MTEMI ISIKE NA MAJESHI YA VON PRINCE CHAPTER 2
wakachimba shimo na wakachomeka mikuki na miti yenye ncha kali ndani yake kisha wakaliwekea fito nyembamba kwa juu na kulifunika kwa majani wakaweka kiti juu yake ili atakapokuja Nyanso wamkaribishe akae katika kiti hicho atumbukie shimoni ili mikuki imchome mpaka afe.
Kwa bahati wakati wakipanga mipango hiyo nje alikuwepo mtoto wa kaka yake Ifuma akiitwa #Kipini aliwasikia yote waliyopanga , Kipini yeye alikuwa mwehu ndipo alipokuja shangazi yake Nyanso kuitikia wito wa Mt Isike yeye Kipini alianza kumwambia Nyanso
"sengi ngenewikale hanahohisumbu wasimbagaliina watulaga na masonga walikova wakuwulage, ngeneugeme kwikalanaho"
ndipo Nyanso na wazee wakabaki wanashangaa mlinzi mmoja wa Nyanso akaenda akakiondoa kile kiti akakikalia yeye kwanza , akasimama akaanza kuchoma choma na mkuki pale palipokuwa kiti akaona mchanga unatumbukia ndani ya shimo ndipo Nyanso akamuuliza Mt Isike
"nasumulakii mbona uliova kuniwulaga? Mt Isike akawa hana jibu. Nyanso akakasirika sana akaamua kuondoka na kurudi Ndevelwa
Tags
TaboraYetu