TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

SARAFINA 03

SARAFINA 3
   Maisha yaliendelea huku wakifanya biashara ya genge sarafina aliamka mapema na kwenda sokoni kununua bidhaa Kisha anaenda kupanga mida ya saa nne mama yake anaenda kumsaidia nae anarudi nyumbani kwenda kupumzika biashara yao ulienda vizuri walipata wateja wengi.

Siku moja sarafina alitoka sokoni na kuanza kupanga bidhaa kibandani  Mara lilikuja gari na kusimama mbele ya kibanda Chao aliacha kupanga vitu na kuangalia ni Nani  alimuona Romani alishuka kwenye gari alimfuata mpaka pale aliposimama  Romani alimuangalia Kisha akaangalia litu vilivyopangwa pale gengeni Kisha akasema

" Nakuona binti wa mfanyabiashara maarufu   unapambana  vizuri Sana  nilijua utakuwa ombaomba kumbe unajiweza.

" Romani umefuata Nini hapa na kwanini unanifuatilia tumeshawaachia kila kitu hakuna mmachotudai  naomba ukae mbali na maisha yetu.

" Hata hivyo sikuwa nafikiria Kama nitawafuata Ila Kuna Jambo limenifanya mpaka nimeamua kuwatafuta  Ila siwezi kuongea chochote na wewe kwakuwa Ni poyoyo huna unaloelewa ingekuwa vizuri ningeongea na mama yako huwenda tungeelewana.

" Basi unaweza kwenda maana mama yangu hayupo hapa 

" Nitampataje?

" Nenda nyumbani kwenu kwenye tundu la choo inama Kisha ita mama sarafina atakusikia na atakuja kukusikiliza shida zako. Sarafina alipomaliza kuongea akageuka na kuendelea kupanga vitu vyake.  Roman alicheka kwa dharau Kisha akasema

" Naona umekuwa mswahili lakini sio kosa lako ni mazingira unayoishi lazima ufuate tabia zao naondoka Ila nitarudi. Roman alipiga hatua chache Mara akamuona mama sarafina alisimama kumsubiria alipofika karibu alimsalimia

" Shikamoo mama

" Sina haja na salamu yako wewe mnafki umefuata Nini hapa?  Sarafina alipoona mama yake kasimama anaongea na Roman nae aliamua kusogea asikie kinachoongelewa

" Nimekuja kuonana na wewe Kuna document za mzee inasemekana zilikuwa ndani  tulikuwa tunazihitaji 

" Mmmh documents gani  kweli nyie watu  hamtosheki mmechukua kila kitu chetu na bado mnatufuata huku au mnataka roho zetu .

" Hatuna haja na nyie tunataka documents Basi na usipozitoa kwa hiyari yako tutazichukua kwa nguvu. Sarafina alichukizwa na majibu mabovu ya Roman akadakia kwa kusema

" Hebu ondoka  hakuna mwenye hizo documents hapa.

" Sawa naondoka Ila nitarudi kwa Mara nyingine Tena. Roman alienda kupanda gari yake na kuondoka huku sarafina na mama yake walienda kibandani kwao

" Mama hivi ni kweli una documents

" Hapana mwanangu si nilikwambia tangu siku nyingi kwamba Sina chochote ninachojua  na sijui wanachokitafuta kwetu ni nini.
Siku hiyo mama sarafina alikuwa mnyonge na mwenye mawazo sarafina alipomuuliza mama yake anatatizo alikataa na kumwambia yupo sawa sarafina hakutaka kurudi nyumbani na kumuacha mama yake kwenye Hali Ile baada ya muda mama sarafina  alimkumbuka kitu akamwambia mwanae
" Sarafina wewe kaa hapa Mimi naenda nyumbani kupumzika na Kama ukiona umechoka funga tu urudi nyumbani
" Usijali mama nenda kapumzike. Mama sarafina aliondoka haraka na kuelekea nyumbani kwake alipofika alifungua mlango akaingia Kisha akajifungia alifungua begi lake na kutoa Lile faile alifungua na kuangalia vitu vilivyomo  alijikuta anatetemeka  Mara mlango uligongwa alishituka  na kulifunika haraka huku akihangaika alifiche sehemu gani  alifunua godoro na kuliweka Kisha akaweka sawa na kwenda kufungua mlango

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post