UTUNZI WA RIWAYA
JINA LA RIWAYA: BARUTI (WAKILI MWEMA)
Mtunzi: JUSTIN BARUTI
Mwaka: 2024/2025
WhatsApp: +255752474397
UTANGULIZI
Baruti ni riwaya ya kubuni na kinathari iliyotungwa na kuandikwa na Justin Baruti inayozungumzia kuhusu maisha ya kijana mmoja aliyejitoa uhai na maisha yake katika kupambana na mauaji ya albino na biashara haramu ya viungo vya binadamu na hatma yake katika kuleta harakati za ukombozi katika jamii.
Kiufupi Baruti inaangazia maisha ya kijana mmoja jina lake anaitwa Baruti ambaye ana ulemavu wa kusikia, amejitoa uhai na maisha yake kuwapa wengine nguvu katika jamii
Riwaya hii kwa jina lingine inajulikana kama WAKILI MWEMA huku mwandishi akifafanua WAKILI ni mtu aliyepewa dhamana juu ya mtu mwingine, akikusudia kufikisha ujumbe katika jamii kwamba
"Kulinda, kusimamia na kutetea haki za watu wenye ulemavu na wenye mahitaji maalum katika jamii ni la kila mtu"
SEHEMU YA 01
Katika jiji la Dar es Salaam ilikuwepo familia moja ya kitajiri, waliishi mke na mume pamoja na mtoto wao mmoja jina lake anaitwa Jennifer
Jennifer alikuwa ni mwanafunzi anayesomea shahada ya sheria katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam hivyo haikuwa rahisi kwa Jennifer kufanya kazi za nyumbani, wazazi wake mara nyingi walikuwa wakisafiri sana tokana na shughuli zao za kila siku. Waliweka mfanyakazi wa kiume jina lake aliitwa BARUTI.
Baruti alikuwa ni kijana mpole, mkarimu na mwenye huruma. Mungu alimpa hekima ya kufanya maamuzi sahihi katika maisha yake, lakini hata hivyo ukiachana na sifa zake hizi alikuwa na tatizo moja tu yaani hasikii vizuri ni sawa na kusema "Katika maisha ya mwanadamu kila kitu kina pande mbili kama ilivyo shilingi. Upande mmoja una nguvu, upande mwingine una madhaifu yake"
Siku moja Baruti aliamka asubuhi na mapema kuosha vyombo huku sebuleni Baba Jennifer akiwa anasoma biblia, gafla baada ya Baba Jennifer kuona muda umeenda aliamua kumuita Baruti amtume dukani maandazi ya chai ili aondoke, aliita zaidi ya mara 3 lakini Baruti hakuitika
Tatizo sio kwamba hakuitika, anaweza akasikia sauti lakini akapata shida kwenye matamshi ndio unaambiwa mtu hasikii vizuri, haya matatizo sikia kwa mwingine lakini usiombe yakukute
Baruti hakutambua sauti hiyo inatoka wapi, alihisi ni sauti ya Baba Jennifer anaimba kwaya maana ni mchungaji maarufu katika kanisa moja jijini Dar es Salaam
Baada ya Baba Jennifer kuona anamuita Baruti haitiki aliamua kumfuata kwa hasira baada ya kuona ana kiburi
"Hivi wewe mtoto una matatizo gani, nakuita mara ngapi huitiki" Alisema Baba Jennifer
"Shikamoo boss, unaendeleaje"
"Nimekuuliza nimekuita mara ngapi huitiki"
"Jamani naomba unisamehe boss wangu nilikuwa naosha vyombo sijasikia unaniita"
"Hivi ulikuwa na mawazo, una uhakika sijakuita..."
"Hapana boss nipo sawa, nakwambia ukweli toka kwenye uvungu wa moyo wangu" Alisema Baruti kwa woga huku akiinamisha macho yake chini
"Futa hiyo kauli, sasa sikia nikwambie, chukua hii hela nenda dukani niletee maandazi urudi uoshe vyombo"
Baruti akachukua hiyo hela lakini nafsi yake ilimuuma baada ya kutolewa maneno makali na boss wake
Akiwa njiani anaenda dukani gafla...
USIKOSE SEHEMU YA 02
NB:HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA, SI RUHUSA KUTUMIA KAZI HII BILA IDHINI KUTOKA KWA MTUNZI
Tags
riwaya