SARAFINA 4
Mama sarafina alifungua mlango na kuchungulia
" Ooh mama Hilda karibu.
" Asante nimekuona hakuna kufuli nijua upo nilikuwa naomba chumvi . Mama sarafina aliingia ndani na kuchukua chumvinkisha akampa jirani yake
" Asante jirani . Mama Sara aliingia ndani na kufunga mlango alikaa kitandani na kumshusha pumzi
" We Mungu wangu hizi documents ndizo zinazotafutwa na Mambo mengi muhimu yamo muhu natakiwa kuwa makini na hili sijui niliweke wapi sehemu yenye usalama.
Sarafina alirudi nyumbani lakini mama yake hakumwambia kitu chochote. Ilipita wiki moja siku moja wakiwa kwenye biashara yao mama Hilda alienda huku akiwa anakimbia alipofika aliinama na kushika magoti yake hukubakihema
" Mama sarafina Kuna watu wasiojulikana wamevamia pale nyumbani wakatuita watu wote tuliokuwepo na kutukusanya pamoja Kisha kututishia kutuuwa endapo tutapiga kelele walitaka tuwaache wafanye kazi yao walivunja mlango wenu na kuviruga kila kitu sijui walikuwa wanatafuta nini. Sarafina alitokambio na kumuacha mama yake akifunga kibanda alipofika nyumbani alikuta vitu vimetupwa ovyo na vingine kuvunjika
Alianza kuokota kimoja baada ya kingine baada ya dakika chache mama yake alifika aliki alikuwa hayupo vizuri presha ilipanda na kumfanya azidiwe wakamkimbiza hospital.
" Eee Mungu wangu mtihani gani huu unanipata na haya yote atakuwa anafanya Roman sijui kwanini wanatuandama hivi.
Mama sarafina alipata matibabu akapewa dawa wakarudi nyumbani sarafina alimlaza mama yake kitandani na kuendelea kuweka vitu vizuri.
" Mama unajua haya yote anafanya Romani hivibtungekuwa na hizo documents tungehangaika hivi tungeishi maisha magumu kiasi hiki.
Mama sarafina hakumjibu mwanae
Siku zilisogea sarafina aliendelea na biashara akiwa anahudumia mteja Roman alifika sarafina hakumjali aliendelea kuhudumia wateja
" Sarafina naomba tuongee Mambo ya msingi
" Kumbe na wewe unajua Mambo ya msingi kwanza Sina muda huo walikaa na kukusikiliza Bora ungeondoka.
" Hebu acha dharau unataka hili ninalotaka kukwambia litakusaidia kwenye maisha yako nisikilize Kama mnazo zile documents naziomba alafu nitakupa asilimia hamsini ya hisa kwenye kampuni pia nitawapa nyumba ya kuishi . Sabrina alimuangalia Roman Kisha akamcheka
" kweli umeishiwa nyie si wajanja mnauwezo wa kumiliki kila kitu pambaneni Sasa au mmeshaanza kudhurumiana na huyo baba yako mkubwa nisikilize kwa makini hatuhitaji chochote kutoka kwenu tumeridhika na haya maisha tunayoishi. Roman alimbembeleza Sana Ila hakuambulia kitu ilibidi aondoke.
Roman hakuacha kuwafuatilia siku moja mida ya saabili usiku mama sarafina alikuwa anapika chakura Cha jioni huku sarafina akiwa anafanya mahesabu ya mauzo aliyouza kwa siku hiyo mlango ulifunguliwa kwa nguvu sarafina na mama yake walishituka aliingia Roman na baba yake mkubwa
" Jamani ndio ustaarabu gani huu mnaingia bila kugonga ungekuta watu wanavaa je? Aliuliza mama sarafina
" Hilo halituhusu pia hatujaja hapa kujibu maswali naomba documents najua wewe ndio unazo. Alisema baba yao mkubwa akimwambia mama sarafina
" Lakini shemeji wewe ndio ulikuwa unajua Mambo mengi ya marehemu ndugu yako Mimi hizo documents Sina hata Kama zilikuwepo mule ndani zitakuwa zilichukuliwa siku Ile ya msiba au tumezia kwenye Ile nyumba maana tulichukua nguo zetu tu.
" Sio kweli kwenye Ile nyumba nilikagua mlivyoondoka kulikuwa hakuna kitu. Alisema Roman
" Basi na sisi hatuna kitu mnaweza mkaondoka msitujazie watu hapa. Roman na baba yake mkubwa waliondoka .
Roman hakuacha kuwafuatilia aliwafanyia fujo za kila aina ukafikia hatua aliwachonganisha na mwenye sehemu wanapouzia genge lao mpaka wakafukuzwa. Siku aliyokuwa anafukuzwa Roman alienda na kumuangalia huku alimcheka Jambo Hilo lilimuumiza Sana sarafina.
" Mama tutaishije Sasa pale kibandani tumeshafukuzwa.
" Mwanangu kunajambo nataka tuongee naomba iwe Siri hizo documents ninazo. Sarafina alimsogelea mama yake
" Mama kumbe siku zote umekaa na documents na nikikuuliza lakini ulikataa na kuendelea kunificha
Ni kweli nilikuwa sijui sijui Ila sikuile tulivyokuwa tunapanga vitu ili tuondoke ndio nikaliona kwenye nguo zangu sikupata muda wa kulikagua nikaweka tu kwenye begi sikukumbuki Tena kukuangalia mpaka Roman alipokuja kuulizia ndipo nilikumbuka
" Sasa liko wapi? Aliuliza sarafina kwa shauku kubwa
" Nashukuru Mungu siku ya pili yake nilienda kukuficha nilifunga kwenye nguo nikaweka kwenye mfuko na kumpeleka kwa mama yako mdogo Ila siku mwambia kitu anajua Ni nguo nataka kumpeleka kwafundi. Sarafina alishusha pumzi kisha akamwambia
" Mama hutakiwi kukaa kwenye huu mji Hawa watu wanajua fika documents unazo wewe hawataacha kukufuatilia.
" Sio naondoka tunatakiwa tuondoke wote Mimi na wewe.
" Hapana mama tukiondoka wote watashituka hawataacha kutufuatilia wewe nenda Mimi nitabaki hapa.
" Hapana sitaweza kwenda kuishi kwa amani Roman lazima atakusumbua
" Sijali kuhusu yeye hata hivyo nitaenda kuishi kwa mama mdogo huku nikipambania kurudisha Mali zetu nahitaji kulipiza mama . Sarafina aliongea na mama yake akamuelewa.
Kulipokucha mapema Sana sarafina alienda kuchukua mzigo wa mama yake kwa mama yake mdogo na kurudisha nyumbani kwao sarafina alikagua zile documents huku akiachia tabasamu Kisha akamsogelea mama yake na kumkumbatia tutashinda mama unatakiwa kuondoka kesho .
" Lakini mwanangu roho inaniuma Sana naogopa utapata matatizo naomba tuondoke wote alafu utarudi. Wakiwa wapo kwenye maongezi mlango uligongwa sarafina akaenda kufungua Mara alisukumwa na kuanguka
Tags
simulizi