TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

MISS TRINNIE 02

MISS TRINNIE 
SEHEMU YA PILI
Mwandishi - Queen Lizzie 
__________________________________
Nilijikaza hatua mdogo mdogo nilizihesabu mpaka nje, upande wangu wa kulia hatua kama ishirini hivi nililiona gari moja kali Prado.
Haraka niliifata. 
"Mambo mamy 😁"
Nilimsalimia Sophia baada ya kuingia ndani ya gari huku nikijichekesha chekesha lakini Sophia hakunichekea 🙈 na wala hakuonesha uso wa kutaka ujamaa na mimi. 😎
Alikuwa mwanamke mmoja mweusi, uso wake ulikuwa mkavu na si wakuvutia na aliyaficha macho yake kwa miwani meusi, 
"Umenichelewesha sana"😎
"Ooh sorry mamy..nilikuwa na..na...🙆‍♀️"
"Hold on girl, no need to explain (tulia binti, hakuna haja ya kujielezea) kaa unisikilize😎"
Sofia alisema kwa sauti kavu, ilinibidi niwe mpole huku moyoni nikimlaani maana alikuwa akionesha dharau ambazo kama sio hiyo milioni kumi yake basi ningekuwa tayari nishamtukana🤦‍♀️ ila kwakuwa bosi anuniwi nilitulia huku nikiweweseka. 
"Hii kazi unayoenda kuifanya kuna wasichana zaidi ya mia nane ambao wangeweza kuifanya hata kwa nusu ya gharama niliyokupa wewe...niambie utaweza kazi?" 
"Eeeh...nitaweza"
"Hahaha binti nauliza tena utaweza kazi ?😎"
"Ndio nitaweza "
Nilimjibu kwa kujiamini. 
"Ok..."
Yule mwanamke alisema kisha akageuka upande wa pili, aliokota bahasha kubwa akanikabidhi.
"Hiyo simu yako imekaa kimasikini sana sidhani kama itafaa."
Yule mwanamke alisema huku akiniangalia kwa mtindo wa kuninyali, yaani kunipandisha na kunishusha kisha akaendelea.
"Hata hayo mavazi yako pia...kama ndio aina ya mavazi uliyo nayo hayatofaa pia..hayana mvuto.😎"
Yule mwanamke aliniambia , daah 🤦‍♀️
Niliitazama suruali yangu ya jinsi niliyoinunua shilingi 25000 pale kariakoo pamoja naTshirt yangu ya kisasa ambayo niliinunua shilingi 20000 nilijikuta naishiwa nguvu 😭😭
Na yote tisa kumi hata ile simu yangu Samsung J7 nayo niliambiwa ni ya kimasikini na haitofaa kwenye kazi, nguvu ziliniisha lakini nilipiga moyo konde maana wahenga wanasema "mtumikie kafiri ili upate unachotaka" nilipoa.
Niliifungua ile bahasha ya kaki aliyonipa , woow 😳😘🥱
Nilikutana na 'Iphone 13' mpyaaa , nikafukua fukua nikakutana tena na    noti nyekundu nyekundu nyingiii ambazo kiidadi kwa haraka haraka sikujua ni ngapi ila zilikuwa nyingi, nilijikuta natabamu kama chizi kaona jalala jipya , yale matusi yake yote niliyasahau 😁😆
Halafu mwisho kabisa nilikuta picha moja kubwa , ya mwanaume mmoja hivi handsome wa maana 😍😘, mrefu kavaa suti nyeusi , mwanaume yule kiumri alikuwa anacheza kwenye miaka ishirini na tano mpaka ishirini na saba😘🥰.
"Huyo ndiye mume wangu mwenyewe..."
Sophia alisema.
Maneno ya sofia yalinifanya niitazame ile picha kwa mara nyingine tena. na mwisho nikajikuta nabaki mdomo wazi, maana Sophia kimuonekano alikuwa kama si miaka thelathini na nane , tisa basi miaka 40. Huyo mwanaume anayesema ni mumewe kwake alikuwa mdogo sanaaa kitu ambacho kidogo ni tofauti kwa mila na tamaduni zetu za kiafrika 😳😳.
"Hiyo simu ndio ambayo utakayoitumia kwenye kazi yako, ni namba yangu tuu ndiyo ambayo utaisevu humo na kama itatokea namba nyingine basi iwe ya mume wangu, kwanzia sasa utatumia majina bandia, pia hata sehemu unayotokea itakuwa bandia..yaani kila kitu kuhusu wewe kitakuwa bandia, pia unahitajika kuwa na mavazi mazuri ya gharama sio kwa hivyo vituko vyako 😏"
Yule mwanamke aliita pamba zangu za kutokea "vituko" 😫
"Sawa mama..😁"
Niliitikia huju nikitabasamu kama si huyo anayetukanwa 🤦‍♀️
"Malipo ni baada ya kazi ila gharama zote kipindi ukiwa unaifanya kazi hii nitazisimamia mimi, kwanzia makazi, chakula, usafiri na kila kitu, ila ukiifanya hii kazi kinyume na ninavyotaka hizi gharama zote utazitapika ukiwa umesimama wimaa 😬"
Yule mwanamke alisema huku akiipiga piga mikono yake, niliogopa.
"Aaah usi..usi..usijali mama"
"Ok shuka...baadae nitakupigia tutaongea"
Yule mwanamke alisema kisha akageukia upande wa pili kuashiria kwamba hataki tena kuendeleza stori na mimi. 
Nilishuka kwenye gari yake huku mkononi nikiwa na ile bahasha ambayo ilikuwa na picha ya mumewe, pesa, na simu 🤦‍♀️
Walau sasa nilikuwa nimechangamka maana nilipata neema nisiyoitarajia. 
Lakini yote tisa bado kichwani nilikuwa na maswali ambayo yalikosa majibu 🤦‍♀️
"Kwanini amlipe mtu ili achepuke na mumewe, yaani wakati watu wanaua na kujenga uhasama na michepuko ya waume zao yeye alitoa pesa na kumlipa mchepuko wa mumewe why...?"
Nilitamani kumuuliza swali hili lakini nilikosa hata pa kuanzia, pia nilijaribu kumuuliza rafiki yangu, Irene ambaye ndiye aliyeniunganisha na mwanamke huyo lakini hata naye majibu yake hayakuwa ya kuridhisha. Kiufupi alikuwa hajui, ni wazi mwanamke huyu alifanya siri hakutaka watu wajue kwanini anamfanyia yale mumewe.. 

ITAENDELEA.......

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post