ANANIUMIZA NAOGOPA KUMWAMBIA NO 3
MTUNZI JOGOO POLL
NO 0657 774735
yule kaka ndio akawa anaenda chumbani kwa yule dada ameshikwa mkono na yule mwanamke mwenye nia ya kumchuna sio kama mimi nina nia anioe niwe mkewe nikaona apa nifanye kitu nimuokoe yule kaka asiingie kwenye ule mtego.
nilibeba ndoo ya maji kama nawai chooni alafu nikajifanya nimeteleza nikapiga yowe kwa nguvu kabla yule kaka ajaingia chumbani ila yowe niliita mama weeee yalaaa.
yule kaka ni mpole mwenye utu alinikimbilia akanipa pole uku anawai mguu kuunyosha yani aliwaza nimeumia mguu basi alipo shika mguu nilisisimka sana sababu nampenda nikisema ivi nimesisimka kwa wale wakubwa wanajua nimemaanisha nini maana nimeshikwa na mtu niliyempenda.
basi yule kaka akawa anapeleka mkono juu anashusha chini ananichua kupitia viganja vyake mimi natamani aendelee tu maana nishafanikiwa 1 kashagusa mwili wangu madada wengine waliamka wakanipa pole ila kuna jitu 1 lilikuja lilinikela likamwambia kaka yule ebu muache kwanza kumchua ebu anyanyuke kwanza tujuwe wapi kaumia anaweza kukanyaga.
alinikela sana nikanyanyuliwa nikajifanya mguu aliokuwa ananichua ndio unauma naona bajaji imekuja nikaingizwa kwenye bajaji ili nipelekwe osp.
namsikia yule mwanamke anamwita kaka yule wewe kaka njoo acha wengine nao wamsaidie si washaamka wote.
moyoni natamani kumjibu wewe dada ukome na kudanga kwako ila ndio siwezi naomba kaka yule akatae maana mimi siumwi Bali nimemuokoe yeye asiende kwenye mtego wa mdangaji namsikia kaka akisema.
izo nguo azina umuhimu sana nikamwacha mgonjwa mimi napenda sana utu kuliko Mali taka.
uku anaingia kwenye bajaji.
deleva wa bajaji akasema uyu uyu anatosha asije akabanwa mgonjwa wengine mkapumzike tu.
nilifulai nikasema deleva wa bajaji kanena tulikaa wawili tu nyuma ya bajaji nilitamani ajuwe isia zangu kwake ila siwezi kumwambia naanzaje nikamwambia kaka naisi kizungu zungu akanijibu.
fumba macho dada usiangalie mbele.
deleva wa bajaji akasema wewe mwambie asogee kwa pembeni alafu akulalie kwenye mapaja aache kunyanyua shingo juu.
nilifulai deleva wa bajaji kama anajuwa isia zangu juu ya kaka uyu nilisogea kwa pembeni nikamlalia mapajani dah nilisikia raha nilitamani osp iwe mkoa niendelee kulala kwenye mapajani kwa ninaye mpenda.
basi nilimsikia deleva wa bajaji anamuuliza kaka uyu nimekusikia umesema unapenda utu kuliko Mali taka unamaanisha nini ??
kaka akajibu yule dada ameanua nguo zangu sasa anasema nikachukue nguo chumbani kwake nimuache mgonjwa sasa ndio maana nikamjibu vile sababu nikwambie kitu Mali taka ni izi nguo tunajistili mwili tu ila Mali mzuri ni matendo matendo yanafanya njia ya pepo iwe safi kabisa na mungu ametusisitizia sana matendo mema umenielewa sijui.
deleva wa bajaji akasema nimekuelewa kwani yule dada aanue nguo zako una mausiano nae??
kaka yule akajibu apana sina mausiano naye.
deleva wa bajaji akasema lafiki yangu nakushauri kitu acha mazoea na yule dada yule dada sio anakuita ndani lengo lake nguo yule anataka afanye mapenzi na wewe ili akuchune yule ni paka wa bar tunamjua vizuri na kundi lake lote sisi madeleva tunajua mengi sana sababu usiku tunawabeba sana awa wewe kama nguo zako mwambie akuludishie kwenye kamba atakuja kukualibia maisha yako bule.
kaka akasema dah unayosema kweli naisi najalibu kuvuta picha la tukio alilonifanyia asubui alivua kanga ndani chumbani kwangu akajifanya imedondoka dah.
deleva wa bajaji akasema yule kukaa mtupu mwenzio aoni tabu kazi yake yenyewe lazima akae nusu mtupu ili amvutie mtu akatoe nusu iliyobakia awe mtupu kabisa yule anajiita chake mkononi mguu ukutani yani afai kabisa kuwa mwanamke wa mtu uyu anafaa kuwa ivyo ivyo kuwa mwanamke wa jamii yenye tabia mbaya.
kaka akasema deleva nashukulu sana kwa kuniambia ukweli japo mimi simaindi sana ivyo vitu najuwa madhara yake naona lafiki zangu kazini wanaongea peke yao kama machizi kisa mapenzi yani utamkuta anajisonya sonya mimi sitaki kwa sasa mpaka nitapompata mtu aliyetulia nitakuwa nae.
deleva wa bajaji akasema nikwambie kitu kama ungeweza au sijui kama nitakuuzi nisamehe mimi naona ungemchukua uyu dada tunayempeleka osp mngeendana uyu dada anayo heshima zote kijiwe kizima tunamuheshimu na mpaka wale mafisi wa kijiwe wanasema yule dada anafaa kuwa mke na si demu unajuwa kuna msichana anajiweka yeye muonekano wa kuwa demu si mke
ngoja nikufafanulie kwa mfano wa vitendo utamuona msichana kavaa kipensi mapaja yote nje uyu kajiweka kidemu si mke mke anajistili wewe unazani angekuwa demu uyo wala asingesema kaka nasikia usingizi ungestukia kashakulalia ghafla tu mademu watu wa kujiongeza ongeza tu.
kaka akasema kwanini.
deleva wa bajaji akasema sikia nikwambie kitu madem akipanga chumba ataki umpeleke gest ila chumbani kwake anapafanya gest pasipo mwanaume kujua akikwambia nina chumba changu twende ukikubali imekula kwako bora ungeenda gest ungelipa pesa kidogo kuliko kwake
picha inaanza anakuaga anaenda chooni kwanza kipindi icho mpo bar kumbe chooni kule anaenda kuseti mipango yake anamwambia shoga yake zima umeme nyumba mzima alafu kama kawa toa na feni yangu chumbani kama kawa
alafu analudi kwako twende nyumbani mnaenda wewe unaona kitonga kumbe umeingia kwenye 18 ya demu anaenda kukunyonyoa manyoya
ukifika ndani tu dem anajifanya anawasha taa alafu anajiongelesha umeme umekatika au kabla ajaongea neno la pili unasikia odi shoga yake yule anagonga akimfungulia mlango tu shoga anasema zamu yako kununua umeme ebu nipe pesa nikanunue mbona unatutesa wenzio na joto saizi tunataka tupumzike na mabwana zetu.
kidume unaanza kunyonyolewa sasa utasikia baby mpe elf 15 ya umeme uyo zamu yangu leo kidume unazama mfukoni unatoa 15 ile ukimpa 15 shoga yule yule anamwambia mwenzie ivi
shoga kaja fundi feni kasema usije ukamlaumu anasafili feni ina wiki 3 kwa fundi na wewe unatia aibu unazani anakudai mamilioni kumbe 15 tu.
utasikia tena baby mpe 15 akanichukulie na iyo feni akitoka kununua umeme anaipitia.
kidume unanyonyoka tena pesa paa.
kumbe umechezwa sheree ao ndio madem.
"Mimi nilitamani nicheke kumbe kuna wanawake wanafanya michezo ya upigaji pesa kama ivi.
kaka akasema duu asante kwa somo nadhani tushafika osp ngoja nimuamshe ili twende naye ndani.
deleva akasema poa ila mwambie ukweli awe wako mmefanana tabia.
kaka akasema mwenzio kutongoza sijui ila uyu dada katulia kweli shida namuanzaje??
deleva wa bajaji akasema utajuwa leo utamwanzaje mimi nawaacha osp.
waliniamsha wakanibeba mpaka kwa dokta dokta akasema tumsubili nililala tena mapajani kwa kaka yule.
deleva wa bajaji akasema kazi kwako mimi nasepa akaondoka.
tulibaki wenyewe sasa yani...........
ITAENDELEA
Tags
simulizi