NILIOLEWA NA WAKWE NA SIO MUME
1-05
Naitwa Ratifa ni mtoto wa kwanza kwa mama yangu kuhusu baba sijui maana yeye alinikana tangu tumboni nimelelewa na bibi na babu pamoja na mjomba maana alikua na mchango mkubwa kwenye mkuuji wangu tulikua tunaisha kijiji X mkoni pwani yani nikisema kijijini naamaanisha ndani ndani huko mbwinde kabisa
katika maisha yangu ndoto yangu kubwa ilikua ni kujakuishi Dar yani nilikua tayar nije huku kwanjia yoyote sikutaka kuzeekea kwenye kijiji kile japo ndio sehemu niliyozaliwa lakini sikutaka kabisa maisha yangu yawe kule basi nilisoma nikamaliza darasa la 7 niliamua kijifelisha makusud maana sikutaka kuendelea na masomo niliamini nitapoteza muda na nitachelewa kuzifikia ndoto zangu
kweli majibu yalitoka mimi sikuweza kuendelea kwanza hata huko kusoma ni changamoto shule ni mbali sana pia maisha ya pale nyumbani ni magumu sana yani hata wakati nasoma shule ya msingi nilikua napitia changamoto had nilikua naomba nimalize tu
Mama yangu nae alipata mwanaume akamuoa alikua anaishi kijiji cha tatu kutoka hapa kwa babu niliona kabisa kama sitojipambania mwenyewe nitazeekea kule maana babu alizaa watoto 3 wakwanza mjomba ambae alikua mlezi wangu mkubwa wapili mama na huyu wa tatu ni mwanaume ila kwakipind hicho yeye alikua yupo Dar ila bado hakua na maisha mazur na yeye ndio alikua akinipa ahad nyingi kwamba siku moja atakuja kunichukua twende tukaish Dar
tamaa yangu kubwa nilitaka kuja kufanya kazi za ndani niliamini ndio utakua mwanzo wangu mzur wa kuingia jiji la Dar lakini babu yangu alinikatalia mimi kuja kufanya kazi za ndani kwa sababu yamakosa aliyowahi kuyafanya mama yangu alikuaja Dar kufanya kazi matokeo yake aliambulia mimba tu isiyo na baba ndio nikazaliwa mimi familia ilichukia sana kile kitendo kwahy hawakutaka kulisikia tena hilo swala la kwenda mjini kufanya kazi za ndani kwa mtoto wa kike
niliumia sana maana rafiki zangu wengi waliondoka kuja mjini kufanya kazi za ndani mimi ndio nilikataliwa kipind hicho nina miaka 15 nikajiona mjinga bora ningesoma nisogeze umri na mambo ya kijijini sio muda nitaozeshwa kweli bwana nilikaa nyumbani miaka 2 nikawa nishatimiza 17 wachumba hawakauki nyumbani kutaka kuja kunioa nilikua nakataa na kwabahat nyumbani wahakua wakinifosi nashukuru mjomba alikua muelewa sana nilimwambia kama nitakua tayar kuolewa basi nitasema
nilipata kibarua rafiki yangu aliniunganishia alipokua anafanya kazi ila ni mbali na nyumban lkn tulikua tunaenda na kurud kwa basker yule mwezangu hakua na ndoto nyingi maana alishakua na mahusiona tayar walikua wanaishi pamoja na mchumba wake
watu weng wakikijini walipata kazi mahar pale kulikua na shamba kubwa kama heka 10 nililizungushiwa uzio ndani ya shamba kulikua shughur nyingi za kilimo na ufugaji wa kuku wa madoli wale wamayia kwahiyo kulikua kunazalishwa mayai mengi maana kuku walikua wengi sana na walikua wanalima mazao ya biashara kama matikiti maji na mengineyo kwahiyo sisi tulikua tunafanya kazi mbali mbali tulikua tunalipwa kwa siku 3000 ilikia pesa nyingi kwa kijijini na hiyo kazi yake sio ndogo ukirud mgongo wote aufanyi kazi
niendelea na ile kazi miez 6 ilikua kumuona boss ni mara moja kwa wiki isipokua wasaidi wake boss alikua anakuja kila j mosi kuja kufata mayai na kuya safirisha mimi kazi yangu ilikua kuokota mayai nilikua nakoma jamani nachoka hatar tunaokota asubuh na jioni
basi nilipata bahat ya kupendwa na bosi alikua akija hataki nifanye kazi anataka tuongee tena wote mtu namkewe walikua wastaafu na ndio wamiliki wa pale jamani nilikua natamni kila siku iwe j mosi nauvivu wangu
walikua wakinihoji mambo mengi kuhusu maisha yangu nilikua sifichi niwaambia kila kitu waliniuliza kama nipo tayar kuolewa maana wamenipenda niwe mkamwana wao kuna mtoto wao mmoja bado ajaoa nilibaki natabasamu tu maana niliona kabisa naenda kutimiza ndoto yangu ya kwenda kuishi Dar. narud
NILIOLEWA NA WAKWE NA SIO MUME 2
Basi nilikua nafuraha sana niliona naenda kuitimiza ndoto yangu ya kwenda kuishi Dar yani nilishapanga mipango mingi nikamua kumuuliza shangazi hv kama nitapata mchumba mtaniruhusu niende Dar kwanini unaniuliza kwani tayar ushapata mchumba nini hapana bado sijapata ila nimeuliza tu nataka kujua atuwezi kukuzuia kama ukiolewa basi utakua cyo mali yetu tena utakua upo chini ya mumeo kwahy mnaweza kwenda kuishi popote
nilifurah nikaingia zangu getoni kwangu asubuhi ikafika nilikwenda kwenye majukumu yangu nilikua nafanya kazi nikipata pesa nampa mjomba ili isaidie majukumu ya nyumban ndio alikua kama baba kwangu na bahati mbaya hawakujaliwa kua na mtoto kipindi hicho kwahy nilikua kama mtoto wao
wakati tukiwa njiani kuelekea kazini nikawa naongea na rafiki yangu aitwa Mamu ndio yule aliniunganisha kazini nilikua nashauku kubwa nikamwambi mwezio nitaondoka Dar muda si mrefu kwanani kwa mume wangu nikamjibu kwamumeo kwahy unataka kuolewa aliuliza nikamwambia ndio nimepata mchumba tukioana tu naondoka zangu
Ratifa rafiki yangu huyo mwanaume umekutana nae wapi maana muda wote tupo kazini isiwe yule supervisor kashaanza kukudanganya mimi namjua yule hakuna muoji pale maana hiyo ndio gia yake yakuwapata wasichana wa pale wengi kashatembea nao
nikajibu hapana bwana siyo yule ni mtu mwingine tofauti siwezi kunasa kwenye mtego wake si unaujua msimamo wangu nakushukuru sana rafiki yangu kwakunimbia mambo mengi kuhusu huyo supervisor wala sina mpango nae alinitongoza nimemkataa mimi sina mpango wakuolewa huku hata hivyo ndio maana sitaki kujiingiza kwenye mahasiano na mtu mwisho akanipotezea ndoto zangu zakwenda kuishi Dar
hv huko Dar umesikia kuna nini hasa rafiki yangu hadi kumekuchanganya kias hicho kwahy mfano asipotokea mtu wa Dar hautoolewa nikajibu nitaolewa ila nitachelewa sana maana hapa nilipo hata miaka 18 bado siwezi kujikatia tamaa Mamu sitaki kuzeekea huku huo ndio msimamo wangu
nitabadilisha msimamo labda nione nishafika miaka 30 sijapata mwanaume wa Dar alicheka sana Mamu haya ngoja tuone kwahy huyo shemeji yangu umepanga kunitambulisha lini nikamwambia cjui maana hata mimi mwenyewe cmjui pia sijawah kukutana nae
Vp kama ukimwona alafu ujampenda nikajibu bwana we labda acnipende yeye lkn kwa upande wangu vyovyote alivyo nitampokea
kwahy wazazi wake ndio wamekupenda ndio wamendipenda niolewe na mtoto wao
ukoo gani huyo mwanaume uwenda nikamjua kwawale wandengereko wanapenda kutumia majina ya ukoo nikamwambia umjui bwana
maana tulikua tunafanya kazi sehemu moja ila majukumu tofauti kwahy tukiingia kazini kila mtu anaenda kwenye jukumu lake hata maboss wakija mara nyingi wanafikia huku kwenye kuku ndio ilikua shabaa yao kubwa ya biashara
huku upande wa kilimo hua kuna muda kama mnavyojua mazao yakivunwa yaandaliwe tena
basi stor ikaishia pale tulifika kazini kama kawaida ilikua j mosi nilikua naipenda hii siku maana nakua na maboss tu wananituma tuma mimi naona rah tu nilikua najikuta kama tayar nishakua mkwe wao
waha boss zangu ni watu wadini ya huyu wakike alikua navaa majuba na nikabu dini iliwajaa sana
tulikua tunaongea mambo mengi wakaniuliza kama naweza kuishi na mazingira yao maana wao awataki mtu mapepe anataka mtu aliyetulia nilikua naitikia kila kitu nipo tayar
siku hiyo boss wangu wakike alinipa zawad
niliipokea nikaifungua nilifurahi kuona kilicho ndani boss aliniambia nimezipenda ndio maana nikakuchukulia natamani kukuona ukiwa umevaa basi ilikua zawadi ya nguo niliingia ndani nakuanza kujaribu moja moja ziliinipendeza sana sikuwai kuvaa nguo mpya toka kukua kwan mara nyingi nilikua navaa nguo za kupewa kutoka kwa ndugu muda mwengine zinakua kubwa basi unavaa hivo hivo yani yale maisha ya nyumbani yalinifunza mengi ndio maana nilitamani sana kuyapambania maisha yangu sikutaka kabisa kuishi pale
alinisifia umependeza sana mwanangu nikajibu asante mama kwa zawad ila siwezi kuchukua aliniuliza kwanini nikajibu hata kama nikichukua siwezi kuzivaa lkn nimekuletea wewe Ratifa aliniambia siwezi kuchukua hizi ni nguo ni gharama sana nyumbani wakiniona nazo mjomba atanisema na hata kunipiga pia mjomba wangu ni mkali sana
mwambie nimekupa mimi hapana mama asante ila siwezi .
NILIOLEWA NA WAKWE NA SIO MUME 3
Nilishikilia msimamo wangu japo nilizitamani lkn ingekua tatizo kubwa nyumbani akasema sawa nimekuelewa mwanangu nitaiweka hii zawad mpaka siku ukiwa rasmi nilifurah nikawa natumwa kazi ndogo ndogo nafanya ili kujiongezea maksi kwa wakwe wenyewe wanasema miguvu ukweni
siku ikaisha nikarud nyumbani alinipa 10000 baada ya kukataa zawad akasema utakua unanunua anachokitaka niliipokea nikasema asante nilifika zangu nyumban niliingia ndani kupumzika huku tabasamu lingi moyoni mwangu basi ilipita miezi 3 baadae sikuwaona mabosi zangu ila kulikua kuna mtu anakuja kufata mzigo tu basi
nilipoteza matumaini nilitamani kwenda kumuuliza supervisor kuhusu mabosi lakini nilishindwa sababu alikua akinichukia tangu nilipomkataa na ukimkataa tu anakufukuza kazi maana kuna muda wafanya kazi wanapunguzwa kama kutokana kazi zinakua hakuna ila mimi alishindwa kwaajili ya ukaribu wangu na mabosi lkn alikua anipendi
nikawa mnyonge nilipoteza matumaini ya ndoto zangu kuna huyo kaka alikua ananipenda tangu tukiwa shule akawa ananibembeleza aniowe nilikua sitaki hata kumsikia alimfata Mamu na kumlalamikia Mamu akawa ananiambia utakuja kujuta siku moja nakwambia na huo ujinga wako kuna muda inabidiukubali hatma yako
hakuishia hapo alimfata had bibi lkn bado nilikataa sikutaka kabisa maisha ya kijijini ila bibi akujua kwanini nakataa nilikua nawaambia kua bado sipo tayar yule mkaka akasema mimi nitakusubir utakapokua tayar
niliitikia tu kuondoa ngoma juani maana aling'ang'ania lkn langu rohoni nikasema hapa lazima nifanye kila njia niondoke hapa hata kutoroka kama ikibid lkn siwezi kuzeekea hapa
nilipanga plan B na ile 10000 yangu sikuwah kuitumia lkn nikawa najiuliza nitaenda kufikia wapi hilo ndo nilikua lizaniumiza kichwa na kunifanya nivunjike moyo
siku hiyo nipo zangu kazini nikaja kuitwa nilipoenda sikuamini alikua ni bosi wangu yule mama nilitamani kumkumbatia
ila niliogopa macho ya watu maana kila mtu ana roho yake ule ukaribu tu ulikua unawapa watu maswali nilimsalimia pale safar hii hakuja na mumewe ila alikuja na mkaka wa makamu tu alikua akiniangalia niliona aibu maana nilikua mchafu kama ningejua kua wanakuja leo ningevaa nguo yangu ya safari nilihudhunika sana maana hiyo nguo nilovaa ilikua sket ya mwanamke nyonga na blauz yake nikafunga kanga vile anafunga shingoni
basi nilimsalimia yule kaka nikabaki nimeinama chini wao walikua wanaongea ila sikuelewa maana walikua wanaongea kingereza nikabaki natoa macho tu
walivyomaliza yule kaka aliondoka kukagua mazao shambani mimi na bossi tukawa tunaongea akaniambia usijisikie vibaya yule mwanangu kashazoea kuongea kingereza tukiwa pamoja nikajisemea moyoni kwahy huyu ndio babu harusi wangu mmmm hii safar ya Dar itaniponza mbona mkubwa sana
vip Ratifa mbona umezubaa sana yule ni mwanangu wa kwanza ila yy tayar anafamilia yake nikasema sawa huyu wa pili yeye bado ajaoa ndio nilitaka akuoe wewe au tayr ashapata mchumba hapana nilijibu haraka maana imebid nikuulize maana atujaonan miezi 3 nilikua namuuguza baba yako alikua anaumwa nikamwambia poleni sana asante tunashukuru ajambo
hv unamiaka mingapi nina miaka 18 nimetimiza mwezi huu ok vizur nimefurah tayar unafaa hata kuolewa maana ushakua mkubwa unajua shemeji yako amesema nini nikajibu hapana sijamuelewa akasema alikua anakusifia kua wewe ni mzur kama angekua ajaoa angekuoa yeye amekupenda sana nilitabasamu tu
nataka tuanze taratibu za ndoa haraka kila kitu kipo sawa wiki hii tutakuja kwenu j mosi ijayo waambie wazazi wako kuna wageni niliitikia kwa furaha kubwa niliporud nyumbani nilimwambia shangazi na bibi walifurah sana ikafika cku kweli walikuja walifata taratibu zote mambo yalikua ya haraka sana
tulipewa mwezi mmoja na nusu kama mjuavyo mambo ya tamaduni nilichezwa na kuolewa kabisa basi picha linaanza babu harusi hakuja nilikuja kuolewa na shemeji yangu. narud
NILIOLEWA NA WAKWE NA SIO MUME 4
Basi mwali wenu kama nilishonewa satini ya kijani na fundi maiko kama mnione nilivyosijapendeza nikavalishwa zangu na mtandio wakumelemeta asubuh nilitolewa kimila kisha nikaingizwa ndani maana ndoa ilikua saa kumi basi bibi mie waoji walikuja awakua wengi ilikuja gar ndogo na gar ile inayotumika kusafirishia mayai walikuja kutokana na mazingira
tuliozeshwa baadae alikuja bwana harusi nilishangaa kumuona shemeji maana hata mimi nilikua na shauku kubwa kumuona huyo mume maana muda mwingi niliambiwa yupo bz alinipa mkono pale alikaa pembeni yangu kidogo wambea wa kijiji kizima walikuja kutaka kumuona mume wangu na ukizingatia nilikataa wanaume wengi basi walijaa ndani kuja kumuona huyo nilimpenda mimi wengi walichekaa
ila mimi nilijua wanacheka nini basi mwisho wakapungua mule ndani ila nilichoshukuru wengi awakujua kua naolewa na mtoto wa boss shemeji aliitwa nje maana hata mimi ilibid nipewe taarifa kuhusu dharula ya bwana harusi mpaka kutokuwepo kwenye ndoa na uwepo wa mbadara wake
walikuja wambea wa kijiji wale walikua wanacheka mwanzo wakaanza kuongea na mimi kiluga vp mwezetu mtoto mdogo kuolewa na mtu mzima kama yule yani sisi tulijua kujishauwa kule atakuja mzungu kukuoa mwanaume mkubwa yule si anakuzaa yule
wala sikuwajibu nilikaa kimya wakatoka nje rafiki yangu Mamu akaniuliza wew mbona kama huyu baba ni mkubwa sana kwako una miaka 18 uwoni kama kakuzid sana umri kwakipind kile shemu alikua na miaka 38 nikamwambia mimi sijali kanizidi miaka mingap hata hivyo huyu sio mume wangu ila ni mbadala tu kutokana mume wangu kapata dharula
jipe moyo shoga vp kama walikudanganya hv unajua unachokifanya shoga kwakua tu utaki kuishi hapa upo tayar kwa chochote
nikamwambia mimi sijali chochote ninachotaka ndoa tu hata kama huyu ndie mume wang mimi naona sawa basi sawa alinyanyuka maana mume feki aliingia ndani alininyanyua na kunibeba kuelekea nje alinipakiza kwenye gar na mashangazi kaja yangu pamoja na makolokolo nilituzwa
tuliondoka zetu mpaka mpaka ukweni ndoto zangu zilitimia jamani hatimae nilifika dar ilikua usiku sana maana hapo kijijini kwetu kuja stend ni mbali hadi kuanza safar ya kuja Dar sio mchezo nilioneshwa chumba changu ni kapewa nguo za kubadilisha kulikua na watu kidogo walikuja kunipa na hongera na kunikaribisha pia niliwasikia wakisema masikini kapata mke mzur mashaallah alafu mdogo hadi raha nikabaki kimya bibi mie kwa uzur ninao mashaallah nahisi mama alitembea muhind maana nina rangi yangu japo maisha ya kijijini maana cjafanana na mama hata kidogo labda nywele tu maana nina kipilipili cha maana nikapumzika had asubuh alikuja mke wa shemeji yani mjengezi mwezangu alinikaribisha vizur tukawa tunaongea aliniletea begi lilijaa nguo nyingi madela mabaibui nk
kisha akatoka nje lkn huyu dada anaonekana mtu wa bz kila muda maana hata kuja alikuja asubuh ule usiku sikumuona baade watu walitawanyika alikuja mama mkwe na shemeji waliniambia Ratifa utakua hapa hadi siku mumeo atakaporud maana mambo yameingiliana kasafir kikazi na sisi atukutaka kughailisha hii ndoa tukaamua kuja kukuoa tu ufikie hapa mpaka mumeo akirud akukute hapa
nikasema aina shida mama
kama umetuelewa tunashukuru vp umeziona zawad zako nikajibu ndio asante mama basi sawa alinyanyuka na kutoka nje nilibaki na shem kama shem alikua ananiangalia sana mpaka nikawa naona aibu Ratifa aliniita nikaitika natumaini utakua mke mzur kwa mdogo wangu na mkwe mzur kwa wazazi wangu
nikamjibu sawa aina shida lkn bado alizid kuniangalia tu kisha akasema Samiri anabahati sana kukupata natamani kurudisha muda nyuma uwenda ingekua bahati yangu alinyanyuka na kuondoka
nilifunga mlango kwa ndani nikaanza kuruka ruka kitandani chumba kizur hatar kilichokuwepo moyoni mwangu ni furaha ya kuja mjini wala sikufikiria ndoa wala haikua tatizo kwangu hata kama angekaa mwaka shida yangu imeshaisha maana nilimua kujitoa sadaka simjui mume sijawahi kumuona na kibaya zaid hata kupima atujapima
nililivuta shangazi kaja langu nikatoa nguo zangu nyingi zilikua kanga tu doti 20 na magauni yangu ya ajabu ajabu zilipita siku kadhaa nikawa nipo ukweni ushamba umenijaa zile nguo nilizopewa nikawa naziweka kwaajili ya safar navaa manjenga yangu niliyotokanayo nyumbani mama mkwe alinivumilia mwisho akaniambia kwanini usifae nguo nilizokupa zawad acha kuvaa hizo nilikua mshamba hasa ila alikua anajitahid kunielekeza
nilikaa pale ukweni miezi 3 bila kumuona mume nilinunuliwa simu lkn sikuwah kupigiwa na mume hata siku moja pamoja na vipodoz nilikua napendwa mpaka raha jamani kulikua na dada wa kazi alikua akinifundisha kupika c mnajua kijijini hakunaga mambo mengi ya mapishi kama mjini na mengineyo
hatimaye ilifika siku ya Samiri kurudi maandalizi yalikua mengi kulipikwa akaletwa mtu nilichorwa piko kama vile naolewa hata siku ya ndoa sikuchorwa kama vile maana sikuayaelewa yale maua alikuja mtu alinifanyia make up nilipewa baibui jipya la gharama bibi mie alikuja mke wa shem wangu siku hiyo tukawa tupo wote basi shem alikuwepo pia
kama kawaida yake alikua akiniangalia tu muda wote na hv nilipakwa make up uwiii ndio alizid kuchanganyikiwa baada ya muda aliienda kumfata Samiri na kurud nae mimi nilikua chumbani kwangu na yule mke wa shem baada ya kusikia wageni nje aliniambia mimi nibaki kwaajili ya mume wangu moyo wangu ulikua unaenda kasi kwa hofu
nilikaa chumbani mpaka nilikoma baadae sana ndio aliingia ndani nilinyanyuka nakumpokea lakini. nakuja
NILIOLEWA NA WAKWE NA CYO MUME 5
Nilinyanyuka kutoka kitandani nakusimama nilifanya kama alivyonielekezwa na bibi katika mafunzo ya ndoa kua mwanaume azoewi inabid uwe mbunifu kila siku uje na kitu kipya na nikweli yani bibi na babu ni wazee lakin siyo kwa mahaba yale
nilinyanyuka mwali wenu kumpokea mume lkn wala hakujali alikua bz na cm yake aliongea tena kilichoniuma sikuelewa anaongea nini nmaana alikua anaongea kingereza alikaa kwenye sofa na aliendelea namaongezi ya kwenye cm nilimama mpaka nilichoka nikaamua kukaa nikabaki namshangaa tu mume nilipata mzuri mashaallah na kiumri hakua mkubwa sana aninipita miaka 11 bas nilikua pembeni yake tu namsubir amalize kuongee na simu
tulisikia hod alikua dada msaidiz alituletea chakula cha usiku nilikipokea nikaingiza ndani alipomaliza kuongea na cm nikamsalimia lkn mwezangu hakujali chochote nilimkaribisha chakula alikula akaenda kuoga hakuongea chochote tangu alivyofika alitoka nje kwenda kuongea na wakwe nilimsubir mwisho nikapitiwa na usingizi maana
nilikuja kustuka asubuh nakuta mwezangu yupo kwenye sofa nilimsalimia za asubuh mume wangu wala akujibu zaid aliomba tuongee
akaanza kuniuliza maswali mengi nikawa na jibu akaniuliza unaelimu gani nikamjibu darasa la saba oooh my god yani mama yangu sijui alifikiria nini jamani kwenda kunitafutia mwanamke kama wewe cyo wa hadhi yangu kabisa nitakupeleka wapi na darasa la 7 lako na ushamba ulionao alinishika hiv wewe unavyoona tunaendana kua mke na mume yani niwe mkweli tu mimi sijakupenda kabisa wew syo typ yangu kabisa
kwanza ninae wakuendana nae kwahy kaa ukijua hilo amekupenda mama yangu ila cyo mimi
kwahy wala usijipe shida juu yangu nilitaka tu mama yangu alidhike
alitoka zake nje nilibaki mule ndani asubuh yangu ilianza vibaya sana niliinuka na kwenda kwenye kioo nilijiangalia nikasema kwanini hanipend anasema mimi cy typ yake na nikweli alikua na elimu na muonekano mzur na hata tabia yake ilikua tofaut na kaka maana kaka yake alikua mpole na dini amemkaa kichwani alikua kama wazazi wake ila huyu akua na dini hata kidogo maneno yake yaliniuma lkn nilijipa moyo nikajiambia tulia Ratifa haupo hapa kwaajili ya ndoa kwako ndoa ni kama daraja tu ipambanie ndoto yako
tulikaa pale siku 3 nje tulikua waigizaji wazur nje kama anaipenda lkn ndani hakua hata akinigusa analala kwenye sofa mimi kitandani na niligundua kua Samiri alikua mtoto wa mama had pale alipofikia ni kwaajili ya mama yake mkwe wangu wa kiume alikua ni mwalimu mstaafu ila mama mkwe alikua na kazi nzur hata alivyostaafu yeye alikua anaiongoza familia ila nilipenda alikua akimpa heshima kubwa mumewe uwezi jua kama yeye ndio alikua vitega uchumi ving
basi hatimae tulienda kwetu huku sasa ndio nilienda kuonja joto la jiwe
niliamini maneno ya Samiri kua alimaanisha aliposema hanitaki niliteseka sana jamani siwezi kusahau yale maisha alikua anaongea na wanawake live mbele yangu kuna muda anaongeanao kingereza muda mwengine kiswahili nilifanya kila njia ili kumuweka karibu lakni nilishindwa nilikua namtega lakni hategeki
alikua na huyo mwanamke wake alikua anakuja had nyumbani kumfata wanaongea kingereza hapo wanacheka mimi kimya yani nilikua mtumwa wa mapenzi ndani ya ndoa Samiri akunichukulia kama mkewe hata kidogo hata kulala na mimi akutaka kabisa
na tulivyohamia kwake ndio kabisa alinipa had chumba changu taratibu nikaanza kuumia sababu niliinza kumpenda alafu yeye hana habar na mimi
tuliishi nyumba moja na yeye miezi 3 lkn hakunigusa kabisa lengo la kuja Dar likaanza kunipotea nikawa naumia na yale maisha nilikua naishi na mume wangu nilijiona cna thamani tena yani nikisema hakunijali naamanisha alikua ananiona kama dada wa kazi tu
ilikua kawaida kila j pili tunaenda ukweni kushind usiku tunarud kwajinsi alivyokua ananiigizia mbele ya wazazi wake awakuweza kujua chochote na mimi sikutaka kusema japo nilikua naumia sana
bas kuna muda mume wangu aliondoka shem akaniita tuongee akawa ananiuliza maswali kuhusu maisha ya ndoa nayaendeleaje nikajibu mazur tu sikutaka kumwambia mtu yoyote ninayoyapitia
mama mkwe alinijali sana alipa kila kitu pesa alininunulia mavazi kuna muda nilitamani hata niishi pale kuliko nyumbani kwangu maana hakuna maana yoyote ya kuishi kule hakuishia kunijali mimi tu aliijali had familia yangu pia lkn ndio hivo sina amani nina miez 6 ya ndoa lakini ajanigusa kabisa
nikuumuliza ananijibu kua hana hisia na mimi na hataki kufanya makosa ninaweza nikapata mimba wakati yeye ana malengo yake na mwanamke mwengine
na akasema nataka nioe mwanamke wa typ yangu kwahy ila nitakupa kila unachokita wewe sema mimi nitakupa uwendelee na maisha yako na mimi yakwangu na hata hivyo nataka iwe siri yetu usimwambie mtu yoyote nyumbani nitatafuta muda mzuri wakuwapa taarifa hata hivyo wiki ijayo naenda kumuoa yule mwanamke. anayekujaga hapa.
Full 1000
WhatsApp 0781858056
Tags
simulizi