JINSI YA KUPIKA KEKI YA MAZIWA ( MILK CAKE ) NYUMBANI.
MAHITAJI NA VIPIMO
i. Siagi - Kikombe 1
ii. Sukari - Kikombe 1
iii. Unga - Vikombe 2
iv. Maziwa - 1/2 (nusu) Kikombe
v. Mayai - 4
vi. Baking Powder - 1 Kijiko cha supu
vii. Arki rose - kidogo
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
A)JIKO LA OVEN
1. Washa oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.
2. Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.
3. Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.
4. Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.
5. Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)
6. Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.
7. Ipike (Bake ) mpaka iwive.
8. Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande.
B)JIKO LA MKAA
washa jiko lako la mkaa.
2. Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.
3. Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.
4. Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.
5. Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)
Chukua sufuria umimine MCHANGANYIKO WAKO kisha uweke jikoni.
Funika MCHANGANYIKO WAKO huku ukiweka moto juu na kuacha chini kidogo.
Tags
Jikoni Leo