DijitoStore - Business software

JINSI YA KUPIKA KEKI YA CHUNGWA

JINSI YA KUPIKA KEKI YA CHUNGWA
MAHITAJI
👉Machungwa 2
👉Sukari robo
👉Mayai 5
👉Mafuta robo chupa
👉Vanilla kijiko 1 cha chai
👉Baking powder kijiko 1 cha chai
👉Unga wa ngano robo kilo
~ Blueband au siagi kijiko kimoja cha chakula (si lazima kuweka lakini).

🌷MAANDALIZI🌹
🌴Chukua mayai yakoroge vizuri pamoja na vanilla, tia sukari na endelea kukoroga🌲

🌳Saga maganda ya chungwa vijiko 2 weka ktk mchanganyiko wako na ukoroge. Epuka kuweka maganda mengi keki itakuwa chungu☘️

🌿Kamua juisi ya chungwa robo kikombe changanya vizuri, chukua mafuta changanya💐

🍃Chukua baking powder kijiko 1 changanya na unga Kisha tia kwenye mchanganyiko wako na ukoroge vizuri🌱

🌺Chukua chombo cha kuokea kipake blueband kisha nyunyizia unga kidogo kisha oka keki yako kwa joto la 170° au kwa jiko la mkaa.🌾
kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post