JINSI YA KUPIKA MKATE KUMIMINA / SININIA / MCHELE NYUMBANI.
MAHITAJI NA VIPIMO.
I. 1 kikombe cha mchele
ii. 1 kikombe cha nazi ya unga
iii. 1 kikombe cha sukari kupungua kidogo
iv. 1 kikombe cha maji au maziwa vuguvugu
v. 1 kijiko cha chai cha hamira
vi. iliki kiasi upendavyo
vii. ute wa yai moja
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
i. Osha na kuroweka mchele siku moja ndani ya maji ya baridi.
ii. Saga ndani ya blender, mchele, tui, maji au maziwa, iliki, na hamira mpaka mchanganyiko uwe lani kabisa.
iii. Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke(ufure).
iv. Mchanganyiko ukifura, washa oven moto wa 350°. Mimina sukari pamoja na ule ute wa yai ndani ya mchanganyiko na uchanganye vizuri.
v. Ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
vi. Chukua sufuria umimine mafuta kidogo. Washa jiko na uweke sufuria ipate moto kiasi.
vii. Mimina ule mchanganyiko ndani ya sufuria uuwache kama dakika 5 hivi kiasi mkate uanze kushikana.
viii. Funika sufuria na uvumbike(bake) ndani ya oven kama dakika 35-40 hivi, au mpaka mkate uive na uwe rangi ya hudhurungi juu yake.
Note: waweza oka kutumia jiko la makaa
ix. Epua na uwache upoe kabisa kabla ya kukata. Ni bora kuula siku ya pili yake.
Note : Mchele mzuri ni Vip au Pisholi.
Tags
Jikonileo