VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS)
.
Ni vidonda vilivyo wazi ambavyo hutokea katika kuta za tumbo,sehemu ya juu ya utumbo mdogo au kwenye kuta za koromeo kutokana na bacteria waitwao H.pylori na asidi inayozalishwa kwenye kuta za tumbo
Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine kama kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito. Nk
.
.
AINA YA VIDONDA VYA TUMBO
Kuna aina tatu ya vidonda vya tumbo
1.GASTRIC ULCERS
Hivi ni vidonda ambavyo hutokea ndani ya tumbo,kwenye kuta za tumbo
2.ESOPHAGEAL ULCERS
Hivi ni vidonda ambavyo hutokea ndani ya koo la chakula,kwenye kuta za koo la chakula
3.DUODENAL ULCERS
Ni vidonda ambavyo katika sehemu ya juu ya utumbo mdogo uitwao duodenum
.
.
CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ila vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;
1.Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
2.Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin(bayer), (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
3.Msongo mawazo (stress)
4.Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
5.Kunywa pombe na vinywaji vikali kupitiliza.
6.Kuto kula mlo kwa mpangilio maalumu
7.Uvutaji wa sigara.
8.Kansa ya tumbo
.
.
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na kuendelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vina dalili kama;
1.Kupata maumivu ya tumbo ya kuwaka moto (kuunguza) baada na kabla ya kula
2.Kupatwa na kiungulia(heartburn) karibu na chembe ya moyo
3.Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa
4.Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu
5.Kupata haja kubwa ya rangi ya kahawia au nyeusi chenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu
6.Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
7.Kushindwa kupumua vizuri
.
.
JINSI YA KUEPUKANA NA VIDONDA VYA TUMBO
1.Kunywa maji mengi
2.Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakupunguza na mawazo
3.Punguza (balance) kiwango cha lehemu (choresterol) mwilini
4.Usivute sigara
5.Punguza au acha kunywa pombe
6.Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
7.Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9
Tatizo la Vidonda vya tumbo linatibika kufuatana na mda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakidharau dalili za vidonda vya tumbo na kudhani kuwa hakuna madhara makubwa.
MATIBABU:
Kwa matatizo ya vidonda vya tumbo,watu wengi wamekuwa hakihangaika sana kupata matibabu sahihi na badala yake wamekuwa wakitumia dawa za kutuliza matatizo ya vidonda vya tumbo na si kutibu tatizo moja kwa moja.
Zipo tiba nzuri kabisa ambazo hutibu matatizo ya vidonda vya tumbo kwa haraka sana na tiba ya kudumu
Endapo wewe ni muhanga wa tatizo hili la vidonda vya tumbo basi wasiliana na mtoa huduma wetu ili aweze kukutia tiba nzuri ya vidonda vya tumbo. Piga simu au tuachie ujumbe mfupi Sasa hivi
Simu/whatsapp: +255716778844
Tags
AFYA