(1-5 )
*THEOPISTA*
NILIOLEWA ILI NISOMESHWE.
Na 1.
Maisha yanachangamoto nyingi sana,muda mwingine unaweza kujihisi unagundu au haujawahi kuwa na bahati,muda mwingine mambo yanayotutokea yanapelekea tuishi maisha tusiyiyapenda,maumivu ya kwenye mioyo yetu muda mwingine yanaweza kupelekea tukafanya maamuzi ambayo sio sahihi.
Naitwa Theopista,ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watano,ni binti nilielelewa katika misingi ya dini sana mpaka kupelekea kuogopa kufanya mambo mengi sana.
Niliishi na wazaz wangu mpaka pale baba yangu alipofariki mwaka 2005,nilikuwa nipo kidato cha pili,BABA alikuwa mwalimu,ingawa hatukuwa na kipato kikubwa ila tuliishi maisha ya furaha upendo na amani,maisha yetu yalibadilika baada ya baba kufariki.
Mama yangu alikua ni wale wa mama wa nyumban wanaoletewa kila kitu hivyo hakuwahi kujishughulisha na chochote hivyo baba kufariki lilikuwa pengo kubwa katika familia yetu maana hatukuwa tunaweza kujisimamia kwa lolote.
Ndugu walitutenga wakiogopa majukumu kwa kuwa ni familia kubwa.
Upande wa baba walikuwa nauwezo kiasi lakin hakuna ata mmoja alietaka kutusaidia.
Kuna rafiki mmoja wa baba alimpa Mama mtaji wa biashara kwa kuwa Mama hakuwa mzoefu biashara ilikufa.
Maisha yetu yalikuwa yakuomba omba.
Kuna baadhi ya majirani walikuwa wakitusaidia ila n kwakiasi kidogo sana.
Nilisoma kwa bidii sanaa nikiamin mimi kama Dada natakiwa kupambana kwaajili ya kesho ya ndugu zangu.
Nilimaliza kidato cha nne mwaka 2007 na baada ya kumaliza niliamua kujiingiza kufanya kazi sokoni walau ikitokea nimefaulu nipate pakuanzia.
Namshukuru Mungu nilifaulu,nilipata division one ya pointi 9 nilifaulu vizuri kiasi kwamba ningeweza kusomea kitu chochote kile .
Ishu ikaja kwenye kufuatilia cheti,kwakuwa nilikuwa nadaiwa ada na michango mingine sikuweza kupewa result slip,hivyo ikabidi nitowe pesa yote niliyonayo ili niweze kupewa result slip.
Matokeo yalitoka nikachaguliwa kujiunga na advance katika shule ya bagamoyo mkoani pwani,shida ikawa sina nauli wala ada,Mama yangu alitoka na kuanza kuomba kwa watu ili walau nipate nauli ya kujiendeleza kimasomo ila alidhalilishwa sana na baadhi ya watu wakimtaka kingono ili wamsaidie kiasi cha pesa anachohitaji.
Kwa kuwa anaupenda utu wake alikataa ila alikuwa anaumia sana kuniona nina juhudi na hakuna wa kuniendeleza.
Aliapa kwa namna yoyote atapambana ili nisome huenda nikaja kuwa msaada kwa familia yangu.
Nilianza kuhangaika kuomba misaada kwa ndugu au hata kufanya vibarua vidogo vidogo ili walau nisome ila pesa haikutimia maana pia unakuta muda mwingine kidogo ninachopata natoa tule.
Nilienda kwa ndugu wa baba ambao mara nyingi baba aliwawwzesha maana amesomesha wadogo zake wote na kuwatafutia kazi 'na hata kupelekea sisi kukosa chanzo chochote cha pesa maana pesa nyingi alikuwa anasaidia ndugu zake ila hakuna alienisaidia.
Mmoja nilimuomba walau aninunulie mahitaji yashule alinipa elfu mbili akanambia kamaliza laki saba kwenye shughuli ya rafiki yake hivyo hana pesa.
Poor Theo......
COMMENT ZIKIWA ZA KUTOSHA NITARUDI CHAP
*THEOPISTA*
NILIOLEWA ILI NISOMESHWE.
Na 2.
Ilipoishia
Mmoja nilimuomba walau aninunulie mahitaji yashule alinipa elfu mbili akanambia kamaliza laki saba kwenye shughuli ya rafiki yake hivyo hana pesa.
Poor Theo......
Songa nayo ........
Nilihuzunika sana,ndugu wa upande wa Mama hawakuwa na uwezo maana familia yetu ndio kidogo tulikuwa na kitu na ndio familia iliyotegemewa sasa ndio hivyo baba hayupo.
Ila ikapitishwa harambee ya ukoo,namshukuru Mungu nilipata ada na nauli pamoja na pesa kidogo ya matumizi.
Nilifurahi sana kwenda shule,maana nilishajikatia tamaa na kuhisi mimi kusoma ndio basi tena.
Nilikuwa na bidii na juhudi ya hali ya juu katika masomo yangu nilichaguliwa kusomea combination ya PCB,nilitaman kuja kuwa daktari mkubwa siku moja..
Niliishi maisha ya kiuchumi sana maana najua hata nikiishiwa pesa hakuna wakunisaidia,nikapata wazo la kuanzisha biashara,nikawa nauza rim paper na pipi na kalamu.
Mtaji haukuwa shida maana nilianza na mtaji wa elfu 16 na ndio ilikuwa pocket money yangu hivyo nikaona bora niizungushe walau nipate pesa kidogo ya kujikimu.
Sikutaka kuendelea kuomba ndugu maana wanalawama zao.
Namshukuru Mungu ingawa sikuwa napata pesa kubwa lakin nilianza kujitegemea kwa mahitaji yangu madogo madogo na kuna kipindi hata pesa ndogo ndogo nilikuwa natuma nyumban maana najua hali halisi ya nilipotoka.
Namshukuru Mungu nilimaliza kidato cha sita salama nikarudi nyumban kwaajili ya kusubiri matokeo,nilinawiri na kupendeza maana nilikuwa napata vipesa kidogo kipindi nasoma na nilikuwa najinunulia vimafuta na nguo walau nisionekane nimepauka.
Baada ya kurudi tu kuna rafiki wa baba alikuja akaanza kutusaidia,Mama alipendeza na wadogo zangu walimpenda.
Alifiwa na mkewe kipindi sisi wadogo na anamtoto wake wa kwanza ambae ni mkubwa kwangu wakiume anasoma Uganda.
Kumbe bana mzee yule alikuwa anayake ya rohoni.
Maisha haya tusali sana na kumuomba Mungu atupe umri mrefu wa kuangalia watoto wetu.
Matokeo yalitoka nilipata divison one ya sita nilikuwa na uwezo wa kwenda kusomea ninachokitaka ila sasa sikuwa hata na pesa ya fomu ile elfu 10.
Ikabidi nimuombe yule baba anisaidie na kweli alitoa akanipa laki moja ya kufanyia kila kitu pamoja na matumizi yangu madogo madogo .
Siku moja nilienda kumtembelea rafiki yangu mimi pamoja na mdogo wangu anaenifata n wakike,bahat mbaya mvua ikatukuta huko na usiku ulikua ushaanza kuingia,ikabidi tusubiri mvua iishe ndio twende nyumban.
Basi mvua ikaisha kwenye saa tatu kasoro usiku na tulipokuwa tunaishi hakukuwa na nyumba nyingi ila kwa kuwa tulikuwa wawili hatukuogopa.
Tukafika sehemu kuna kama kichochoro tukapishana na vijana wawili kwa kuwa kulikuwa giza hatukuwatilia maanan.
Mmoja akamshika mdogo wangu mkono mwingine akanishika mimi.
Tulishtuka nikaanza kupiga kelele ila kwa eneo tuliokuwepo nyumba zilikuwa mbali hivyo ilikuwa n ngumu mtu kutusikia.
Wale vijana tulikuwa tunawafahamu mmoja wao anaitwa Charles alishawahi kunitongoza ila siku mkubali maana kutokana na hali ya kwetu niliona kama kujiingiza kwenye mahusiano n kujiangamiza.
Sasa akaniuliza Theo Jibu langu vipi.
Nikamwambia ukweli kuwa Mm sina hisia nae atafute atakae mpenda.
Nikashangaa kashika simu akawa anampigia mtu.
Oyooo Ndege kaingia tunduni njoon tuchune manyoya.
Uwiii Theo mimi
COMMENT ZIKIWA ZA KUTOSHA NITARUDI CHAP
*THEOPISTA*
NILIOLEWA ILI NISOMESHWE.
Namba 3&4
Ilipoishia ...........
Sasa akaniuliza Theo Jibu langu vipi.
Nikamwambia ukweli kuwa Mm sina hisia nae atafute atakae mpenda.
Nikashangaa kashika simu akawa anampigia mtu.
Oyooo Ndege kaingia tunduni njoon tuchune manyoya.
Songa nayo.................
Sikuwaelewa ila tukawa tunajitahidi kujitoa kwao,mimi nikabahatika kumpiga yule mwanaume mabiringanya yake teke akaniachia nikaenda kupambana na yule mwanaume aliemshika mdogo wangu ila kwa bahati mbaya wale waliopigiwa simu wakawa wamefika ikabidi nikimbie nikaombe msaada kwa watu lakin maskin grace mdogo wangu wakati narudi nikiwa na wanakijiji nikakuta tayari wale vijana wameshambaka na wamekimbia,nililia sana pamoja na mdogo wangu,tukamchukua tukampeleka hospitali wakampima na ikathibitishwa kweli amebakwa,Mama alikuja hospitali tukaanza kulia mimi Mama pamoja na mdogo wangu Jack.
Niliumia namna mdogo wangu alivyotolewa usichana wake kikatili namna ile..
Tulieuhusiwa kurudi nyumban ila mdogo wangu hakuwa sawa akawa ni mtu wa kujitenga na kulia hovyo wakati huo alikuwa kamaliza kidato cha nne.
Nikawa ndio mfariji wake mkubwa,yule baba akawa anaendelea kutusaidia na kuwa bega kwa bega na sisi kwenye matatizo yote.
Namshukuru Mungu nilichaguliwa UDOM kusomea ukunga na nila sikuwa na nauli wala direct cost ingawa nilipata mkopo asilimia mia ila nilitakiwa kulipa directcost ili niweze kuingia chuoni,na pia sikuwa nimemaliza kulipa michango hivyo nilikuwa na pesa kidogo ya vubarua ninavyofanya nikalipa shule ishu ikawa n direct cost.
Yule baba akaniita siku moja kwake,nilikuwa natoka kanisani.
Sikuona shida maana amekuwa kama mzazi wangu.
Nilipofika akanambia nifunge macho tuombe Mungu anisaidie nipite mapito ninayoyapitia mimi pamoja na familia yangu,nikafanya kama alivyosema na kweli tulianza maombi.
Tukiwa katikati ya maombi nikaahisi napapaswa,kuangalia ni yule baba.
THeo nataka nikufanye mwanamke wa pekee katika haya maisha naomba nikuoe uwe mke wangu,nilishtuka sana maana sikutegemea maneno yale kutoka kwa mtu kama yeye,nikamuomba niondoke akanitolea PC akanipa na pesa kama laki hivi akanambia nikafanye shoping maana chuon natakiwa nivae vizuri.
Sikumjibu nikaondoka nikaenda kumuambia mama..
Ingawa nilikuwa na shida ila sikutaman kuingia katika mahusiano au ndoa ya aina ile.
Na isitoshe sikuwah kuwa kwenye mahusiano yoyote huko nyuma .
Mama yangu akaanza kulia,nilijisikia vibaya sana..
Wale vijana waliombaka Jack mdogo wangu sikuwaona tena maana tulitaka kupeleka kesi mahakaman lakin hawakuonekana kabisa na kwa bahati mbaya Jack akagundulika n mjamzito na amefaulu kuendelea na Advance..
Mama alikuwa n mtu wa kulia,mpaka nikawa najisikia vibaya maana ndugu walijua nikienda chuo sitohitaj tena msaada hivyo hakuna aliekuwa anahangaika na sisi kabisa.
Yule baba akaanza kupakaza sifa mbaya kwenye familia yetu kuwa ameacha kutusaidia kwa kuwa kaona sisi n malaya.
'na akadai kuwa tunasingizia mdogo wangu kabakwa ilikuficha aibu ya mimba.....
Kwa kuwa matokeo yalitka mwezi wa saba na nilitakiwa kureport chuo mwezi wa kumi mwishoni nikaona nikatafute vibarua ili walau nijue nitaanza je maisha yangu.
Katika mihangaiko yangu nikakutana na kijana mmoja ambae tulikuwa tumezoeana maana nilienda kuuza sokon alikuwa anaitwa BRison ila nilizoea kumuita Bri
Yule kijana alikuwa anauza dagaa na samaki dykan ila halikuwa duka lake alikuwa kaajiriwa tu. mimi nauza mboga.
Kwa muda mfupi tukazoeana hisia za mapenzi zikaaanza kututawala.
Yeye kama mwanaume anavunja ukimya na mimi sikuvunga nikakubali wito.
Alikuwa ananiheshimu sana na tulikuwa tunapenda sana ingawa n kwa muda mfupi sana..
Hakuwa na uwezo ila alihakikisha ninafuraha alikuwa kila tukikutana ananiletea lolipop au apple yaani hakuwa na pesa ila alijikaza kuniletea zawadi.
Basi siku ikafika nikaenda chuo huku ujauzito wa mdogo wangu ukaendelea kukua na Bri akanisaidia baadhi ya mahitaji nikaenda chuo..
Mwezi ukapita kuanzia nireport chuo siku moja nikapigiwa simu 'na mtu kuwa mdogo wangu Jack kakutwa mferejin akiwa ametapakaa damu na alikuwa na simu namba ya mwisho kuwasiliana nayo ilikuwa yangu na kweli niliwasiliana na Jack muda mfupi uliopita akanambia anajisikia vibaya poor Jack kumbe alikuwa amejaribu kutoa mimba
*THEOPISTA*
NILIOLEWA ILI NISOMESHWE.
Namba 5.
Ilipoishia ...........
Biashara zote ninazofungua zinakufa na mahitaji ya watoto n mengi na sijawah kufika hata robo yake mahitaji yao.
Najua hata binti yetu atatusamehe.
Nilijikuta nalia..
Songa nayo...........
Nilihisi maumivu anayoyapata mama yangu kwaajili ya kutulea,nilijisikia vibaya sana.
Jion ilifika mama akarudi nyumban.
Akanikuliza kuhusu maamuzi yangu yakumkubalo Dany.
Sikuwa na jibu maana sikuwa na hisia nae kabisa japo alikuwa ananipenda sana nikamuomba mama anipe Muda wa kulifikiria hilo zaÃdi.
Kesho yake nikampigia Bry akawa ananiomba tusex au hata nimzalie ili apate kibali cha kunioa.
Niliogopa sana kufanya chochote nikajiapiza kulipigania penzi langu kwa namna yoyote.
Bry walizaliwa watoto wawili yeye pamoja na dada yake mkubwa,walikuwa wanapendana sana.
Siku moja dada yake Bry akanipigia akiniomba nisije kumuacha Ndugu yake maana ananipenda sana.
Ni kweli najua Bry ananipenda Ila sikujua nimuweke nani upande wangu kati ya mama au mpenzi.
Kila nikifikiria majonzi ya mama yangu nilikua naumia sana,maana amepambana na kudhalilishwa Sana kwaajili ya kutulea sisi,katika kitu sikuwa napenda kukiona ni huzuni katika uso wa mama yangu.
Siku moja nikawa nimetoka kurudi nikamkuta Dany na mama.
Dany alinunua stoking ya vitu ikiwa n mchele,unga na mafuta akamletea mama.
Nilivyomuona nikajisikia vibaya,sikutaka hata kuongea nae nikapitiliza ndani nikaanza kulia.
Mama akaniita niongee na mgeni .
Haya Theo embu toa jibu zuri kwa mwenzako akawa anataka kuondoka nikasema nimekubali.
Yule kijana alifurahi Sana ila mama yangu alinyong'onyea kuliko nilivyofikiria.
Posa ikaletwa siku tatu baada ya kujibj,nilishindwa hata kuipokea nikawa nalia na sikumwambia Bry lolote maana nilihisi nitamuumiza na kingine nilikuwa na umizwa na huzuni ya mama hivyo nikaona ni bora nikubali anachokitaka huenda nikapunguza majonzi yake...
Siku zilienda muda wa kurudi chuo ukafika,Dany akanilipia nauli akaninunulia PC na kunipa pesa ya matumizi.
Nilijisikia vibaya maana hata sikuwa na hisia nae,nilikuwa nawaza namna yakumwambia Bry ukweli nilijua nitamuumiza Sana ila niliona ni bora nihuzunike kuliko ahuzunike mama yangu.
Nikarudi chuo mahusiano na Bry yakaendelea nikawa naendelea kuwasiliana na Bry maana ndio kidogo nikiongea nae moyo wangu unatulia ingawa Dany alikuwa ananitafuta na alionekana kunipenda kweli ila sikuwa na hisia nae kabisa.
Akawa anataka tuanze kypanga mipango ya harusi.
Nikawa namkatia maana nilihisi nitakuja kumuumiza.
Bry akabadilika akawa anataka a sex na mimi ili kumuaminishia Kama nampenda.
Kutokana na malezi niliyolelewa nilikataa akawa anasema simpend na sina malengo nae ndio maana sitaki kutimiza analolitaka.
Akawa hana aman kabisa na mimi,nisipomtafuta anagomba,nikichelewa kupokea simu anambia namsaliti kiufupi hakuwa na aman kabisa.
Tags
simulizi