuru lakini sijafanya hivi kwaajili ya pesa, kuwa na amani kabisa" Alexia aliitia mikono ya Brenda na kuondoka akiwa anachechemea kidogo.
"Dada?" Aliita Sharukh aliyekuja kumalizia game lile.
"Nilikwambia mimi, usiende mazoezi saa 12 hii nikupeleke na gari ukakataa ona sasa kilicho kukuta utaendaje kwenye intaview ukiwa na ngeu hivyo si watu watadhani wewe ni mwizi?"
"Ni Dada yako?" Aliuliza Brenda.
"Ndiyo na wewe ni nani?"
"Aaammm mimi ni mtu aliyenisaidia hata hivyo nimemwambia nimpeleke kwetu akapate matibabu kidogo lakini amekataa"
Brendaaaa!!!! Oooohh mjukuu wangu, Unadhubutuje kutoka jamani na kuja huku mwenyewe wakati unajua hali uliyonayo.
"We nawe amka acha kulala" Madam Suu alimshtua Uncle Fredy aliyekuwa amelala akiwa amesimama.
"Madam Suu!!!!
"Bibi nilivamiwa na kibaka ila huyu Dada hapa amenisaidia"
"Ooohh ahsante sana mjukuu wangu!! Mungu akubariki sana'.
"Amina Bibi, nimefanya kwa wema tu binadamu lazima tusaidiane" alijibu Alexia.
"Ni kweli ila nakushukuru sana jamani, embu mpee business card" alimwambia Fredy ambaye hakuwa pamoja nao macho yake aliyashayafunga kutokana na usingizi kumlemea.
"Nimesema mpe Business card" alirudia Madam Suu na kumpiga na rungu yake ya mguu.
"Madam Suu mbona unanitesa hivyo, natolea wapi Business card asubuhi hii"
"Jamani bibi mimi nimefanya siyo kupata malipo wala kulipwa ninyi kuweni na amani hata hivyo naomba niende kuna mahali napaswa kwahi leo kwaajili ya Intaview "
"Ni wapi hapo? Nielekeze ni wapi nitawapigia simu na kuwaambia wewe ni mtu wangu wakupe kazi"
"Jamani Bibi Asante, lakini napenda wanichagua kwa uwezo wangu ila nashukuru kwa kuonyesha kujali naombeni niende"
Dada ungechukua tu ofa yao, nani atakuajiri na mangeu hayo kama mwizi? Alihoji Sharukh
Twende. Alexia alimshika mkono kisha akazama naye ndani ya gari.
Alishusha kioo na kumuaga Madam Suu pamoja na Brenda.
"Muda mwingine usitoke njee ukiwa mwenyewe , mtaa umebadilika huu siku hizi"
"Sawa nashukuru " alijibu Brenda na Alexia alipandisha kioo.
"Hapa tumemaliza lazima uingie kama Sekretar "
"Wepesi sana kudanganyika hii kazi tunaimaliza haraka" alijibu Alexia.
"Uko saw Mjukuu wangu?"
"Ndiyo"
"Popote ulipo umizwa?"Aliuliza Madam Suu.
"Hakuna"
"Fredy mpigie simu Dr Lulu aje, Fredy!!! Aliita na kugeuka nyuma hapo alimkuta akiwa amesimama vile vile na macho amefumba.
Alimshika na fimbo yake kwenye kola ya shati kisha akaanza kumvuta ili atembee
"Yani dada yake aliniachiaga shida tu na matatizo, ni mkubwa lakini akili za kitoto zimejaa Tele kwenye hiyo kichwa yake"
*SEHEMU YA TANO*
Brenda akiwa ana shuka ngazi ni kama tukio la nyuma lilianza kumjia kichwani kwa kusikia sauti ya baba yake.
"Su....... siyo mtu mzuri katika hii familia, ficha huu urithi mbali sana asiuone"
Kauli hiyo ilimrudia rudia na kumfanya adondoke kutoka kwenye ngazi hadi kushuka chini mzima mzima
"Heeeeeee" alipiga kelele Uncle Fredy kwani alimuona
"Madam Suu!!! Brendaaa!! Brendaaaa!!! Aliita na Susan alikuwa wa kwanza kufika.
"Nini kimetoke? Brenda binti yangu".
"Amekutw na nini?" Aliuliza Madam Suu akija haraka haraka.
"Amedondoka tu , alisimama pale akawa kama ameshika kichwa chake na kubiringita"
Dr Lulu alishafika pale kwani alipigiwa simu saa nyingi sana.
"Nipisheni kidogo" aliomba wampishe na kumtizama kwa kuyafumbua macho yake.
Amepigiza tu kidogo na kupoteza faham,nahitaji akae sehemu yenye hewa Safi kw wingi"
"Fredy mpeleke garden" Madam Suu alitoa amri hiyo na Fredy alim beba akisaidiana na mwanaye Wengah hadi kumfikish kwenye garden hapo walimuweka chini ya mti mmoja.
"Atakuwa sawa binti yangu?" Alihoji Susan akionyesha ni mwenye hofu kwa kutikisa tikisa mikono yake.
"Yeah" alijibu Dr Lulu
🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼
"Kazi imekuwa rahisi zaidi ya tulivyodhani, tunapaswa kujipongeza" Sharukh aliwapatia Glas moja moja ya kinywaji kisha na yeye akaokota ya kwake.
"Kadri kazi inavyokuwa rahisi mwanzo wake, basi inaonyesha ugumu wa mbeleni" alijibu Issan na kujiwekea vitu.
"Ni sawa ila mwanzo mzuri, hivyo tunapaswa kujipongeza unajua hii ndiyo kazi yetu ya kwanza yenye fedha kibao alafu ndiyo kazi yetu ya kwanza kufeli kushindwa kuimaliza kwa wakati"
"Yeah nakubaliana na wewe, lakini nikitizama muda unapaswa kujiandaa na kuwa njiani kwaajili ya Intaview " Sharukh alikumbushia hilo.
"Sharukh, sina hata haja ya kwenda kufanya Intaview kwasababu mimi tayari ni mfanyakazi"
"Hahahaah cheerrssss"
Walipeana Cheers ila sasa Bwana Gaidi Issan yeye alikuwa akiikumbuka mikono milaini ya Brenda iliyomshika kwa mara ya pili.
Aliwatizama vijana wake na kuongeza kinywaji kwenye glass yake kisha akajiweka.
🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼
"Ni sauti tu ya baba ndo nimeikumbuka lakini sikumbuki alikuwa akinisemesha nini" alidanganya Brenda.
"Kwahiyo kumbukumbu zimeanza kurejea kidogo kidogo, vile vidonge una tumia?"
"Ndiyo"
"Sikudhani kama vingeleta matokeo mapema hivyo, unajua yan kuna namna akili yako ilivyo nashindwa ku identify" alijibu Dr Lulu.
"I.Q yangu ni kubwa sana kumbuka hilo Dr Lulu "
"Hahahaha sawa mama I.Q" alijibu Dr Brenda na wote walicheka isipokuwa Susan ambaye aliwaza kama Brenda ameshaanza kukumbuka siku ya kifo cha Baba yake basi huwenda akakumbuka jambo ambalo hakuhitaji alikumbuke la siku hiyo.
Alitoka na kumpigia Dereva Sajad.
"Yes haloo"
"Brenda ameshaanza kukumbuka baadhi ya vitu siku ile ya birthday yake na unafaham haipaswi kuwa hivyo, kama ataanza kukumbuka ya kuwa alituona sisi tuki......
"Punguze presha Susan mke wangu, kila kitu mume wako atakishughulikia wewe relaxe mambo yetu yote yanaenda kama tulivyopanga"
"Lakini vipi kama akikumbuka alituona tukifanya mapenzi kabla ya kukumbuka wapi aliweka urithi?"
"Huniamini au? Hatuta mruhusu yeye akumbuke chochote kuhusu sisi, kumbuka tumeanza muda mrefu sana kufuatilia hizi mali na sasa tunaenda kuzipata hakuna yoyote anayeweza kuharibu mipango yetu"
"Sawa nakuamini" alijibu Susan na kukata simu kisha alikumbuka usiku wa birthday ya Brenda ulivyokuwa.
"Mke wangu, leo ndiyo siku ya kifo cha Mr Modest..... leo atafariki na kila kitu chake kitakuwa chetu tayari urithi fake umesha kamilika tunapaswa ku enjoy" Sajad alianza kum busu tu taratibu.
"Ni sawa ila subiri hadi, likamilike hili ndo tu enjoy"
"Inamaana sina ruhusa ya ku enjoy na wewe? Kumbuka wewe ni mke wangu mimi tuna ndoa ya Kanisani Susan na mimi mume wako leo nakuhitaji ki unyumba"
Sajad alimvuta karibu na kuanza mchezo ule mchafu akimuinamisha kwenye meza wakati wakifanya uchafu wao.
Susan alitizama mbele na hapo macho yake yaligongana na macho ya Brenda aliyekuwa amesimama mlangoni na kuwatizama.
Kumbukumbu za Susan zilikata hapo na kujilaumu.
"Kwanini sikuufunga ule mlango na mimi? Kwanini nikakubali kufanya ujinga ule pale?
Lazima nimfuate Brenda na nijue amekumbuka nini.
"Su...... siyo mzuri katika familia hii" Brenda aliikumbuka Ile kauli akiwa chumbani kwake na alivuta dayari yake na kuandika hayo maneno.
"Suuu...... nini sasa mwenye jina la Suu ambaye siyo mwema kwenye familia yetu?
Susan aligonga mlango na Brenda alificha dayari yake chini ya mto.
"Karibu mama"
"Nimekuletea matunda fresh ule binti yangu"
"Ahsante" aliyapokea na kuanza kula taratibu huku akimtizama Susan ambaye alitafuta Gia ya kumuingilia.
"Umekumbuka nini kuhusu siku yako ya Birthday?"
"Kwanini unajali alicho kikumbuka?" Aliulizwa na Madam Suu akitoka uwani.
Susan aliinuka kutoka kitandani alipokaa na kutoa heshima.
"Unahofu kwamba atakukumbuka wewe ndiyo uliyemuulia baba yake?"
"Bibi mbona unapenda sana kumkandamiza mama?' Aliuliza Brenda.
"Angekuwa hajabebea mimba hapa huyu, ningesema tu kuna mahali amekuiba" alijibu Madam Suu na Susan alionekanaga kama fala tu mbele yake.
"Mi naenda" Susan aliondoka na maneno hayo.
"Brenda, najua huyu ni mama yako ila kuwa naye makini yani simpendi huyu mwanamke simpendi kweli kweli"
"Lakini Bibi, unampa mama yangu wakati mgumu kweli kweli, just imagine unapambana na mtu ambaye hasubutu kukurudishia hata ukucha ni vibaya"
"Wewe ndo unajua harudishi hata ukucha, ila namjua huyu mwendawazimu amevaa tu ngozi ya kondoo njee ila ndani nili chui lilafi" alijibu Madam Suu.
Brenda alimtizama Bibi yake na kauli ya Su ilijirejea.
Alikipiga piga kichw chake.
"Vipi mbona unapiga kichwa? Kinauma? Nimpigie Dr? Aliuliza Madam Suu
"Hapana, niko sawa Bibi" alijibu Brenda.
"Kama hauko sawa unaniambia".
"Niko sawa usiwe na mashaka"
"Umekumbusha mahali ulipoweka karatasi za urithi?"
"Hapana"
"Jitahidi ukumbuke ni muhimu sana na usimwambie mtu yoyote isipokuwa mimi tu"
"Wewe tu?"
"Ndiyo kwasababu sina ninaye muamini katika hii nyumba hivyo ni bora uniamini mimi tu"
"Sawa Bibi"
"Then leo naelekea kwenye kampuni na kama unavyofaham, ulipaswa uwende leo lakini naona hauko vizuri"
"No Bibi niko sawa"
"Hapana huwezi kwenda na hiyo ngeu tena hapo kichwani, nitaenda mimi na huyo mama yako na nitahakilisha nakuchagulia sekretari mzuri atakaye kusaidia na kukubeba wewe na madhaifu yako uliyonayo kwa sasa hivi"
"Lakini Bibi mimi siyo kilema"
"Najua ila nahitaji mtu makini upande wako, sidhani kama nitaishi muda mrefu baada ya baba yako kuuwawa najiona kabisa sina muda mwingi" alijibu Madam Suu.
"Bibi hapana bhana maneno gani sasa hayo?" Alihoji Brenda.
"Nahitaji uwe makini iwa kila hatua unayo ipiga na ujue umejaza maadui wengi kuliko marafiki tena walio karibu na wewe"
🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼🥷🏼
Madam Suu aliingia ndani ya kampuni ya mwanaye na heshima alipewa kila mahala kwani yeye ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa kampuni ile kabla ya kumuachia kijana wake Modest..
Aliingia hadi ndani katika ofisi ya mwanaye Modest.
"Badilisha bango hili weka jina la Brenda na ita kikao cha body members wote"
"Ndiyo Madam Suu na vipi kuhusu usaili wama sekretari?" Aliulizwa.
"Naenda kuteuwa mmoja sasa hivi" alijibu Madam Suu na kuomba aongozwe walipo hao wanao omba kazi.
Wote waliinuka kwa heshima baada ya kumuona hata Alexia naye aliinuka akiwa amejiziba ziba na kwa kitambaa kichwani mwake akificha ngeu za kujisababishia yeye mwenyewe ili kupata uaminifu.
"Nini maana ya sekretari?" Alimuuliza mmoja wao
"Se....See......seeee.....sekretari ni .......
"Ondoka" alifukuzwa baada ya kuleta tu kigugumizi.
"Elezea kwa ufupi Microsoft Excell?" Alimuuliza swali mwingine.
"Aaammmhh Microsoft Excel (jina kamili ni Microsoft Office Excel) ni sehemu ya Microsoft Office. Pia inapatikana kwenye mifumo ya Mac. Imeundwa na Microsoft na ni programu ya wamiliki. Inatumika kwenye mifumo ya uendeshaji Microsoft Windows na Mac OS X.
Inaweza kufanya mahesabu na majedwali. Kwa mfano, inaweza kufanya chati na picha zingine kutoka kwenye meza za data. Pia ina lugha kubwa ya programu inayoitwa Visual Basic For Appilication (VBA). Excel ni sehemu ya Microsoft Office. Matoleo ya sasa ni 2016 kwa Windows na 2016 kwa Mac"
"Wacha vyeti vyako pale, kasubiri njeee"
Alipeleka vyeti mbele na kutoka njee akisubiria majibu.
Mwishowe alimfikia Alexia.
Alimtizama na kumkumbuka ni yule aliyemsaidia mjukuu wake asubuhi.
"Upi umuhimu wa mkataba kwa mwajiriwa?"
"Mkataba ni moja kati ya haki za muhimu sana kwa mwajiri wakati mwingine kuliko hata fedha na marupurupu anayopaswa kulipa. Mkataba wa kazi hutoa muelekeo wa ajira ya mfanyakazi , huonyesha usalama wa ajira haki na wajibu wa mfanyakazi pamoja na haki na wajibu wa mwajiri huelezea majukumu ya msingi ya mfanyakazi, muda na mahali pa kazi na masuala mengine muhimu kisheria".
"Nyamaza" sauti ya Issan ilisikika katika kiwambo cha sikio la Alexia aliyesidiwa kujibiwa hilo swala na yeye kurudia maelezo yake.
"Weka vyeti vyako pale kasubirie njee"
Madam Suu alimpatia maagizo hayo tena
Alexia aliweka na kusema.
"Huyu m Bibi ni mshezi sikutegemea angenifanyia ufedhuli huu"
"Nilikwambia kazi ikionekana nyepesi mwanzo ujue ina ugumu sana mbele, Inshort Madam Suu siyo mwepesi wa kuwaamini watu" alijibu Issan
SOMA MUENDELEZO KWA SH 1000
NJOO WHATSAPP 0743433005
Tags
simulizi