MISS TRINNIE 😘
SEHEMU YA KWANZA
Mwandishi - Queen Lizzie
_______________________________________
Ilikuwa kama saa nane hivi mchana kijua kilikuwa kikali pia kulikuwa na pirika pirika za hapa na pale lakini pirika hizi hazikunishughulisha bali nilijishughulisha zaidi na kinywaji changu 🍸🍹 ambacho kilikuwa juu ya meza pamoja na saa yangu ya mkononi .
Kila mara niliangalia saa kisha nikainua macho yangu huku na kule lakini nilipokosa kukiona kile ambacho nilichokitarajia niliigeukia glass yangu na kuendelea kunywa juisi, nilifanya hivyo zaidi ya mara moja.
Lakini muda wote huu kichwani nilikuwa na mawazo mengi sana pia kitete na hofu viliushambulia moyo wangu, na hofu hii haikusababishwa na kitu kingine zaidi ya kile ambacho kilinifikisha eneo lile, pamoja na mtu ambaye nilifika kuonana naye mahala pale.
Mtu huyu alikuwa ni mwanamke lakini naweza kusema ni mwanamke wa ajabu sijawahi kuona😎
"Hivi ni kweli ni mume wake haswaaa...kwanini sasa anataka kumfanyia hivi, lengo lake haswa ni nini, au ni mtego...lakini Mudrik mkewe namjua na haishi Tanzania sas huyu anataka nini🤦♀️"
Nilijiuliza maswali zaidi ya kumi lakini hakuna hata moja ambalo nililipatia jibu zaidi ya kuumiza kichwa na kuendelea kuutesa moyo wangu kwa hofu🤦♀️
Nikiwa nimekaa nikiendelea kunywa juisi yangu ya matunda ambayo sikuona hata radha yake, mara ghafla simu yangu ya mkononi iliita.
Niliitoa nikatazama kioo "Sofia..."😳
Nilijisemea macho nikiwa nimeyatoa, nilijishauri kwa sekunde kadhaa kisha nikaamua kuipokea.
"Halooo...."
"Tayari nishafika nipo nje hapa..upande wa kuingilia, ukitoka tu utaiona prado nyeusi "
"Aaa...sawa...sa..."
Nilisema lakini kabla sijamaliza simu ilikatwa. 😒😒
Pumzi ndefu niliivuta kisha nikajishauri mara mbilimbili niende au nisiende maana pesa nilikuwa naitaka lakini pia sikuwa na imani na huyu mwanamke niliyetambulishwa kwa jina la Sophia.
Mwanamke huyo sikuwahi kukutana naye kabla na wala sikuwahi kumuona laivu zaidi ya picha , na pia nilitambulishwa na rafiki yangu mmoja hivi, na hii yote ilikuwa ni baada ya mwanamke huyo kutoa dili la milioni kumi. 🤑🤑
Na kama ilivyo kawaida yangu nilikuwa na shida sana na pesa na nilikuwa nipo tayari kufanya chochote kile kwa ajili ya pesa hivyo haraka niliomba kuunganisha naye.
mwanamke huyu alikuwa na mwanaume wake wa ndoa na kwa maelezo ambayo nilipewa ni kwamba mwanamke huyo na mumewe walikuwa na watoto wawili na walidumu kwa zaidi ya miaka kumi.
Dili lenyewe lilikuwa hivi, mwanamke huyu alikuwa anahitaji mwanamke wa kuchepuka na mumewe 🤦♀️🤦♀️
Yaani unachepuka na mumewe ukishamaliza unachukua pesa zako unaondoka. Hapo ndipo tatizo kwa upande wangu lilipoanza, kivipi akubali kuchitiwa tena sio kuchitiwa tu bali atoe pesa kabisa kwa mtu atakayechepuka na mumewe wa ndoa🤦♀️
Mwanzoni nilihisi huenda labda ni mtego ambao niliwekewa, maana kiukweli nilikuwa kwenye mahusiano na mume wa mtu aitwaye 'Mudrik' ambaye alikuwa ni mume wa mtu ila mkewe alikuwa akiishi nje ya nchi, na mara nyingi nilikuwa nikienda kwake na tukijirusha katika viwanja mbalimbali vya starehe na yote tisa kumi, huyo Mudrik ndiye ambaye alikuwa akinilipia ada chuoni pamoja na gharama zingine za maisha na kunifanya nionekane binti wa kisasa🤦♀️🤦♀️
Nilikuwa na hofu sana ila kuna muda nilijipa moyo kwa kuamini kwamba rafiki yangu Irene ambaye ndiye alinipa dili hili, hawezi kunitumbukiza mtaroni lakini pia kuna muda hofu ilinishambulia , hela niliitaka lakini ujasiri niliukosa japo siku kadhaa nyuma nilikubali kila kitu😫
Ngrrrr! ngrrrrr! ngrrrrrr!
Simu yangu iliita tena na nilipoangalia ni yule yule sofia.
"Wewe mbona unanipotezea muda.."😎
"Oooh..so...sorry madam, nakuja"
Nilijibu 🤦♀️
Niliokota vitu vyangu kisha nikainuka zangu lakini hata hivyo ni hatua tatu tu ndizo, kabla ya kupiga ya nne nilisimama
"Hivi Huu sio mtego Kweliiiiiiii...? "🤔
ITAENDELEA...........
Tags
simulizi