SIMULIZI MPYA
MWANA WA MIUJIZA O1
UTANGULIZI
Riwaya hii inasimulia hadithi ya Tumaini, mtoto wa kike aliyezaliwa katika familia inayotamani mtoto wa kiume
Baada ya kutupwa msituni na baba yake, Tumaini anaokolewa na mwanafunzi mmoja, Sara
Tumaini anapookolewa, anaanza kufanya miujiza isiyoelezeka, akiwashangaza na kuwasaidia watu wa kijiji anachoishi
Hadithi hii inaonyesha safari ya Tumaini kutoka kukataliwa hadi kuwa mkombozi wa kijiji, ikisisitiza nguvu za upendo, msamaha na imani
Jina hili linaangazia uwezo wa kipekee wa Tumaini na jinsi anavyobadilisha maisha ya watu wanaomzunguka
UTANGULIZI
Katika kijiji kidogo kilichopo mkoani Shinyanga familia ya Mzee Danielle na mke wake Fahma waliishi maisha ya kawaida lakini yenye changamoto zao
Kijiji hiki kilikuwa na mandhari ya kuvutia na miti ya miembe na mikorosho ikipamba mazingira, nyumba yao ya udongo ilikuwa imezungukwa na mashamba ya mahindi na mtama, na sauti za ndege zilikuwa zikisikika kila asubuhi zikileta uhai na amani
Familia hii ilibarikiwa kuwa na watoto watano wote wa kike. Fahma alikuwa mama mwenye upendo mwingi lakini mume wake Mzee Danielle alihisi aibu kwa sababu hakuwa na mtoto wa kiume
Alitamani sana kupata mtoto wa kiume ambaye angeweza kurithi jina lake na mali zake. Kila mara alipokuwa akizungumza na marafiki zake, alionekana mwenye huzuni na kukata tamaa lakini mke wake alimtia moyo na faraja
Siku moja Fahma alipata ujauzito tena, Mzee Danielle alifurahi na kujawa na matumaini makubwa kwamba hatimaye angepata mtoto wa kiume
Alikuwa akimwomba Mungu kila siku akisema:
“Ee Mungu nipe mtoto wa kiume ili niweze kujivunia mbele ya wenzangu”
Wakati wa kujifungua ulipowadia, Fahma alijifungua mtoto wa kike tena na walimpa jina Tumaini, jina lililokuwa na maana kubwa kwao. Fahma alijawa na furaha kubwa akimshika mtoto wake mikononi mwake na kumkumbatia kwa upendo, alimwangalia Tumaini kwa macho ya matumaini akijua kwamba mtoto huyu alikuwa baraka kubwa katika maisha yao
Lakini kwa Mzee Danielle hili lilikuwa pigo kubwa alipomuona mtoto huyo, alihisi kama ndoto zake zote za matumaini zimevunjika
Alimwangalia Fahma kwa hasira na kusema:
“Hii ni aibu kubwa, nilitarajia mtoto wa kiume lakini umenizalia mtoto wa kike tena”
"Mume wangu tafadhali usimkatae Tumaini, yeye ni mtoto wetu na anahitaji upendo wako, mimi sijapanga tupange mtoto wa kike, mpangaji ni Mungu sio mwanadamu”
“Sijui nitawaambia nini watu wa kijiji, nilitarajia mtoto wa kiume lakini sasa nina watoto wa kike sita, hii ni aibu kubwa”
“Mume wangu, Tumaini ni baraka, ataleta furaha na matumaini katika maisha yetu tafadhali, mpe nafasi” Alisema Fahma kwa moyo wa huruma akimhurumia sana mwanae
“Sina nguvu ya kumkubali, hii ni zaidi ya uwezo wangu”
Mzee Danniel akaondoka eneo hili akiwa na hasira baada ya kuona mambo yameenda kinyume na matarajio
Ndugu msomaji wa riwaya hii, naomba niweke msimamo wangu kidogo hapa kwa nini hili utokea katika jamii
Mume analalamika kwa sababu ya matarajio ya kijamii na kitamaduni kwamba mtoto wa kiume ndiye mrithi wa familia na jina. Hii inasababisha shinikizo kwa wanawake kuzaa watoto wa kiume
Jamii inapaswa kuelewa kwamba jinsia ya mtoto haipaswi kuamua thamani yake. Watoto wote wa kike na wa kiume ni baraka kutoka kwa Mungu na wanastahili upendo na fursa sawa
Kubadilisha mitazamo hii itasaidia kujenga jamii yenye usawa na haki zaidi
Maisha yaliendelea kawaida huku Tumaini akikua katika mazingira ya upendo wa mama yake na kukataliwa na baba yake. Fahma alimlea mwanae kwa upendo na kumfundisha thamani ya maisha, akijua kwamba Tumaini alikuwa na hatma kubwa mbele yake, hatma ambayo ingemletea heshima na furaha kwa familia yao lakini kivuli cha matarajio ya baba yake kilikuwa kikimfuata
Siku moja Tumaini aligundua kuna jambo baya linakuja tokea katika maisha yake, lakini kitu cha kushangaza hapa Tumaini bado ni mdogo atagundua nini sasa, mimi sijui endelea kufuatilia
Tumaini alijua kwamba kuna hatari ilikuwa inakuja mbele yake, ni kuhusu baba yake kumkataa huenda kuna jambo baya litatokea
Baba wa mtoto akashukua shoka...
USIKOSE SEHEMU YA PILI
Tags
simulizi