SARAFINA 1
Sarafina ni binti wa miaka 22 ametoka kwenye familia inayojiweza baba yake mzee kijazi alikuwa Ni mtu mwenyewe uwezo kifedha alimiliki biashara kubwakubwa alimpenda Sana binti yake alimpa maisha Bora pamoja na elimu.siku moja mzee kijazi alimwambia mwanae
" Sarafina mwanangu hivi unajua unakaka yako kwa mama mwingine?
Sarafina alifurahi maana alitamanikuwa na ndugu
Wa kuzaliwa nae
" Baba mbona hukuniambia mapema Kama Nina Kaka na Yuko wapi?
" Yupo hapahapa mjini Ila siku sio nyingi nitawakutanisha .
" Nitafurahi Sana nilikutana nae anaitwa Nani?
" Anaitwa Roman. Ni kijana mmoja Safi Sana Ni mchangamfu na mwenye upendo. Baada ya siku mbili kupita mzee kijazi alimkutanisha Roman na sarafina . Wawili Hawa walifurahi kukutana mzee kijazi aliwasisitiza upendo na kusaidiana kwani wao Ni ndugu wa damu moja na wapo wawili tu . Kila mmoja aliahidi kumpenda mwenzie .
Roman alikuwa anashirikiana na baba yake kwenye biashara zake. Siku moja sarafina alimuuliza mama yake
" Mama kwani mama yake na Kaka Roman Yuko wapi?
" Mwanangu maswali Kama hayo unatakiwa umuulize huyo baba yako au Roman mwenyewe maana Mimi Sina ninalilijua.
" Mimi nilijua wewe utakuwa unajua kwani baba ana wake wawili?
" Jamani Sara hayo maswali Mimi siwezi kukujibu kaa na baba yako ndio umuulize atakupa majibu. Kwakuwa sarafina alikuwa na hamu ya kujua alimsubiri baba yake alipokuja alimuuliza
" Baba napenda kujua kwa undani maisha ya kaja Romani pia kuhusu mama yake alipo na pia ingekuwa sio vibaya ningejua una wake wawili. Mzee kijazi alicheka
" Sara mwanangu umeniuliza maswali mengi kwa wakati mmoja Ila nitakueleza kila kitu.
" Roman anaishi na mama yake kuhusu kuwa na wake wawili hapana MKE wangu ni mmoja tu ambae ni mama yako kuhusu mama Romani nilikuwa nae kabla ya kuwa na mama yako. Sarafina alitabasamu
" Nimeshakuelewa.
Ilipita miezi miwili mzee kijazi aliugua ghafla akiwa kazini na kukimbizana hospital lakini alipokuwa njiani alipoteza maisha. Ilikuwa ni pigo kwa familia yake sarafina alilia Sana kwasababu baba yake ndiye alikuwa rafiki. Mwili wa mzee kijazi ulipofanyiwa uchunguzi ilionekana alilishwa sumu na ndio iliyommaliza. Waliandaa msiba taratibu za mazishi zilifanyika baada ya hapo ndugu walikaa kikao na kutaka kupanga miradhi ndugu wa mzee kijazi walijimilikisha baadhi ya Mali na nyingine wakawaacha watoto
Mama sarafina hakukubali
" Shemeji hicho mnachokifanya sio sawa hizo Mali nilichuma Mimi na mume wangu nilipika maandazi na kutembea mitaani Leo hii mnataka kunishutumu sitakubali.
" Wewe mwanamke unamdomo Sana hizi Mali ni za ndugu yetu unataka kutuambia hizi Mali zimepatikana kwa kuuza maandazi
" Lakini tambueni wakati naanza maisha na ndugu yenu hatukuwaa na maisha kula yenyewe ilikuwa ya tabu nilihangaika na mwanangu mgongoni kwenda kufua kwenye majumba ya watu ili tupate hela yakula leo. Tuondoles ngonjera zako utakaa hapa kwenye hii nyumba kuhusu hela ya kidume huyo hapo Roman atakuwa anawapa akiokoteza huko kazini kwake. Mama sarafina hakutaka kuendelea kuwasikiliza
" Sina muda wakupoteza nitaenda mbele kutetea haki yangu. Alinyanyuka na kuingia ndani sarafina alinyanyuka na kumfuata mama yake.
Miezi ilikatika Hali ilikuwa ngumu nyumbani kwakina sarafina . Sarafina akaamua kumfuata Romani ofisini kwake.
" Kaka Roman nimekuja kuchukua pesa nyumbani hakuna kitu.
" Hivi nyie mmekaa tu huko mnategemea Mimi niwapatie pesa unatakiwa utafute pesa ili umsaidie mama yako.
" Basi naomba uniwezeshe au tuje tufanye kazi hapa.
" Kwa hapa hakitawezekana kwanza utafanya kazi gani?
" Lakini baba mkubwa alisema hii ni kampuni yetu wote.
" Sikiliza nikwambie baba mkubwa amemchukua Mali nyingi za marehemu mzee nenda kaongee nae hapa wewe huna urithi wako hapa nitamiliki Mimi kidume kwanza kwa ushauri ungeenda kutafuta bwana uolewe. Sarafina alipoona kashfa zimezidi aliamua kuondoka.
Siku moja wakiwa nyumbani kwao hawana hili Wala lile alikuja Roman na watu wengine na kuanza kuwazungusha
" Unaona nyumba ulivyokuwa nzuri Haina shida yoyote .
" Ni kweli ni nzuri Sana Sasa haipungui hata kidogo?
" Hapana boss wangu fanya Kama tulivyoongea.
' sawa Basi twende tukamalizane alafu vipi kuhusu Hawa wapangaji
" Hawa usijali wataondoka .
" Sawa . Wale watu na Roman wakawa wanaondoka sarafina akamuita Romani
" Romani unataka kuuza nyumba yetu?
" Ndio baba mkubwa kanotuma niiuze kwahiyo mjiandae muondoke
"Sasa tutaenda wapi?
" Hilo halinihusu mtajua wenyewe huyu jamaa akishalipa pesa anakuja kuwatoa.
" Sasa unafikiri sisi tutaenda wapi
" Mimi sijui na Wala halinihusu kwanza unanichelewesha acha niende nikachukue pesa. Roman aliondoka na kuwafuata wale watu sarafina alirudi kwa mama yake akamkuta mama yake kajiinamia huku machozi yakimtoka
" Mama acha kulia
" Acha nilie mwanangu nahisi dunia yote imeniinamia kweli Mimi ni wakudhurumiwa Mali zangu nilizochuma na mume wangu kwa tabu jua liliniwakia na mvua ilininyeshea. Sarafina alifikiria kitu Kisha akamuuliza
" Mama kwani hati ya nyumba iko wapi?
" Zilikuwa chumbani kwenye droo. Sarafina alinyanyuka na kuelekea chumbani kwa mama yake mama yake alimfuata wakaanza kupekua
" Unamtafuta Nini?
" Nataka hiyo hati ya nyumba .
" Ilikuwa hapa . Mama sarafina alifungua droo nakuanza kunitafuta lakini hakuiona
" Sarafina haipo itakuwa wameshachukua lakini wamechukua lini? Sarafina alichoka na kukaa kitandani
" Hapa hatuna ujanja inabidi tuondoke nilijua wanataka kutumia ujanja hawana hati. Walikaa kimnya kwa muda huku akitafakari wataenda kuishi wapi na wataendeshaje maisha yao
Tags
simulizi