HIVI NDIVYO VITUKO VITATU VYA HAYATI RAIS ROBERT MUGABE AMBAVYO KAMWE HAVITOSAHAULIKA.
Mbali na hotuba zake za kupinga nchi za Magharibi kuingilia au kutaka kushawishi tawala za nchi za Afrika na uamuzi wake wa kuwapokonya ardhi wazungu nchini Zimbabwe mwanzoni mwa miaka ya 2000, Robert Mugabe anasifika kwa kuwa mchekeshaji mzuri kiasi cha kusemwa kwamba anaweza kushindana na wachekeshaji maarufu zaidi duniani.
Rais huyu wa Zimbabwe aliyekuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo kwa miaka zaidi ya 36. Pia, alikuwa anatoa kauli tata sana,
#Hebu sasa tuzipitie baadhi ya kauli hizo:
5. KUMCHUMBIA RAIS OBAMA.
Miongoni mwa mambo yanayofurahisha wengi sana ni tukio la harusi. Lakini Rais Mugabe alipotangaza kwamba ana mpango wa kumchumbia na kumvalisha pete ya uchumba Rais Obama, wengi walishangazwa. Akiongea katika kituo cha utangazaji cha taifa, Rais Mugabe alisema, “Nimeshaamua – kwakuwa Rais Obama anaunga mkono ndoa za jinsia moja, anahamasisha watu wenye uhusiano wa jinsia moja na anazungumzia kwa furaha – kwahiyo itabidi nisafiri kwenda Washington DC, nipige goti na kumvalisha pete ya uchumba kwenye kidole chake.”
Nani angejuwa kwamba Obama angepata bahati kubwa kiasi hiki?
Hata hivyo, Rais Mugabe akabadili gia ghafla na kuanza kuishambulia Mahakama ya Juu Zaidi ya Marekani kwa kutoa uamuzi wa kuidhinisha ndoa za jinsia moja katika majimbo yote 50 nchini humo.
4. ALIVYOMROPOKEA ASKOFU DESMOND TUTU KWENYE KADAMNASI.
Baada ya Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini kusema kwamba Rais Mugabe ni mfano mzuri sana wa madikteta wa Afrika kwamba ni kinyago kichotengenezwa na baadaye kumtisha aliyekitengeneza, Rais Mugabe hakuweza kumkalia kimya. Aliamua kuikuza mada hiyo kwa kusema mbele ya kadamnasi, “Kale (Desmond Tutu) ni kaaskofu kadogo sana kenye hasira, kaovu na kenye chuki binafsi.” Kauli hii aliitoa mwaka 2004 lakini mwaka 2013 Mugabe alimchokonoa tena Askofu huyu wa Kanisa la Anglikana, safari hii kwa msimamo wake wa kuunga mkono uhusiano wa jinsia moja.
“…. eti tuna mwanaume anayeheshimika, tena ana cheo cha Askofu. Tutu anatakiwa kujiuzulu kwa sababu anaunga mkono wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, jambo ambalo ni ovu kabisa. Sisi hatuwataki watu wa aina hii.”
Labda vita yao hii ya maneno ilisababishwa na kila mmoja kumchukia mwenzie kwa sababu Askofu naye alibwatuka mara moja kwa kusema, “Namsikitia Mugabe kwa kila namna ambayo mtu anaweza kufikiria kwa sababu alikuwa kiongozi mzuri sana miaka ya nyuma.
3. ALIPOZUNGUMZIA KIWANGO KIKUBWA CHA RUSHWA KIWANGO NCHINI NIGERIA.
“Inamana tumekuwa kama Naijeria kwamba unatakiwa kuingiza mkono mfuko ili upate kila unachohitaji?”, ndio lilikuwa swali lake. Kauli hii ilitolewa na Rais Mugabe alipokuwa akizungumza kwenye chakula cha mchana katika sherehe ya kutimiza miaka 90 na kuendelea, “Ukipanda ndege nchini Naijeria basi utaona wahudumu wa ndege wanajizungusha tu bila kuruhusu ndege ipae mpaka wapewe rushwa.”
Kitendo cha Mugabe kushambulia kiwango kikubwa cha rushwa nchini Naijeria kilionesha kupingana na takwimu za viwango vya rushwa duniani ambapo Naijeria ilikuwa nafasi ya 144 huku Zimbabwe ikiwa nafasi ya 157 mwaka 2013. Mwaka 2015, Naijeria ilikuwa nafasi ya 136 huku Zimbabwe ikiwa nafasi ya 150.
Zimbabwe ni nchi yenye kiwango kikubwa zaidi cha rushwa lakini watu wengi walikuwa hawajui mpaka Rais Mugabe alipoamua kutania Wenzake............
Tags
Hadithi Za Kweli