TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

SAFARI YA TANGA ILIOGEUKA SAFARI YA KUZIMU 03

*SAFARI YA TANGA ILIVYOGEUKA KUWA SAFARI YA KUZIMU*
*SEHEMU YA TATU*
______________________________________
SAFARI IKAANZA: 
"Aaanh wewe ni mkazi wa Tanga bwana..."
"hapana.."
"ushawahi kufika kabla..."
"hapana...."
"unafikia sehemu gani maana Tanga ni kubwa kuna , Handeni, Lushoto, Kilindi,Pangani, muheza..korogwe..?"
"Eeenh Korogwe pale babu"
"Aaanh korogwe...!, aah bhana korogwe ni mji mzuri sana kwa kuishi na hata kibiashara pia watu wake ni wakarimu sana...hii korogwe unayoisikia sasa ni jina la mtu mmoja hivi ambaye alikuwa ni mmoja wa wakazi wa mwanzo kabisa miaka hiyo..jamaa alikuwa anaitwa mkorogwe yeye alikuwa mzigua alikuwa anaishi katika kijiji kimoja hivi kinaitwa..kilole.., ushawahi kupasikia huko..?"
"hapana.."
"hahahahaaaa....basi utaenda kupaona huko kama utapata nafasi ya kutembea tembea.. mimi pia ni wa hapo hapo korogwe, hahahaa"
alisema mwanaume yule ambaye kiumri alikuwa ni mzee kama wa miaka hamsini na tano kama si hamsini na sita au saba , si chini ya hapo, mzee yule alikuwa mcheshi sana pia alikuwa muongeaji na kiundani alionekana kulifahamu vyema jiji la Tanga kuliko hata nilifahamuvyo mimi. kwangu mimi ilikuwa ni mara ya kwanza sikuwahi kufika kabla na nilikuwa naelekea kwa kazi maalumu ambayo bosi wangu aliniagiza na wala sikuwa najua nafiikia wapi na nitakaa kwa muda gani lakini mzee yule alionesha kuwa 'mzawa' kabisa kwanzia mavazi yake, rafudhi yake mpaka umbo lake vyote vilionesha kuwa yeye ni 'mtanga' haswa .
alikuwa mweupe mno kama walivyo watanga wengi,
alivaa kizabao cheusi ambacho kilitanguliwa na kanzu kubwa nyeupe iliyong'aa , kichwani alitupia kofia moja maridadi ambazo huvaliwa na waislamu mara nyingi hasa wakati wa ibada.
Mzee huyu alijitambulisha kwa jina la Sheikh Mzimbili, nilikutana naye dakika chache tu baada ya kulipanda basi la Saibaba pale Ubungo, ambalo ndilo nililichagua kalitumia katika safari yangu hiyo, siti yangu ilikuwa namba 23 na yeye yake ilikuwa namba 24 hivyo tulikaa kwa ukaribu.
pamoja na ukarimu wake, ucheshi lakini kamwe sikuvutiwa naye kwani alikuwa akiongea na kucheka mara kwa mara tena kwa nguvu kitu ambacho kiliwafanya abiria wengine watutazame kila mara.
ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuelekea mkoani Tanga hivyo nilihitaji zaidi kukaa mwenyewe nifikirie mambo yangu pia niangaze madhari nzuri ya njiani kupitia dirishani ambapo ndipo upande ambao siti yangu ilikuwepo lakini hata hivyo mzee yule alininyima nafasi hiyo, kwani muda wote alikuwa akiniongelesha hata pale nilipoonesha kumpuuzia.

"Aaah..hivi ulisema unaitwa nani bwana...maana kichwa changu hiki kwa kusahau sahau vitu..."
"Razack ila wanapenda kuniita 'Donsoh'.."
nilimjibu kwa ufupi kisha nikakaa kimya.
"ewaaaa...bhana 'Bhana'..umeoa wewe.."
"ku..ku..kuoa..mimi kuoa.., anataka kunipa mke au.."
nilijiuliza kimoyomoyo lakini nilipokosa majibu niliamua kumjibu mzee yule japokuwa majibu yangu yaliuruka ukweli yaani nilimuongopea.
"enhee mzee..nimeoa"
"oooh mashallah ...hongerah sana kijana, hivi unajua kwanini nimekuuliza hivyo..."
"hapana.."
"Bhana wanawake wa Tanga ni warembo na wazuri haswa...kisura kirangi mpaka kimaumbo..wanapendezesha machoni na wanatamanisha moyoni...mfano unamuona yule paleee..."
Yule mzee alisema  kwa sauti ya chinichini kisha kidole chake cha shahada alikinyoosha mpaka mahali alipo mwanadada mmoja hivi ambaye alikuwa amekaa kwenye siti moja iliyopa upande wa pili siti ya nne kutoka tulipokuwa sisi, masikioni alikuwa na 'hearphone' , japo sikutambua kama alikuwa anasikiliza mziki ama aliziegesha tu kama mapambo lakini kitu pekee nilichogundua kilikuwa ni uzuri, mdada yule alikuwa ni mzuri mithili ya malaika. baibui kubwa jeusi ambalo lilifanikiwa kumpa stara lakini kamwe lilishindwa kulificha umbo lake zuri la kuvutia ambalo lilionekana vyema hata pale alipokaa, kichwani alijifunga hijabu, alionekana mtulivu asiye na pupa. nilimtizama mwanamke yule kwa zaidi ya sekunde arobaini huku ubongo wangu ukifanya kumchambua kwa kila nilichokiona, lakini ghafla uchambuzi wangu ulifika tamati pale tu sauti nzito ya upole ambayo niliisikia mimi tu , ilipotua katika masikio yangu,
"umemuona..eeenh"
"ndio.."
"Sasa yule ni mtanga... na huko unapoenda utakutana na wengi zaidi ya yule... "
Maneno ya yule mzee yalinifanya nimgeukia tena yule mwanadada kwa sekunde chache,kisha moyoni nikajikuta natamani dereva apaze gari ili niwahi kuwaona maana mimi na warembo bhana ni damu damu, nipo tayari nisile lakini sio kupitwa na warembo na hili hata Jasmine mwenyewe ambaye ndiye alikuwa mpenzi wangu alikuwa akilitambua na mara nyingi lilitufanya tugombane lakini kamwe sikukoma.
"sitaki ushauri , nikizeeka ntaacha"
ndilo lilikuwa jibu pekee ambalo mara nyingi nilikuwa nikiwapatia wale ambao walikuwa wakijifanya wananishauri juu ya tabia yangu mbayo
"ila bwana kuwa makini, mkoa wa Tanga unasifika kwa majini hasa ya kike..unaweza kumuona msichana mzuri kumbe ni jini...."
Maneno ya yule mzee yalinistua , niliacha kumuangalia yule mrembo
"Jini...!"
"Eenh bwana..kwani huwajui majini wewe"
"na..nayajua"
"basi ndio hivyo, bhana fanya kilichokuleta..na kama utataka msichana basi kabla hata hujamfata jaribu kuwasiliana na wenyeji, sawa bwana"
"sa...sa..sawa mzee, nimekuelewa"
"eeenh unielewe kweli...hahhahaa.."
yule mzee alisema kisha akaweka nukta, aliingiza mkono wake katika fuko lake kubwa ambalo alikuwa amelipakata katika mapaja yake kwa muda wote tangu mwanzo wa safari , na alipoutoa alitoka na kijitabu kidogo ambacho kilikuwa na maandishi mengi ya kiarabu. alikiweka mapajani mwake kisha akakiinamia na hapo ndipo ulikuwa mwisho wa kuisikia sauti yake, hakuongea tena. na mimi hapo nikapata hafueni , ule usumbufu wote sasa ulikuwa umefika tamati.
safari iliendelea dereva alijitahidi kuiramba rami huku akifata maelezo kadhaa ambayo yalikuwa yakitolewa kupitia vibango vichache vya barabarani.
wakati safari ikiendelea na yule mzee akiendelea kusoma kitabu chake nami kamwe sikuacha kumtazama yule mwanadada ambaye mwanzoni kabisa nilioneshwa na Mzee, kama mfano wa wanawake wa 'Tanga' ambao natakiwa kuwa makini nao , lakini kadri nilivyomtizama mwanamke yule ndivyo kadri ambavyo nilivyojikuta nayasahau mawaidha ya yule mzee na moyo wangu ulizidi kudunda kwa tamaa kwani kitendo cha kumtizama tu mwanamke yule nami nilikuwa tayari nishamtamani.
"huyu..lazima nipite naye, akishuka tu ninaye..., huyu mzee ushauri akawape wajukuu zake sio mimi.."
nilijisemea kimoyomoyo

Itaendelea....

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post