TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

SARAFINA 02

SARAFINA 2
   Sarafina alimuangalia mama yake Kisha akamuuliza 
" Mama inamaana baba alikuwa hakushirikishi katika Mambo yake?
" Kuna baadhi alinishirikisha  
" Kama yapi?
" Baadhi ya biashara zake na Mali tulizokuwa tunamiliki.
" Unajua alipokuwa anahifadhi documents zake muhimu? 
Ni hapa kwenye hii droo watakuwa wamezichukua zote maana baba yako mkubwa ndio alikuwa mtu wake wa karibu na alimwambia Mambo yake mengi na kwa haya wanayofanya watakuwa wamesomba kila kitu tuondoke mwanangu tusije tukapata aibu nenda kafungashe vitu vyako. Sarafina alinyanyuka na kuelekea chumbani kwake pia mama yake alifungua kabati na kupanga nguo
Nakuanza kutoa vitu vyake na kupanga kwenye begi mmara akaona faile alichukua na kukuangalia 
" Hili faile limewekwa na Nani huku .alipotaka kulifunua aangalie alisikia geti limefunguliwa aliweka kwenye begi haraka haraka na kuweka nguo kwa juu Kisha akafunga begi. Ilisikika sauti ikimuita sarafina . Sarafina alitoka pamoja na mama yake wakaenda seblen alikuwa ni Romani na wale wateja waliokuja kununua nyumba wakiwa wameongozana na vijana wawili
" Jamani hapa pameshauzwa mnatakiwa muondoke. Aliongea Roman 
Sara na mama yake hawakuongea kitu walienda chumbani kuendelea kukusanya mizigo yao walipomaliza waliondoka mama Sara aliondoka huku aligeuka nyuma kuangalia nyumba yake.
" Mama tunaelikea wapi
" Tutajua huko mbele ya safari mwanangu 
" Basi tungeenda kwa mama mkubwa
" Hapana sitaki kwenda kwa ndugu yoyote nawajua ndugu zangu tutapata sehemu ya kuishi. 
Sarafina na mama yake walienda kutafuta nyumba huko changanyikeni. Walianza maisha yao mapya japo mwasho ulikuwa mgumukuzoea mazingira ya uswahilini.
" Siku moja usiku mida ya saa tano usiku sarafina alishituka usingizini na kumkuta mama yake amekaa huku mkono upo shavuni.
" Mama mbona hulali unawaza nini?
" Nawaza jinsi nilivyokuwa mpumbavu nimepoteza Mali zangu nilizozihangaikia kwa tabu eti leo hii naishi maisha haya kweli.
" Lakini ndio yameshatokea mama inabidi tukubaliane nayo.
" Sarafina mwanangu wewe hujui tu wakati nakutana na baba yako alikuwa Hana kitu kabisa yeye alitoka kwenye familia masikini pia Mimi hivyohivyo lakini alijikuta najishuhulisha na biashara zangu ndogondogo pia nilikuwa nafua kwenye majumba ya watu tukawa tunapata hela ya kula na kulipa Kodi siku moja nilienda kwa mama mmoja ambae nilikuwa namfanyia kazi nyumbani kwake yule mama alikuwa anaumwa hakuwa na mtu wa kumsaidia mume wake alifariki na kumuachia nyumba mbili na maduka pia walikuwa na gari ya kutembeleana hakubahatika kupata mtoto ndugu walimdharau hakuna Alie mjali hivyo Mimi nikamsaidia kwa kila kitu hata alipozidiwa nilihamia nyumbani kwake ili kumuuguza . Yule mama alikuja akafariki baada ya mazishi ndugu walijitokeza na kugombania Mali zake lakini kwa bahati yule mama aliacha wasia na kumpa mwanasheria wake aliandika Ile nyumba aliyokuwa anakaa na duka moja nipewe Mimi na Mali nyingine zote ziuzwe pesa zipelekwe kituo Cha kulelea watoto yatima kuanzia hapo maisha yangu na baba yako yalibadilika tulisimamia like duka tukapata faida na kufungua duka lingine pia tukajenga nyumba Ile tuliyokuwa tunakaa Ile ya urithi tuliiuza tukaongeza biashara tukaendelea kujenga nyumba nyingine tatu moja ni Ile anayokaa baba yako mkubwa nyingine akamleta mwanamke wa kijijini kwao bila Mimi kujua ambae ni mama Romani . Nilikuja kugundua wakiwa na mtoto wa mwaka mmoja na wewe ukiwa na umri huohuo kwahiyo wewe na Roman mmepishana miezi mitatu tu.
" Kumbe tumezaliwa mwaka mmoja
" Ndio.
" Sasa ikawaje ulipogundua?
" Mwanzo baba yako alikataa kuwa sio kweli nikataka waondoke kwenye Ile nyumba mama Roman alimuomba Sana kwakuwa hakuwa na kwakwenda kwavile alikuwa na mtoto nilamuonea huruma Nika muacha pia baba yako aliniambia hayakuwa karibu nae ilikuwa ni bahati mbaya tu kumbe ilikuwa ni uongo waliendeleza uhusiano wao mama Roman akabeba ujauzito mwingine lakini hakufanikiwa kujifungia ukitoka baada ya wao kugombana baba yako alimpiga wakati anakimbia akaangukia tumbo mimba yake ikatoka. Mimi na mama Roman tulikuwa maadui hatujawahi kupatana nahisi hii mipango yote itakuwa wamepanga baba yako mkubwa na mama Roman ili kutukomoa hata hivyo najuta kumuachia kila kitu baba yako Mambo mengine ningesimamia mwenyewe yasingetukuta haya. Sarafina alimsogelea mama yake akamkumbatia
" Basi mama yangu usilie
" Naumia sarafina unajua hizi Mali zote niza kwako
" Basi mama hebu lala kwanza. Sarafina alimlaza mama yake na kumfunika shuka. Nae akajilaza lakini hakuweza kupata usingizi alifikiria maneno aliyoambiwa na mama yake yalimuumiza 
" Kumbe Hawa wajinga Wana ng'ang'ania Mali za mama yangu sitakuwa dhaifu naapa kupambana

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post