TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

BARUTI 3

𝗝𝗜𝗡𝗔 𝗟𝗔 𝗥𝗜𝗪𝗔𝗬𝗔: 𝗕𝗔𝗥𝗨𝗧𝗜 (𝗪𝗔𝗞𝗜𝗟𝗜 𝗠𝗪𝗘𝗠𝗔)
𝗠𝗧𝗨𝗡𝗭𝗜: 𝗝𝗨𝗦𝗧𝗜𝗡 𝗕𝗔𝗥𝗨𝗧𝗜
𝗠𝗪𝗔𝗞𝗔: 2024/2025
𝗦𝗠𝗦 & 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣: +255 752 474 397

𝗦𝗘𝗛𝗘𝗠𝗨 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗧𝗨
𝗜𝗟𝗜𝗣𝗢𝗜𝗦𝗛𝗜𝗔
Maskini binti wa watu hakujua, akamshika begani Baruti kama ishara ya kumuita, wakati anamuita gafla moyo wa Baruti ukashtuka paah! hakuamini alichokiona mbele ya macho yake

Baruti alikutana na binti mmoja mrembo sana anayevutia lakini alikuwa ni mlemavu wa ngozi jina lake aliitwa Brianna, walikuwa awafahamiani kabisa ndio mwanzo wao wa kujuana

"Usiniogope.... usiniogope"

Yalikuwa ni maneno ya upole toka kwa Brianna, lakini Baruti alikuwa ni muoga katika maisha yake, alizoea kujitenga na kukaa peke yake

Jennifer alienda kwa baba yake kumuuliza Baruti yuko wapi;

"Baba, Baruti yuko wapi"

"Eti baba Baruti yuko wapi hivi umeshindwa kujiandaa uende chuo upo na huyu kijana...sawa nimemtuma dukani aniletee mkate"

"Lakini baba"

"Lakini nini..."

"Baba unayofanya kwa Baruti sio mazuri, kumbuka yeye ni binadamu kama walivyo binadamu wengine, anastahili kupendwa na kuthaminiwa utu wake, nadhani hapa tulipofika ni pabaya, kuanzia leo nisipomuona humu ndani, nipo tayari kuhama hii nyumba"

𝗞𝗶𝗽𝗲𝗻𝗱𝗮 𝗿𝗼𝗵𝗼 𝗵𝘂𝗹𝗮 𝗻𝘆𝗮𝗺𝗮 𝗺𝗯𝗶𝗰𝗵𝗶, kile upendacho kukifanya huna budi kukipenda na kukithamini kwa moyo wako wote

Jennifer alikuwa na mapenzi makubwa sana kwa Baruti, alimchukulia kama rafiki mkubwa sana wa maisha yake, licha ya changamoto mbalimbali walizopitia walikuwa wakifarijiana

Baba Jennifer alivyomtuma Baruti dukani kununua mkate alikuwa jambo sahihi, ukizingatia kwamba hata ndani ya nyumba yao mkate ulikuwepo, hapa kuna jambo la siri limepangwa dhidi ya Baruti, endelea mbele ya riwaya hii utajua

Halikuwa jambo rahisi kwa Brianna kumzoea mtu yoyote katika maisha yake, ukizingatia kwamba yeye ni mlemavu wa ngozi yaani albino, anastahili ulinzi wa kutosha

Baruti baada ya kukutana na Brianna alikuwa anamuogopa sana na akatamani kukimbia asije akapewa kesi ya mauaji

"Wewe ni nani" aliuliza Baruti

"Mimi naitwa Brianna, ni mwanafunzi wa kidato cha nne, naishi hapo mbele kidogo....hapa ni kama nimepita una tatizo gani nikusaidie"

"Mwanafunzi...? binti sikia nikwambie, mimi sikujui wala sikufahamu naomba tusikutane tena, kwaheri"

"Jamani we kaka umekuaje"

"Nimesema hunijui sikujui kwaheri"

Baruti akatoka mbele ya huyu binti, akakimbia kwenda dukani kununua alichoagizwa, kufika dukani masikini anajikuta mikono mitupu, hata hela ya kununua mkate hajui ilipo

Akageuza njia kurudi alipotoka, alianza kutafuta pesa lakini hakuiona, macho yake yakagongana na Brianna

Brianna akatoa elfu tano na kumkabidhi Baruti ili amalize tatizo lake

Baruti alirudi nyumbani, kilichokuta hakuamini, alipigwa kofi zito la kushtukiza na Baba Jennifer baada ya kuona mkate na kurudi nyumbani amechelewa

"Hivi we kijana nimekutuma maandazi au mkate"

"Boss umesema mkate" alijibu kwa woga

"Nimesema maandazi sio mkate, usiniletee ujinga na hayo matatizo yako, nipo tayari kukufukuza humu ndani, kuhusu kazi sahau, kesho beba vitu vyako uondoke naleta mtu mwingine"

Baruti baada ya kusikia hivo alihuzunika sana na kumbembeleza boss wake asimfukuze kazi lakini juhudi zake ziligonga mwamba, alikubali matokeo...!

𝗠𝗔𝗠𝗕𝗢 𝗬𝗔𝗠𝗘𝗞𝗨𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗭𝗜𝗧𝗢...!

𝗕𝗔𝗥𝗨𝗧𝗜 𝗔𝗧𝗔𝗘𝗡𝗗𝗔 𝗪𝗔𝗣𝗜 𝗡𝗔 𝗝𝗘𝗡𝗡𝗜𝗙𝗘𝗥 𝗔𝗧𝗔𝗝𝗜𝗦𝗜𝗞𝗜𝗔𝗝𝗘...?

𝗜𝗧𝗔𝗘𝗡𝗗𝗘𝗟𝗘𝗔 𝗦𝗘𝗛𝗘𝗠𝗨 𝗬𝗔 𝗡𝗡𝗘

𝗞𝗨𝗛𝗨𝗦𝗨 𝗛𝗜𝗜 𝗥𝗜𝗪𝗔𝗬𝗔

𝗕𝗮𝗿𝘂𝘁𝗶 𝗻𝗶 𝗿𝗶𝘄𝗮𝘆𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗯𝘂𝗻𝗶 𝗶𝗹𝗶𝘆𝗼𝘁𝘂𝗻𝗴𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗮𝗻𝗱𝗶𝗸𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗝𝘂𝘀𝘁𝗶𝗻 𝗕𝗮𝗿𝘂𝘁𝗶 𝗶𝗻𝗮𝘆𝗼𝘇𝘂𝗻𝗴𝘂𝗺𝘇𝗶𝗮 𝗸𝘂𝗵𝘂𝘀𝘂 𝗺𝗮𝗶𝘀𝗵𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝗶𝗷𝗮𝗻𝗮 𝗺𝗺𝗼𝗷𝗮 𝗮𝗹𝗶𝘆𝗲𝗷𝗶𝘁𝗼𝗮 𝘂𝗵𝗮𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗶𝘀𝗵𝗮 𝘆𝗮𝗸𝗲 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗸𝘂𝗽𝗮𝗺𝗯𝗮𝗻𝗮 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝘂𝗮𝗷𝗶 𝘆𝗮 𝗮𝗹𝗯𝗶𝗻𝗼 𝗻𝗮 𝗯𝗶𝗮𝘀𝗵𝗮𝗿𝗮  𝗵𝗮𝗿𝗮𝗺𝘂 𝘆𝗮 𝘃𝗶𝘂𝗻𝗴𝗼 𝘃𝘆𝗮 𝗯𝗶𝗻𝗮𝗱𝗮𝗺𝘂 𝗻𝗮 𝗵𝗮𝘁𝗺𝗮 𝘆𝗮𝗸𝗲 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗸𝘂𝗹𝗲𝘁𝗮 𝗵𝗮𝗿𝗮𝗸𝗮𝘁𝗶 𝘇𝗮 𝘂𝗸𝗼𝗺𝗯𝗼𝘇𝗶 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗷𝗮𝗺𝗶𝗶

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post