Namna ya Kuondoa Matangazo Kwenye Application za Simu yako
Kuna wakati unatumia smartphone yako kufanya vitu vya msingi mara ghafla unashangaa tangazo limetokea katikati ya screen yako, hii uchukiza watu wengi sana. Zifuatazo ni namna za kuondoa matangazo yanayo tokea katikati ya screen maarufu kama “Pop up Ads”.
Fungua Browser yako ya simu kisha bonyeza vidoti vitatu kwenye kona kulia chagua settings kutoka kwenye list, kisha chagua Advanced Settings kutoka kwenye menu hiyo. Hakikisha ‘Block pop-ups’ imewekwa on hiyo itakusaidi kila unapo tumia browser yako.
Kama unatumia application ya Google Chrome unaweza pia kuzuia matangazo hayo. Fungua application yako ya Chrome kisha bonyeza vidoti vitatu vilivyo upande wa kulia, sogeza chini mpaka utakapokuta ‘Site Settings’, alafu Pop up bonyeza sehemu hiyo kisha utaona maandishi yakibadilika kuwa “Pop-ups Block” kama matangazo yataendelea rudia hatua hii na ubonyeze tena kwenye option hiyo hiyo.
Ondoa matangazo kwa njia ya Google Chrome Data Saver,njia hii ni nzuri zaidi kuliko njia zote na inasaidia kuongezeka kwa kasi ya kuperuzi kwenye internet.
Fungua application yako ya Chrome kisha bonyeza vidoti vitatu vilivyo upande wa kulia kisha bonyeza “settings” chini kabisa ya settings akikisha kuna tiki kwenye neno “Data Saver” bonyeza kitufe kionyeshe On.
Pia unaweza kutumia Application kama vile “Adblock” application hii inawapa watumiaji wake kuperuzi kwenye browser ambayo inazuia matangazo kabisa. Unaweza kupata application hii kutoka Google Play store bure Kabisa