TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

VAILETH NA VANESSA

1 - 5
VAILETH NA VANNESA
WATOTO mapacha 
WSP 0743433005 
Full 1000..........***.............
Ni watoto wawili mapacha waliojikuta wanalelewa katika kituo cha watoto yatima cha Mtakatifu Maria kilichopo Kimara jijini Dar es saalam.
Jina la kulwa aliitwa Vaileth kwa kifupi Vai na Doto aliitwa Vannesa kwa kifupi walimwita Nessa.
Watoto hao walikuwa kivutio kikubwa sana haswa kwa wazungu wengi na watu wengi walokuwa wanakuja kufadhili kituo hiko cha mtakatifu Maria kwani walikuwa wacheshi sana pia walikuwa wazuri kwa sura na kufanana kwao pia kuliwavutia wengi sana.
Maana wasipoongea huwezi kuwatofautisha lakini Vai ndo alikuwa mcheshi zaidi ya Nessa.
Sio kuwa kituo hiki cha watoto yatima hakikuwa na watoto wengine.
Walikuwepo wengi tu ila watu wengi waliwapena Vai na Nessa zaidi kwa sababu ya uzuri na ucheshi zaidi ya watoto wengine pale kituoni. 
Mkuu wa kituo hiko walimwita Father alex na palikuwa na masista wengi sana ambao walikuwa wanalea watoto katika kituo hiko.
Wote walikuwa na umri wa miaka kumi.
Watoto hawa hawakubahatika kuendelea na masomo maana waliishia Darasa la tano kutokana na hali ya chini ya uchumi ya kituo hiko cha mtakatifu Maria.
Siku moja walikuja wageni kutembelea kituo cha mtakatifu Maria.
Ilikuwa ni familia ya Tajiri mmoja aliitwa Mr Danniel alienda kituo hiko kupeleka zawadi kidogo walizowanunulia watoto wa kituo hiko cha mtakatifu Maria.
Mzee Danniel aliongozana na mke wake na watoto wake wawili Ramson na Robson.
Ni familia iliojaliwa watoto wawili wa kiume wenye umri kati ya miaka 15 na 17.
"wanangu mnaona watoto wanavoishi maisha magumu"
aliongea mr.Danniel akiwaambia wanae kabla hawajashuka kwenye gari yao ya kifahari sana.
"baba unajua natakiwa saa kumi nikacheze Game maana nishalipa hela tufanye kilichotuleta tuondoke mda unazidi kwenda" aliongea Robson ambae ni mdogo kwa Ramson.
"mwanangu nimewaleta ili mjue wengine wanavoishi na mjue namna ya kuishi nao siku nyingne mtakuja kuwasalimia peke enu"
alijibu mama yao.
Wakati maongezi hayo yakiendelea Ramson alikuwa kimya akiangalia watoto wa kwenye kituo hiko wakiwa wansubiri kuwaona wageni waliokuja na Gari ni wakina nani.
Wengni walikuwa wanaligusa gusa gari hilo huku wakiwa na furaha tele.
"ona sasa wanavolichafua gari letu"
alifoka tena Robson
"mwanangu mbona huna utu wewe hebu tushuke tukawasalimie watoto wenzenu"
alijibu mama yao
"hawa sio wenzangu mimi, yan wenzangu ni wakina David tu sio hawa wachafu wachafu hata hawajasoma"
alijibu Robson.
Robson ni mtoto mwenye Jeuri sanaa na anamajivuno na mali za baba yake.
Lakini Ramson alifurahi sana kuwaona watoto wale walivokuwa wanaishi kwa Furaha mwisho Ramson alifungua mlango wa gari na kushuka watoto wa kituo cha mtakatifu Maria walimkubatia Ramson kwa Furaha sana wakiongozwa na Vai.
Lakini siku hyo Nessa alikuwa amekaa pembeni tu kwenye jiwe anaangalia.
"ona sasa wanavyomchamfua Ramson"
aliongea Robson kwa dharau
"we Ramson hebu rudi kwenye gari wanakuchafua hao"
Robson aliongea huku anamvuta shati kaka yake.
Lakini kabla hajamvuta kaka yake vizuri alishangaa mama yake akifungua mlango wa alipokuwa amekaa na kumwambia 
"shuka twende ukaone watoto "
Robson aliambiwa na mama yake
"i can't mom, they are very dirty "
aliongea Robson.
"Hebu nitolee ujinga wako mpumbavu mkubwa wewe hebu shuka kwenye gari humo"
alijibu baba yake kwa ukali.
Robson alishuka kwa shingo upande.
Walikaribishwa ofisini moja kwa moja na baada ya maongezi mafupi na Father Alex walzungushwa maeneo mbali mbali ya kituo hiko.
Ilikuwa ni mara ya pili kwa familia hyo kuja kuona watoto yatima hapo na huwa wanapeleka mafuta ,mchele, unga na vitu vidogo vidogo.
Lakini mama Robson alimwona mtot amekaa pembeni tu kwenye jiwe haongei na mtu akaamua kumfata alipokuwa amekaa
"ujambo mtoto mzuri"
aliongea mama Robby
"sijambo shikamoo"
alijibu Nessa.
"Marhabaaa unaitwa nani"
aliulizwa Nessa
"naitwa Vannesa"
alijibu Nessa.
"una jina zuri sana mtoto mzuri mbona umekaa hapa peke ako hujumuiki na wenzako"
aliulizwa Nessa.
"amna mama"
alijibu Nessa na kusimama akitaka kuondoka,
mama Robson alitamani kujua sana Vannesa anamatatizo gan hadi kawa mnyonge vile.
"Vannesa"
aliita mama Robby
"abeee"
aliitika Vannesa na kurudi.
"niambie mwanangu unamatatizo mimi nitakusaidia"
aliulizwa Vannesa kwa upole na kubembelezwa.
"nataka kurudi shule"
alijibu Vannesa huku akianza kulia.
"kwani husomi"
aliulizwa Vannesa kwa upole
"Mimi na dada Vai na watoto wengine wote hatusomi Father Alex hajapata fedha ya kutulipia ada, natamani na mimi nisome nije nisaidie yatima kama nyie mlivokuja, natamani na mimi niendeshe gari lakini sijaweza kusoma"
alijibu Vannesa huku akilia.
Maneno hayo yalimchoma sana mama Robby alijikuta akifuta machozi.
"usijali mwanangu Father Alex atapata Ada utarudi shule sawa eeh"
alijibu  mama Robby huku akitoa hela na kumpatia Vannes.
"hapana Mama kampe Father Alex ili anunue sukari tunywe chai"
alijibu Vannesa na kuinuka akaondoka.
Mama Robby alimshangaa sana yule mtoto kukataa hela....
#itaendelea......

Niliituma whatsapp hii hadithi but kuna people zimeomba nitume huku pia.....
Like page uendelee kupata story kali.....

VAILETH NA VANNESA
WATOTO mapacha 
WSP 0743433005 
Full 1000.
#ilipoishia
Mama Robson alishangaa sana mtoto yule kukataa hela
#sasa_endelea
Baada ya kukaa na watoto yatima kwa mda mrefu kidogo familia ya Mr.Dannyiel walikuwa wanataka kuondoka.
"kwaherini watoto"
walikuwa wanaaga.
Lakini Robson yeye alikuwa hataki hata watoto wale wamguse maana alikuwa anajisikia sana.
"karibuni tena"
aliitikia Vai ambae alikuwa anapendwa sana na wageni ambao huwa wanakuja kutembelea watoto.
Mama Robson alipomuona Vai alitabasamu.
Hakujua kama sio Nessa maana watoto hawa walifanana kiasi ila wakiwa pamoja Vai ni mrefu kiasi kwa Nessa.
Familia ile waliondoka zao.
Wakiwa njiani Mama Robison alianzisha maongezi.
"wanangu mmefurahi kukaa na watoto wenzenu kwa mda mfupi"
aliuliza mama Robson.
"ndio mama mimi nafurah wanavoishi kwa Furaha na wamechangamka sana"
alijibu Ramson.
"na wewe Robson je umefurahia"
aliulizwa Robby
"mama nitafurahi vipi kukaa na watoto wachafu vile na nilisema saa kumi nishalipa hela ya mashindano ya Game mnaona sasa ni saa ngapi? Siji tena mimi"
alijibu Robby huku akiwa na hasira.
Baada ya Robby kuchafua hali ya hewa mle ndani ya Gari palikuwa kimyaaa.
Walifika Nyumbani kwao mlinzi alifungua geti la nyumba yao ya kifahali na wote wakashuka na kuingia ndani.
Walikuta wafanyakazi wamepika chakula cha jion kila mmoja aliingia chumbani kwake.
Walioga na kushiriki chakula cha jion na kuingia ndani kupumzika.
Wakiwa chumbani Baba na Mama Robson.
Mama Robson alianzisha maongezi.
"mme wangu"
aliita mama Robson.
"niambie mke wangu"
aliitika Baba Robson.
"unajua sisi tumeishi mda mrefu sasa tukitafuta mtoto wa kike bila mafanikio"
alisema mama Robby
"ni kweli mke wangu"
alijibu mumewe
"sasa mme wangu pale kwenye kituo cha watoto yatima nimevutiwa na mtoto mmoja anaitwa Vannesa, ni mtoto mkarimu mpole na ana upendo unaonaje tukimchukua tumlee na tumsomeshe kama mwanetu"
aliongea mama Roby kwa kubembeleza.
"aaaaakh mke wangu yan leo tu ushatamani kuchukua na mtoto pale uleee"
aliuliza baba Robson
"ndio nimempenda sana yule mtoto huwezi amini pamoja na shida walizonazo nimempa hela amekataa anasema nimpe Father Alex ili anunue sukali wanywee chai"
alizidi kusisitiza mama Robby
"eeeeeeh amekataaa hela"
alijibu mumewe kwa mshangao mkubwa
"ni kweli mme wangu na ni mtaratibu sana"
alijibu mkewe,
"tutalijadili taratibu sasa hivi tupumzike maana kesho tunatakiwa kazini mke wangu"
alimjibu mumewe.
Mke wake alikubali na wakapumzika,
siku hyo ilipita na kesho yake palipokucha kama kawaida ya ile familia Baba Robby alijiandaa kwenda kazini na Robby na Ramson walipitiwa na basi la shule wakaenda zao shuleni.
Mama yao n mfanyabiashara anamiliki duka la nguo na vipodozi hvyo huwa anachelewaga kutoka kwenda kwenye biashara huwa anaondoka mida ya saa nne asubuhi hivi.
Lakini siku hyo aliondoka saa mbili akiwa na malengo yake mwenyew.
Aliwasha gari lake aina ya Benzi na kuondoka.
Mama Robby alipitiliza hadi kituo cha watoto yatima cha mtakatifu Maria.
Alipofika alienda kwenye ofisi ya kituo hiko.
"naomba kuonana na Father Alex"
aliongea mama Robson baada ya kumsalimia sista wa eneo hilo.
"Father Alex amesafiri kikazi safari ya Ghafla kwa wiki mbili kwa hyo tunawez kukusaidia unahitaji nini mama"
sista yule alijibu Jibu ambalo mama Robson hakulifurahia kabisa.
"asante"
alijibu mama Robby na kuanza kuondoka hapo kituoni.
............***..............
Siku zilizidi kwenda mbele huku mama Robby akilazimisha na kushikilia msimamo wake akitamani Vannesa aje aishi pale nyumbani akiwa hajui kama Vannesa ana pacha wake.
Baada ya Mume kukubali hilo swai waliamua kuwaambia watoto wao ili wajue wanaletewa mgeni mle ndani.
Wakati wa chakula cha jioni baba yao aliamua kuwaambia.
"wanangu"
alianza baba yao
"naaam!"
waliitika
"kuna mambo tunafatilia tukikamilisha hapa ndani tutakuwa tunamgeni hapa ndani na tutaishi nae wote kwa pamoja"
alimaliza baba yao
"mgeni gani?"
aliuliza Robby
"tumeamua kuwaletea mgeni ambae atakuwa ni dada enu hapa ni mtoto wa kituo cha mtakatifu Maria anaitwa Vannesa"
alijibu mama yao
"yani mama na baba mnaenda kuleta machokoraa humu ndani waje kuwa dada hapa ndani"
aliuliza Robby kwa dharau
"we mtoto wewe mdomo wako uo ukome"
alijibu Ramson
"ukome wewe mwenyewe mimi siwezi kukaa na machokoraa meza moja kula chakula kwanza hawajasoma pili wananuka tatu ni yatima watauwa wazazi wetu"
aliongea Robby kwa Jeuri na dharau na kuanza kuondoka akisusa chakula.
"Robbby.....Robby....."
hivi huyu mtoto yupoje?"
alifoka baba yake mzazi.
"mama mimi siwezi kukaa na masikini humu ndani huo ndo uamuzi wangu"
alijibu Robby
"sasa kama hii nyumba ni yako sawa endelea kuwa jeuri ila kama ni yangu na mama yako atakuja na atakaa hapa mpumbavu wewe na usile tena unamsusia nan chakula unajua kutafuta wewe"
aliongea baba yao huku akifoka sana
Robby alisimama sana pale njiani akajisemea moyoni mwake..
"nitajua cha kufanya siwezi kukaa na machokoraa humu ndani"
#ntaendelea_kesho

Like page usipite mashare, malike macoment.......

VAILETH NA VANNESA
WATOTO mapacha 
WSP 0743433005 
Full 1000.#ilipoishia

Robson alisimama akaisemea moyoni mwake
"nimepata wazo siwezi kuja kuishi na machokoraa huku ndani"
#sasa_endelea
Robson akatabasamu na kumjibu mama yake
"nimekubali mchukue tuishi nae"
mama yake akafurah sana na kumwambia
"nilikuwa nawaza sana mwanagngu unapepo gani"
Robby akauliza "kwani anaitwa nan"
"anaitwa Vannesa"
alijibu mama yake.
Robson alirudi mezan kuendelea kula chakula.
Baada ya kumaliza kula Walienda ndani kupumzika mezani walibaki Ramson Na Robson wakiwa wanajisomea.
"Ramson upo tayar kuish na yatima humu ndani?"
alivunja ukimya Robyson na kumuuliza kaka yake
"wanahaki ya kusaidiwa kwa hyo acha mama amsaidie huwezi jua atakuja kukusaidia nn"
alijibu Ramson
"Ramson usiwe hvo usikubali kuishi na chokoraaa atatuambikiza ufukara"
Roby alizid mshawish kaka yake.
"Roby hebu niache nisome acha makelele"
alikanya Ramson
Robson alikasirika sana baada ya kuona kaka yake anamkatalia anachotaka.
Walimaliza kusoma na wakaingia ndani kupumzika.
Kesho yake walijiandaa kwenda shuleni lakini Roby hakuwa na furaha.
Kama kawaida basi lilikuja kuwapitia na safar ikaanza.
Walifika shuleni ambapo wanasoma ila Roby hakuingia darasani wala nn alikaa tu nje.
"ingia darasan wewe"
kaka yake alimwambia mdogo wake
"hapana we tangulia darasan kwako mi ntaenda tu"
alijibu Roby.
Ramson anamjua mdogo wake anakiburi hvyo alimwacha na akaingia zake darasani kwake.
Baada ya Robby kumwona kaka yake kashaondoka aliangalia mazingira ya pale shule hakuna anamwona akatoroka zake.
Akakodi taksi
"unaenda wapi dogo"
dereva taksi akamuuliza Robby
"nipeleke mtakatifu Maria kimara"
alijibu Robby
"unayo 20 alfu."
dereva taksi alimuuliza Robby
"wewe nipeleke pesa sio tatizo"
alijibu Robby kwa jeuri.
Dereva taksi alimsikiliza mteja wake akampeleka moja kwa moja hadi kimara katika kituo hiko cha watoto yatima.
"nikusubiri au niondoke"
aliuliza dereva taksi
"usiondoke hadi nimaliza kazi yangu nitakulipa"
alijibu Robby
Robby alishusha kioo kidogo na kumwita mtoto mmoja jirani na kituo hiko.
"wewe mambo"
alisalimia Robby
"poa"
alijibu mtot huyo
"chukua hii hela nenda kule ndani kaniitie Vannesa"
alisema Robby huku akichomoa noti ya elfu kumi.
Mtoto huyu alifurahi sana kupewa hela hyo aliingia ndani ya kituo hko moja kwa moja na kwenda kumwita Vannesa.
"unaitwa Nessa"
alisema huyo mtot baada ya kuingia ndani.
"nani anamwita"
alidakia dada yake ambaye n Vai
"kwan wewe ndo Nessa"
alijibu huyo mtoto.
Nessa twende alisema mtoto huyo huku akimshika mkono Nessa na kuondoka nae.
Dada yake hakufurahi alisimama aangalie mdogo wake anaitwa na nan.
Akaona tu gari nyeupe hakujua nan yupo ndan waa anamwitia nn mdogo wake alihisi tu ni wageni wanaokujaga kuwaona pale kituoni.
Vai aliketi hakuhangaika tena.
"huyu hapa!"
alisema aliyetumwa baada ya kumleta Nessa.
"asante "
aliitika Robby na huyo mtoto akaondoka.
"ingia kwenye gari"
aliambiwa Nessa.
"hapana Father Alex akiniona atanipiga"
alijibu Nessa.
"aaaaakh we ingia hakuoni mtu"
alijibu Robby kisha akafungua mlango na kumvutia Nessa kwenye gari.
"dereva sogeza gari mbele kidogo"
aliamuru Robby
"hapana mimi siend popote"
alianza kuogopa Nessa
"nan akuchukue wewe chokoraaa tulia"
alijibu Robby.
"sikiliza wewe nina jambo moja tu nataka kukwambia sitaki nikuone unakuja kukaa kwenye nyumba yetu.
Na ole wako maama angu aje akufate ukubali"
alionya Robby.
"kwani mimi nakaa kwenu"
aliuliza Nessa 
"nini wewe? Unanijibu mimi hvo"
Robby alifoka sana akamshushia kibao Nessa
"nimesema usije kujaribu kuja kwetu kukaaa maana nitakuua"
Robby alisema tena huku akimtishia Nessa kumkaba.
Nessa alikuwa analia tu maana hakuelewa anaenda vipi kwa kina Robby.
"sitaki makelele humu"
aliamuru Robby tena.
Muda wote huo Robby anafanya hayo dereva taksi alikuwa kimya tu.
"toka kwenye gari humu"
aliamuru Robby huku akimpiga Nesa.
"nasema tokaaa masikini mkubwa wewe"
Nessa alikuwa anahangaika tu maana hakujua mlango unafunguliwa vipi.
"Bado unazidi kubaki wewe chokoraaa huelew Toka"
Robby akagundua hajui kufungua mlango wa gari.
Robby alifungua mlangu Nessa akaanza kushuka taratibu Robby akamsukuma Nessa hadi Nessa akaanguka chini.
"ondoa gari na wewe"
Robby alimwamuru dereva.
Nessa alipoanguka tukio hilo aliliona dada yake Vai.
Vai alikimbia na kumwinua mdogo wake pale chini.
"kwanini umepanda gari la watu na yule ni nani"
Vai alimuuliza Nessa maswal mfululizo
lakini Nessa hakujibu kitu alikuwa analia tu.
"umeumia au"
Nessa aliulizwa tena.
Lakini hakujibu kitu.
"weew mimi si nakuuliza au hadi mimi unanificha"
alifoka Vai.
"niache"
alijibu Nessa
"nikuache nni  hebu niambie tatizo nn"
aliuliza tena Vai
"nimepigwa na mtu me simjui anasema nisiende kwao"
alijibu Nessa.
"haiwezekani mtu aje akupige bila kosa kwann hajamwita  mtu mwingne hadi akupige wewe utakuwa unamjua wewe kama huniambii ntakusemea kwa Father Alex"
Vai alimtisha Nessa.
"mimi simjui kweli sikudanganyi"
alizidi kukana Nessa.
#itaendelea

Like page, share twenzetu na vigongo vipya.....kila day.....Hadithi...VAILETH NA VANNESA
WATOTO mapacha 
WSP 0743433005 
Full 1000.
#ilipoishia
"haiwezekani mtu atoke huko aje akupigi, kwa nni asimwite mtu mwingne, kama husemi ukweli ntamwambia Father Alex"
alitisha Vai
"mimi simjui kweli"
alizidi kukana Nessa
#sasa_endelea
"kama humjui kweli twende tukamwambie Father Alex maana huyu mtu atakuja tena kukupiga"
Vai alimwambia mdogo wake
"hapana dada hawezi kunipiga tena wala hawezi kuja tena maana ataogopa tusiseme"
alisema Nessa.
Nessa ni mtoto mtulivu sanaaa na mwenye upendo mwenye kujua kuvumilia changamoto zote za maisha hvyo alivumilia lile tukio na kulipotezea.
.................***...................
Baada ya Robby kuondoka eneo lile alipitiliza moja kwa moja shule japo alichelewa lakini aliingia darasani.
Hakuna aliemuuliza umetoka wap maana begi lake lilitangulia hvo walimu walijua alikuwepo maeneo ya jirani.
Baada ya vipindi kuisha kama kawaida walitawanyika kila mtu alipanda basi lake  na kurudi nyumbani.
...........*%*............
Siku zilizidi kusonga mbele huku mpango wa mama na baba Robby kwenda kumchukua Nessa ukianza.
Waliamua kwenda kuongea na Father Alex.
Siku hyo walienda bila watoto wao.
Father Alex aliwasikiliza kwa makini lakini hakuwa tayar kumwacha wamchukue Nessa maana hakujua wanadhamira gani.
"utaratibu wa kuchukua watoto hapa lazima uwe na barua kutoka ustawi wa jamiii, kituo cha polisi pia upite kanisa la katoriki hapo wakikukubalia sisi hatuna shida tutawapa.
Kwani mnataka mtoto gani"
aliuliza Father Alex
"anaitwa Nessa"
alijibu mama Robby.
"aaaaaaakh Mungu wangu mnamtaka Nessa tena!?"
aliuliza Father alex kwa mshangao
"ndio"
alijibu baba Robby
"hapana haiwezkani kumchukua Nessa peke yake maana hapa Nessa anapacha wake anaitwa Vai hivyo siwezi kumuacha Nessa akaondoka peke yake bila Vai"
alimaliza Father alex
"Mungu wangu Nessa anapacha!"
alishangaa mama Robby
"ndio"
alijibu Father
"tunaomba utuitie wote"
aliomba mama Robby ashuhudie mwenyewe.
Baada ya ombi hilo Father Alex aliwaita Vai na Nessa ili waje wawaone.
Baba na mama Robby walishangaa sana jinsi watoto hawa walivofanana.
Hata mama Robby alishindwa kumtambua Nessa ndo nani.
Aliwaangalia mmoja mmoja.
Nessa akatabasam baada ya kumwona mama Robby lakini Vai alipoona Nessa katabasamu na yeye akatabasamu hvo wakamvuruga kabisa mama Robby hakujua nani Nessa nani pacha wake.
"kama unavowaona hawa watoto hatuwezi kuwatenganisha"
alisema Father Alex
"sawa itabidi tuwachukue wote"
alijibu baba Robby
Nessa aliposikia kuchukuliwa alikumbuka lile tukio la kupigwa kisa kuchukuliwa.
Alikumbuka yule mtoto alomwambia atamuua endapo ataenda kwao.
"mimi siendi popote pale nitakaa hapa hapa kituoni"
alisema Nessa huku kainama chini.
"kama Nessa haend na mimi siend popote pale"
alidakia Vai.
Father Alex na wazazi wa Robby na Ramy walishangaa kwann watoto hawa wanakataa kwenda kukaa kwenye familia ya kitajili kama ile.
"kwanni wanangu hamtaki kuishi na sisi"
aliuliza mama Robby
Hakuna aliejibu wote walikaa kimya.
Father alex alishangaa sana maana hakuna mtoto anaechukuliwa kwenda kulelewa akakataa.
"Father Alex tunafanyaje sasa"
aliuliza Baba Robby.
"usijali nendeni niongee nao ntawapa majibu kesho"
alijibu Father Alex na wote wakaondoka.
"Nessa na Vai rudini hapa."
aliamuru Father Alex maana alikasilika wale watoto kukataa kwenda na ukizingatia ile familia inaletaga sana msaada pale kituoni.
"kwanini hamtaki kwenda kulelewa na wazazi wenye upendo kama hawa"
aliuliza Father Alex.
Lakini wote walikaa kimya.
"sisi tunapenda kukaa hapa"
alijibu Nessa
"tena wewe Nessa ndo uliefatwa mwenzako angesafiria mgongo wako ona unavomfanya mwenzako asisome ona lakini Nessa. Mngeenda kusoma shule nzuri huko, maisha mazuri tena mngefanikiwa mngekuja kusaidia watoto wenzenu wenye shida hapa"
aliongea father Alex maneno yaliyomchoma sana Vai.
"kwani wale watu wanataka kutusomesha"
alihoji Vai.
"ndio"
Father alex alimjibu.
"sawa tutakupa jibu baadae"
alijibu Vai.
"hapana Father Vai atakupa jibu lake baadae ila mimi sipo tayari"
Nessa alishikilia msimamo wake
"Vai nenda Nessa ubaki hapa"
aliamuru Father Alex.
Baada ya Vai kutoka Father Alex alianza kumbana nessa kwa maswali akitaka kujua kwann hataki kukaa nyumba ya Mr.Danniel.
"mimi nataka kukaa hapa tu"
alijibu Nessa.
Nessa hakutaka kusema ukweli kwanni hataki kwenda kwenye nyumba ya Mr.Danniel.
Alihisi aliekuja kumpiga na kumtishia ni mtoto wa Mr.Danniel.
"wewe sio mtoto mzuri tena kama husemi ukweli nini kinakufanya ukatae haya mtoto mbaya kaendelee na mambo yako" alijibu Father Alex.
"mimi sio mtoto mbaya"
Nessa alijibu huku akianza kulia.
"mtoto mzuri akiulizwa kutu anajibu ila wwe unaeficha siri ni mtoto mbaya"
Father Alex alizidi kumchimba Nessa.
Nessa alilia huku akidai yeye ni mtoto mzuri.
"kama wewe ni mtoto mzuri niambie kwanini hutaki kwenda"
Father Alex aliuliza.
#itaendelea....

Fanya kulike ma page usiachwe hata siku moja kwa hadithi kali na bomba......

VAILETH NA VANNESA
WATOTO mapacha 
WSP 0743433005 
Full 1000.
#ilipoishia
"kama wewe ni mtoto mzuri niambie kwanini hutaki kwenda"
aliuliza Father Alex
#sasa_endelea
Nessa hakutaka kusema chochote,
"nimepazoea tu hapa siwezi kukaa mbali na watoto wenzangu"
alidanganya Nessa.
"utakuwa unakuja kutuona sawa mtoto mzuri"
alizidi kumchombeza Father Alex
"sawa nimekubali"
alikubali Nessa kwa shingo upande.
Father Alex  alifanya mawasiliano na Mr.Danniel  kuwa mambo yamekaa vizuri.
Mr, Daniel na mke wake walianza kufata taratibu zote kwa ajili ya kuwachukua watoto wale kwa ajili ya kuwalea na kuwasomesha.
Ndani ya wiki moja taratibu zote zilikamilika na waliamua kufanya sherehe kidogo pale kituoni kuwaaga Vai na Nessa maana wanaenda kuanza maisha mapya.
Watoto wenzao walilia hata masista wa pale kituon nao walitoa machozi maana Vai na Nessa ni watoto wanaopendwa sana pale kituoni pia walikuwa ni kama kivutio kwa uzuri wao na ucheshi japo Vai ndo aliezidi ucheshi.
Baada ya hafla fupi kuisha mr.Danniel waliondoka na mke wake kwenye gari alipanda Vai na Nessa.
Gari ilipoanza kuondoka watoto wenzao walianza kulifata waliona ndugu zao wanawaacha.
Hata Vai na Nessa walikuwa wanalia kwenye gari.
Father Alex hakulia japo moyo ulimuuma.
Gari iliondoka na walienda moja kwa moja kuwafanyia shopping.
Waliwatengene nywele zao hadi wakawa na hadhi ya kitajili kama familia ya mr.Daniel.
Baada ya kuzungushwa mjini maeneo mbali mbali na kununuliwa kila walichoona kinawafaa mapacha hawa walipita sehem kwa ajili ya kula.
Baada ya kukamilisha taratibu zote walianza safari ya kurudi nyumbani.
Watoto hawa walifurahi kwani walikuwa wanaenda kuanza kusoma ila hawakufurahi kukaa mbali na wenzao waliowazoea kuwa nao pamoja siku zote.
Gari liliondelea kwenda huku Mr.Danniel akiwa anaendesha na mke wake alikuwa anawaangalia watoto hawa walivokuwa wazuri alikuwa anajifuta machozi kwa kitambaa chake cha mkono.
Gari lilifika nyumbani kwa mr.Danniel.
Geti kubwa lilifunguliwa.
Nessa n Vai walikuwa wanashangaa nyumba ilivyokuwa kubwa yenye ghorofa mbili.
Walishangaa jinsi magari ya kifahari yalivokuwa yamezunguka nyumba ya mr.Danniel.
Hawakuamini kama wao wataishi katika hiyo nyumba.
"nessa na Vai, tumefika wanangu hapa ndo nyumbani"
alisema mama Robby.
"asante mama"
walijibu kwa pamoja.
Walifunguliwa mlango wa gari kisha wakashuka.
"bakariiii we bakariiii"
aliita mr.Danniel.
"ndio bosi"
alikuja mlinzi aliyekuwa getini
"shusha hvi vitu vya kwenye gari vyote upeleke ndani mwite na amina mshirikiane"
aliamuru Mr.Daniel.
"sawa bosi"
alijibu Bakari.
Mr.Danniel alianza safari ya kuingia ndani.
"twendeni wanangu"
alisema mama Roby.
Waliinia ndani walishangaa kuona kule ndani kulivo kuzuri.
Hawakuamini kama wao ndo wataishi katika mjengo kama huo.
Walikumbatiana huku machozi yakiwatoka.
"msijali wanangu mambo ya kawaida"
aliwaambia mama Robby.
Walionesha chumba chao cha kulala ambacho kina choo na bafu humo humo.
Walikataa kukaa vyumba tofauti.
Baada ya kuzungusha humo ndani na kutambulishwa wafanyakazi wa humo ndani.
Walikaa kwenye masofa wakiangalia televisheni.
Ilifika misa ya saa kumi Robson na Ramson wanatoka shuleni.
Basi liliwaleta na waliingia ndani.
Hawakuamini kuona watoto kama malaika wamekaa kwenye makoch walivofanana.
"heee makubwa haya yani mama kaamua sasa kutoa fotokopi ya yule chokoraaa akaleta wawili.
Ramson tukifanya mchezo hawa watatoana fotokopi wataletwa wengine"
alisema Robson kwa dharau.
"hebu kelele mbona una matatizo sana wewe"
ramson alimkanya mdogo wake na kwenda kuwasalimia Vai na Nessa.
"hamjambo"
alisalimia Ramson maana yeye anamiaka 17 na hawa ni watoto wa miaka 11 tu.
"hatujambo shikamoo"
walisalimia kwapamoja Vai na Nessa.
"marhaba mnaitwa nan"
aliuliza Ramson.
"mimi vai na huyu Nessa"
alijibu Vai.
"wewe nessa nilikuambia nini"
alidakia Robson kwa ukali, hadi nessa akaanza kuogopa.
"nakuuliza nilikuambia nni?yani nilichokwambia hujafanya ukaamua kumbeba na chokoraa mwenzako ukamleta humu ndani"
alifoka Robson.
"roby unavuka mipaka hivi we mtoto wangu kweli mbona huna adabu wala heshima"
alidakia mama yake ambae alikuwa amesimama kwenye ngazi akiangalia maongezi na mapokezi ya wanae kwa wageni.
"mama haiwezekani uokote machokoraa ukaleta hapa me siwezi kuishi nao"
alidai Robby.
"kama huwezi utaenda kukaa bording au kwa bibi yako mpumbavu wewe"
alidakia baba yake ambaye alitoka baada ya kusikia sauti ya mwanae Robby maana anamjua ni kichaa.
"kijijini siendi na boarding siend na hawa watajuta kuja kukaa kwa watu kwani misaada tunayowapa haiwatoshi ndo maana ni yatima"
alizidi kufoka Robson
kauli iliyowafanya Nessa na Vai kuona maisha ya ile nyumba magumu sana maana siku ya kwanza tu tena masaa machache tu wanatukanwa vile hawakujua siku zingine itakuwaje.......

#itaendelea.....

Special for team popo kama kuna popo yupo macho aje inbox tuchat kidogo so lonly then sina usingizi.....
Soma mpaka mwisho kwa sh 1000
Soma kupitia whatsapp inbox namba ni 0743433005 *Kama upo KENYA 🇰🇪  na unataka HADITHI, kutuma pesa kwenda TANZANIA 🇹🇿 kwa kupitia M PESA fuata process hii* 👇🏿👇🏿
_NB: Minimum amount ni Ksh 101_

1. Dial 📞  *840# kwenye simu yako ya mkononi.

2. Chagua "Tuma Pesa Nje ya Nchi"

3. Chagua "Tanzania".

4. Ingiza nambari ya simu ya mpokeaji wa pesa nchini Tanzania. *_Kwa ajili ya simulizi tumia namba hii  255743433005 uandike ilivyoandikwa hapa_* jina la mpokeaji/recipient  ni *AGOSTINO NDOSSI

5. Ingiza kiasi cha pesa unachotaka kutuma Starts at 101Ksh

6. Chagua chanzo cha mapato yako.

7. Chagua sababu ya kutuma pesa. (Malipo)

8. Ingiza nambari yako ya siri ya M-Pesa.

*Bonyeza "Tuma/Send* na itanifikia bila shida, ukishalipa nitaarifu kupitia WhatsApp nikutumie story yako uliyolipia au ulizolipia

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post