TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

OUR SECRET

*OUR SECRET*
*1-5*
*_________________________________________*

*SEHEMU YA KWANZA*
"Shoga angu, ofisi imechangamka bhana, naona leo watu wamefika mapema utazani sio wao wanaifikaga ofisini saa 3 " alizungumza mwana dada Golya ambaye alikuwa ni secretary kwenye ofisi kubwa sana ya kibiashara hapa jijini dar es salaam. "Nani achelewe na madam anafika leo ? Uwepo wa madam kwenye hii ofisi ni majanga mazito kulaleki, bora mume wake ila yeye " alijibu msichana mwingine ambaye pia ni mfanyakazi kwenye ofisi hiyo. "Na anafika saa ngapi maana akija halafu atukute tunapiga domo atatufuta kazi " "Ata ajulikani anakuja saa ngapi, ngoja niendele ofisini kwangu mie, maana hapa nitakayefukuzwa kazi ni mimi ofisi yangu ipo uko juu hapa chini nasubili nini, baadae shoga angu " Msichana huyo ambaye muonekani wake tu ulimuonesha kuwa nadhifu na machachali, alishika njia na kuanzakuondoka alitembea hatua kadhaa na kurudi nyuma chapu. "We nawe unaniacha naondoka ikiwa kitambulisho changu unacho wewe, shoga angu unitakii mema " "Minah unajua wewe ni machachali Mpaka umepitiliza kitambulisho si nilikupa muda ule ambao ulienda kufata kahawa " alijibu secretary na kuangua kicheko. Msichana huyo aliyejulikana kama Minah alitoka mbio na kurudi ofisini kwake kwaajili ya kwenda kuangalia kitambulisho chake. Majila ya saa 3 asubuhi nje ya ofisini hiyo, yanaonekana magari kadhaa ya kifahari na anashuka mwanamama ambaye muonekano wake tu lazima ukushtue, alikuwa mzuri kuliko kawaida, mavazi yake ya bei na mapambo yalimpendezesha zaidi. Muda huo huo alishuka mkaka fulani hivi machachali, mkaka muhandsome wa kwenda kabisa, hivi ushawai kutana na mkaka ambapo ukimuangalia tu unajiambia kimoyomoyo huyu akiwa wangu nitatulia ? Basi muonekano wa huyu Jamaa unaweza kukufanya uzungunze hayo maneno. Wafanyakazi wa ofisi hiyo walitoka nje kwaajili ya kumpokea boss wao wa kike aliyesemekana kuwa nje ya nchi kwa muda kidogo na siku hiyo aliweza kurudi.Akili za wadada ziliama na kufocus katika kumuangalia mkaka huyo ambaye alikuwa na tabasamu pana usoni mwake, mkaka huyo alisalimia kila mtu, tena sio tu kwa maneno bali pia kwa kushikana nao mikono. Kwa pamoja wafanyakazi wakampokea boss wao na kwenda kwenye hall lao la mikutano. "Shoga angu huyu kaka ako na mkono laini hatari " alizungumza minah kwa kunong'ona na alikuwa akimwambia Golya secretary wa ofisi hiyo. Wafanyakazi wote walikaa kitini na kutulia, mmama huyo ambaye ni boss wa ofisi aliinuka na kuanza kuzungumza. "Aaah kwanza kabla ya yote niwapongeze sana kwa ufanyaji wenu mzuri wa kazi, nimependa sana hongereni sana sana sana " Alizungumza mama Huyo kwa busara na watu wote wakapiga makofi. Watu wakiwa wanapiga makofi, aliingia msichana fulani hivi, alikuwa amevalia gauni yake kubwa, miwani ya macho, alikuwa na nywele ndefu sana lakini sasa aliziweka hovyo hovyo msichana huyo alionekana kuwa na wasiwasi sana. "And who are you ?" Madam mkuu wa ofisi alimuuliza msichana huyo."Naitwa Sanipher " alijibu msichaa huyo kwa sauti ya wasiwasi. "What are you doing here are you lost ??" Msichana huyo kwa wasiwasi na wenge ambalo alikuwa nalo alijikuga akiangusha pochi yake hivyo akaanza kuinua pochi yake na kuacha kujibu swali ambalo aliulizwa. "Kwani hakuna security wamtoe huyu kichaa hapa ??" "Aaah mom, atleast tungemsikiliza labda ana matatizo " alijibu kijana huyo ambaye alichanganya wanawake wote wa ofisi hiyo. Kijana huyo kwa mwendo wa kigentlemen alimsogelea mwanadada yule na kuanza kumuokotea vitu vyake ambavyo vilimwagika kutoka kwenye pochi yake kisha akamuuliza kwa upole. "Aaah ulikuwa na dhumuni la kuja uku au umepotea njia ??" "Mimi ni mfanyakazi Mpya, niliweza kufanya interview week iliyoisha na leo ni tarehe yangu ya kuanza kazi, samahanini kwa kuchelewa ni foleni ya magari imenichelewesha " alijibu msichana huyo ambaye alijitambulisha kama sanipher."Oooh nina taarifa zako kutoka kwa mume wangu, na kwanini umechelewa ?' Alijibu mama huyo akiwa serious. "Aaah" sanipher alitaka kujibu lakini kijana yule aliwai na kusema. "Mama nafikili tungeendelea na ratiba husika " Baada ya muda kila mtu akakaa sawa na kikao kika anza. "Kwa faida ya kila mtu, naitwa madam Jane, ni CEO msaidizi wa ofisi, na CEO mkubwa ni mume wangu, na huyu mbele yenu ni kijana wangu anaitwa Philly ni mtoto wangu wa kwanza na wa mwisho" Mama huyo alikaa kimya kwa muda kisha akaendelea. "From now on Philly ndio atakuwa CEO wenu mpya maana sisi kama wazazi tunamajukumu mengine ya kufanya na ndio maana mnaona leo baba hayupo, nawaomba sana sana, sapoti na kila kitu ambacho mmekuwa mkitupatia mumpatie na Philly asije akapata changamoto, mimi kuwa mbali haimaanishi kuwa sitakuwa nikifatilia, mwendo ni ule ule, niko makini sawa " "Sawa madam" walijibu waajiliwa hao kwa pamoja. Baada ya utambulisho wa kila mtu na kila kitengo, kikao kiliisha na madam akaaga lakini kabla ajaondoka akasema."Minah, utakuwa bega kwa bega na Philly, hakikisha leo anapata detail za kazi zikiwa kwa njia ya summary , na wewe mfanyakazi mpya mchelewaji nifate nje " Mwanamama huyo alianza kuondoka na sanipher ambaye ni mfanyakazi mpya akamfata nje. "Sanipher umefanya zaidi sasa, ile unaingia tu nilitamani ata kucheka, haya hiyo miwani ya kizee umetoa wapi ??" Aliuliza mama huyo akiwa anacheka. "Usinichekee sasa watu wataona " sanipher alijibu uku anaangalia uku na uku. "Anyway majukumu mema hakikisha unamsaidia mumeo kwenye hili " "Hakuna shida madam" "Eti madam, haya Mkorea mweusi see you " Sanipher na mama huyo waliagana kisha sanipher akarudi ofinisi. SONGA NAYO... Niite sanipher, binti msomi na niliyezaliwa kwenye familia yenye pesa ya kutosha, nimezaliwa nchini marekani, ukiniuliza kwanini mimi ni mweusi, jibu ni kwamba mama yangu ni mwafrika na baba yangu ni mzungu.Ukiniuliza kuhusu kuongea kiswahili kwa ufasaha, mimi nimekuwa fans mkubwa sana wa lugha mama ya mama yangu, yaani mama yangu ni mswahili pure hivyo nilipenda lugha yake zaidi na kuifanyia kazi. Nikiwa chuoni uko Logos niliweza kukutana na Philly Na kuanzisha nae mahusiano, kitu ambacho kilinipa furaha kuhusu Philly ni Mtanzania pure. Mahusiano yetu yaliweza kuzaa matunda na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 5 kwa sasa, lakini pia hatukuishia tu kuzaa na ndoa tulifunga, kwahiyo mimi na Philly ni watu ambao tumefunga ndoa na tunalala kitanda kimoja na kujifunika shuka moja. TUENDELEE. Nilirudi ofisini na niliendelea kuigiza vile vile kuwa ni mgeni na ni muoga muoga, lakini akili yangu ni fire moda wote iko juu juu. Nikiwa natembea kwa kushangaa juu, niliweza kupamiana na mkaka ambaye aliweza kuangusha file lake ambalo alikuwa ameshikilia mkononi. "Oooh am so sorry, sikuwa nimekuona, Aah sio kukuona sikuwa mwangalifu " niliomba radhi na kuinama kumuokotea."Kuwa makini wewe sio unashangaa kama uko feli, mtu umevaa miwani na bado hauoni" "Nisamehe " "Nitokee hapa " "Eeeh sa mbona unanifokea kama hivi muone kwanza na pua lake kama toki " nilizungumza kimoyomoyo. Kwakuwa nilishaoneshwa ofisi yangu nilinyoosha na kwenda ofisini kwangu. "Woooooh " nilishusha pumzi nzito sana na kukaa kwenye kiti. Ukiachana na mimi kuwa msomi na kila kitu mimi pia ni kichwa maji, najua uwezi kunielewa, yaani mimi akili yangu iko juu juu, can you imagine , nimekuja ofisini halafu pochi nimeacha kule kwenye chumba cha mkutano. Nilitoka mbio mpaka kwenye chumba cha mkutano lakini niliishia mlangoni tu kwani mlango ulikuwa umefungwa. Kwa haraka nikaenda kwa secretary na kumuomba funguo kwani kwenye maelezo yalieleza kuwa secretary ndiye mtu anayekaa na funguo za ofisi."Aaah samahani, naweza kupata funguo za chumba cha mikutano nimeacha mkoba wangu " nilimwambia kwa utaratibu uku nikiweka miwani yangu vizuri usoni. "Huu sio muda wa kufungua chumba cha mikutano, ni muda wa kifanya kazi, and kwakuwa wewe ni mgeni, muda huu ungerudi ofisini kwako na kupitia nini kilifanyika ili usije kuharibu kazi za watu " Jamani sasa mimi kosa langu ni nini kuomba funguo tu au, mtu unaongea neno moja unajibiwa maneno afu moja maana yake nini 😢. Niliganda nikimuangalia msichana huyo ambaye alijifanya kuwa bize na kazi zake. "We mapokezi naomba funguo hizo " nilijikuta nikianza kuonesha utaila wangu. "What, did you call me mapokezi ? Are you mad or something??" Alifoka Golya na kunitupia peni ambayo alishika mkononi. "Eeeh umu ndani watu wakiwa na hasira ndio wanaongea kingereza kumbe " nilizungumza kimoyomoyo. "Am sorry lakini unafanya kazi mapokezi na sijui jina lako" Nikiwa naendelea kujielezea Philly alikuja akiwa ameweka mikono yake mfukoni, nilimuangalia gentlemen wanguanavyotembea na tabasamu lake nikajisemea kimoyomoyo.. "MY man, may man my man " Katika kumuangalia sana Philly, akuwa mzembe alichofanya ni kunikonyeza. "Oooh usijali haina haja ya kukupa funguo nitaenda kukufungulia " secretary akaanza kuigiza kuwa mtaratibu. "Shukrani sana " nilijibu. Kwa pamoja tulishika njia na kwenda kwenye chumba cha mikutano, nilishtuka baada ya kukuta vitu vyangu vikiwa chini, yaani kila kitu kipo sehemu yake ni kama mtu alishika pochi na kuanza kusambaza. Nika...

*SEHEMU YA PILI*
 Nikainama na kuanza kuokota vitu vyangu, yaani watu wana roho mbaya awakujali ata simu yangu waliitupa chini na iliweza kuweka Alama kwenye kioo nishukuru kuwa kulikuwa na protecta. "Ahahaaha, mwaya watu wakajua ni mpira wakacheza danadana " alizungumza Golya ambaye kwa muda mfupi niliweza kujua baadhi ya tabia zake. Nilimaliza kuokota vitu vyangu na kumshukuru Golya ambaye hakuonesha kujali zaidi alinicheka tu. Nilishika njia na kurudi ofisini kwangu, nikachukua ma file na kuanza kupitia baadhi ya kazi, kila nilipoona kuwa kuna mapungufu nikaanza kuweka sawa, na mapungufu yalikuwa ni mengi sana katika utendaji wa kazi, na kwakuwa nilikuwa kwenye kitengo cha maendeleo ya kampuni nikaamua kuweka sawa.Nikiwa bize nafanya Kazi simu yangu iliita nilipoangalia pale juu ilikuwa ni namba ya mume wangu ambayo niliisave hubby ❤. Kwa tabasamu pana na bashasha nikapokea. "Yes honey " nilizungumza kwa manjonjo. "Unaendeleaje mke wangu, na unaonaje siku ya kwanza kazini ??' Philly wangu aliniuliza kwa sauti fulani hivi nzito na ya kubembeleza. "Nainjoy ujue " "Sani, umeanza mambo yako tupo kazini ujue " "Hey kijana acha kumaanisha mambo, namaanisha nainjoy kuwa ofisini""Oooh uwe unaongea kwa kudadavua umenichanganya ujue, anyway hiyo miwani umetoa wapi ujue nimecheka sana " "Unanicheka jamani" nilizungumza kwa sauti ya kudeka kidogo. "Amna, simaanishi kukucheka ila umenichekesha" "Aaah ni miwani ya bibi mzaa baba nilimuibiaga Enzi zangu " Nikiwa bize nabebika na baby wangu sina ili wala lile aliingia minah kwa jazba sana na kuanza kunifokea. "Nimekutumia email nusu saa iliyopita wala hujibu uko bize unabebika, binti hii ni sehemu ya kazi " "Baby ni nani huyo anakufokea kama anamtindio wa akili ?? Philly aliuliza.Nilikaa kimya kidogo kisha nikajibu. "Nipo kwenye majukumu nitakupigia baadae " kisha nikakata simu. "Binti umekuja kushangaa ghorofa si ndio ?" Minah aliendelea kunifokea. "Aah samahani, sikuwa nimeona, naangalia hapa then nakujibu " Minah aliniangalia kwa dharau akaachia bonge la Sonyo na kutoka nje. Ile anatoka na mimi ndio nikafungua email yake, yaani email ilikuwa imetumwa ndani ya dakika 7 tu zilizopita halafu ananiambia nusu saa jamani. Kwakuwa na mimi uchizi naujua vizuri nikatoka nje na kumfuata, uzuri nilimkuta kwa shoga yake Golya (secretary) ."Minah umesema email umetuma nusu saa lakini kwangu ina dakika 7, ni hii au kuna ingine ??" "Kikubwa umeiona fanyia kazi " alinijibu kwa dharau na kuniangalia kama anaangalia kinyesi cha mtu mzima. "Jifunze kuacha kudanganya " nilimwambia. "What did you just say ??" Kaanza na kingereza chake, umu ndani watu wakiwa na hasira ndio uwa wanatelemka na kingereza kweli jamani. "Aaah, amna naenda kukujibu " nilijibu na kutaka kuondoka lakini Minah akanirudisha. "Rudi hapa, naonge na wewe unaondoka ? Aaah tafuta mtu akuambie mimi ni nani umu ndani sawa, kwahiyo umeshuka ngazi zote hizo na kunuka jasho kwaaili ya kuja kuniuliza kuhusu muda niliotuma hiyo kazi ??"Minah ni muongeaji mzuri sana, anaongea kama amemeza memory card, sikutaka kumuonesha mimi ni mtu gani nilichofanya ni kujishusha kisha nikarudi kuendelea na shughuli zangu. Muda wa kuondoka ulifika, nikatoka nje ya ofisi na kuanza kushangaa shangaa uku na uku. Phili alitoka ofisini kwake, na moja kwa moja akasogelea gari yake na kutaka kuondoka lakini alisimama baada ya kuitwa na Minah. "Aaah samahani, si unaenda nyumbani ??" Minah alimuuliza Philly. "Yaaah, na wewe je" "Sikai mbali na pale nyumbani, aaah nilikuwa naomba lifti, maana gari yangu inashida kidogo, fundi atakuja kuweka sawa then ataniletea nyumbani " "Amna shida "Basi walipanda kwenye gari na kuondoka muda huo sanipher mimi nilibaki nikishangaa shangaa uku na uku. Sema watu wa ofisi hiyo walikuwa wanahela, yaani mtu anakaa chimba unye uko na bado Anabolt gari ya kumepeleka nyumbani, mtu uko peke yako hauna ata mizigo una kodi gari ya nini si uchukue boda tu usepe. Nilishangaa shangaa mwisho nilikodi boda boda na kuwai nyumbani. Ajabu ingawa Philly aliwai kuondoka lakini mimi ndio niliwai kufika nyumbani. "Ahahaha, haha eeeh " kilikuwa ni kicheko cha mtoto wangu. "Kipipi unacheka nini ??" Nilimuuliza binti yangu."You're so much fun mama, ona nywele zako, ona hizo glasses umevaa 😁, ouk achana na hiyo vipi hii outfit mama " Ila kiukweli nilikuwa kama kituko, nguo nilizovaa na viatu ni vitu saba tofauti hivyo nilichekesha sana. "Aaah kipipi, tabia mbaya hiyo, mama amechoka sana ametoka kwenye majukumu, uwezi mu hug mama ??" Basi binti yangu alinisogelea na kunikumbatia. Maisha ya home ni safi kabisa, wafanyakazi kama wote hivyo sikuwa na majukumu sana, jukumu langu ni kumpikia mume wangu na mtoto, yaani kitu ambacho siwezi ruhusu ni mfanyakazi kumpikia mume wangu au kumfulia, kiufupi majukumu ya mume wangu ni yangu tu. Niliingia chumbani na moja kwa moja nikaenda kwenye kioo nilicheka sana, nikajipiga na picha kisha nikaingia bafuni kukoga.Baada ya yote, nikapigilia mavazi yangu ya siku zote, yaani mimi ni mtu wa mini skirt, short pens na vest. Hapo nilibana nywele yangu vizuri na kutoka nje. Baada ya dakika kama 15 hivi aliingia Philly akiwa amechoka mno alijikuta akishusha pumzi tu kama ametoka kukimbizwa. Nilimpokea na kumpeleka chumbani, nilianza kumtoa nguo zake uku nikimpa pole ya majukumu. "Aaah Minah ni pasua kichwa walahi " alizungumza Philly. "Utamzoea " nilijibu. "Aaah ni kazi nzito sana kumzoea yule msichana, ukimuangalia unaeza kusema labda akana akili vizuri hivi, kana maneno mengi, imagine namwambia nimpeleke kwake ananiambia anataka kuja na mimi hapa nyumbani ""So ikawaje ??" "Si unanijua me ni mzee wa kupokea simu hewa, nikajifanya napokea simu ya dharula na nikamshushia njiani mie, so kuchelewa kwangu ni baada ya kubadili njia ambayo imenizungusha sana, kwanza nishukuru Google map otherwise ningepotea" Nilijikuta nikicheka tu. "Unanicheka ??" "Nooh ". "Tukaoge " "Nishaoga" Mume wangu uwa aelewi kabisa, alichofanya ni kuninyanyua na kunipeleka bafuni, polepole tukaanzakuoga, ila sasa sisi ni watu ambao hatukuwai kuzoeana hisia ziko palepale tukaamua kumalizana uko uko 😊. ******** Siku iliyofuata ni mimi ndio niliwai kuondoka nyumbani na kumuacha Philly nyumbani. Nilifika ofisini mapema sana, na kumkuta golya akiwa ameshakaa kwenye sehemu yake ya mapokezi. "Naona leo foleni ya magari haijakuzonga binti " "Za asubuhi golya " niliamua kumsalimia tu maana yeye amekosa adabu na ajui kusalimia. Ofisi ilikuwa na wasichana 8 na wengi walikuwa bize na kazi zao na majukumu ila awa wawili minah na golya ndio walikuwa vivuluge wakuu wa ofisi."Sina shida na salamu ila nikuulize, unavyotokaga uko nyumbani hakuna mtu anakuambia jinsi unaonekana ??" Nilijiangalia na kuanza kuzunguka zunguka kisha nikamuuliza. "Naonekanaje ??" "Jana ulikuwa kama homeless, halafu leo ukaamua uje kama upinde wa mvua, una rangi kibao mwilini mwako" Nilijiangalia lakini kwakuwa kazini sikuona ubaya wa nguo zangu, nilitabasamu na kujibu. "Mbona nimependeza" Mpenzi msomaji, siku hiyo nilikuwa nimevaa gauni ndefu ya kijani, tena kijani kile cha CCM, kichwani nywele nimabana na kibanio chekundu, tena sijabana vizuri maana nilikuwa na nywele nyingi na ndefu lakini pia sikuzivuta vizuri ukiangalia unaweza sema ni kiota chandege 😁, miguuni nimevaa buti yangu moja matata ya pink inawaka hatari, pochi yangu nyeupe na gauni niliibana na mkanda mweusi utanipenda tu na ndio maana golya aliniambia niko kama upinde wa mvua. Nikiwa naendelea kuongea na Golya ndipo akaingia minah na Philly tena walikuwa wameshikana mikono nikabaki nikiwatolea macho

*SEHEMU YA TATU*
Minah alikuwa akilinga na kuachia meno yake yote kama mwehu vile, wafanyakazi wengi waliweza kuwaona maana ndio ulikuwa ni muda wa watu kuingia ofisini. Ukiacha na kila kitu najua kama tupo kazini lakini kitendo cha my wangu kushikana mikono na Minah kiliniuma, vile moyo wangu uko mwepesi nilijikuta machozi yakianza kunilenga lenga. Niliona kama wanaweza kupelekana mpaka ofisini hawa watu nilichofanya ni kujiangusha tu wasiniletee ujinga. Halafu vile mke ni mke Philly aliachia mkono wa Minah na kuja kuniokota pale chini. "Leteni maji " alizungumza Philly akiwa na wasiwasi sana. Lakini kwakuwa tulikuwa hatutaki watu wajue kuwa sisi ni watu tunajuana Philly aliniamsha kwa kunitikisa tu hakuniita jina langu.Kwakuwa nilikaa vizuri na mkono wangu uliweza kufika kwenye mgongo wake nilimfinya tu na hapo aliweza kujua kuwa sio ishu ambayo ni serious. Maji yaliletwa pale nikamwagiwa kigogo na niliamua kufungua macho yangu pole pole. Minah alisogea na kuniinua kwa upole akaniuliza. "Unajisikiaje ??" "Kizunguzungu " "Aaah boss Philly unaonaje akarudi tu nyumbani na kupumzika au aende kwanza hospital ndio aende nyumbani maana anaonekana kutokuwa sawa" Minah aliongea kama mtu ambaye anajali kweli kweli, niliwaangalia kwa muda kisha nikazungumza."Amna nitakuwa sawa, kuna dawa uwa nakunywa ile asubuhi nilisahau kwaajili ya kuwai daladala ila nitakunywa " Minah na Golya walinishika uku na uku na kunipeleka ofisini, nilifika na wakaniweka kwenye kiti kisha minah kwa dharau akazungumza. "Kwahiyo umejisikia raha kushikwa na mwanaume wangu ?, mkijiona kuwa mna afya mgogolo muwe mnabakigi majumbani kwenu msije mkatufia hapa " Golya alivyo chawa sasa akaanza kujichekesha chekesha pale, niliwaangalia na kuwasikitikia kisha kwa dharau wakatoka nje. Baada ya kama nusu saa alikuja Philly wangu, haraka akafunga mlango vizuri na kunisogelea. "Uko sawa kweli wewe ??""Usiniulize kama hivyo uku umekuja kufanya nini ?" "Sanipher acha ujinga wako ujue, MI nina wasiwasi na hali yako, mtu umeanguka kama vile, mara sijui umenikonyeza sielewi uko sawa au unaumwa, nambie mama which is which" "Kwanini mlishikana mikono na minah ??" "Eeeh, kwani umechukia ??" "Philly ujue unajitoa akili wewe, yaani kwanini umemshika mkono kama vile, mnaingia wenyewe kama mnafunga harusi vile" "Acha wivu mke wangu utakuuwa ooh, kwahiyo kisa wivu ndo ukajiachia kama vile ? Ungeumia ujue oooh "Nilimsogelea mwanaume wangu na nusu na kimkumbatia, ila sisi bhana wala hatujali kuwa tuko ofisini, wenyewe tukaanza kukisi. "Mama hii mishen ya mama ikiisha turudi tu kwetu walahi, saa hizi nakosa muda wa kuwa na wewe " "Kurudi wapi ? Vile nataka hizi drama ziendelee, najisikia amani sana, nafurahi kuliko kawaida, aswaah awa wasichana ambao wanamdharau mtu kwa kumuangalia tu. Tukiwa tunaendela kuongea na kushikana shikana, mlango uligongwa, haraka Philly akasogea na kuja kujificha chini ya meza yangu. Nilipoona kuwa kila kitu kiko sawa, nilisogea na kufungua mlango na kuendelea kuigiza kuwa ni zaidi ya zoba. "Haya tangu lini milango ya ofisi inafungwa ??" Lilikuwa swali la kwanza kabisa ambalo minah aliniuliza baada ya kumfungulia."Aaah nilikuwa natoa mdudu kwenye nguo yangu maana alikuwa akinitambaa mgongoni na kuning'ata ndio maana nikafunga mlango " "Soon utatuamishia kunguni umu ndani, aaah Philly Yuko wapi maana nimeambiwa alikuja uku " "Amekuja na kuondoka " nilijibu. "Alikuja kufanya nini ??" "Kuangalia naendeleaje " Minah alionekana kuchukia na kwa hasira akabamiza mlango na kuondoka zake. Philly aliinuka pale chini ya meza na kuanza kucheka."Etii Philly amekuja kufanya nini ?, aka kasichana ni kakichaa ujue " "Haya baba toka chapu unatafutwa uko kwa nguvu zote" Philly alinikisi na kuondoka zake. ****** Mwezi mzima ulipita uku maigizo yakiendelea lakini manyanyaso na dharau dhidi yangu yalikuwa mengi na makubwa mno kuna muda nilikuwa natamani ata tuache maigizo lakini ndo hivyo tena tupo bize kufanya kazi ya mama mkwe. Kiukweli mimi na mume wangu tulikuwa tunafanya hivyo kwa kufuata maelezo ya mama mkwe ingawa hakuwai kutuambia ni kwanini tunafanya hivyo. Siku hiyo majila ya saa 4 asuhuhi nikiwa ofisini kwangu nafanya shughuli zangu, niliweza kusikia kelele za uku na"Etii Philly amekuja kufanya nini ?, aka kasichana ni kakichaa ujue " "Haya baba toka chapu unatafutwa uko kwa nguvu zote" Philly alinikisi na kuondoka zake. ****** Mwezi mzima ulipita uku maigizo yakiendelea lakini manyanyaso na dharau dhidi yangu yalikuwa mengi na makubwa mno kuna muda nilikuwa natamani ata tuache maigizo lakini ndo hivyo tena tupo bize kufanya kazi ya mama mkwe. Kiukweli mimi na mume wangu tulikuwa tunafanya hivyo kwa kufuata maelezo ya mama mkwe ingawa hakuwai kutuambia ni kwanini tunafanya hivyo. Siku hiyo majila ya saa 4 asuhuhi nikiwa ofisini kwangu nafanya shughuli zangu, niliweza kusikia kelele za uku nauku na haraka nikatoka nje na kwenda kuangalia ni nini kinaendelea. Nilifika mapokezi na kumkuta Minah akigombana na mfanyakazi mwenzie, alikuwa ni mdada ambaye alikuwa kimya sana pale ofisini na mara nyingi alikuwa bize na kazi zake. Minah na msichana huyo awakuwa wakigombana kwa kutupiana maneno tu bali pia walikuwa wameshikana nywele na kuvutana, na watu wengine walikuwa wakiangalia tu pasi na kugombelezea. Na kiherehere changu nilisogea na kutaka kuwagombelezea lakini mkaka mmoja pale ofisini aliweza kunivuta na kuniambia. "Usije ukajaribu kugombelezea, ushawai kuamishiwa ugomvi wewe, yaani, kitendo tu cha kugombelezea kitakupoza Minah ata kuwasha mabao na hauta amini macho yako "Nilimuangalia mkaka huyo na kutaka ata kucheka, yaani mwanaume mtu mzima kabisa anaanza kuongea maneno kama hayo kwa mtoto wa kike kwahiyo anamuogopa Minah au ni kitu gani. "And na wewe unajiita ni mtoto wa kiume wakiuwana hapa nani atakuwa Shahidi ??" Niliuliza kwa jazba maana alinikela mtoto wa kiume anakuwaje na nidhamu ya uoga. "Dada jichanganye " mkaka huyo aliendelea kusisitiza. Sikutaka kujali nilichofanya ni kusogea na kumvuta mmoja wapo ili waweze kuachiana. "Mna nini nyie amuoni kama hii ni sehemu ya kazi ??" Nilifoka baada ya kuwatenganisha. Muda huo kila mtu alikuwa amepigwa na butwaa kuona nimeingialia ugomvi huo."Sanipher ni wewe ndio umenipushi kama hivyo au ?" Minah aliuliza kwa hasira sana. "Mnadhalilisha ofisi sawa, mnawezaje kupigana tena mapokezi amjaona sehemu zingine ??" "Sanipher nisikilize, unajua Minah anadharau sana, anatoka na mume wangu halafu namuambia aachane nae ananitunishia kifu anataka kitu gani kwenye maisha yangu, bado ananitishia kunifukuza kazi kisa mwenye boss ni mama yake mkubwa" alizungumza Sada msichana ambaye alikuwa mpole sana pale ofisini. Kwa hasira Minah akaondoka, na kila mtu akatawanyika, nilimtuliza sada ambaye alikuwa akilia sana kisha akainuka na kwenda ofisini kwake. "Shoga angu umeyakanyaga iki kipigo ulichomuepusha nacho mwenzio kinakupata wewe sasa" alizungumza Golya uku akicheka cheka."Unanichulia poa kwa huu muonekano wangu au ?, golya uwe na aibu siku moja moja na ujue kipi sahihi na kipi sio sahihi " "Haya dada usinga kama usinga, kihelehele tu kimekujaa mpaka umeniondolea burudani yangu " Nikiwa naendelea kuzozana na golya ambaye uchawa ulimzidi kupitiliza, alikuja Philly na kuniita kwa hasira sana. "Sanipher nakuitaji ofisini kwangu sasa hivi " Kwanza nilitetemeka na kwa sauti ua wasiwasi nikajikuta nikimuuliza golya. "Kwanini ameniita kwa hasira sana, kutakuwa kuna shido ??""Umelikologa dada, kama ulikuwa ujui, Philly na minah ni watu wenye mahusiano kwa muda mrefu, bado kufunga ndoa sasa hivi wanapika na kupakua " Aaah kweli Golya ni chawa zaidi nilitamani ata kucheka lakini nguvu hizo sikuwa nazo haraka nikawao ofisini kwa Philly ambapo niliitwa.. "Kwanini umemtandika mwenzio vibao bila sababu ??" Phillly alinitundika swali pale tu nilipoingia Ofisini mwake. "Aaah, me sijampiga mbona, sijampiga kabisa " "Na hizi alama za vidole mashavuni ametoa wapi ??" "Boss sio mimi, huyu alikuwa akipigana na Sada pale mapokezi muulize ata golya. Philly hakutaka mambo mengi alishika simu yake na kupiga sehemu mbili tofauti baada ya dakika kadhaa sada na golya waliingia ofisini na kwa pamoja wakazungumza."Tumeitikia wito boss" "Aaah, mnajua kabisa sipendi drama sitaki drama kwenye ofisi, naomba mjue kuwa mimi ni mkali na mkorofi kuliko chochote, najua nyote mnamuogopa mama sana, ila bora mcheze na mama kuliko mimi, Nina uwezo wa kuwafuta kazi wote sasa hivi " alifoka Philly na kutufanya sote tuinamishe nyuso zetu chini isipokuwa Minah ambaye alikuwa akijitilisha huruma. "Nani na nani walikuwa wakipigana hapo mapokezi ??" "Hakuna boss " alijibu golya haraka haraka uku akimuangalia Minah usoni. "Boss Philly hakuna watu waliokuwa wakipigana, ila miss Sanipher hapa alitoka nje na kutukuta pale mapokezi pasi na sababu akamchapa kibao Minah na kumwambia kuwa aachane na wewe kwani anakupenda sana "Eeeh nyieeh eeeh watu wanaweza kukugeuka kwakweli, yaani mtu ambaye nimemtetea na kumgombelezea yeye ndio ananigeuzia kibao. "Asanteni mnaweza kwenda isipokuwa Sanipher mpaka tumalize hili " Walitoka nje wakiwa na furaha sana nilibaki nikishangaa na kujiuliza nini kimetokea yaani sada nimetoka kumtetea halafu muda huu yeye ndo kanikandamiza. "Pole mke wangu " Philly alinipa pole. "Aaah hii ofisi ni pasua kichwa walahi, natamani ungeona kilichotokea halafu na kile ambacho sada amesema" "Usijali Sani wangu, nimeona kila kitu, infact mimi nilifika pale kabla yako ila nilisimama kwa mbali sana na kushuhudia kila kitu, hapa kitu najiuliza imewezekanaje sada kumtetea Minah baada ya kila kitu, maan minah amempa sada kipigo cha kutosha kabla ya wewe kufika""Nitapata jibu baby usijali " "Haya mama kapumzike" Kwakuwa ilikuwa ni ijumaa ofisi iliwai kufungwa nasi tukarudi majumbani kwetu kwaajili ya kwenda kuanza weekend tukiwa na familia

*SEHEMU YA NNE*
.......Sijui ni mimi tu, au kuna wengine, sanipher mimi uwa napenda kutumia weekend nikiwa na familia yangu tena nyumbani, ikiwa kuna watu wanapenda kutumia weekend zao kwenye viwanja tofauti tofauti. Siku ya jumamosi niliamka asubuhi na mapema na kuanza kuwasaidia wadada wa kazi, kazi ndogo ndogo ambazo walikuwa nazo. Nikiwa bize naandaa kifungua kinywa cha Philly, muda huo huo Philly alikuja na kunikumbatia kwa nyuma, hapo kidogo aliwashtua wadada wa watu na kuwafanya watuangalie kwa macho ya kuibia. Niligeuka na kumuangalia mume wangu ambaye ndio kwanza alikuwa ametoka kuamka. "Aaah baby nimeamka naangalia uku na uku sikuoni jamani" Philly alilalama uku akizungusha vizuri mikono yake kwenye kiuno changu."Aaah jana nilimuaidi kipipi kuwa nitamuandalia breakfast nzuri kabisa, hivyo nimeamka kwaajili ya kumuandalia " "Kwahiyo unaandaaa kwaajili ya kipipi tu na mimi je ??" "Aah utaandaa mwenyewe, kipipi ameniambia wewe ni mtu mzima nikuache ujihudumie " "Khaaah " Philly aliishia kuguna tu. "Go and shower baby the nakuletea kifungua kinywa chako " Philly alinisogelea kidogo na tukakisi kidogo kisha akaondoka. Ile nageuka ili niendelee na shughuli zangu nilijikuta nikianza kucheka baada ya kuwakuta wadada wa kazi wakiwa wamefunika macho yao kwa mikono. "Ooooh ameshaondoka" niliwaambia.


Sijui ni makosa au laah lakini kwa sehemu ambayo tulikuwa mimi na Philly kukiishi ni jambo la kawaida sana ila uku Tanzania naona ni kama limekuwa jambo la ajabu sana. Niliandaa kifungua kinywa na kupeleka chumbani kwa binti yangu kwanza. "Umeamka mama " nilimwambia binti yangu baada ya kumkuta akivikwa nguo na mdada ambaye alimuogesha. "Aaah, usiniulize like you care, mama mimi na baba nani mkubwa ??" Kipipi aliniuliza. "Aaah kipipi umeanza tena mambo yako, dada unaweza kwenda nitamalizia " niliamua kumtoa mdada wa watu maana kipipi anaongea mno unaweza kusema sio mtoto wa miaka mitano (5). "Uwezi nijibu swali langu mama eti ??""Kipipi, baba anaumwa ndio maana " "Ujanijibu mimi na baba nani ni mkubwa ? " "Ni baba " "And unaenda kulala na baba unaniacha mimi mtoto nalaa peke yangu, I'll call grandma na kumwambia akuje kunichukua " "Kipipi umeona kitu nimekuandalia au ??" Nilimuuliza uku nikifunua sahani yake ya chakula, yaani ukitaka kuchanganya akili ya mwanangu basi ni kwenye mambo ya misosi hakuna kitu unamwambia kipipi juu ya chakula. "Mama pizza " kipipi alipiga kelele na kukimbilia kwenye sahani hakujali tena kuhusu kuvaa wala maswali yake ya kiutuuzima.Sikuishia hapo nilianza kumlisha mwaya mtoto wangu, nikiwa namlisha kipipi, Philly alikuja akiwa amevaa, lakini pia alikuwa naangaika kufunga saa yake ya mkononi. "Morning daddy " kipipi alimsalimia baba yake baada ya kumuona. "Morning princess how are you ??" "Am fine papa, njo ule pizza ila usije kweli kweli " Kwenye tabia za kipipi kwakweli sina cha kuongea, niseme kuwa nilijizaa mwenyewe, ila sasa vya kurithi uwa vinazidi na kipipi aliweza kunizidi asilimia kadhaa. "Aaah narudi baby, mama amenipigia anasema kuwa minah anaumwa sana na hana mtu wa kumpeleka hospital wala kumuangalia" "Oooh basi sawa, utaniambia nini kinaendelea, but wewe kwake utapajua kweli ??""Nimeshatumiwa location don't you worry, kipipi badae " Philly aliaga na kuondoka. Kiukweli nilijiskia wivu sana yaani Philly kwenda nyumbani kwa Minah tena akiwa mwenyewe, ukizingatia minah ni msichana wa hovyo sana. Nilibaki nyumbani nikiwa na wasiwasi juu ya Minah, kuna muda akili iliniambia kuwa Minah aumwi ni ametaka tu kuwa karibu na Philly ndio maana ameigiza kuwa anaumwa. ******* Kwa upande wa Philly safari yake ilianza na kwakuwa nyumbani na Minah hakukuwa mbali hivyo hakuchukuwa muda mrefu kufika. Philly alifika pale na kumkuta Minah akiwa mzima wa afya, na alikuwa amevalia nguo za kimitego, naukizingatia ile shape yake ya kiafrika walahi alijua kuvutia msichaa huyu na weusi wake mng'avu. "Karibu sana Philly " minah alimkaribisha Philly kwa bashasha na malingo ya hali ya juu. "Asante, aaah naona mgonjwa si haba umechangamka " alizungumza Philly uku akiendelea kusoma mazingira ya nyumba hiyo. "Aaah nashukuru Mungu nimetumia dawa na sasa najiskia powa kidogo, but still nitaitaji kwenda hospital baadae " "Baadae ya saa ngapi Minah, you know mama anawasiwasi sana juu yako ndio maana amenituma nije na niweze kukupeleka hospital na moyo wake uwe na amani " alizungumza Philly kwa wasiwasi na msisitizo. "Relax Philly, kila kitu kiko sawa, but thanks so much for coming, I didn't expect kwamba utawai kufika mapemanamna hii na kunikuta nikiwa naendelea kukuandalia chakula " "Unamaanisha nini ??" "Philly acha utoto basi " alijibu Minah na kuanza kumsogelea Philly karibu kabisa, na kuanza kumshika shika. Philly kwa uwoga na wasiwasi alianza kurudi nyuma na mwisho akaangukia kwenye kochi, Minah alitabasamu na kwenda kukaa juu ya Philly kwa mahaba mazito kabisa. Philly wangu alihema kwa kasi kana kwamba ni mtu ambaye alikuwa akikimbizwa, Philly alimuangalia Minah kwa macho ya kulegea na sauti ile ya mwisho kabisa ya kuonesha kuwa ameshikika akamuuliza Minah. "Unataka kufanya nini Minah ??""Tulia na uniache nikuoneshe upande wa pili wa dunia ambao naamini kabisa uko ulikokuwepo haukuwai kufika uku ambako nakupeleka, nataka kukupeleka sehemu ambayo wanawake wako weupe wa uko ulikotoka awakuwai kukupeleka " Philly alifumba macho yake na kwa pamoja wakiwa na ushirikiano wa kutosha wakaanza kukisi. "Hakuna kwenda" nilijikuta nikipiga kelele nikiwa namlisha binti yangu. My zangu ndio kwanza Philly alikuwa ananiomba ruhusa lakini mawazo yangu yalifika mbali sana na kunifanya nimkatalie Philly kwenda alikotaka kwenda uko. "Mmmh, una maanisha kunikataza au unanitania ??" "Nikutanie kitu gani namaanisha kuwa hakuna kwenda, mimi yule msichana sijawai kumuamini, na sio yule tu msichana yeyote yule awezi kuwa na ukaribu na wewe Ata akiwa ndugu yangu ""Eeeh we mwanamke jamani huo wivu ni wa aina gani ?, unawivu mpaka unapitiliza come on baby uwezi jua anaitaji msaada kiasi gani" "Aaah huruma nitoke mie, naona maneno yako yanaanza kunishawishi, tuseme kuwa wewe haupo nani angemsaidia ? Ana mashoga kibao pale ofisini, kama yuko serious sana basi atawapigia " nilizungumza kwa hasira sana na kwa hasira nilitoka kwenye chumba cha mtoto wangu na kwenda nje. Philly aliendelea na kumlisha mtoto na alipomaliza akaja nje ambapo nilikuwa nimekaa nikiwa na mawazo yangu mengi mengi tu. "Uko na hasira ??" Philly aliuliza uku akinyoosha mikono yake na kuweka kwenye mabega yangu kwani alikuwa kwa nyuma yangu. "Siwezi kuwa na hasira ukiwa umenisikiliza ""Nafurahi kusikia hivyo mpenzi, aaah kuna kitu nilikuwa naitaji kukuambia" "Umeanza na wewe kitu gani tena ??" "Si unisikilize mama " "Nakusikiliza " "Aaah hii mambo ya mimi kwenda kazini na gari halafu wewe unatumia usafiri sijui wa pikipiki mara bajaji, inanikela sana, kusema ukweli nakosa Amani kabisa, nimewaza tununue ata gari ya bei rahisi uwe unaenda nayo kazini " alizungumza Philly wangu akiwa na hali ya huzuni usoni mwake. "Oooh about that, mama pia aliniambia lakini nimekataa mwenyewe, am happy with it, unajua kuna life sijawai ku experience kwahiyo nahisi huu ni muda sahihi kabisa wa Mimi kupitia haya na kujifunza ""Una uhakika ??" "Usijali mtoto wa mama mkwe " "Bongo Pameanza kukuharibu mke wangu mpaka unaniita mimi mtoto wa mama mkwe " "Natamani kujua kila kitu, ili nikutambie mzaliwa " "Jinga wewe " ****** Hatimaye weekend iliisha powa kabisa na siku ya jumatatu kama kawaida tukaingia kwenye majukumu. Siku hiyo, nilivaa zangu sketi fupi ya rangi nyekundu, Shati ya mikono mirefu ya blue, pochi ya pink, halafu nikapigilia na la kuchumpa moja matata sana halafu rangi yake ni njano 😁󰚓 ukirudi kwenye pochi, siku hiyo sikutakakubeba pochi nilichukua begi la kipipi wangu, na kuweka vitu vyangu, si unajua tena mabegi ya watoto Midoli nini, kichwani niliamua kubana mabutu matatu ambayo ata mistari haikuwa sawa. "Nooh baby this is to much, hizi mavazi umetoa wapi, unanifanya na mimi niwe nakucheka baby " alizungumza Philly kwa kicheko cha hali ya juu mpaka akawa amashindwa kufunga Tai yake. "Na hiki ndo kitu kinatakiwa wewe cheka tu kipenzi changu " "Leo umekuwa kama mwanasesele " Kiukweli sijui maana ya mwana sesele ila nilicheka tu maana kicheko cha Philly kilinichekesha sana. Kwakuwa nilikuwa nimeshavaa kila kitu, nilitoka na kwenda chumbani kwa mtoto wangu na kumuaga kwa kumkiss tu kwani alikuwa bado amelala kisha nikashika njia ya kwenda kazini.njiani nilikuwa kituko kwakweli, mavazi yangu yalimfanya kila mtu aniangalie mara mbilimbili na wengine walidiliki ata kuchukua video kwaajili ya kuweka mtandaoni. Ile naingia tu ofisini wa kwanza kuonana nae alikuwa ni William mkaka ambaye ni mmbea wa ofisi, aliponiona tu akaangua kicheko, na kwakuwa ni mmbea sana alicheka na kujiangusha chini, imagine huyo ni mtoto wa kiume. ITAENDELEA..... 

*SEHEMU YA TANO*
Nilibaki nikimshangaa William ambaye alikuwa kijichekesha pale chini kana kwamba ni kichaa ameona ndugu zake. "Akili zako ziko vizuri au ??" Nilijikuta nikimuuliza william kwa hasira sana. "Unanichekesha bhana usiongee, sanipher umekuwa mtu wa fashion show za kuchekesha umu ofisini haya, nambie hapo umevaa vitu gani ?, uoni aibu uko ulipotoka " alizungumza william uku akiinuka pale chini na kujikung'uta vumbi. "Kwahiyo kupendeza kwangu ndio kumekufanya ucheke na kuanguka chini badala ya kunisifia " "Sanipher sitaki kuwa mnafikili ujapendeza hata kidogo"Muda huo huo alifika golya akiwa na minah, waliingia na kuanza kunicheka, golya alisogea kwenye meza yake na kuweka mkoba wake kisha akazungumza. "Ifike hatua ofisi itambue nini inafanya, huyu msichana ni kituko tu hapa ofisini haya hii ni kitu gani tena amevaa ? Minah utakuja kushusha credit zako hapa ofisini kwaajili ya huyu msichana, fikilia siku wale wawekezaji wakija na kumkuta akiwa hivi " Nilibaki nikishangaa lakini pia nilijiuliza huyu golya anataka kumaanisha nini kwamba nifukuzwe kazi au ni kitu gani. "Msichana nifate ofisini " alizungumza minah kisha akashika njia na kuelekea kwenye ofisi yake. Kwakuwa mimi ndio niliitwa na minah nilishika njia na kwenda ofisini kwake, nilifika na kusimama pembeni mwa mlango kwa heshima zote uku nikisubili azungumze. "Nyumbani unakaa na nani sanipher??""Mwenyewe " nilijibu. "Hauna ata kioo ?, hauna ata rafiki akakufundisha jinsi ya kuvaa ?, na kubana nywele ? " "Sina rafiki " "Siwezi kushangaa, hakuna mtua anaweza kuwa na rafiki kama wewe, hakuna mtu anaweza kuwa na rafiki wa hovyo kama wewe, nakupa week moja tu ya kubadili hayo mavazi yako otherwise ni kukufuta kazi, maana muonekano wako unaharibu sifa ya ofisi, tazama wenzio tunavyovaa, halafu jiangalie na wewe " alizungumza minah kwa kufoka utazani yeye ndiye mmiliki wa ofisi. Nilipewa vichambo vyangu pale kisha nikatoka na kwenda kuendelea Na shughuli zangu za kiofisi. ******Siku iliyofuata, walahi niliona sasa ile ofisii wasiendelee kunichukulia poa, nilichofanya ni kupigilia mavazi yangu matata sana, kiatu changu kirefu na pochi moja kali mno, ukija upande wa nywele nilikuwa niko vizuri sana kwa kuweka style nzuri, hivyo siku hiyo nilijua kupendeza bhana. Muda wote huo Ambao nilikuwa najiandaa mume wangu alikuwa ameshaondoka kwani alidai kuwa ako na kazi nyingi sana ofisini ata hivyo mimi na yeye hatuwezi kuongozana. Baada ya kujiandaa na kila kitu, kwa mara ya kwanza tangu nimeanza kwenda kazini, siku hiyo nilibolt gari na nashukuru ilikuja gari nzuri kabisa. Nilifika ofisini kwa mwendo wa madaha si unajua tena ukijijua kuwa umependeza lazima ulinge na kujishaua basi nilijua kujishaua kwakweli.Nilitembea kwa mwendo wa madaha, ni kama Mungu alitaka nionekane maana nilikuta baadhi ya wafanyakazi wakiwa pale mapokezi, Minah pamoja na Philly pia walikuwa hapo. Walahi nilijua kuchanganya watu akili, kila mtu aliachia mdomo wazi kwa kunishangaa, Philly wangu alitabasamu na kushindwa kujizuia kabisa kwa mwendo wa haraka akanisogelea. "Weeeh unataka kufanya nini ?" Nilimuuliza kwa sauti ya chini ili watu wasiweze kusikia. "Aaah umenichanganya mama, umependeza mno " alijibu Philly kwa kunong'ona. Philly alinishika mkono na kuniongoza njia na kwasauti ya juu akasema. "Leo sanipher amependeza mno, halafu ananukia hatari sana, mnaonaje leo nikamtoa ata lunch ""Boss umenena halafu ukanena tena, weeeh sanipher, weeh we binti kumbe ni mrembo kiasi hiki, uwiiiih aka kashape sasa aghaaaah, bonge ya chombo " alizungumza william mcharuko wa kiume wa ofisi. "Minah unasemaje kuhusu sanipher leo ??" Philly alimuuliza minah makusudi maana alionekana kukasilika. "Aaah amependeza mno, and tutampeleka lunch leo amejua kufurahisha ofisi" alijibu minah lakini nilijua kabisa amejibu ki unafiki. "Aaah nitampeleka mimi tu, sanipher amejua kuvuluga akili yangu leo, mama naomba nikubebee pochi nikupeleke ata ofisini kwako tu moyo wangu ulizike " "Aaah boss Philly Asante nitaenda mwenyewe " "Aaaah jamani, usinikatili, jamani eti kuna ubaya kama nitambebea sanipher pochi mpaka ofisini kwake ??""Hakuna baya tajiri " Basi Philly alichukua pochi yangu na akiwa amenishika mkono akaniongoza njia kuelekea kwenye ofisi yangu. Kiukweli kila mtu alinisifia kuwa nimependeza. "Hivi kumbe huyu msichana ndio mrembo kiasi hiki ??" Golya alijiuliza kwa sauti. "Kila mtu akaendelee na kazi zake na muache kupiga umbea hapa " alifoka minah kisha akaondoka. Mimi na my wangu tulifika ofisini ile kuingia tu Philly akabana mlango na kunikumbatia kwa nguvu kabisa. "Umependeza sana mke wangu, unanipa amsha amsha ya kuwatambia watu kuwa wewe ni mke wangu wa ndoa"."Jichanganye na akili yako mbovu hiyo, uwatambie kitu gani na tuko kazini, wazo la kupendeza nimelipata jana, nimeona kuwa naweza kufanya kazi yangu nikiwa kwenye muonekano mzuri na inaweza kuleta chachu zaidi " "Achana na masuala ya kazi, uko tayali nikupeleke lunch leo mama ??" "Philly bhana kaendelee na kazi mume wangu badae tutaenda " Basi tulikiss kidogo kisha Philly akatoka nje. Nilianza kufanya shughuli zangu kwa ustadi wa hali ya juu, gafla mlango wangu ukafunguliwa kwa nguvu sana na Minah akaingia. "Oooh karibu " nilimkaribisha Minah. "Ni nini hiki kinaendelea ??" Minah aliniuliza."Kazi za ofisi madam Minah " nilijibu kwa dharau uku nikiacha nilichokuwa nafanya na kumuangalia vizuri usoni. "Ni nini umepanga? Kwanini unaweka ukaribu na Philly wangu ?, we msichana kumbe ni mpuuzi eeh " "Polepole madam, kuhusu Philly sijui unaongea nini, na kuhusu kunishobokea kwake kamwambie aache kunishobokea mimi sio level zake " nilijibu kwa kujiamini. "Usinijibu kama unavyotaka " "Minah unaweza ukatoka nje sasa, hizo hasira zako unaweza kwenda kumwambia kaka yako Philly uko nje na sio mimi ". "Philly sio kaka yangu, ni mume wangu mtalajiwa nakuomba kaa nae mbali ""Ninachojua Philly ni kaka yako, unataka kujua nimejuaje, ngoja nikuambie kuwa wewe ni mtoto ambaye umelelewa na madam Jane, ameanza kukulea tangu ukiwa na miaka 12 pale tu alipokuchukua kwenye nyumba ya watoto yatima, that means Philly ni kaka yako, niachie mimi niwe wifi yako basi " Minah alibaki akishangaa na kutoa macho kama fundi saa amepoteza nati.... ITAENDELEA...

Full 1000
0743433005

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post