KANUNI YA RECIPROCITY INAVYOFANYA KAZI KATIKA MAHUSIANO..
Kanuni ya RECIPROCITY ni moja ya Kanuni au sheria zinazofanya kazi sana katika saikolojia ya Mwanadamu na Jamii kiujumla.
Kanuni hii inasema kuwa...
" Unapopokea jambo fulani jema kutoka kwa Mtu, unajitengenezea mazingira ya kumfanyia jambo jema huyo Mtu kwa wakati mwingine. "
Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba ikiwa mtu fulani akikutendea jambo jema au kukupatia kitu leo, ndani yako utajitengenezea mazingira ya kujihisi unadaiwa kumfanyia jambo lingine lolote jema kama malipo kwa jambo alilokufanyia mwanzoni.....
Ni Ile hali ya kujiona kama una deni la kulipa pale unapofanyiwa tendo jema na Mtu na ukahisi kabisa kuna ulazima wa kufanya hivyo,
Kanuni hii ya RECIPROCITY ina nguvu sana katika ufanyaji kazi wake maana huwa inamfanya Mtu ajihisi kulipa wema aliofanyiwa na Mtu mwingine bila hata ya kudaiwa wala kuambiwa alipe huo wema aliofanyiwa...
Ndio maana katika kuielezea hapo mwanzo nilisema kuwa ni kamuni inayofanya kazi katika Saikolojia ya Jamii nzima na si Mtu mmoja tu, inafanya kazi katika maeneo yoyote na kwa wakati wowote haijali Mtu, eneo au nyakati ya kufanyika kwake kazi...
Na moja ya maeneo ambayo Kanuni hii inafanya kazi ni eneo la Mahusiano au mapenzi na ndilo nitakalolielezea,..
Kanuni ya RECIPROCITY huwa inatumika sana katika mahusiano ya mapenzi, na Watu ambao wanajua namna ambavyo Kanuni hii ya RECIPROCITY inavyofanya kazi huwa wanafaidika nayo zaidi Iwe nikwa ubaya au Kwa uzuri...
Kuna baadhi ya Watu huwa wanatongoza kwa kutumia kanuni hii ya RECIPROCITY, kuna usaliti mwingi unatendeka katika mahusiano kwa chanzo cha hii Kanuni ya RECIPROCITY, yaani kwa kiasi kikubwa Kanuni hii imeteka eneo kubwa la Mahusiano ya mapenzi na katika maeneo mengine ya kajamii....
Unaposikia Mdada au Binti Mwanafunzi kanunuliwa chipsi au kapewa lift na bodaboda kisha akakubali kufanya mapenzi na Mwanaume aliyemnunulia hizo chipsi wala usishangae ni Kanuni ya RECIPROCITY imetumika Kutokea Kwa hilo jambo...
Unaposikia Kijana ameangukia katika penzi zito la " Shuga Mami " kwa sababu ya vipesa alivyokuwa anahongwa jua kilichomfanya akubali sio hivyo vipesa bali ni hii Kanuni ya RECIPROCITY imemsukuma amkubalie huyo Mumama....
Ewe Binti uliyepo shule, unayejitunza na unayeitafuta Ndoa yako hapo baadae, Ukiona Mwanaume anakupa ofa kila siku ni heri uzikatae mapema maana kuna siku inakuja usiyoijua utajikuta unamkubalia njama yake ya kufanya mapenzi na wewe bila ya yeye kutumia nguvu kubwa zaidi ya hizo ofa anazozitoa kwako ambayo ndoo Kanuni ya RECIPROCITY...
Hizo ofa unazopokea kila siku kutoka kwake taratibu zinakujengea mazingira ya kujihisi Kwa kufikiri kuwa unadaiwa na unatakiwa kulipa fadhila ya kile anachokufanyia ambayo ndoo huo mwili wako, na hapo ndipo mabinti wengi huangukia kwenye kuwapa miili yao Wanaume ambao hawaendani nao Kwa Kanuni Hii ya RECIPROCITY ilivyotumika kwao...
KIJANA/ MWANAUME au uliyeoa hutakiwi kumlaumu au kumpiga Mpenzi wako ukigundua kuwa anakusaliti, jitafakari kwanza huwenda Kuna huduma za mahitaji huzitoi Kwa mwenzi wako, hivyo kakutana na Wanaume wanaojua kutumia Kanuni hii ya RECIPROCITY wakamshawishi Mchumba au mke wako akusaliti Kwa huduma za mahitaji walizokuwa wakimpatia.....
Tags
Mahusiano