MTEMI ISIKE NA MAJESHI YA VON PRINCE 01
Mt ISIKE Alitawala kuanzia mwaka 1885, yeye alikuwa mtoto wa Mt Kiyungi kama alivyokuwa Swetu Kalonga ambaye aliwaua nduguze wa tumbo la Fundikira ili tumbo la Kiyungi litawale kwa nafasi bila kuingiliwa na tumbo la Fundikira. Swetu Kalonga kwa mara nyingine tena alimshawishi kaka yake Isike wawaue tumbo la Fundikira ili wajihakikishie utawala utabaki katika tumbo lao la Kiyungi. Mt Isike alikubali ndipo akapanga mipango na wazee (wanikulu) wamwite Nyanso Bint Fundikira toka kwake Ndevelwa na akifika Ikulu ya Itetemya wamuue
Tags
TaboraYetu