MBINU ZA KULENGA SHABAHA KWA KUTUMIA BASTOLA NA MANATI
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Leo tupo katika kulenga Shabaha.
Tutaangazia ulengaji wa shabaha kwa kutumia silaha kama bastola, bunduki na manati na uhusiano wake katika kulenga shabaha katika maisha yetu ya kila siku yaani kutimiza vipaombele vyetu.
Ulengaji wa shabaha unahusisha akili, nguvu ya mwili na Hisia. Uwiano mzuri baina ya utulivu wa Akili, uimara wa mwili na mzunguko wa hisia wakati unalenga shabaha.
Kulenga shabaha ni kipaji na wakati mwingine ni ujuzi.
Haya Taikon nisiwe na maneno mengi msije mkachoka.
Hizi ni mbinu za kulenga shabaha kwa kutumia bastola;
1. Chagua mkao au pozi thabiti/ imara.
Kabla hujafikiria kulenga ikiwa huna uzoefu wa kulenga shabaha kwa kutumia silaha kama bastola au Manati basi ni muhimu kuchagua pozi au mkao thabiti kulingana na mwili wako. Hapa tunazungumzia mhimili wa mwili wako kuanzia kwenye mabega, mikono na miguu.
Hii utafanya hivi,
I) ule mguu wako ambao hauna nguvu utaupeleka mbele kidogo kisha utakunja goti katika pembe ndogo alafu mguu wenye nguvu utauweka nyuma lakini huu utakuta Straight.
Ãi) mabega na mikono utayaweka katika mhimili thabiti kuelekea mbele kidogo kuelekea mguu legevu lakini hakikisha unapata uthabiti
iii) Kwa upande wa manati, mkono dhaifu utashika kipago kile chenye umbo la V. Shikia kuanzia pale kwenye pembe ya V hakikisha unashika kipago hicho kwa uthabiti, kisiende kulia wala kushoto yaani Weka uwiano.
2. Usiweke pozi au mkao huo kwa muda mrefu.
Piga shabaha. Usikae muda mrefu. Hii hupelekea misuli yako kuanza kutetema na kama utapiga utapoteza shabaha.
Ukishapiga weka bastola chini au kama utapiga tena basi badilisha Angle(pembe) kisha piga tena. Ukipiga katika angle ileile ya awali ni rahisi kukosa kwa sababu ya mitetemo ya misuli.
Vuta manati yako huku macho yako yakiangalia katikati ya kipago ile V. Hakikisha unachokilenga(object) unakiona katikati chini na ndani kabisa ya ya V.
3. Tumia zaidi jicho lako lenye nguvu
Hakikisha jicho lako linaloona vizuri ndio ulitumie. Ukitaka kujua jicho lako ni lipi lenye nguvu yaani linaloona Vizuri (clear) fumba jicho moja kisha angalia kwa jicho jingine. Alafu fumba jicho lingine alafu angalia na lile jingine ambalo ulilifumba awali.
Jicho lenye nguvu ndio liwe msingi wa kulenga shabaha yako.
Wengine hufumba jicho moja lile wanaloliona ni dhaifu.
Kwa upande wa manati, jicho lenye nguvu lipite katikati ya kipago ile V ambapo lione object ndani ya V ikiwezekana kwenye pembe ya V pale chini.
4. Vuta Pumzi kisha Bana.
Hii hakikisha unaifanya baada ya kuona Shabaha. Hii itakusaidia kuzuia mitetemo na kutingishika.
Usibane pumzi kwa muda mrefu. Baada ya kuona target vuta Pumzi, achia
5. I-control Trigger(kilimi cha Bastola) vizuri.
Kidole ulichokiweka kwenye Kilimi cha bastola kisiwe sehemu ya mhimili wa mwili wakati unapiga shabaha.
Vuta kilimi kwa kushtukiza zingatia kidole kilichopo kwenye Kilimi kisiwe sehemu ya mhimili wa mwili. Hii itakusaidia kulenga shabaha. Ukivuta kilimi polepole uwezekano wa kukosa target ni mkubwa tofauti na ulivuta kwa kushtukiza yaani tap paaaap! Lakini sio taaaaaap! paaaap!
Kwenye manati, uzivute mipira ya manati kabla ya target kuipata. Ukishapata target vuta kwa kushtukiza kisha achia.
6. Kuwa na sehemu mahususi ya kulenga.
Kama ni kichwa au kifuani au miguuni.
Usipige shabaha pasipo kujua unalenga eneo gani la object. Hii itafanya akili yako kukosa utulivu na kushindwa ku- concentrate.
7. Ikiwezekana fundishwa na mlenga shabaha mzoefu.
Mbinu hizohizo ndizo zinatumika katika kutimiza shabaha katika vipaumbele vyako
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Tags
Fasihi