TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

NGUVU YA MAAMUZI 01

𝗝𝗜𝗡𝗔 𝗟𝗔 𝗥𝗜𝗪𝗔𝗬𝗔: 𝗡𝗚𝗨𝗩𝗨 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗠𝗨𝗭𝗜
𝗠𝗧𝗨𝗡𝗭𝗜: 𝗝𝗨𝗦𝗧𝗜𝗡 𝗕𝗔𝗥𝗨𝗧𝗜
𝗠𝗪𝗔𝗞𝗔: 2024
𝗦𝗠𝗦 & 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣:
+255 752 474 397
𝗨𝗧𝗔𝗡𝗚𝗨𝗟𝗜𝗭𝗜

𝗡𝗚𝗨𝗩𝗨 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗠𝗨𝗭𝗜 ni hadithi ya kusisimua kuhusu Emmanuel, kijana anayekabiliana na maumivu ya moyo na changamoto za maisha. Baada ya kupoteza upendo wake wa dhati, anaanza safari ya kujikomboa na kugundua nguvu ya maamuzi yake. Kupitia huzuni na matumaini, Emmanuel anajifunza kwamba maamuzi yake yanaweza kubadilisha maisha yake na ya jamii yake

𝗦𝗘𝗛𝗘𝗠𝗨 𝗬𝗔 𝗞𝗪𝗔𝗡𝗭𝗔

Bukoba kata ya Rwamishenye ilikuwa na mandhari ya kuvutia, yenye milima na mabonde yaliyofunikwa na kijani kibichi

Hapa ndipo Emmanuel na Hawa walipokutana mara ya kwanza, upendo wao ulikuwa ni wa dhati kama maua ya waridi yanayochanua katikati ya jangwa, wenye harufu na rangi angavu

Walipokutana mara ya kwanza walihisi kama walikuwa wameumbwa kwa ajili ya kila mmoja, walikuwa na ndoto ya kuoana na kuishi pamoja maisha yenye furaha na mafanikio

Siku moja walikuwa wamekaa chini ya mti mkubwa wa mkuyu wakitazama machweo ya jua, jua lilikuwa linazama taratibu likiiacha anga ikiwa na rangi ya dhahabu na machungwa

Emmanuel alimshika mkono mpenzi wake Hawa kwa upole akihisi joto la upendo wake likimzunguka, lakini hata hivyo waliishi maisha magumu sana, kila mmoja aliweza kumvumilia mwenzake

"Hawa najua maisha yetu ni magumu lakini naahidi nitafanya kila niwezalo kuboresha hali yetu, nakupenda kwa dhati ya moyo wangu, nitakupenda milele"

"Nina imani nawe Emmanuel hata usiwaze, sitaweza kukusaliti hata siku moja, upendo wetu ni kama huu mti wa mkuyu wenye mizizi imara na matawi yanayokua na kustawi kila siku. Tutashinda changamoto zote"

Hawa ameweka ahadi katika maisha ya Emmanuel kwamba hawezi msaliti katika maisha yake, aliamini kwamba kwa pamoja wangeweza kuzishinda changamoto za maisha

Hawa alikuwa ni binti mrembo sana, alikulia katika familia ya kawaida, macho yake yalikuwa ni makubwa ya kahawia yaliyong'aa kama nyota ya usiku, na tabasamu lake lilikuwa la uwezo wa kuangaza hata nyakati za giza

Alikuwa na sauti nyororo yenye utulivu ambayo ilimpa Emmanuel faraja kila walipokuwa pamoja

Kutokana na uzuri huo wavulana mtaani walimsumbua sana, lakini Hawa alisimamia msimamo wake kwa Emmanuel

Ndugu msomaji wa riwaya hii, maisha hayana huruma ilimlazimu Emmanuel kuondoka Bukoba kwenda mkoa mwingine ambapo huko alipata kazi, ilikuwa ni uamuzi mgumu sana lakini alitakiwa akubaliane na hali, ilikuwa ni njia pekee ya kuboresha maisha yao

Siku ya kuondoka ikawadia, Hawa alijikuta akimwaga machozi yasiyo na idadi lakini alijitahidi kujizuia, machozi yalizidi kutoka bila hiari

"Emmanuel naomba usinisahau tafadhali, nitakusubiria mpenzi wangu hata iwe miaka mingapi"

"Hawa, wewe ni ua la moyo wangu, nitakupenda daima, nitakaporudi tutaoana na kuishi maisha ya furaha"

Hawa alimsindikiza Emmanuel hadi kituo cha basi, walikumbatiana muda mchache huku machozi yanatoka machoni mwao

"Nitakumiss sana Emmanuel lakini najua hii ni kwa ajili yetu sote" alisema Hawa kwa huzuni

Walibadilishana ahadi za upendo, ahadi hiyo ilikuwa ni kuachana kwa muda

Emmanuel akaingia ndani ya gari hili kuanza safari gafla...

𝗜𝗧𝗔𝗘𝗡𝗗𝗘𝗟𝗘𝗔 𝗦𝗘𝗛𝗘𝗠𝗨 𝗬𝗔 𝗣𝗜𝗟𝗜
   ••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
𝗕𝗔𝗥𝗨𝗧𝗜 𝗪𝗥𝗜𝗧𝗜𝗡𝗚 𝗦𝗘𝗥𝗩𝗜𝗖𝗘𝗦 ✍️✍️


JE UNAHITAJI HUDUMA YA UANDISHI (KUANDIKIWA AU KUFUNDISHWA)?

Naandika makala mbalimbali

¤ 𝗛𝗮𝗱𝗶𝘁𝗵𝗶, 𝗿𝗶𝘄𝗮𝘆𝗮, 𝘁𝗮𝗺𝘁𝗵𝗶𝗹𝗶𝗮 𝗻.𝗸

¤ 𝗠𝗮𝗽𝗲𝗻𝗱𝗲𝗸𝗲𝘇𝗼 𝘆𝗮 𝗺𝗶𝗿𝗮𝗱𝗶 ( 𝗣𝗿𝗼𝗷𝗲𝗰𝘁 𝗮𝘂 𝗯𝘂𝘀𝗶𝗻𝗲𝘀𝘀 𝗽𝗿𝗼𝗽𝗼𝘀𝗮𝗹𝘀)

¤ 𝗠𝘂𝗵𝘁𝗮𝘀𝗮𝗿𝗶 ( 𝗠𝗶𝗸𝘂𝘁𝗮𝗻𝗼, 𝘃𝗶𝗸𝗮𝗼 𝗻.𝗸)

¤ 𝗪𝗮𝘀𝗶𝗳𝘂 𝗯𝗶𝗻𝗮𝗳𝘀𝗶 ( 𝗠𝘁𝘂, 𝗸𝗮𝗺𝗽𝘂𝗻𝗶, 𝘁𝗮𝗮𝘀𝗶𝘀𝗶 𝗻.𝗸)

¤ 𝗠𝗮𝘀𝗵𝗮𝗶𝗿𝗶, 𝘁𝗲𝗻𝘇𝗶 𝗻.𝗸

¤ 𝗕𝗮𝗿𝘂𝗮 𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶

𝗣𝗶𝗮 𝗻𝗮𝗮𝗻𝗱𝗶𝗸𝗮 𝗺𝗮𝗸𝗮𝗹𝗮 𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶 𝗸𝘂𝗵𝘂𝘀𝘂 𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝗮𝘂 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝘆𝗼𝘆𝗼𝘁𝗲 𝗶𝗹𝗲 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗷𝗮𝗺𝗶𝗶 𝗸𝘂𝗹𝗶𝗻𝗴𝗮𝗻𝗮 𝗻𝗮 𝘂𝘇𝗼𝗲𝗳𝘂 𝗮𝘂 𝘂𝗲𝗹𝗲𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗻𝗴𝘂 𝘄𝗮 𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝗵𝗶𝗹𝗼 ( 𝗠𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼, 𝗻𝗱𝗼𝗮 𝗻.𝗸)

𝗞𝗶𝘂𝗳𝘂𝗽𝗶 𝗺𝗶𝗺𝗶 𝗻𝗶 𝗺𝘄𝗮𝗻𝗱𝗶𝘀𝗵𝗶 𝗺𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗸𝗶𝗽𝗮𝗷𝗶. 𝗞𝗔𝗥𝗜𝗕𝗨 🙏🙏

𝗠𝗔𝗪𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜𝗔𝗡𝗢

𝗦𝗠𝗦 💬 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣 🔔 +255 752 474 397

𝗦𝗠𝗦 𝗧𝗨 𝗨𝗦𝗜𝗣𝗜𝗚𝗘 𝗡𝗔𝗢𝗠𝗕𝗔 𝗧𝗨𝗖𝗛𝗔𝗧, 𝗡𝗜𝗡𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗡𝗚𝗔𝗠𝗢𝗧𝗢 𝗬𝗔 𝗨𝗦𝗜𝗞𝗜𝗩𝗨 🦻🦻

𝗔𝗦𝗔𝗡𝗧𝗘 🙏🙏

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post