𝗝𝗜𝗡𝗔 𝗟𝗔 𝗥𝗜𝗪𝗔𝗬𝗔: 𝗡𝗚𝗨𝗩𝗨 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗠𝗨𝗭𝗜
𝗠𝗧𝗨𝗡𝗭𝗜: 𝗝𝗨𝗦𝗧𝗜𝗡 𝗕𝗔𝗥𝗨𝗧𝗜
𝗠𝗪𝗔𝗞𝗔: 2024
𝗦𝗠𝗦 & 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣:
+255 752 474 397
𝗦𝗘𝗛𝗘𝗠𝗨 𝗬𝗔 𝗣𝗜𝗟𝗜
Emmanuel akaingia ndani ya gari gafla ikanyesha mvua kubwa ya kutisha, hali iliyosababisha hawa watu wawili kupotezana katika mazingira ya kutatanisha lakini Hawa aliendelea kuwa na imani kwamba mpenzi wake atafika salama
Wakati Hawa anarudi nyumbani, njiani alikutana na kijana mmoja mwenye sura ya kuvutia na mavazi ya kifahari, jina lake aliitwa Goodluck yaani Good kama Good luck
Goodluck alikuwa kijana tajiri, mwenye biashara nyingi na mali nyingi mjini Bukoba ingawa alijua Hawa na Emmanuel wapo katika mahusiano ya kimapenzi lakini hakujali hilo
Goodluck alimsalimu Hawa kwa tabasamu la kuvutia
“Habari yako dada mrembo, naweza kukusindikiza nyumbani”
Hawa alihisi aibu kidogo lakini alikubali kwa heshima "Asante lakini naweza kujisindikiza mwenyewe”
Goodluck hakukata tamaa “Ningependa tu kuzungumza nawe kidogo, najua maisha yako na Emmanuel yanaweza kuwa magumu lakini ningependa kukusaidia kwa namna yoyote”
Hawa alihisi mchanganyiko wa hisia, alimpenda Emmanuel kwa dhati lakini maisha yalikuwa magumu sana bila yeye. Goodluck alikuwa na kila kitu ambacho angeweza kutamani lakini moyo wake ulikuwa kwa Emmanuel
Safari ya Emmanuel kuelekea Mwanza ilienda vizuri kwa kudra za Mwenyezi Mungu, aliahidi atapambana katika maisha yake kwa juhudi ili baadae aje kuwa na Hawa
Baada ya masaa kupita, Emmanuel alifika salama jijini Mwanza akiwa amechoka lakini alijipa matumaini
Mwanza ilikuwa na mandhari tofauti kabisa na Bukoba, mji ulijaa kelele za magari na watu wakikimbizana na shughuli zao za kila siku
Emmanuel alihisi upweke na mara nyingi alikumbuka nyumbani na mpenzi wake wa moyoni, Hawa
Emmanuel akakodi gari kwenda kiwanda kimoja cha samaki, alipokelewa vizuri na uongozi na kuahidi atafanya kazi kwa bidii katika kiwanda hicho cha samaki
Alikuwa na ndoto ya kuboresha maisha yake na kurudi Bukoba akiwa na uwezo wa kumtunza Hawa akijua kwamba maisha yalikuwa magumu lakini aliamini kwamba juhudi zake zingezaa matunda
Usiku mmoja baada ya kazi ngumu, Emmanuel alikaa kando ya Ziwa Victoria akitazama mawimbi madogo yakipiga ufukweni
Alijikumbusha ahadi yake kwa Hawa na hii ilimpa nguvu ya kuendelea kupambana, alijua kwamba upendo wao ulikuwa na nguvu ya kushinda changamoto zote
Hawa akiwa Bukoba alijaribu kumkwepa Goodluck lakini kijana huyo tajiri hakuwa na nia ya kumuacha
Alimpelekea zawadi na kumwalika kwenye hafla mbalimbali. Hawa alihisi kuvutiwa na maisha ya kifahari lakini moyo wake ulikuwa bado kwa Emmanuel
Siku moja Hawa aliamua kumwambia Goodluck ukweli:
“Goodluck nakushukuru kwa wema wako lakini moyo wangu uko kwa Emmanuel, yeye ni maskini lakini ananipenda kwa dhati na mimi pia nampenda”
Goodluck alihisi huzuni lakini aliheshimu uamuzi wa Hawa
“Ninaelewa Hawa natumaini kwamba utapata furaha unayostahili”
Hawa alihisi faraja baada ya kumwambia Goodluck ukweli, alijua kwamba upendo wake kwa Emmanuel ulikuwa wa kweli na alikuwa tayari kuvumilia changamoto zote kwa ajili ya mpenzi wake
Baada ya muda kusonga, Hawa alihisi kuchoshwa na ahadi za Emmanuel ambazo aliona kama ni hewa
Maisha yalikuwa magumu na upweke ulimzidi. Goodluck alikuwa na mali na uwezo wa kumtunza, alionekana kama suluhisho la haraka kwa matatizo yake
Hawa akaamua kumsahau Emmanuel na kumgeukia Goodluck bila kujua athari za maamuzi hayo
Goodluck alifurahi sana Hawa alipokubali kuwa naye, alimpeleka nyumbani kwao na kumtambulisha kwa familia yake
Familia ya Goodluck ilimkaribisha Hawa kwa furaha, waliona kwamba alikuwa chaguo bora kwa kijana wao
Harusi ilianza kupangwa kwa haraka na maandalizi yalikuwa ya kifahari
Wakati huo huo huko Mwanza, Emmanuel alikuwa akiendelea kupambana, alikuwa ameanza kuona matunda ya juhudi zake, wakiwa kwenye kiwanda sasa anaendesha mitambo ikasikika sauti kubwa ya kushtua ikisema....
𝗨𝗦𝗜𝗞𝗢𝗦𝗘 𝗦𝗘𝗛𝗘𝗠𝗨 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗧𝗨, 𝗦𝗘𝗛𝗘𝗠𝗨 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗧𝗨 𝗜𝗡𝗔𝗛𝗨𝗦𝗨 𝗛𝗔𝗕𝗔𝗥𝗜 𝗭𝗔 𝗞𝗨𝗦𝗛𝗧𝗨𝗔, 𝗦𝗘𝗛𝗘𝗠𝗨 𝗛𝗜𝗜 𝗬𝗔 𝗣𝗜𝗟𝗜 𝗜𝗡𝗔𝗬𝗢𝗛𝗨𝗦𝗨 𝗠𝗔𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗣𝗬𝗔 𝗜𝗠𝗘𝗜𝗦𝗛𝗜𝗔 𝗛𝗔𝗣𝗔
Tags
riwaya