TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

HUWEZI KUJITAMBUA KAMA HUJAJIFAHAMU KIUNDANI KATIKA MAENEO HAYA MATATU

Huwezi Kujitambua Kama Hautajifahamu Kiundani Katika Maeneo Haya Matatu... 
_______________________
Huwa inashangaza sana pale unapomkuta mtu anampambanua mtu mwingine vizuri sana, kuliko hata yeye mwenyewe anavyoweza kujipambanua! 

Kwa kweli huwa inanisikitisha sana! Huwa inaniuma sana mpaka ndani ya moyo wangu!

Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba huwezi ukajifanyia yaliyo ya kikuu endapo hutoweza kujijua vizuri wewe ni nani!

Kitu cha kwanza unachopaswa kujua ni kwamba, kila binadamu maisha yako hapa duniani yanathaminishwa kupitia sehemu hizi kuu tatu..

Vilevile unatakiwa ufahamu kwamba, ni kosa kubwa sana kwako kutokuzifahamu hizi za kujifahamu kiundani, kwani ndizo zinazotawala pamoja na kuongoza maisha yako...

Mbali na hilo ninawiwa kukufahamisha kwamba, sehemu hizi ndizo hutawala namna unavyofikiria, unavyohisi pamoja na namna unavyofanya matendo mbalimbali...

Kwa ujumla ni muhimu ukaweka akilini mwako kwamba, sehemu hizi ndizo zinatawala kila kinachotokea maishani mwako...

Mpenzi msomaji, unatakiwa kujua kwamba, huwezi ukajitambua wewe ni nani endapo hutajifahamu kiundani katika sehemu hizi kuu tatu za kujifahamu kiundani:

1.  Ufahamu Wa Kujipambanua..
____________________________

Idadi kubwa ya watu hawawezi kujipambanua kuwa wao ni akina nani! 

Hali hii imewafanya watu wengi washindwe kujiua wao ni akina nani na waliumbwa kuja kufanya nini hapa duniani!

Cha kuchukua hapa ni kwamba, eneo hili la kujifahamu kiundani linahusu ule uwezo wako wa KUJIPAMBANUA kuwa, wewe ni nani, umebeba mawazo gani, umebeba kusudi gani, una matamanio gani, malengo yako ni yapi, ndoto zako ni zipi pamoja na yule mtu unayetaka uje uwe hapo baadae...

Mpenzi msomaji huna budi kujipa tathmini juu ya suala hili.
Je, unajifahamu vizuri kwamba wewe ni nani, umebeba maono gani? umebeba kusudi gani?
Na unaweza ukafanya nini?

Unatakiwa kujua kwamba endapo utakosa ufahamu wa KUJIPAMBANUA, huwezi ukapiga hatua kubwa maishani mwako..

Watu wengi hawajui wao ni nani na hawawezi kabisa hata siku moja kujielezea kuwa wanaishi ili wakamilishe nini hapa duniani...

Hali hii imewafanya wabaki kuwa watu wa kawaida tu kwa vile hawana malengo, maono pamoja na natamanio makubwa maishani mwao!
Kutokana na suala hili hata kiwango chao cha kujitambua kinabaki kuwa duni!

Je wewe ukiulizwa unaweza ukajipambanuaje kwa watu?

Unapaswa ujitafute ili ujue unaweza ukajielezeaje kwa watu!

Unatakiwa ujipambanue kwa watu wewe ni nani!

2. Jinsi Unavyojiona...
______________________
Sehemu hii huhusu picha mbalimbali ulizozotengeneza akilini mwako kuhusu wewe Pamoja na vile Unavyojiona!

Kadhalika sehemu hii huhusu ule ufahamu wa jinsi Unavyojiona ndani mwako kuanzia: Nguvu zako, uwezo wako, ukuu wako, pamoja na thamani yako..

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba watu wengi wanajiona wao ni wadhaifu, hawastahili na hawawezi kufanya jambo lolote lile la maana maishani mwao...

Hali hii inawafanya wadidimize kabisa kiwango chao cha kujitambua...

Kama wewe utakuwa ni msomaji mzuri wa Biblia, ni matumaini yangu ushawahi kuusoma mstari huu "kama ajionavyo nafsini ndivyo alivyo"..

Kinachomaanishwa hapa ni kwamba, ukijona kuwa huwezi hutaweza Kweli kwani umejiona hivyo...

Kitu kingine unachopaswa kujua ni kwamba huwezi ukaenda mbali zaidi ya pale ulipoishia kujiona...

Hii inamaanisha kwamba kama umejiona wewe ni maskini huwezi ukaufikia utajiri..

Kama umeona wewe huwezi kufanikiwa hutoweza kufanikiwa...

Kitu kimoja cha msingi sana unachopaswa kujifunza hapa ni kwamba, vile unavyojiona ndani yako ndivyo utakavyoonesha mwitikio wako kwa nje..

Na hapa ndipo kanuni ya uakisi wa mambo huthibitika...
Kanuni hii inasema kwamba "ulimwengu wako wa nje utaakisi ulimwengu wako wa ndani"

Mantiki yake ni nini Sasa? Hii inamaanisha kwamba kile kilichoonwa ndani ndicho kitathibitika njee..
Je unajionaje ndani yako my friend?

Kumbuka huwezi ukaenda mbali zaidi ya pale ulipoishia kujiona..

Kitu unachopaswa kufanya kuanzia saa hii anza kujiona wewe kwa viwango vingine kabisa!
And i strongly believe that I'll See you at the top!

3. Jinsi  Unavyojithamini...
_____________________
Sehemu hii huhusu thamani uliyoiweka maishani mwako! Yaani ni kwa Kiasi gani unavyojipenda, unavyothamini utu wako pamoja na unavyojiwazi mema!

Kwa maneno mengine naweza kusema kwamba, kujifahamu katika eneo hili kunahusu thamani kubwa uliyoiweka kuhusu wewe na maisha yako...

Kwa mantiki hiyo kadri unavyozidi kujiwazia mema, kujipenda pamoja kujithamini ndivyo unavyozidi kujifanyia ya kikuu, na kadri unavyojifanyia yaliyo ya kikuu ndivyo unavyojitengeneza kuwa Bora...

Kadri unavyojitengeneza kuwa bora ndivyo unavyoongeza kiwango chako cha kujitambua! 

Je ni kweli unajipenda?
Na Kama unajipenda kwanini huwa unajiwazia mabaya?

Kwanini huwa unasema Maisha yenyewe ni mafupi?

Kwanini huwa unajisemea kuwa maisha yako hayana maana?

Kwanini huwa unajiona hufai? 

Anyway unatakiwa uanze kujipenda kuanzia saa hii! 

Jipende sana bosi Wangu kwani umebeba thamani kubwa sana ndani yako...

Unachopaswa kujua ni kwamba hakuna atakayekupenda zaidi ya Wewe mwenyewe unavyojipenda...

Hebu jipende ili upate kutimiza wajibu kuhusu maisha yako aise..

Hivyo ndivyo unapaswa ujifahamu kiundani!

Endapo utajifahamu katika maeneo hayo matatu, ni matumaini yangu utakuwa umepiga hatua fulani kimaisha!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; mwalimu, mwandishi muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi life coach and consultant!

Unaweza ukawasiliana na Mimi kupitia Whatsapp no +255744284329

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post