SIMULIZI: BINTI MSAHAULIFU. SEHEMU: 04
ILIPOISHIA.......
"Tuondoke hapa!! Tupo hatarini sana, tutaenda kuongea mbele ya Safari!!"
Aniseth alisimama kwa unyonge sana, walielekea kwenye gari huku kila mtu akiwa haamini kitu kilichotokea.
ENDELEA NAYO....
Ilikuwa ni mwaka mmoja baada ya kutokea tukio la Ndalu kupoteza maisha. Leo Katika Gereza kuu la Tanzania kulionekana baadhi ya wafungwa walikuwa wakiachiliwa kuwa huru tena.
Kuna mfugwa mmoja baada ya kuwa huru alionekana akilia sana mpaka baadhi ya washikaji wake walimwendea huku wakimuuliza.
"Oyoo!!! Mbona una umama mwingi sana au hukutaka kuwa huru!!? Shauri yako watakurudisha tena usote Ndani."
Mfugwa huyo alinyanyua kichwa chake huku akitaka kumjibu.
"Ni kheri Wewe!! Unatoka huku ukipokelewa na ndugu zako tena kwa usafiri private!! Je, mimi? Ni Nani anayeweza kuniona wa thamani Sana katika Dunia hi!! Sikufanya Tukio kwa kukusudia ila ilinilazimu iwe hivyo!!"
Jamaa aliamua kumpotezea maana kila mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake, Ilibidi ampigepige bega kama kumtia nguvu kisha alimwachia maneno kadhaa.
"Kosa sio kosa ila kosa ni kurudia kosa!! Wewe kapambane kutafuta maisha, hakikisha taswira iliyopo katika jamiii unaibadilisha upya na iwe Kama ya Mwanzo."
Katika wafungwa hao hao alionekana kijana mmoja aliekuwa kapanda hewani, yeye muda wote alikuwa ni mtu wakutafuna big G huku akiambatanisha masihara mengi, pia alikuwa ni mtu wakucheka na wenzake muda wote.
Mkuu wa Gereza pamoja na wafanyakazi wenzake, walimuita kisha alimpatia mkono huku akimtakia kila la kheri kwenye maisha mapya ya kijamii tena!! Alimuita Mara mbilimbili.
"Albert!! Albert!! Ni wakati wako mpya wakwenda kuanza maisha upya tena!! Ila uwe unakuja kutusalimia angalau Mara moja moja uwepo wako tunajivunia!! Ulikuwa Ni mtu mzuri Sana!!"
Albert aliishia kutabasamu kama kawaida yake huku akiendelea kutafuna big g!!
"Kila Weekend nitakuwa nakuja kuwasalimia jamaa zangu!! Ila na nyie mpunguze kutupiga na hivyo virungu!!"
Walicheka wote kwa furaha huku wakimsindikiza kwa macho, huku kila mtu akitathimini yaliyo ya Moyoni kwakee..
"Ni kijana mzuri sana.. sizani kama hata hilo kosa alifanya ila alikubali kutumikia kifungo bila ridhaa yake!!" Ni baadhi ya maneno ya mkuu wa Gereza aliyatafakari.
Huku Getini Albert alikuwa akiwasalimia wenzake huku akijaribu kuwaaga, baadae alitoka hadi getini kisha Alisimama na kusoma maneno yalioandikwa pale " GEREZA KUU LA WAFUNGWA" Huku akiyarudia maneno yale yale mara mbili.
Wakati yupo pale alishtushwa na sauti ikimuita,, Ilibidi ageuke kumtizama!! Alikuwa ni Askari alikuwa ni rafiki yake wa karibu sana, alifika pale nakumpatia kimfuko kidogo Kisha alimwambia.
"Ondoka mazingira haya!! Unaweza kukamatwa tena!! Nimekupatia kiasi kidogo cha fedha kitakachokusaidia hapo baadae..!!"
Albert alichukua usafiri wa hiace maana Gereza lilikuwa mbali kidogo na mji, alipita mjini kununua nguo kwa baadhi ya zile pesa alizopewa kisha alichukua Hotel moja kupumzika siku hiyo. Huku akitafakari mambo mia kwa sekunde moja.
"Kuna wakati unatamani kufanya kitu ila nafsi inakuuma tenaa.. Lakini sikutumikia kifungo bure pasipo kuwa na kosa lazima nitalipa hata muda niliopoteza haijalishi ni sekunde lazima watalipa!!"
Alijaribu kutafuta usingizi japo aliupata kwa shida sana, aliamka na kwenda kwenye maduka ya simu kisha alinunua kisimu kidogo na kwenda kusajili line, alirudi kwenye Hotel aliyofikia kisha alichukua simu yake huku akijaribu kuingiza namba za simu baadhi lakini kila akijaribu kupiga aliambiwa namba imefungiwa mwishoe alikata tamaa kabisa!! Aliweka simu pembeni kisha alivuta shuka kutafuta usingizi mpaka kukapambazuka.
Asubuhi kulikucha Albert alielekea kwenye Makampuni kutafuta kazi angalau apate pesa kidogo ya kukimu mahitaji yake ya kila siku, alifika kwenye kampuni moja kuomba kazi lakini aliambiwa hawahitaji wafanyakazi kwasasa nafasi zimejaa.
Ilibidi aendelee huku na kule kutafuta kazi lakini ilikuwa changamoto siku hiyo hakufanikiwa, aliamua kurudi Hotel aliyofikia, aliangalia kiasi cha pesa kilichobakia ilikuwa ni laki mbili TU, inamaana tayari kashatumia laki mbili, kula na kununua Mavazi. Alikaa Chini huku akitafakari jinsi ya kuibajet hiyo hella Ilibidi ahame kwenye hio hotel akatafute angalau chumba Cha kuishi, Alipata chumba kwa mwezi alilipia elfu kumi na tano, ikabidi alipie miezi mitatu, kiasi kingine akanunua vyombo na Chakula!!
Maisha yaliendelea takribani ya Mwezi mmoja alikuwa tayari kapata kazi ya kuosha magari!! Siku hiyo kuna mkuu wa Gereza alikuwa akipita pita mitaa ile kwa mbali kidogo alimuona Albert ilibidi asimamishe gari yake baadae alimuita akawa amempatia business card, Huku akimsisitiza asiache kumtafuta.
Baada ya mapambano kuisha jioni Albert alikuwa Nyumbani kwake, Aliangalia kapu la unga ndipo anagundua unga umebaki kama robo, mchele nao vilevile ndipo anakumbuka ile Namba aliyopatiwa na mkuu wake wa kazi Ilibidi ampigie.
"Hallow! Mkuu Ni Mimi Albert.."
"Ooh!! Umenitafuta muda mwafaka kabisa!! Uko wapi siku hizi!! Na unaishi wapi kwasasa!! Nipe direction Kuna watu nawaagiza wafike hapo."
Albert alifanya kumuelekeza kisha alikata simu akawa amejilaza kwenye kigodoro chake!! Kama robo saa alisikia honi za gari zikiwa sambamba kwenye nyumba anayoishi. Jirani yake alikuja kumuamsha.
"Oyoo!! Unalala Sana!! Naona leo umeondoka na spea za gari wenye nazo wameijia!! Wapelekea basii.."
Albert alimpuuzia maana alimchukulia jamaa msumbufu Sana kwakee, aliendelea kuuchapa lakini alisitushwa na Sauti ikimuita.
"Oyoo!! Albert... Amka bhana unalalaje Huku hujala?"
Albert Alifungua Macho nakubaki akiduwaa kumbe Ni jamaa yake wa karibu sana muda mwingi alikuwa akimsaidia pindi yupo Magereza.
"Haaaa!! Ni Wewe kumbe! Mwanzoni nilipuuzia Nina jamaa angu hapa jirani huwa Ni msumbufu Sana!!"
"Achana nae!! Hii Ni Amri kutoka kwa Mkuu wetu!! Amekuhitaji ukakae kwake!! Chukua kilicho Cha muhimu vingine utaachia majirani zako!! Halafu mbona hukunitafuta mapema mpaka ukaanza pitia hizi Shida!!"
"Aaa!! Mwanaume hupambana kwa upande wake!! Nilijaribu kujiunga na wenzangu ili siku moja nifikie malengo!!"
"Umekula Lakini..!!?"
"Nimekula mchana!!!"
"Okay!! Twende kwanza utaenda kuongea Nyumbani ukifika!!!
Waliongozana Hadi kwa Mkuu wao wa kazi, Walifika na kupokelewa na mkewe pamoja na Binti mmoja walikuwa pale, Muda kidogo Mkuu wa Gereza Alifika akawa amekaa na familia yake kuwatambulisha.
"Albert hii Ndio familia yangu!! Nina mke mmoja!! Watoto watatu kwasasa wapo kazini kwao, Mtoto wangu wa Mwisho Ndio Binti yangu anaitwa Betrida!! Au kifupi muite Betty!! Pia Kuna Dada yenu Mkubwa yeye yupo Jikoni anaandaa andaa!!"
Betty Alidakia kumuuliza Baba yake.
"Kwahiyo huyu Ni Kaka Albert!! Si tutakaa nae siku zote ee!!?"
Mama Aliishia kutabasamu tu, Kisha Alimvuta masikio.
"Maswali mengi Sana Binti yangu!! Wewe Nenda Jikoni umsaidie Dada kuandaa Chakula!!. Mgeni wetu karibu Sana ujisikie Nyumbani!! Pole kwa matatizo yaliyokupata ila Baba kaniambia mapema!! Kwahiyo jisikie Amani muda wote!!"
Ilikuwa Ni wiki moja tangu Albert afike pale, Alikuwa tayari ameizoea familia ile hasa ukilinganisha na yeye alivyomcheshi walitokea kuzidi kumuamini sana.
Siku hiyo Mkuu wa Gereza Alikuwa na kampuni ya studio kubwa, iliyokuwa ikimuingizia pesa kwa waimbaji na waigizaji wengi walikuwa wakiitumia Studio yake kufanyia kazi zao, Ilibidi amuingize Albert Baada ya kumuona Ni mtaalamu Sana wa mambo ya Mtandao ili azidi kuboresha kampuni yake.
Siku hiyo Alifika kumtambulisha Kama miongoni mwa wafanyakazi wapya watakaokuwa wakisimamia upande wa kurecord!! Nakupiga picha pamoja na kuedit CD, video kwa ueledi Zaidi.
Watumishi walimpokea vizuri kulingana na yeye alivyokuwa mcheshi kazi zilizidi kuimarika na kuchukua umaarufu mkubwa katika jiji Hilo.
Siku zilizidi kusonga mbele, leo Albert aliamua kumuomba Boss wake achukue likizo akaione familia yake, Boss Hakuwa mgumu alimpatia likizo, lakini kwa Upande wa Betty nae aling'ang'ania kuondoka na Albert mpaka Babake akawa mkali.
Albert Ilibidi aongee vizuri na Boss wake ambae kwa muda huo alikuwa akimuita Baba yake Kama mlezi.
"Baba Achana nae Mimi nitaongea nae vizuri atanielewa tu."
Baada ya maongezi Albert aliamua kumfuata Betty chumbani kwake, muda huo alikuwa akilia huku kajifungia mlango, walisaidiana na mama yake lakini Betty aligoma kufungua. Albert Ilibidi amruhusu mama yake akapumzike yeye atalishughulikia.
Ilibidi ammbeleze kwanza baadae aliweza kufungua.
"Kwanini Unalia hivyoo!! Mimi nitakuombea ruhusa kwa baba lazima niondoke na Wewe!! Unajua Mdogo wangu nimekuzoea Sana kwahiyo nahitaji kampani yako na Mimi nisiwe mpweke!! Sawaa Betty!!"
Baadae alifanikiwa kumtuliza wakawa wameondoka nae siku hiyo aliamua kumpeleka Out wakareflesh mind.
"Lakini Kaka!! Mimi nitakuwa mpweke Sana!! Ujue nimekuzoea."
"Usijali sikawii kurudi!! Wiki moja TU nitakuwa Hapa unajua kazi italala kwenye kampuni ya Baba!!"
"Uwahi bhana!! Ukichelewa nakuwa siendi Chuo!!"
Albert alibaki akimtizama Betty mpaka alianza kujua, tayari kameshampenda Ndio maana kanamkatalia abaki.
"Okay!! Twende Nyumbani muda umeenda!!!"
"Kakaa!! Halafu Nina Swali!! Wewe huwa una Girlfriend!!?"
"Mhuu!! Kwanini umeniuliza hivyoo!!''
"Sijawahi kukuona una Ukaribu Sana na wasichana!! Huwa naona mnapiga story tu!!"
"Betty mchunguzi Kweli!! Kuna Siku utaona tu, Wewe endelea kuchunguza.."
"Kwahiyo kumbe unaye!!?"
Albert Aliishia kucheka Kisha Alimvuta masikio.
"Kula Haraka twende!! Laah! hivyo nitamwambia mhudumu akufungashie!!"
°°°°°°°°°°°°°°°°
Huku Upande wa Tinnah kwa muda wa mwaka mmoja aliajiriwa kwenye kitengo kilichokuwa kinahusika na haki za Watoto alikuwa akifanya biashara. Siku hiyo aliamua kujipumnzisha nje ya kampuni Yao kulikuwa Kuna mdada mmoja anauza soft drinks.
Wakati akiwa amekaa pale alimuona kuna kijana alishuka pale akawa ameingia Dukani baadae aliagiza juice ya parachichi akawa ametulia kwenye meza Huku akiendelea kunywa juice. Tinnah alibaki akimtizama mkaka yule baadae aliamua kumfuata Kisha alimwandikia maandishi Huku akimuuliza.
"Aniseth!! Inamaana hujaniona!' Ndivyo unavyokuwaga Busy ukiwa mtaani!!?"
Kijana Yule Alishtuka baada ya kusikia jina la Aniseth make yeye alikuwa ni Albert ilibidi amgeukie kisha alitoa Prova yake iliyokuwa imeungana na kofia iliweza kuficha sura yake.
"Unaongea na Mimi au !!?"
Tinnah ilibidi asogeze kiti chake kisha alifanya kumfinya kwenye mkono wake aliokuwa kashikilia Glass, kutokana na ucheshi wa Albert ilibidi abaki akimtizama kisha aliachia tabasamu!!
"Kweli wewe wanifananisha, Mimi sio Aniseth unaemtaka Wewe!! Japo niliwahi kuwa na rafiki yangu Aniseth ila alitangulia mbele za haki, so umenifananisha."
"Hapana mbona unakuwa na masihara hivyo!! Uachage hiyo tabia utanifanya nikuchukie ee!! Ila leo umekuwa mcheshi Sana!!!" Alimaliza kuandika na kumpatia.
Albert aliona Tinnah anazidi kumzingua ilibidi amalizie kunywa juice yake kisha alisimama ili aondoke huku akimuacha Tinnah anabaki kumshangaa, baadae alirudi Hadi kwenye ile meza alifika akamuinamia kisha alimnong'oneza sikioni.
"Hata Wewe Umefanana na mtu muhimu kwangu!! Japo hayupo tenaa!!"
Kisha aliondoka, Muda huo Tinnah Ilibidi asimame Nakuanza kumfuata kinyume nyume.
Albert aligundua kabisa kuna mtu anamfatilia ilibidi akae chemba huku akimsubiri apite.
Tinnah Alimpoteza Ghafla Albert Ilibidi aanze kumtizama Huku na kule baadae alishikwa mkono akawa amevutwa chemba na Albert kisha alimuziba mdomo. Muda huo Tinnah alibaki akimtizama Albert machoni kuna kama kumbukumbu alianza kukumbuka.
Albert baadae Alimuachia kisha alimsihi awe makini baadae alimuuliza tena.
"Kwani Nyumbani kwenu wapi halafu mbona unapenda mambo ya kitoto kitoto huwezi ukaongea mpaka uniandikie!? Halafu usinifatilie Mimi pita na njia yako sawa mtoto mzuri!!"
... Itaendeleaa.....
Tags
simulizi